ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 10, 2010

FBME YATOA MSAADA KWA HOSPITALI YA SEKOU TOURE.

Katika kukabiliana na uhaba wa vitendea kazi na nyenzo kwa hospitali zetu nchini benki ya FBME kupitia tawi lake la Mwanza leo imekabidhi msaada wa mashuka na foronya 400 kwa hospitali ya mkoa wa Mwanza (SEKOU TOURE).
Meneja wa benki ya FBME tawi la Mwanza Joseph Gwalugano akikabidhi msaada huo kwa mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza Dr. Meshark Mmasi.

“Msaada huu ni sehemu ya mikakati ya FBME tuliyojipangia, kwa sababu tupo karibu na jamii na tunapaswa kujitolea kwa ari na mali katika kuhakikisha kuwa jamii inanufaika na misaada " Kauli ya Joseph Gwalugano ambaye katika picha hii anaonekana kulia kabisa akikabidhi msaada huo kwa mganga mkuu wa hospitali ya Sekou toure Dr. Onesmo Kimbera.

Wadau wa FBME wakishiriki zoezi la kutandika shuka hizo kwenye vitanda wodi ya akinamama wajawazito na watoto hospitalini hapo.

Ni maelezo toka kwa muuguzi juu ya jinsi shuka hizo zitakavyotumika kwenye wodi ya watoto waliokumbwa na majanga ya moto.

HAPA ni ndani ya jengo jingine lililo jipya kabisa la wodi ya watoto hospitalini hapo, Jengo limekamilika likisubiri vifaa na ufunguzi kisha lianze kazi.

Shukrani kwa benki ya FBME mwanza.

Tupe maoni yako

2 comments:

  1. Hii ni kazi nzuri sana ya tawi la FBME - Mwanza, Tunawashukuru sana kuleta misaada kwenye jamii, inaonyesha jinsi gani mnavyo thamini jamii inayowazunguka. Joseph G, Annah L, Winnie M, Allawi M na wengine mchango wenu tuna uona sana tu!

    ReplyDelete
  2. Thanks Kaka G. Sengo. Uko faster!!!

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.