ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 18, 2018

HRW: WATU 15 WALIUAWA WAKATI WA KAMPENI ZA KURA YA MAONI BURUNDI; MATOKEO YA AWALI YATANGAZWA.


Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema kwa akali watu 15 waliuawa wakati wa kampeni za kura ya maoni ya kuifanyia marekebisho katiba huko nchini Burundi.
Ida Sawyer, Mkurugenzi wa Human Rights Watch katika eneo la Afrika ya Kati amesema leo Ijumaa katika taarifa kuwa, wamenakili kesi 15 za mauaji wakati wa kampeni hizo, mbali na kesi sita za ubakaji.
Kadhalika shirika hilo la kutetea haki za binadamu limenakili kesi nane za watu kutekwa nyara wakati wa kampeni hizo. 
Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, baadhi ya maafisa wa serikali walisikika hadharani wakitoa mwito wa 'kuhasiwa wafuasi wa upinzani' waliokuwa wakipinga kufanyika kura hiyo ya maoni.

Rais Nkurunziza akipiga kura jana Alkhamisi

Kura hiyo ya maoni ilifanyika jana Alkhamisi chini ya mazingira ya taharuki na wasi wasi, haswa baada ya kuenea habari za kushambuliwa wanaharakati wa upinzani waliokuwa wakipinga kufanyika zoezi hilo.
Matokeo ya kura hiyo ya maoni yanasubiriwa leo Ijumaa, na iwapo kwa uchache asilimia 50 ya wapiga kura wataunga mkono mabadiliko hayo ya katiba, watakuwa wamemsafishia njia Rais Pierre Nkurunziza ambaye amekuwako madarakani tokea mwaka 2005, kusalia uongozini hadi mwaka 2034.
Mwandishi wetu Hamida Issa ametuandalia ripoti maalumu kuhusu matokeo ya awali ya kura hiyo ya maoni.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.