ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 4, 2022

CHUO CHA RUAHA CDTI CHASHIRIKI KWA VITENDO UJENZI WA ZAHANATI KIJIJI IKUVILO



 Mkuu wa chuo cha Ruaha (CDTI) Godfrey Mafungu akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake akifafanua kwa namna gani wanashirikiana na serikali ya kijiji cha Ikuvilo katika ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho ili waweze kupata huduma ya afya.  Mkuu wa chuo cha Ruaha (CDTI) Godfrey Mafungu akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake akifafanua kwa namna gani wanashirikiana na serikali ya kijiji cha Ikuvilo katika ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho ili waweze kupata huduma ya afya. Baadhi ya wananchi,wanafunzi wa chuo cha maendeleo ya jamii Ruaha na viongozi wa chuo hicho wakishiriki kwa vitendo uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa zahanatai ya kijiji cha Ikuvilo

 

Na Fredy Mgunda,Iringa.

CHUO cha maendeleo ya jamii Ruaha (CDTI) kwa kushirikiana na Serikali ya Kijiji cha Ikuvilo kata ya Luwota wameamua kujenga zahanati kwa lengo la kuwasogezea wananchi huduma ya afya kupatikana jirani.

 

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwanza mkuu wa chuo cha Ruaha (CDTI) Godfrey Mafungu alisema kuwa wameamua kuunga mkono juhudi za serikali ya kijiji cha Ikuvilo na kuamua kushirikiana nao kuhakikisha wanapata huduma za afya.

 

Mafungu alisema kuwa wameshiriki katika hatua mbalimbali za awali za ujenzi wa zahanati hiyo ambayo itakuwa mkombozi kwa wananchi wa kijiji hicho.

 

Alisema kuwa malengo ya sasa ni kuhakikisha wanafanikisha ujenzi wa zahanati hiyo baada ya miezi sita huku akitoa rai kwa wananchi kuchangia shughuli za maendeleo ya kijiji.

 

Mafungu alisema kuwa maendeleo ya kijiji cha Ikuvilo yataletwa na wananchi wa kijiji hicho hivyo wananchi wanatakiwa kujitoa kuhakikisha wanachangia maendeleo ya kijiji.

 

Alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Ikuvilo kutachangia kuboresha huduma za afya na kupunguza vifo vya wananchi wa kijiji hicho kwa kuwa huduma ya afya walikuwa wanaipata umbali mkubwa.

 

Mafungu alimazia kwa kusema kuwa huduma ya afya ni muhimu kwa maendeleo ya jamii yote hiyo kupatikana kwa huduma hiyo wananchi watapiga hatua moja ya kimaendeleo.

 

Kwa upande wake mkufunzi wa chuo cha maendeleo ya jamii Ruaha Galiatano Alisema kuwa wananchi wa Kijiji cha Ikuvilo wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa huduma bora za afya hivyo chuo kikaamua kuanziasha ujenzi wa zahanati ya Kijiji hicho.

 

Alisema kuwa wanafanya kazi za awali kama somo kwa Wanafunzi wa chuo hicho ambacho Wanafunzi wake wanasoma masomo ambayo yanahusika katika kuhudumia jamii kwenye maendeleo.

 

Galiatano Alisema kuwa uongozi wa chuo cha maendeleo ya jamii Ruaha kipo tayari kufanya kazi na Serikali ya Kijiji yoyote ile bora mradi jambo liwe la jamii.

 

Alisema kuwa Wanafunzi na wadau wa chuo cha maendeleo ya jamii Ruaha waliojitokeza kwenye shughuli za kimaendeleo ya ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Ikuvilo walikuwa 277 na walifanya kazi ya uchimbaji wa msingi,utoaji wa mawe na ukusanyaji wa kokoto kutoka eneo moja hadi lingine ikiwa ishara ya ushirikiano na serikali ya Kijiji.

 

Rais wa Serikali Wanafunzi chuo cha maendeleo ya jamii Ruaha Jacob Arusha alisema kuwa lengo la kushirikiana na Serikali ya Kijiji cha Ikuvilo ilikuwa ni kusaidia kuboresha huduma ya afya kwa wananchi wa Kijiji hicho.

 

Alisema kuwa Wanafunzi wa chuo cha maendeleo ya jamii Ruaha wanafuraha kutoa mchango wao katika maendeleo ya kuboresha huduma ya afya kwa wananchi wa Kijiji cha Ikuvilo.

 

Arusha alisema kuwa wameamua kufanya hivyo kwa kuwa wakiwa chuoni wanasomea masomo ambayo watajihusisha na maendeleo ya wananchi.

 

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikuvilo Meshack Mlawa alisema kuwa wananchi wanakumbana na changamoto ya ukosefu wa huduma ya afya ambayo imekuwa ileta madhala makubwa kwa wananchi.

 

Alisema kuwa wananchi wanasafiri umbali wa zaidi ya kilometa 18 jambo ambalo limekuwa linasababisha vifo kwa wananchi.

 

Mlawa alisema kuwa wanaushukuru uongozi wa chuo cha maendeleo ya jamii Ruaha kwa kukubali kushirikiana katika ujenzi wa zahanati hiyo ambayo itasaidia kuboresha huduma za afya.

 

Alikiri kuwepo kwa vifo vya mama na mtoto kipindi unapofika muda wa kwenda kujifungua kutokana na kuifuata huduma ya afya mbali na changamoto ya barabara.

 

Mlawa alisema kuwa Serikali ya Kijiji wamefanikiwa kufyatua jumla ya tofali 10040 ambazo zitatumika katika ujenzi wa zahanati hiyo na kutimiza ndoto ya Kijiji kuwa na huduma ya afya Kijiji hapo.

 

Alisema kuwa Kijiji hicho kinajumla ya wananchi 2699 ambao wote wanahitaji huduma ya afya kwa ajili ya maendeleo na Kijiji hicho kilisajiliwa mwaka 1978 na hakijawahi kupata huduma ya afya toka kisajiliwe.

 

Jane njavike mwananchi wa Kijiji cha Ikuvilo alisema kuwa wamekuwa wanapata changamoto kubwa kiasi ambacho inawabidi kusafi umbali wa zaidi ya kilomete 18.

 

Alisema kuwa wanawake wengi wamekuwa wanajifungulia njiani kutokana na kukosekana kwa huduma ya afya katika Kijiji hicho.

 

Njavike alisema kuwa wananchi wengi wamekuwa wanapoteza maisha njiani kutokana na kuifuata huduma ya afya mbali na kukumbana na changamoto ya usafi kutoka kijijini hapo hadi huduma ya afya ilipo.

 

Alisema kuwa kuanza kujengwa kwa zahanati ya Kijiji kwa ushirikiano Serikali ya Kijiji na chuo cha maendeleo ya jamii Ruaha kutasaidia kuokoa maisha ya wananchi wengi.

 

Njavike alisema kuwa anaupongeza uongozi wa chuo cha maendeleo ya jamii Ruaha kwa uamuzi wake wa kuanzisha ujenzi wa zahanati hiyo ambayo itakuwa mkombozi kwa wananchi wote

DC TANGA AIPONGEZA TANGA UWASA

 

Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Tanga(Tanga UWASA)Devotha Mayala akitoa maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa alipotembelea banda lao kwenye maonyesho ya Biashara.


Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Tanga(Tanga UWASA)Devotha Mayala akitoa maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa alipotembelea banda lao kwenye maonyesho ya Biashara


NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa ameipongeza Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) kutokana na jitihada kubwa wanazofanya katika kutatua kero za maji kwa wananchi kwa kuendelea kutoa huduma nzuri na bora

Alitoa pongezi hizo wakati alipotembelea banda la mamlaka hiyo kwenye maonyesha ya 9 ya biashara na utalii yanayoendelea katika viwanja vya Mwahako Jijini Tanga

Pongezi za Mkuu huyo wa wilaya ya Tanga zimatokana na kazi kubwa inayofanywa na mamlaka hiyo kuhakikisha huduma ya maji safi inapatikana sambamba na kutoa taarifa kwa wananchi.

Alisema Tanga Uwasa wamekuwa wakifanya vizuri katika utoaji wa huduma mbalimbali wanazotoa ikiwemo kuzipatia ufumbuzi kwa haraka changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza.

"Tanga Uwasa hatuna shida sana na nyie kazi yenu nzuri lakini zingatieni kupitia kwenye mitaro ya maji machafu mara kwa mara… wekeni ratiba kama kuna changamoto ziweze kutatulika kwa wakati"Alisema Mgandilwa

Awali akizungumza Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Devotha Mayala alisema kuwa katika maonyesho hayo wamekuwa wakiwapa elimu wananchi juu ya matumizi sahihi ya maji wawapo majumbani.

WAPI PAKUPATA UNAFUU KWA WATOTO WAFANYAKAZI MAJUMBANI?


WAPI PA KUPATA UNAFUU ? Kesi au masuala yote yanayohusu watoto yanahusu pia jamii yote, jeshi la polisi, madaktari, serikali za mitaa, na maafi sa wa ustawi wa jamii katika kila serikali za mitaa.

 Mahakama ya watoto itahusika katika mambo yote yanayohusu watoto. Ikiwa mtoto amefanyiwa vitendo vilivyotajwa hapo juu, wazazi/mwanajamii anaweza kutoa taarifa katika serikali ya mtaa, ambayo kwa kushirikiana na afi sa ustawi wa jamii, wana wajibu wa kufuatilia ulinzi na ustawi wa mtoto huyo aliyedhurika. 

Ikihitajika kwenda mahakamani, afi sa ustawi ana wajibu wa kupeleka maombi mahakamani juu ya nafuu ya au ulinzi wa mtoto huyo. 

 Angalizo: Serikali ya mtaa ina wajibu kutokana na sheria ya mtoto, kuwatafutia na kuwapa hifadhi watoto ambao wametelekezwa au kukosa makazi.

Pia ina wajibu, kwa kushirikiana na afi sa ustawi wa jamii, kuwatafuta wazazi waliotelekeza watoto na kuwarudisha, au kutoa amri ya matunzo. Shirika la Kutetea Haki za Watoto wafanyakazi Nyumbani la Nuru Organisation.

Thursday, June 2, 2022

WATAALAMU FEDHA WANOLEWA MATUMIZI YA TEHAMA.


Bertha Ismail mwananchi

Arusha. Wataalamu wa maswala ya fedha nchini wamekutana jijini Arusha kwa ajili ya kupatiwa elimu ya matumizi ya Tehama katika utoaji wa huduma za kifedha ili kuleta ufanisi zaidi kazini.

Mkutano huo wa siku tatu ulioanza June mosi, unahusisha Wataalamu zaidi ya 400 wa maswala ya kifedha kutoka taasisi mbali mbali za kifedha zikiwemo mabenki, wahasibu, wakaguzi, maofisa wa bima na mapato "TRA".

Akizungumzia malengo ya mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania, Pius Maneno alisema kuwa wanalenga kuwaelimisha zaidi wataalam hao juu ya matumizi ya Tehama katika utoaji wa huduma ambayo ni rahisi na yenye ufanisi zaidi ili kuendana na Kasi ya mapinduzi ya nne ya viwanda.

"Hapa tuna mada 11 tunazo elekezana zaidi ni matumizi ya mtandao katika kutoa huduma zetu za kifedha ikiwemo utoaji wa taarifa sahihi za kifedha na namna ya kuzuia viatarishi vya kuzuia malengo yetu" alisema Maneno.

Maneno alisema kuwa wanatarajia pia kuwanoa washiriki wao katika kutambua mbinu za masoko ya kazi zao, maswala ya Kodi, utawala Bora, jinsi ya kuandaa na kuandika taarifa za kuripoti maswala ya fedha lakini pia kukumbushana majukumu ya wahasibu na Benki Kat utoaji wa taarifa za fedha haramu zinapojitokeza.

"Lengo la haya yote ni kufanya wataalam wetu wajue majukumu yao, lakini kutumia Tehama katika kuhudumia jamii ambayo itarahisisha kazi, itawafikia wananchi wengi kwa Bei nafuu na itapunguza umaskini kwa kukuza uchumi"

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki kuu ya Tanzania "BOT" tawi la Arusha, Çharles Yamo alisema kuwa mafunzo haya wamekuwa wakiyatoa ili kuwafanya wataalam hao waendane na kasi ya dunia kwenye mapinduzi yaliyopo katika utoaji wa huduma za kifedha.

"Katika mkutano huu kubwa ni mapinduzi ya nne ya viwanda katika matumizi ya  Tehama, katika ukuaji wa  uchumi wa uchumi wa jamii na nchi na nchi kwa ujumla wake"

Alisema kuwa wanasisitiza pia maadili katika utoaji wa huduma na wahusika wa kibenki wawe wanatoa taarifa sahihi za mikopo yao na riba lakini pia wakopaji katika taasisi zao ili kupunguza tatizo la mikopo chechefu.

"Tunawasisitiza pia taaisis wa kibenki wawe wanatoa taarifa sahihi za wakopaji wao ili zisaidia taasisi zingine kuzipata na kutumia dhidi ya wateja wanaokwenda kukopa pengine na kujiridhisha endapo mkopo huo hautawaathiri, hiii itasaidia kupunguza mikopo chechefu kwa wateja lakini pia heshima kwa Benki"

Yamo alitumia nafasi hiyo kuwaonya taasisi zinazojihusisha na utoaji wa mikopo mitaani bila leseni ya kufanya biashara hiyo wala kibali cha BOT  kuwa watawachukulia sheria.

"Pia niwaombe mabenki watoa mikopo kwa riba elekezi ya Serikali isiyozidi asilimia 15 kwa mikopo mikubwa ya mda mrefu Hadi asilimia saba ili kuleta maana ya kuwasaidia wananchi wakopaji na sio kuwakandamiza"

BRELA YAANIKA MAFANIKIO YA ONGEZEKO LA WATU KUSAJILI MAKAMPUNI KIPINDI RAIS SAMIA

 

WAKALA wa Usaji wa Biashara na Leseni Tanzania (BRELA) umesema kwamba wamekuwa na mafanikio makubwa ya ongezeko la mwitikio wa watu kusajili Makampuni,Majina ya Biashara sambamba na kupata leseni za biashara zao  tokea Rais Samia Suluhu alipoingia madarakani.


Hayo yalisemwa na Msajili Msaidizi kutoka Brela Seleman Seleman wakati wa maonyesho ya 9 ya biashara na utalii yanayofanyika jijini Tanga ambapo wamekuwa wakitoa elimu juu ya umuhimu wa wananchi kusajili biashara zao.


Alisema kwamba kwa kipindi kimoja tokea Rais Samia aingie madarakani wameweza kusajili makampuni 11422 ambapo kwa najina ya biashara wameweza kusajili majina ya biashara 22251 lakini pia alama za biashara wamesajili 3056 ambapo katika leseni za kundi A wametoa leseni 12704.


“Kwa kipindi hiki kimoja cha mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan kimeonyesha mafanikio makubwa ukilinganisha na vipindi vingine jambo ambalo limeonyesha ari kwa watu kusajili makampuni, majina ya biashara lakini pia kupata leseni za biashara zao, “alisisitiza Seleman.


Aidha amesema kuwa hali hiyo pia imewaongezea ari wao kama watendaji wa Brela ambapo kupitia matamasha mbalimbali wanashiriki ili kuifikia jamii ambapo walengwa wakiwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo.


“Wito wangu kwa wafanyabishara kabla ya kuanza kufanta jambo wawe wanapitia na kutafuta taarifa kwanza kwa wahusika ambao ni Brela kupitia mitandao ya kijamii au website zetu zinazoeleza sisi tunafanya nini na ikiwa kama kuna sehemu mtu hajaelewa kuna namba ya huduma kwa wateja hivyo watu wanaweza kupiga na kupata taarifa sahihi hii itawapunguzia wateja kupewa taarifa na watu ambao si sahihi, “alibainisha Seleman.
 
Wakizungumza katika banda hilo baadhi ya wakazi wa jiji la Tanga waliotembelea akiwemo Richard Otto alisema alilazimika kufika hapo ili aweza kujua namna ya kusajili jina la biashara na kampuni kwa kuwa alikuwa hajui umuhimu wa kusajili biashara yake.


Aidha alisema wanachonufaika nacho baada ya kufika hapa Brela ni kurasimisha biashara hasa kwa vijana ambao wamekuwa wakifanya biashara bila kusajili na hivyo kushindwa kutambulika.
“Tunashukuru tumepata suluhisho  njia za kufanya mwanzoni huu mfumo ulikuwa unasumbua pale ulipoanzishwa mfumo wa usajili online lakini sasa ivi nimeambiwa taratibu zimekaa vizuri, “Alisema, Otto.
 

Hata hivyo kwa upande wake mkazi wa Korogwe ambaye alitembelea banda hilo Veronica Temu alieleza kufurahishwa na uwepo wa wakala huo kwenye maonyesho hayo kwamba utawasaidia kufanya usajili wa biashara zao ikiwemo kutumia simu yake au kompyuta akiwa nyumbani kwake na hivyo imewarahisishia kwa kiwango kikubwa.

TMDA: MATUMIZI YA TUMBAKU YANAWEZA KUSABABISHA MATATIZO KWENYE VIA VYA UZAZI

 

Afisa Mwandamizi wa Elimu kwa Umma na Huduma kwa wateja Roberta Feruzi akitoa elimu kwa wananchi waliojitokeza kwenye banda la TMDA kwenye eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea Maonyesho ya Biashara na Utalii Jijini Tanga
Afisa Mwandamizi wa Elimu kwa Umma na Huduma kwa wateja Roberta Feruzi akitoa elimu kwa wananchi waliojitokeza kwenye banda la TMDA kwenye eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea Maonyesho ya Biashara na Utalii Jijini Tanga
Afisa Mwandamizi wa Elimu kwa Umma na Huduma kwa wateja Roberta Feruzi akitoa elimu kwa wananchi waliojitokeza kwenye banda la TMDA kwenye eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea Maonyesho ya Biashara na Utalii Jijini Tanga
Afisa Mwandamizi wa Elimu kwa Umma na Huduma kwa wateja Roberta Feruzi akitoa elimu kwa wananchi waliojitokeza kwenye banda la TMDA kwenye eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea Maonyesho ya Biashara na Utalii Jijini Tanga
Afisa Mwandamizi wa Elimu kwa Umma na Huduma kwa wateja Roberta Feruzi akitoa elimu kwa wananchi waliojitokeza kwenye banda la TMDA kwenye eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea Maonyesho ya Biashara na Utalii
Afisa Mwandamizi wa Elimu kwa Umma na Huduma kwa wateja Roberta Feruzi akitoa elimu kwa wananchi waliojitokeza kwenye banda la TMDA kwenye eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea Maonyesho ya Biashara na Utalii Jijini Tanga
Afisa Mwandamizi wa Elimu kwa Umma na Huduma kwa wateja Roberta Feruzi akitoa elimu kwa wananchi waliojitokeza kwenye banda la TMDA kwenye eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea Maonyesho ya Biashara na Utalii Jijini Tanga
Afisa Mwandamizi wa Elimu kwa Umma na Huduma kwa wateja Roberta Feruzi akitoa elimu kwa wananchi waliojitokeza kwenye banda la TMDA kwenye eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea Maonyesho ya Biashara na Utalii Jijini Tanga

NA OSCAR ASSENGA,TANGA

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba nchini (TMDA) imesema kwamba matumizi ya tumbaku yanaweza kusababisha matatizo kwenye via vya uzazi,athari ya kansa ya utumbo mpana na kupoteza nguvu kazi ya Taifa na hivyo kusababisha Serikali kutumia fedha nyingi katika kutibu magonjwa hayo

Hivyo wito ulitolewa kwa wananchi kuacha kutumia tumbaku,uvutaji wa sigara
kutokana na kwamba ni hatari kwa afya zao na athari zake ni kubwa kwa jamii hivyo waache matumizi yake

Hayo yalisemwa na Afisa Mwandamizi wa Elimu kwa Umma na Huduma kwa wateja Roberta Feruzi wakati akizungumza n waandishi wa habari katika eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya 9 ya viwanda,biashara na talii Jijini Tanga.

Alisema wameshiriki maonyesho hayo ili kuweza kutoa elimu kwa wananchi wao kama mamlaka ya dawa wamepewa dhamana ya kusimamia na kudhibiti bidhaa za tumbaku huku wakitoa wito kwa wananchi kuacha kutumia

Aidha alisema wao wanalinda kwa kuelekeza kwamba bidhaa za tumbuka watu waache kutumia bidhaa hizo kwani zimekuwa na athari kubwa sana kwa wananchi  kidogo kidogo ikiwemo kansa lakini kubwa zaidi ni nguvu kazi ya uzalishaji mali kwa maendeleo ya Taifa inapungua .

 “Lakini kubwa ni kundi cha chini ya miaka 18 limekuwa likijiingiza kwenye uvutaji wanatoa wito waache mara moja kwani mandhara yake ni makubwa kwa jamii “Alisema

Hata hivyo alisema wameshiriki kwenye maonyesho hayo kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi waifahamu taasisi lakini kazi yao kulinda ubora wa jamii wanailinda kwa kusimamia ubora,usalama na ufanisi wa bidha za dawa,vifaa tiba na vitenganishi.

“Lakini pia kusimamia uzibiti wa bidhaa zinazotokana na tumbaku,TMDA kuhakikisha jamii na wanatoa elimu juu ya matumizi sahihi ya dawa wengi wamekuwa wakikiuka matumizi ya dawa ipasavyo kutokana na kutokupata elimu na kupelekea matatizo kwenye mwili na usugu vimilea”Alisema

Hata hivyo alisema pia wanatoa elimu juu ya utoaji wa tahadhari ya mauzi yanatoweza kutokana na maudhi ya bidhaa za dawa,vifaa tiba na vitengenishi waweze kutoa taarifa.

TASAC YATOA NENO KWA WAKUU WA WILAYA MKOANI TANGA

 

Afisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoa wa Tanga Captain Christopher Shalua wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maonyesho ya 9 ya biashara na Utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Amina Miruko akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maonyesho hayo
Baraka Mashauri ni Afisa kutoka Shirika la Wakati wa Meli Tanzania (TASAC) akizungumza wakati wa maonyesho hayo

NA OSCAR ASSENGA, TANGA

SHIRIKA la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa wito kwa Wakuu wa wilaya za Mkoa wa Tanga na viongozi wa Vijiji kutokuvipokea vyombo vya majini ambavyo havijakidhi vigezo vya kisheria katika maeneo yao kupakia abiria ili nao waweze kuwa sehemu ya mkakati wa kuhakikisha wanaokoa maisha ya abiria.

Lakini pia kuwa sehemu ya kuhakikisha nao washiriki kudhibiti safari zinazofanywa na vyombo vinavyotumika kubeba mizigo kupakia abiria na hivyo kuvunja sheria jambo ambalo linahatarisha maisha.

Wito huo ulitolewa leo na Afisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoa wa Tanga Captain Christopher Shalua wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maonyesho ya 9 ya biashara na Utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.

Alisema iwapo viongozi hao watashiriki kwenye suala hilo itakuwa ni mwarobaini wa kuweza kudhibiti vyombo ambavyo havijaruhusiwa kisheria kufanya shughuli za kubeba abiria na hivyo kuondokana na matukio mbalimbali yanayoweza kujitokeza ikiwemo ajali za majini.

“Lakini pia niwaambie sisi kama Shirika Kabla hatujachukua sheria inabidi tuwaelemishe watu hivyo tumejitahidi sana kutoa elimu kwa maeneo sugu ya watu wanaosafiri kupitia majahazi katika maeneo ya Mkwaja,Kipumbwi na Pangani kwa wamiliki na manahoida wa vyombo”Alisema

Alisema kubwa zaidi ni wao kutambua kwamba wana wajibu wa kuhakiksiha hawavunji sheria na kuhatarisha usalama wa watu wanaotumia vyombo hivyo kwa sababu havijakidhi vigezo ambavyo vinatakiwa kubeba abiria.

“Tumekuwa tukiwasiliana na Taasisi za Serikali ikiwemo viongozi wa Vijiji,Wakuu wa wilaya,Wakuu wa Polisi wilaya na Mkuu wa Mkoa kumpeleka barua kuwataarifu shughuli zinazofanyika maeneo hayo sio halali na zinahatarisha maisha ya abiria na hatua zinazofuata ni kuchukua hatua za kisheria”Alisema

Captain Shalua alisema kwa sababu wanapopewa leseni zinakuwa na masharti kwamba chombo chako ni cha mizigo na hakiruhusiwi kubeba abiria hivyo wanapovunja sheria wanachukuliwa hatua kali ikiwemo kutozwa faini na kuwapeleka mahakamani au vyote viwili kwa pamoja .

“Kama unavyofahamu eneo la Mwambao wa Bandari ya Tanga ni kubwa sana na tunategemea viongozi wa serikali za vijiji tusaidiana nasi kuweza kudhibiti suala hilo kusimamia usalama “Alisema

Hata hivyo alisema wamiliki wa vyombo vya majini na waendesha vyombo hivyo wanapaswa kuzingatia masharti ya leseni yao kwa wasafiri kwa kuwaeleza kwamba hawatakiwi kupanda kwenye majahazi ya mizigo kwa sababu hakuna mtu anayewalazimisha .

“Hivyo wakipata uelewa kuhusu madhara yake watafanya maamuzi sahihi ya kuttokupanda vyombo hivyo na hivyo kusaidia kwa asilimia kubwa kuondokana na changamoto ambazo wanazoweza kukumbana nazo wawapo safarini”Alisema

Captain Shalua pia alisisitiza umuhimu wa vyombo hivyo kwa na vifaa vya kujiokolea ,kabla ya kupanda chombo unatakiwa kuangalia kipo kwenye ubora unaostahili na kinaweza kukusaidia kwenye kusafiri kwenye mazingira salama.

“ Lakini jambo jingine ni namna bora ya kuvaa vifaa vya kujiokolea na kwanini lazima kuwepo na vifaa hivyo kwenye chombo kwani ndio sehemu ya uokozi kuwasaidia pale ajali zinazotokea”Alisema Captain Shalua

Akizungumzia kuhusu vifaa vya kuzimia moto,Captain Shalua alisema vifaa vya kuzimia moto vyombo vya majini vingi vinatumia mafuta ya petrol kwa hiyo wanapenda watumiaji wafahamu namna bora na kifaa gani sahihi cha kuzimia moto unaowaka na kusababishwa na mafuta.

“Kwani watu wengi wanakimbia maji na kiuhalisia huwawezi kuzima moto kwa namna hiyo bali ni vifaa maalumu poda na opovu ili kuweza kizima moto”Alisema

Awali akizungumza Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Amina Miruko alisema wataendelea kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na suala hilo

Alisema pia watahakikisha Bandari Bubu zilizopo kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini zinarasimishwa pale inapobidi na urasimishaji unaofanyika unakuwa rasmi ikiwemo kufanya kaguzi za kushtukiza na kupanga.

Wednesday, June 1, 2022

NHIF TANGA WAELEZEA TIJA YA UANZISHWAJI WA VIFURUSHI VIPYA VYA UANACHAMA

 

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Tanga, Ali Mwakababu akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani kwenye banda lao
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF)Mkoani Tanga umeelezwa kwamba uanzishwaji wa vifurushi vipya vya uanachama vinavyoruhusu watu wengine tofauti na walioajiriwa katika sekta ya Umma kunufaika na bima ya afya umesaidia ongezeko la wanachama.


Hayo yalisemwa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Tanga, Ali Mwakababu wakati wa maonyesho ya 9 ya Biashara na Utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga ambapo alisema kuwa idadi ya wananchama wa mfuko huo mkoani Tanga ni zaidi ya 12,000.

Mwakababu alisema hapo awali watu wengi walifikiria mfuko huo ni kwa ajili ya watumishi wa umma pekee lakini umechukua hatua za kuanzisha vifurushi ambavyo vinawavutiwa watu katika Maonyesho ya Biashara ya siku 10 yaliyofunguliwa huko katika viwanja vya Mwahako siku tano zilizopita.

Meneja huyo alisema wananchi wengi ambao wametembelea banda lao wameonyesha nia ya kweli kutaka kujiunga na mfuko ili kuweza kunufika na huduma mbalimbali zinazotolewa ikiwemo kupata matibabu wanapokuwa wakiugua.

Hata hivyo alisema mpaka sasa tayari wametoa elimu kwa zaidi ya wananchi 150 ya ufahamu ya bima ya afya siku tatu za kwanza za maoyesho hayo na tayari baadhi yao wamejaza fomu za kujiunga na mfuko huo.

Alivitaja vifurushi hivyo kuwa ni pamoja na Najali, Wekeza na Timiza Vifurushi vya bima ya afya.

Akizungumza hasa kuhusu ushiriki wa Maonyesho ya Biashara ya NHIF,
Ofisa Bima ya Afya, Hussein Mponda alisema kuwa Banda la NHIF ni moja ya banda ambalo linavuta watu wengi wanaomiminika kwenye Maonyesho hayo ya Biashara.

Alisema wengi wanaofika kwenye banda lao wanaulizia jinsi wanaweza kujiunga na mpango wa bima ya afya, mbali na kupata uchunguzi wa matibabu bure.

Hata hivyo aliwahamasisha wananchi kuweza kufika kwenye banda lao ili kuweza kupata huduma mbalimbali ikiwemo za upimaji wa afya na kujiunga na bima ya afya waweze kunufaika na huduma za matibabu pindi wanapougua.

Tuesday, May 31, 2022

COASTAL UNION WATIMIZA AHADI YA RC ADAM MALIMA

 

Wachezaji wa Coastal Union wakiwania mpira dhidi ya wa Azam FC wakati wa mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA iliyopigwa mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa Sheirh Amri Abeid Jijini Arusha ambapo Coastal Union ilishinda


NA OSCAR ASSENGA,ARUSHA

MATOKEO ya UshindI walioupata kwa Penalti 6 kwa 5 hadi kuitoa Azam FC kwenye tumaini la kucheza Fainali za Kombe la Shirikisho ni kama sehemu ya Kikosi cha Coastal Union ya Tanga wametimiza Ahadiwaliyoitoa kwa Mkuu wao wa Mkoa Adam Malima.
 

Kabla ya mchezo huo wa nusu fainali za FA kati ya Coastal dhidi ya Azam, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima alitembelea Kambi yA Wagosi wa Kaya huko Mbauda Jijini Arusha.

Katika mazungumzo yake na wachezaji Malima aliwaeleza kuwa wana kila sababu ya kuifunga Azam kwa madai kuwa wameshawahi kucheza nao huku wakiweza kuonyesha kiwango kikubwa mchezoni.

Mbali na hayo Malima alisema, Kikosi hicho cha Coastal kitakapoibuka kidedea kwenye mchezo huo kitaleta sifa njema kwa Mkoa huku akitumiafursa hiyo kuwapatia wachezaji donge nono.

"Najua nina deni lenu niliahidi na nitawapa hata hivyo mchezo huu mnapaswa kushinda na nitawapa kiasi kingine cha fedha"alisikika RC Malima akiwapa morari wachezaji wa Coastal.

Baada ya kusema hayo, nahodha wa Coastal Amani Kyata alimhakikishia Mkuu wa Mkoa Adam Malima kwamba wataishinda Azam kwenye mchezo huo.

Coastal imeifunga Azam kwa Penalti 8 kwa 5 ambapo sasa timu hiyo yenye maskani yake barabara 11 Jijini Tanga itacheza Fainali na Dar Young African.


NGOMA ya Baikoko imeonekana kuwa Nyenzo waliyoitumia Mashabiki wa Coastal katika kuwapa nguvu Wachezaji wao na hivyo kukiwezesha Kikosi cha Wagosi wa Kaya kutinga Fainali za Kombe la FA.


Kabla ya mchezo wa nusu fainali kupigwa, majira ya asubuhi mashabiki wa Coastal waliteka Viunga vya Jiji la Arusha kwa kupiga na kucheza ngoma yao ya Baikoko.

Kitendo hicho cha kuzunguka wakitumbuiza kwa ngoma hiyo mitaani huku  wakionyesha vidole vitatu kama ishara ya ushindi hatua ambayo ilionekana kuleta furaha kwa wapenzi wengi wa soka.

Pamoja na kuzunguka mitaani kwa shangwe, mashabiki hao walihamia mtaa
wa Mbauda walikofikia Coastal na kulakiwa na wachezaji ambao nao
walionekana kuwa na ari ya ushindi.

Shangwe na nderemo zilihamia Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa mashabiki
kupiga ngoma ya Baikoko wakiishangilia timu yao wakati ikicheza hadi
ilipoibuka mshindi.

Mchezo ulikuwa wa vuta nikuvute kwa timu zote kushindwa kupata mabao
hadi dk 90 zilipomalizika na kuongezwa dk 30 nazo zikamalizika kwa
sare hadi ilipofika hatua ya Mikwaju ya Penalti.

ANAYEDAIWA KUMUUWA MKEWE KWA RISASI NAYE AJIUA.

ajiua pic
 Mwanza. Said Oswayo anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi kadhaa mke wake Swalha Salum (28) naye amekutwa amejiua kwa kujipiga risasi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Mairi Makori amethibitisha kujiua kwa mtuhumiwa huyo ambaye mwili wake umekutwa ndani ya maji ya Ziwa Victoria kwenye ufukwe wa Rock Beach jijini Mwanza.

"Mwili huo umeopolewa ziwani eneo la ufukwe wa Rock Beach ukiwa na majeraha ya risasi kichwani. Timejiridhisha kuwa ndiye mtuhumiwa baada ya kutambuliwa na ndugu zake," amesema Kaimu Kamanda huyo.

Amesema mwili huo ulikutwa unaelea ufukweni mwa Ziwa Victoria ufukwe wa Rock Beach ambapo Jeshi la Polisi lililazimika kuwatafuta ndugu kwa utambulisho na kuthibitisha kuwa mtuhumiwa aliyekuwa anasakwa kwa mauaji ya mke wake.

Taarifa za uhakika zilizopatikana zinaeleza kuwa askari polisi wanaopeleleza tukio hilo walipiga kambi eneo la ufukwe wa Malaika kutokana na mawimbi ya mwisho ya mawaskliano ya mtuhumiwa Oswayo kuonekana eneo hilo kwa mara ya mwisho usiku wa kuamkia jana Mei 29.

"Mawasiliano ya mwisho ya simu ya Oswayo yalifanyika usiku wa manane eneo la Malaika; ndio maana Askari Polisi waliweka kambi pale na kweli mwili wake umepatikana hapo hapo," amesema mmoja wa watoa taarifa wetu kwa sharti la kuhifadhiwa jina

TUKIO LA KUUNGUA THE CASK MENEJA KCB BANK ASIMULIA JINSI BENKI HIYO ILIVYOMSHIKA MKONO MMILIKI WAKE

 Usiku wa kuamkia October 25 mwaka 2021, ulikuwa mgumu kwa Mkurugenzi wa moja ya viunga vya burudani vyenye hadhi ya kitalii jijini Mwanza kwani Kiwanja Maarufu Mwanza, The Cask Bar & Grill kiliteketea kwa moto na kuacha maswali mengi ya utata kwamba huenda ingekuwa ndiyo mwisho wake.

Meneja wa KCB Bank tawi la Mwanza, Emmanuel Greyson Mzava, anasimulia alivyolishuhudia tukio hilo na namna benki hiyo ilivyoshiriki harakati za kuirudisha hadhi ya eneo hilo ambalo licha ya kutumika kama sehemu ya burudani pia ni moja ya maeneo yanayo kuza uchumi wa 'Jiji la Sato na Sangara' sanjari na kuisaidia Serikali katika ubunifu wa kuzalisha ajira hasa kwa vijana.

WATUHUMIWA WA WAZIRI MKUU WAFIKIA NANE.

 


Bertha Ismail mwananchi

Arusha. Watuhumiwa wa matumizi mabaya ya fedha za jiji na kughushi nyaraka ambao wanachunguzwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Arusha, wamefikia nane sasa.


Watuhumiwa hao ambao waliokuwa sita, walisimamishwa kazi na Waziri mkuu kasim majaliwa kupisha uchaguzi wa tuhuma zinazowakabili huku kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Arusha pamoja na ofisi ya mkaguzi mkuu wa Serikali "CAG" zikipewa kibarua Cha uchunguzi.


Akizungumzia hilo, kamanda wa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoa wa Arusha, James Ruge alisema kuwa Watuhumiwa hao sasa wamefikia nane.


"Ukiachilia mbali wale Watuhumiwa sita tuliokabidhiwa, lakini Sasa tumeongeza wengine wawili ambao katika uchunguzi wetu tumeona tuwahoji hivyo Watuhumiwa wamefikia nane lakini wengine wengi watafuata"


Watuhumiwa hao ambao Kijaji alikataa kuwataja majina yao, alisema kuwa katika uchunguzi wao wamebaini kuwepo kwa mnyororo mrefu lakini kutokana na kazi hiyo wanaifaya kwa kushirikiana na taasisi nyingi ikiwemo Benki hawawezi kuwataja.

 

"Maneno ni mengi huko mtaani lakini hatuwezi kujibu na kuharibu kazi yetu, kubwa ambayo tumeifanya, hivyo niwaombe wananchi kuwa watulivu tukamilishe kazi yetu na tutatoa taarifa iliyokamilika"


Awali Mei 24 mwaka huu Waziri mkuu Kassim Majaliwa akiwa ziarani mkoani hapa, aliwasimamisha kazi maafisa sita wa Jiji la Arusha akiwemo Mkurugenzi wake Dkt. John Pima kwa makosa ya matumizi mabaya ya fedha za Jiji na tuhuma za kughushi nyaraka.

 Watumishi wengine waliosimamishwa kazi ni Mweka Hazina wa Jiji, Bi. Mariam Shaban Mshana; Bw. Innocent Maduhu (Mchumi), Bw. Alex Daniel Tlehama (Ofisi ya Mchumi,; Bw. Nuru Gana Saqwar (Ofisi ya Mchumi) na Bw. Joel Selemani Mtango, Afisa Manunuzi  ambaye alihamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Longido.


 Alisema kuwa amefikia uamuzi huo kwa  kuwa hawezi kuvumilia kuona fedha za umma zikitumika kinyume na taratibu ambapo alimtaka CAG kuanza uchunguzi kwa kutafuta nyaraka zote kubaini undani wa ubadhirifu huo huku  Akimuagiza Kamanda wa TAKUKURU wa Mkoa kufuatilia kwa ukaribu kujua wahusika wote.


 Katika mkutano na watumishi wa jiji la Arusha, Majaliwa alisema kuwa  Mkurugenzi anatuhumiwa kwa kutosimamia ipasavyo utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na watumishi,  matumizi mabaya ya vifaa vya ujenzi wa miradi kutumika kwa ujenzi binafsi ambapo nondo, matofali, misumari, mbao, gypsum boards, saruji, mchanga, kokoto na bati vyenye thamani ya sh. milioni 44 viliagizwa kupitia kampuni ya Cherry General Supplies and Services na kupelekwa kwenye nyumba binafsi iliyoko Olkereyan, eneo la Njiro chini ya Usimamizi wa Bw. Joel Selemani Mtango.


 “Tarehe 28 Machi, 2022 Mkurugenzi ulimwagiza Mweka Hazina aingize shilingi milioni 103 kwenye akaunti binafsi ya Innocent Maduhu iliyoko NMB zikiwa ni masurufu kwa ajili ya shughuli za kiwanda cha matofali. Ni kwa nini fedha ya kazi hii imeingizwa kwenye akaunti ya mtumishi binafsi badala ya akaunti za Kata?”alihoji Waziri Mkuu.


 “Tarehe 14 Aprili, 2020 uliagiza sh. milioni 65 ziingizwe kwenye akaunti ya Alex Daniel  ya benki ya NMB zikiwa ni malipo kwa ajili ya matenegenezo ya barabara za kata na mitaa. Tarehe hiyohiyo, sh. milioni 65 ziliingizwa kwa Bw. Nuru Ginana zikiwa ni malipo ya kununua vifurushi vya moramu. Hapa jumla ni shilingi milioni 233 ambazo hazikutumika kwa lengo lililokusudiwa,” amesema.


 Mkurugenzi huyo pia anatuhumiwa kuhamisha watumishi 50 kati ya Januari na Mei mwaka huu. “Umefanya uhamisho wa watumishi usiokuwa halisia. 


"Kuanzia Januari hadi Mei 2022, watumishi wapatao 45 wa kada mbalimbali wamehamishwa na wengine watano wamehamishwa mwezi  Mei kwa Maombi yako.”


 Amesema Mkurugenzi na timu yake, walimwomba mwenye kampuni ya Cherry General Supplies awape risiti ya sh. milioni 103 hali iliyosababisha adaiwe sh. milioni 15 na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) fedha ambazo hakuwa nazo na akatishiwa kushtakiwa


KITUO CHA SAYANSI CHA STEMP PARK CHA JIJINI TANGA KIMELETA MAGEUZI MAKUBWA

 

Meneja wa kituo cha Sayansi Maxi George akizungumza wakati wa halfa ya kituo hicho kutimiza mwaka mmoja tokea kilipoanzishwa
Sehemu ya wanafunzi wakifuatilia matukio mbalimbali


Na Oscar Assenga,TANGA

Kituo cha Sayansi cha Stemp Park kilichopo Jijini Tanga kimeleta Mapinduzi makubwa kwenye Sekta ya elimu ambapo kimeweza kuwa kichocheo kwa Wanafunzi kuhamasika kupenda kusoma Masomo ya Sayansi na kuongeza ubunifu.

Stemp Park ipo katika kata ya Kisosora na imeleta mapinduzi makubwa katika masomo ya Sayansi kwa Wanafunzi pamoja na Walimu.

Wanafunzi wanaotumia kituo hicho katika mambo ya Sayansi ni kianzia Chekechea hadi shule za Sekondari.

Akizungumza juzi katika wiki ya Sayansi Afrika Meneja wa kituo hicho Maxi George wakati wa halfa ya kituo hicho kutimiza mwaka mmoja tokea kuanzishwa Kwake iliyokwenda sambamba na maadhimisho ya wiki ya sayansi katika bara la Afrika

Ambapo alisema idadi kubwa ya ubunifu wa kisayansi katika jiji la Tanga umekuwa mkubwa ambapo wanafunzi wamekuwa wakienda kituo hicho na kufanya shughuli zao za ubunifu ambapo wanafanya wa nadharia zaidi.

"Hapa vijana wanapata nafasi ya kuelezwa umuhimu wa Sayansi katika maisha ya kawaida,na katika maisha ya shule kwa kujifinza mambo mbalimbali ya sayansi kwa vitendo na kwa kuona"alisema George

Katika hatua nyingine kituo hicho pia kinawanufaisha walimu wa mkoa wa Tanga kwa kuwapa ujuzi katika kuwafundisha wanafunzi shuleni

"Walimu wanaprogram maalum ambayo inaitwa TOT hii imekuwa chachu ya kuwapa ujuzi katika kuwafundisha vijana,lengo likiwa ni kuchagiza ufaulu kwa masomo ya sayansi"alisema George

Pia aliwaasa wazazi na walezi kuwahimiza watoto wao wajifunze masomo ya Sayansi kuwa sio ngumu bali watu waliaminiashwa kuwa ni ngumu

"Tunatoa wito kwa Wazazi,kuwaachia watoto wajifunze zaidi,pale mtoto anapofanya jambo la ubunifu mzazi amwache akifanye ili apate njia sahihi ya kutengeneza kitu anachokitaka ambacho badae kinaweza kuwa na manufaa"alisema George

Aidha Wanafunzi wanaoenda kwenda kujifunza katika kituo hicho wameeleza kuwa kituo hicho kimewajenga zaidi kwa kuwa wabinifu.

Mmoja wa wanafunzi wa kike Rukia Omari wa Masechu Sekondari anayenda kupata elimu ya Sayansi katika kituo hicho alisema wao wanakabiliwa na changamoto pindi wanapotaka nafasi ya kwenda kujifunza katika kituo hicho kwa kuwa wazazi wanawabana kupatamuda wa ziada ya kujifunza Sayansi

"Mazingira tunayoishi inatufanya wasichana tusiwesawa na wavulana katika kujifunza,ukiomba ruhusa kwenda kujifunza huwezi kupewa,utaambiwa bora umsaidie Mama kazi hivyo kufanya mua wa kusoma usiwepo lakini kwa wanaume iko tofauti akirudi hana kazi"alisema