ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 31, 2022

WATUHUMIWA WA WAZIRI MKUU WAFIKIA NANE.

 


Bertha Ismail mwananchi

Arusha. Watuhumiwa wa matumizi mabaya ya fedha za jiji na kughushi nyaraka ambao wanachunguzwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Arusha, wamefikia nane sasa.


Watuhumiwa hao ambao waliokuwa sita, walisimamishwa kazi na Waziri mkuu kasim majaliwa kupisha uchaguzi wa tuhuma zinazowakabili huku kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Arusha pamoja na ofisi ya mkaguzi mkuu wa Serikali "CAG" zikipewa kibarua Cha uchunguzi.


Akizungumzia hilo, kamanda wa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoa wa Arusha, James Ruge alisema kuwa Watuhumiwa hao sasa wamefikia nane.


"Ukiachilia mbali wale Watuhumiwa sita tuliokabidhiwa, lakini Sasa tumeongeza wengine wawili ambao katika uchunguzi wetu tumeona tuwahoji hivyo Watuhumiwa wamefikia nane lakini wengine wengi watafuata"


Watuhumiwa hao ambao Kijaji alikataa kuwataja majina yao, alisema kuwa katika uchunguzi wao wamebaini kuwepo kwa mnyororo mrefu lakini kutokana na kazi hiyo wanaifaya kwa kushirikiana na taasisi nyingi ikiwemo Benki hawawezi kuwataja.

 

"Maneno ni mengi huko mtaani lakini hatuwezi kujibu na kuharibu kazi yetu, kubwa ambayo tumeifanya, hivyo niwaombe wananchi kuwa watulivu tukamilishe kazi yetu na tutatoa taarifa iliyokamilika"


Awali Mei 24 mwaka huu Waziri mkuu Kassim Majaliwa akiwa ziarani mkoani hapa, aliwasimamisha kazi maafisa sita wa Jiji la Arusha akiwemo Mkurugenzi wake Dkt. John Pima kwa makosa ya matumizi mabaya ya fedha za Jiji na tuhuma za kughushi nyaraka.

 Watumishi wengine waliosimamishwa kazi ni Mweka Hazina wa Jiji, Bi. Mariam Shaban Mshana; Bw. Innocent Maduhu (Mchumi), Bw. Alex Daniel Tlehama (Ofisi ya Mchumi,; Bw. Nuru Gana Saqwar (Ofisi ya Mchumi) na Bw. Joel Selemani Mtango, Afisa Manunuzi  ambaye alihamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Longido.


 Alisema kuwa amefikia uamuzi huo kwa  kuwa hawezi kuvumilia kuona fedha za umma zikitumika kinyume na taratibu ambapo alimtaka CAG kuanza uchunguzi kwa kutafuta nyaraka zote kubaini undani wa ubadhirifu huo huku  Akimuagiza Kamanda wa TAKUKURU wa Mkoa kufuatilia kwa ukaribu kujua wahusika wote.


 Katika mkutano na watumishi wa jiji la Arusha, Majaliwa alisema kuwa  Mkurugenzi anatuhumiwa kwa kutosimamia ipasavyo utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na watumishi,  matumizi mabaya ya vifaa vya ujenzi wa miradi kutumika kwa ujenzi binafsi ambapo nondo, matofali, misumari, mbao, gypsum boards, saruji, mchanga, kokoto na bati vyenye thamani ya sh. milioni 44 viliagizwa kupitia kampuni ya Cherry General Supplies and Services na kupelekwa kwenye nyumba binafsi iliyoko Olkereyan, eneo la Njiro chini ya Usimamizi wa Bw. Joel Selemani Mtango.


 “Tarehe 28 Machi, 2022 Mkurugenzi ulimwagiza Mweka Hazina aingize shilingi milioni 103 kwenye akaunti binafsi ya Innocent Maduhu iliyoko NMB zikiwa ni masurufu kwa ajili ya shughuli za kiwanda cha matofali. Ni kwa nini fedha ya kazi hii imeingizwa kwenye akaunti ya mtumishi binafsi badala ya akaunti za Kata?”alihoji Waziri Mkuu.


 “Tarehe 14 Aprili, 2020 uliagiza sh. milioni 65 ziingizwe kwenye akaunti ya Alex Daniel  ya benki ya NMB zikiwa ni malipo kwa ajili ya matenegenezo ya barabara za kata na mitaa. Tarehe hiyohiyo, sh. milioni 65 ziliingizwa kwa Bw. Nuru Ginana zikiwa ni malipo ya kununua vifurushi vya moramu. Hapa jumla ni shilingi milioni 233 ambazo hazikutumika kwa lengo lililokusudiwa,” amesema.


 Mkurugenzi huyo pia anatuhumiwa kuhamisha watumishi 50 kati ya Januari na Mei mwaka huu. “Umefanya uhamisho wa watumishi usiokuwa halisia. 


"Kuanzia Januari hadi Mei 2022, watumishi wapatao 45 wa kada mbalimbali wamehamishwa na wengine watano wamehamishwa mwezi  Mei kwa Maombi yako.”


 Amesema Mkurugenzi na timu yake, walimwomba mwenye kampuni ya Cherry General Supplies awape risiti ya sh. milioni 103 hali iliyosababisha adaiwe sh. milioni 15 na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) fedha ambazo hakuwa nazo na akatishiwa kushtakiwa


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.