Saturday, December 11, 2010
HABARI
DAKIKA HII HII ....KIPA NAMBA MOJA JUMA KASEJA KAIBUKA SHUJAA BAADA YA KUOKOA MKWAJU MMOJA WA PENATI KATI YA MITANO, NI PENATI ILIYOPIGWA NAYE TONNY MAWEGE NA KUIWEZESHA KILIMANJARO STARS KUSHINDA KWA BAO 5-4 NI KATIKA MICHUANO YA TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP HATUA YA NUSU FAINALI.
KWA UPANDE WA KILIMANJARO STARS MAGOLI YA PENATI YALITUMBUKIZWA KAMA IFUATAVYO:-
1. NSAJIGWA
2. STEPHANO MWASIKA
3. SHAHBAN NDITI
4. MACHAKU
5. ERASTO NYONI
STARS KUKIPUTA FAINALI DHIDI YA IVORY COAST SIKU YA JUMAPILI.
Friday, December 10, 2010
BANGO
SHUGHULI NI KESHO (JUMAMOSI) NA KESHO KUTWA (JUMAPILI) PALE B.O.T CAPRIPOINT MWANZA, WASHIRIKI WAKIWA NI WANAFUNZI WAWAKILISHI WA VYUO MBALIMBALI.
WADAU JIPANGENI VYEMA.
LEO ni siku ya Uhuru wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika. Watanzania wote wanaadhimisha uhuru wa Tanganyika kutimiza miaka 49 tangu wakoloni wa Uingereza walipokabidhi hatamu za uongozi wa taifa hilo, ambalo sasa linajulikana kama Tanzania Bara, kwa wananchi wenyewe, Desemba 9, 1961. Maadhimisho ya siku hiyo yanawapa nafasi na changamoto kubwa Watanzania za kutafakari walikotoka, walipo na wanakokwenda li kuona wapi walikosea, kuteleza au kufanya vizuri, na kupanga mikakati ya kuondoa kasoro na kuweka mipango madhubuti zaidi ya kuendelea kulijenga taifa lao.
TATIZO LA MAJI SAFI NA SALAMA.
Yapo maendeleo makubwa yaliyopatikana kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na serikali na wananchi tangu uhuru. Lakini pamoja na maendeleo hayo, zipo changamoto kubwa zilizokwaza harakati hizo za maendeleo, ambazo wakati wa kusherehekea miaka 49 ya uhuru, tunapaswa kuzitafakari na kuzipatia ufumbuzi utakaolipeleka mbele zaidi taifa letu.
MIAKA 49 YA UHURU WA TZ OYEEE..
NINA AMINI KUWA TUTAFIKA.
VERSE 1...Siwezi Kuishi Bila Upendo wako Ulivyoniteka
Naomba Nihifadhi Kwa Mikono Yako Nisije anguka
Nimezunguka Kutwa Nzima Kama wewe sijamuona
Napigwa Vita Chungu Nzima Lakini Bado Napigana
CHORUS...Wapo walotaka Nikuache Nakusema Sitofika Popote
Ndipo Wakanifanya Niongeze Juhudi Nyingi mpaka siku Niwe wako
Sijali Umenitesa Mara ngapi Ama Nimelia Mara Ngapi
Nia Yangu Ni Moja Siku Moja Tuwe wote Pamoja x2
VERSE 2...Sijasahau Usiku Wa Manane ule Ulivyo Nikana
Mbele Ya Nduguzo Na Bwanaako Yule Ukanitukana
Kwa Mapenzi Nilisimama Kama Chizi Nilionekana
Leo Wakusema Hakuna Najua Waamini Nakupenda
CHORUS... Wapo walotaka Nikuache Nakusema Sitofika Popote
Ndipo Wakanifanya Niongeze Juhudi Nyingi mpaka siku Niwe wako
Sijali Umenitesa Mara ngapi Ama Nimelia Mara Ngapi
Nia Yangu Ni Moja Siku Moja Tuwe wote Pamoja x2
BRIDGE... Penzi Letu Liende mbele lisifike Mwisho oooooo
Tuwe Wote Milele Tushinde Vikwazo oooooo
Wapooooo Ooo oooo oo Wapooooooooooo
Wapoooooooo Wapooooooooooooooo
HOOK ... Sijali Umenitesa Mara Ngapi Ama Nimelia Mara Ngapi
Nia Yangu Ni Moja Siku Moja Tuwe Pamoja Haaaaaa x2
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mh. Serenge Mrenge akizindua vitabu vya mbinu sahihi za kilimo vya shirika lisilo la kiserikali la SUSTAINET hii ni mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa mwaka wa shirika hilo, uliofanyika Lakairo hotel Kirumba jijini Mwanza, nchini Tanzania. Katikati ni katibu mkuu mtendaji wa mradi huo Tom Apina akifuatilia tukio hilo kwa umakini.
VITABU VYA ELIMU JUU YA MBINU SAHIHI ZA KILIMO.
Mradi wa SUSTAINET umefanikiwa kujumuishwa kama sehemu ya mtandao wa UN kupitia shirika lake la chakula na kilimo - FAO umejikita zaidi katika kutoa elimu kwa wakulima wadogo na kushirikiana nao katika kuwaelekeza mbinu sahihi za kuanzisha miradi waweze kujikwamua kutoka katika lindi la umaskini kupitia kilimo chenye manufaa (kilimo cha biashara).
Katika mkutano huo wa mwaka Mada mbalimbali ziliwasilishwa na kujadiliwa na hatimaye maazimio ya mkutano yakawa ni pamoja na shirika hilo kujipanua zaidi kuhakikisha kuwa kila mkulima ananufaika na elimu wanayoitoa.
Mh. Serenge akikabidhiwa seti nzima ya vitabu vya KILIMO toka kwa Edith Omamo ambaye ni mratibu wa Mradi huo wa shirika lisilo la kiserikali la SUSTAINET unaodhaminiwa na watu wa Ujerumani wenye mtandao wa kiushirika kwa vikundi vya watu binafsi kwa nchi za afrika mashariki za Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi.
Mkuu wa wilaya ya Ilemela akiangusha sahihi kwenye moja ya vitabu vya kilimo vilivyozinduliwa.
BOARD MEMBER NA MKUU WA WILAYA.
Traditional practices can be improved and combined with alternative ecological forms of land use, resulting in comprehensive systems for sustainable agriculture. A wealth of experience drawn from every continent confirms that these approaches have great potential, which is still significantly under-exploited. But before these successful approaches can be disseminated on a massive scale, numerous obstacles have to be overcome. Generally the potential users of sustainable agriculture do not have enough access to the information they need. An equally common problem is that political, social and economic structures in a country can inhibit the implementation of such approaches. Under the auspices of its National Strategy for Sustainable Development, the German federal government supports the SUSTAINET project, which aims to overcome these obstacles.
IMEDIZAINIWA TU WADAUUUU..... WACHA NIITOEEE
AyyAaaaaaa!!! Duh! Kama boga vile limepitiwa na tairi la gari. Ngoma kama hii unaambiwa tafuta pua ya marehemu.
Mmmh ajali zingine..TEHE! TEHEee!!!
KhAAh! WE NAWE! sa ndo nini sasa!!!
Monday, December 06, 2010
BANGO
Monday, December 06, 2010
HABARI
Wananchi wanaozunguka eneo la Bonde la Ziwa Victoria wanaendelea kukabiliana na hali ngumu ya maisha na kuishi katika hali ya duni ya maisha, ingawa eneo hilo limejaliwa utajiri wa uoto wa asili na raslimali za kutosha.
MEZA KUU YA KUSANYIKO HILO.
Hayo yamebainishwa leo na Waziri wa Maji Prof. Mark Mwandosya wakati alipokuwa akizungumza kwenye ufunguzi wa kusanyiko la kwanza la uwekezaji katika Bonde la Ziwa Victoria lililofanyika jijini Mwanza na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wawekezaji kutoka katika nchi za Afrika Mashariki.
WAZIRI MWANDOSYA NA BALOZI MWAPACHU WAKIWASILI ENEO LATUKIO.
MH. MWANDOSYA.
Mwandosya amezitaja changamoto zinazochangia kuwepo kwa hali hiyo ni pamoja na umaskini, migogoro ya kiuchumi, ukosefu wa raslimali watu matumizi mabaya ya vyanzo vya maji , uchafuzi mazingira na ukuaji wa kasi ya ongezeko la watu.
HAFSA MOSSI.
Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Hafsa Mossi amesema kuwa kutokana na raslimali zilizo katika Bonde la Ziwa Victoria, ana imani kuwa wawekezaji wenye sifa watajitokeza kuja kuwekeza kwa lengo la kuwaondolea umaskini wakai wanaozunguka bonde hilo.
Amefafanua kuwa mbali na wananchi kunufaika na ajira, kutokana na uwekezaji huo watapata fursa ya kujipatia maendeleo kwa kujifunza mbinu bora za kisasa za uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, vyanzo vya nishati ya umeme na usafirishaji na hivyo kuondokana na umaskini wa kipato.
Kusanyiko hilo la kwanza la uwekezaji katika bonde la Ziwa Victoria linalofanyika kwa siku tatu Malaika Hotel Mwanza ambapo jumatano ni hitimisho, Limefanyika likiwa na lengo la kubainisha faida za kiuchumi na kijamii zilizopo bonde la ziwa victoria na kuweza kuvutia wawekezaji kwenda kuwekeza.
WADAU wakijadili haya na yale mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo.
The Deputy Prime Minister for Uganda (who seated) posses in a group photo with other East African leaders at Malaika hotel grounds yesterday. From right who seated are the RC for Mara Region Enos Mfuru, The Secretary General for East African Community Ambassador Juma Mwapachu, The Minister for Water Prof Mark Mwandosya, The Deputy Prime Minister for Uganda Hon. Eriya Kategaya, The RC for Mwanza Abbas Kandoro and The Executive Secretary for THE Lake Victoria Basin Commission Dr. Tom Okurut.