ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 9, 2013

PAMBA YAISHINDILIA KANEMBWA FC 4-2 DIMBA LA CCM KIRUMBA


Ndani ya mchezo wa ligi daraja la kwanza kuwania nafasi ya kukwea ligi kuu ya Premium Tanzania bara leo Pamba Fc imetembeza kichapo kikali kwa Kanembwa Fc mara baada ya kuidhibu kwa bakora 4-2 kwenye dimba lake la nyumbani jijini Mwanza CCM Kirumba, zaidi sikiliza simulizi za Sports Xtra ya Clouds fm kwa Kubofya play.

KENYA WAAMUA UHURU KENYATTA NDIYE RAISUhuru Kenyatta ndiye Rais wa nne wa Jamuhuri ya Kenya baada ya tume ya uchaguzi kumtangaza kushinda uchaguzi wa kihistoria wa Kenya.
Ni baada ya siku tano tangu wakenya kupiga kura kumpigia kura rais, magavana, maseneta, waakilishi wa bunge, waakislihi wanawake na waakilishi wodi.
Uhuru alipata zaidi ya asilimia hamsini ya kura zilizohitajika ili kuapata ushindi kulingana na mahitaji ya katiba mpya ya nchi.
Matokeo hayo yalionyesha kuwa Uhuru Kenyatta ameshinda na kuepuka duru ya pili ya uchaguzi.
Takwimu kutoka tume ya uchaguzi zinasema Kenyatta ameshinda asilimia hamsini nukta tatu za kura zote zilizopigwa.
Tume ya uchaguzi ilichukua zaidi ya masaa matano kukagua hesabu ya kura hizo kabla ya kutangaza matokeo hii leo siku tano baada ya wakenya kupiga kura.
Matokeo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi yanaonyesha kuwa Uhuru alipata kura 6,173,433 huku mpinzani wake Raila Odinga akipata 5,340,546

RICHARD COMMEY NDIYE MFALME WA UZITO MWEPESI KATIKA BARA LA AFRIKA

Rais wa IBF Afrika, Mtanzania Onesmo Ngowi na Waziri wa Michezo wa Ghana wakimtangaza Richard kuwa Mfalmwe wa Afrika uzito mwepesi


Rais wa IBF Afrika, Mtanzania Onesmo Ngowi na na Promoter wa mpambano huo Michael Amoo-Bediako wakipozi na Mfalmwe wa Afrika uzito mwepesi, Richard Commey
 Richard kulia na Bilal kushoto wakinyemeleana.

Friday, March 8th, 2013-Dar-Es-Salaam, TANZANIA- Richard Commey amedhihirisha uwezo wake wa upigana ngumi wakati alipomtoa kwa TKO bondia Bilal Mohammed na kutangazwa kuwa Mfalme wa uzito mwepesi katika bara la Afrika. Mpambano huo ulifanyika katika ukumbi wa Wills Gym City Engineers katika viunga vya Jamestwon, jijini Accra, Ghana na kuhudhuriwa na wapenzi wengi wa ngumi wakiongozwa na viongozi waandamizi wa Chama cha Ngumi cha Ghana (GBA), viongozi wa Kamati ya Olympic ya Ghana, Meya wa jiji la Accra, pamoja na wWaziri wa Michezo wa Ghana.
Mpambano huo ulianza kwa mbwebwe za aina yake baada ya mabondia wote kuwasili kwenye ulingo wakisindikizwa na mashabiki wao waliokuwa wanacheza ngoma mbalimbali za makabila ya Ghana.
Bilal alianza mpambano katika raundi ya kwanza akikurupuka kutoka kwenye kona yake kama faru na kumfuata Richard kwa nia ya kumsimamisha katika raundi ya kwanza lakini Richard aliweza kuhimili shambulio hilo na kuanza kutoa dozi kwa Bilal.
Katika raundi ya 4 Richard alimpeleka Bilal kwenye sakafu ya ulingo mara mbili kwa ngumi zilizokuwa nzito. Bilal aliweza kuendelea na pambano baada ya kuhesabiwa mara 8! Mashabiki wengi aliuzingira ulingo wakati wote wa mpambano huku wakipiga makalele na ngoma zilizoashia kuwa wawili hao kweli wametawala nyoyo za mashabiki wengi wa ngumi katika nchi ya Ghana.
Mambo yalifikia tamati katika raundi ya saba wakati Richard aliporusha ngumi tatu mfululizo za mchanganyiko na kumpeleka Bilal chini kwa mara ya tatu. Bilal aliamka kwa shida wakati mahesabu ya refarii yalipokuwa yanafikia mwisho na alianza kupepesuka huku refarii akimdaka ili asianguke tena na kuashiria mwisho wa mpambano huo.
Huu ni wakati ambapo Richard Commey alipotangazwa kuwa Mfalme wa uzito mwepesi katika bara la Afrika na ukumbi mzima kuzizima kwa nderemo na shangwe. Kwa ushindi huo, IBF imempatia Richhard Commey nafasi ya kuwania ubingwa wa dunia kwa vijana katika uzito mwepesi mpambano ambao utafanyika tarehe 28 mwezi wa Aprili mwaka huu.
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA

RAIS JAKAYA KIKWETE AMTEMBELEA KIBANDA SOUTH AFRIKA.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mhariri Mtendaji wa Habari Corporation Absalom Kibanda aliyelazwa katika hospitali ya Mill Park iliyopo mji wa Johannesburg, Afrika Kusini jana Ijumaa. Kulia ni Katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana. Bwana Kibanda alipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana juzi usiku. Rais Kikwete yupo Afrika Kusini kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyokuwa mstari wa Mbele katika mapambano dhidi ya Ukoloni na ubaguzi wa Rangi. Mkutano huo umeandaliwa na Chama cha African National Congress (ANC). Picha zote na Freddy Maro.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mhariri Mtendaji wa Habari Corporation Absalom Kibanda aliyelazwa katika hospitali ya Mill Park iliyopo mji wa Johannesburg, Afrika Kusini jana jioni. Kulia ni Katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana. Bwana Kibanda alipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana juzi usiku. Rais Kikwete yupo Afrika Kusini kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyokuwa mstari wa Mbele katika mapambano dhidi ya Ukoloni na ubaguzi wa Rangi. Mkutano huo umeandaliwa na Chama cha African National Congress (ANC).

Friday, March 8, 2013

GEITA KUSHUHUDIA MKALI NANI KATI YA MCHELE MCHELE NA BHUDAGALA.

Tarehe 23/03/2013 wasanii wanaotamba hivi sasa katika mahadhi ya muziki asili toka kabila la Wasukuma, Mchele Mchele pamoja na Bhudagala watapanda jukwaa moja mkoani Geita katika uwanja wa Katoro  kuonyeshana ubabe kwa mashabiki kwamba nani ni mkali katika suala la burudani.

Kipindi kirefu sasa wakali hao nyimbo zao zimekuwa zikisikika kwenye kumbi za starehe kanda ya ziwa, huku kanda zao na cd zikinunulika kama njugu hasa kwa wapenzi wa muziki asili ambao wamekuwa wakiburudishwa na vionjo asili pamoja na ujumbe unaopatikana kiasi cha wengi kutamani siku itokee nao kuwekwa kwenye mizani moja kupimwa yupi ni bora zaidi ya mwenzake. 

Kwa mujibu wa Bwana Livinus Madaraka ambaye ni mkurugenzi wa Tivol Studio Mwanza , waandaaji wa mpambano huo amesema kuwa kampuni yake imeamua kuandaa mpambano huo ili kumaliza utata kwa mashabiki pamoja na wakali hao kutambiana kwenye majukwaa tofauti kila mmoja akinasibu kuwa ni mkali zaidi ya mwenzake, hivyo anaamini kupitia mchakato huo aliyebora zaidi ya mwenzake atajulikana.

SKYLIGHT BAND KULA RAHA ZA PASAKA 2013 NA WAKAZI WA MWANZA

"Na wewe usikose" ni Muhksin Mambo aka Mc Stopper na manjonjo yake kwenye kikao cha matayarisho kuelekea siku ya Pasaka ambapo jiji la Mwanza litashuhudia ujio wa mara ya kwanza wa Skylight Band, itakayoshusha burudani mbili, ya kwanza itafanyika Jumapili ya tarehe 31/03/2013 (Pasaka) ukumbi wa JB Belmount na kisha Jumatu ya Pasaka shangwe zitahamia Villa Park. 
Zaidi sikiliza tangazo...

Wadau wa meza kuu  ya matayarisho ya Bonge la Party la Skylight Band litakalofanyika Rock City, kutoka kushoto ni Jackob Usungu, Justin Ndege, Kingu na Hanry wakiwa  kwenye kikao cha matayarisho kuelekea siku ya Pasaka ambapo jiji la Mwanza litashuhudia ujio wa mara ya kwanza wa Skylight Band, itakayoshusha burudani mbili, ya kwanza itafanyika Jumapili ya tarehe 31/03/2013 (Pasaka) ukumbi wa JB Belmount na kisha Jumatu ya Pasaka shangwe zitahamia Villa Park. 


Sehemu ya wadau wa kamati kuu ya matayarisho wakiwa kwenye meza ya kikao cha matayarisho kuelekea siku ya Pasaka wakisikiliza hoja ikiwasilishwa na Muhksin Mambo, chini ya mwenyekiti wa kikao hicho Bw. Sebastian Ndege ambapo jiji la Mwanza litashuhudia ujio wa mara ya kwanza wa Skylight Band, itakayoshusha burudani mbili, ya kwanza itafanyika Jumapili ya tarehe 31/03/2013 (Pasaka) ukumbi wa JB Belmount na kisha Jumatu ya Pasaka shangwe zitahamia Villa Park. 


Kutoka kushoto ni Meneja wa Burudani wa Villa Park Rama, mratibu wa ujio wa Skylight Band jijini Mwanza mwanadada Yvona Jackob Usungu na Justin Ndege, wakiwa  kwenye kikao cha matayarisho kuelekea siku ya Pasaka ambapo jiji la Mwanza litashuhudia ujio wa mara ya kwanza wa Skylight Band, itakayoshusha burudani mbili, ya kwanza itafanyika Jumapili ya tarehe 31/03/2013 (Pasaka) ukumbi wa JB Belmount na kisha Jumatu ya Pasaka shangwe zitahamia Villa Park. 


Sasa ilikuwa zamu ya mwanakamati Mr. Joshua kuwasilisha mawazo kikaoni. 


Kwa mara ya kwanza jiji la Mwanza litashuhudia burudani ya kipekee ya kisasa iliyokwenda skuli ambapo kwa show  itakayopigwa JB Belmount usiku wa tarehe 31, itakuwa classic ikiwa na vihusishi maalum kwa wahudhuriaji.  

MAANDALIZI YA PASAKA GOSPEL FESTIVAL 2013 YAENDELEA KWA KASI NZURI.

Na Fabian Fanuel
Mratibu wa Pasaka Gospel Festival Albert George Sengo akiongea na Waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusu waimbaji waliokubali kuimba katika Tamasha la Pasaka Gospel Festival 2013 litakalokuwa sambamba na Uzinduzi wa Studio za Digitali Za Cosu Universal Studio jijini Mwanza.

Waimbaji kumi kutoka Dar es salaam, Mbeya, Iringa, Arusha wanatarajia kutumbuiza katika jumuiko la Pasaka Gospel Festival 2013 litakalofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 31/3/2013 jumapili ya pasaka na tarehe 1/4/2013 katika uwanja wa CCM Katoro jumatatu ya pasaka Geita kuanzia saa nane kamili mchana.

Akizungumza na waandishi wa habari, mratibu wa tamasha hilo bwana Albert George Sengo amesema kuwa maandalizi yanakwenda vizuri sana na kuwaomba wakazi wa jiji na Mkoa wa Mwanza na Mikoa ya Jirani kujitokeza kubarikiwa na waimbaji hawa wa nyimbo za injili.

Amewataja waimbaji hao kuwa kutoka Dar es salaam ni Enock Jonas maarufu kama Zunguka Zunguka, Neema Mwaipopo maarufu kama Raha Jipe Mwenyewe, Nesta Sanga, Daniel Safari, John Shaban, Jessica Julius na Isaya Msangi. Kutoka Mbeya Tumaini Mbembela, Kutoka Iringa Dan Sanga, Kutoka Arusha Neema Munis. 


Sambamba na waimbaji hao wapo waimbaji kutoka jiji la Mwanza kama vile Cecilia Kassim, Goodluck Gozbert, Vijana kwaya Nyamanoro, Eagt City Centre na kwaya nyingine ziadi ya ishirini kutoka Mwanza na nje ya Mwanza.


Amekitaja kiingilio katika tamasha hilo la Pasaka Gospel Festival 2013  ni 2000/= kwa kila mtu, Mwanza na Geita na pia siku hiyo kutakuwa na uzinduzi wa studio mpya ya audio na video ya Cosu Universal Studio iliyoko jijini Mwanza.

Viongozi mbalimbali wa Kiserikali na taasisi wamekubali kuhudhuria tamasha hilo kubwa la Pasaka Gospel Festival 2013 ambalo halijawahi kutokea jijini Mwanza. 
p

GAZETI JIPYA LA MASUALA YA AFYA LATINGA MTAANI


BM Publishers
Wanakuletea
Gazeti La TABIBU 
Gazeti Maalum La Maswala Ya Kiafya
Wasiliana Nasi Leo:
Jengo la UMATI Ghorofa ya 3, Mtaa wa Samora/Zanaki
Simu: 022 2124805, 0655 538 644
Barua Pepe: info@bmpublishers.com

Thursday, March 7, 2013

MBEZI WAIBUKA WASHINDI MICHUANO MPINGA CUPTimu ya Mbezi inayohusisha waendasha pikipiki maarufu kama bodaboda ikishangilia ushindi mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza wa michuano ya Mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay police. Mbezi iliifunga makondeko mabao 7-6 na kuibuka washindi

Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga akibadilishana mawazo na  Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh.Pereira Silima ambaye  wakati wa fainali za michuano ya mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay police.

Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga akimtambulisha  Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh. Pereira Silima ambaye ni mgen rasmi  wakati wa fainali za michuano ya mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay police.

Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde akikabithi zawadi kwa captain wa timu ya makondeko Stanley Peter mara baada ya kuibuka washindi wa pili wa mashindanoo ya mpinga Cup yaliyohusisha waendasha pikipiki (bodaboda)  kwa muda wa wiki moja katika viwanja vya oyesterbay polisi. Kushoto pembeni ni kiongozi wa timu ya makondeko bwana Mneke S Mneke

Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh. Pereira Silima akikabithi mfano wa hundi ya shilingi millioni moja kwa captain wa timu ya Mbezi Ally Shila Kulola  baada ya timu yake kuibuka washindi wakwanza wa michuano ya mpinga Cup kwa kushinda Makondeko  mabao 7-6

Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh. Pereira Silima akikabithi kombe  captain wa timu ya Mbezi Ally Shila Kulola  baada ya timu yake kuibuka washindi wakwanza wa michuano ya mpinga Cup kwa kushinda Makondeko  mabao 7-6

Michuano ya mpinga Cup imemalizika rasmi jana baada ya mchezo wa fainali thidi ya timu ya Mbezi na makondeko ambapo, timu  hizo zilitoka sare ya bao 2 -2 na kuingia kwenye mkwaju wa penalti ambapo timu ya kawe iliibuka na ushindi wa mabao 7 -6  
Katika michuano hiyo iliyodumu kwa muda wa wiki nzima na kushirikisha timu nane kutoka katika mkoa wa kipolisi wa kinondoni timu ya  mikocheni  Iliibuka kuwa mshindi wa tatu wa michuano hiyo.

Mgeni rasmi Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh. Pereira Silima alisema” tunawashukuru waandalizi wa michuano hii na wadhamini ambao ni Airtel, Mr price, home shoping center na Rotary Club Dar es Saalam kwa ushirikiano wao mkubwa na mchangao wao katika kuhakikiksha mashindano haya yanafanyika kwa mafanikio.  Hii nijitahada ya pekee kuunganisha michezo na elimu ya usalama barabarani. Tumegundua vipaji vingi hapa tunawaasa wachezaji hawa wajiendeleze mbali na kuendesha  pikipiki kwa muda wa ziada wataweza kucheza mpira na kupata njia nyingine ya kipato kwa michezo ni ajira.

Naye Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga amewashukuru washiriki wote wa michuano hii na kusisitiza  wananchi na watanzania kwa ujumla kutii sheria bila shurutishi.

Akiongea kwa niaba ya wadhamini Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde alisema” mashindano haya yamekuwa ya mvuto mkubwa kwa washiriki na wadau wa michezo zaidi tumeshuhudia jinsi mafunzo ya elimu ya usalama barabarani yalivyoendesha na kuelimisha watumiaji wa barabara waliokuwa wakihudhuria hapa. 

Tunaamini kuendelea na  juhudi hizi tutaweza kupunguza idadi za ajali barabarani. Airtel tunaahidi kuendelea kushirikiana na jeshi la  polisi  usalama barabarani katika shughuli mbalimbali za uelimishaji umma juu ya sheria za barabarani

Michuano ya mpinga cup kwa wilaya ya kinondoni imefika tamati hapo jana na mpango ni kuwa na michuano hii pia katika mkoa wa ilala na temeke na kisha kuendelea na michuano hii nchini nzima.


MJUWE BIBI YANGU MZAA MAMA NA WAJOMBA ZANGU

Bibi Ng'wanamashauri akiwa na wajukuu zake nyumbani kwa Uncle Meshack.

"Ndiyo mimi" ni katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani.

"Sasa umefika pumzika" shangazi alisikika akisema.

"Kaa vyema mama".

Akivalishwa viatu.

Bibi na wadogo zangu.
Picha zote amepiga akiwa mkoani Dodoma nyumbani kwa Uncle Meshack.

Wednesday, March 6, 2013

FORUM SYD YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KONGAMANO JIJINI MWANZA

Meneja wa nchi wa shirika la Kiswidi Forum Syd bwana Godfrey Wawa akizungumza wakati wa ufunguzi kwenye mkutano  wa akinamama uliofanyika leo Monarch Hotel jijini Mwanza ukiwa na lengo la kujadili changamoto wanazokutana nazo akina mama katika harakati za maisha ya kila siku vilevile kutambua umuhimu wa wanawake katika maendeleo ya jamii.

Afisa habari wa Forum Syd Tanzania Bi. Emma Mashauri akitoa maelezo juu ya  mikakati iliyowekwa kufanikisha maadhimisho hayo.

Forum Syd imekuwa ikifanya kazi nchini Tanzania tangu mwaka 1982 ikilenga katika kuchochea maendeleo endelevu, haki na kuzingatiwa kwa sheria, pamoja na kupunguza umasikini.

Kongamano hili limekuja likihusisha na akina baba pia kwa nia ya kutoa elimu ikiwa ni safari kuelekea siku ya Maadhimisho ya akinamama duniani tarehe 8/03/2013

Mkufunzi kutoka Chuo Cha SAUT akiwasilisha mada kwa wanakongamano ilizipate kujadiliwa kwa kina ikiwa ni pamoja na kutolewa ufafanuzi na maamuzi.

Wadau mbalimbali kutoka ndani ya jamii na mashirika ya huduma za kutetea haki na kuzuia ukatili kama vile shirika la kijamii la KIVULINI, wamehudhuria kongamano hili la Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke duniani lililofanyika Monarch Hotel Mwanza.

Kwa utulivu na umakini akinamama wakisikiliza yanayojiri ndani ya kongamano hili la Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke duniani lililofanyika ukumbi mkubwa wa mikutano Monarch Hotel jijini Mwanza.

Sehemu ya wahudhuriaji.

Shirika la Forum Syd lilipata ufadhili kutoka Sida-Tanzania kutekeleza mradi wa Uwajibikaji Jamii nchini Tanzania,mradi ukilenga vijiji na kata za wilaya za karagwe, Magu na Ukerewe ukiwana lengo la kusaidia na kuimarisha jitihada za wadau wa maendeleo kwa kuwajengea uwezo kwa njia ya mafunzo mbalimbali.

Umakini zaidi kusanyikoni.

Burudani nayo ilipata nafasi.

Kula burudani ya Kadogoli ambayo ilitumbuiza. 

MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA NCHINI MAREKANI MWEZI UJAO KURUHUSU ABIRIA WA NDEGE KUSAFIRI NA VISU VIDOGO NA VIFAA VYENYE NCHA KALI VYA MCHEZO WA GOLF


WASHINGTON (AP) — Airline passengers will be able to carry small knives, souvenir baseball bats, golf clubs and other sports equipment onto planes beginning next month under a policy changeannounced Tuesday by the head of the Transportation Security Administration.
The new policy conforms U.S. security standards to international standards, and allows TSA to concentrate its energies on more serious safety threats, the agency said in a statement.
The announcement, made by TSA Administrator John Pistole at an airline industry gathering in New York, drew an immediate outcry from unions representing flight attendants and other airline workers, who said the items are still dangerous in the hands of the wrong passengers.
Transport Workers Union Local 556, which represents over 10,000 flight attendants at Southwest Airlines, called the new policy "dangerous" and "shortsighted," saying it was designed to make "the lives of TSA staff easier, but not make flights safer."
"While we agree that a passenger wielding a small knife or swinging a golf club or hockey stick poses less of a threat to the pilot locked in the cockpit, these are real threats to passengers and flight attendants in the passenger cabin," the union said in a statement.
The policy change was based on a recommendation from an internal TSA working group, which decided the items represented no real danger, said David Castelveter, a spokesman for the agency.
The presence on flights of gun-carrying pilots traveling as passengers, federal air marshals and airline crew members trained in self-defense provide additional layers of security to protect against misuse of the items, he said. However, not all flights have federal air marshals or armed pilots onboard.
The new policy permits folding knives with blades that are 2.36 inches or less in length and are less than 1/2-inch wide. The policy is aimed at allowing passengers to carry pen knives, corkscrews with small blades and other knives.
Passengers also will be allowed to bring onboard as part of their carry-on luggage novelty-sized baseball bats less than 24 inches long, toy plastic bats, billiard cues, ski poles, hockey sticks, lacrosse sticks and two golf clubs, the agency said. The policy goes into effect on April 25.
Security standards adopted by the International Civil Aviation Organization, a U.N. agency, already call for passengers to be able to carry those items. Those standards are non-binding, but many countries follow them.
Box cutters, razor blades and knives that don't fold or that have molded grip handles will still be prohibited, the TSA said.
Reaction to the changes was mostly positive among travelers interviewed Tuesday at Los AngelesInternational Airport.

RAIS WA VENEZUELA HUGO CHAVEZ AFARIKI

Wafuasi wa Hugo Chavez wamekuwa wakimuombea aweze kuugua pole

Katika taarifa kwa taifa, makamu wa rais wa Venezuela Nicholas Marduro ametangaza kufariki dunia kwa rais Hugo Chavez, 58, kufuatia kuugua muda mrefu maradhi ya Saratani. Rais Chavez ametoweka katika hadhira ya nchi hiyo kwa muda mrefu ambapo alikuwa anapokea matibabu nchi jirani ya Cuba.

Alirejea , mjini Caracas mnamo Februari 18 kwa mara ya kwanza kupokea matibau. Hata hivyo maelezo zaidi hayakutolewa juu ya afya yake. Waandamanaji waliandamana katika mji mkuu Caracas mwishoni mwa juma wakidai kuwa watu wa Venezuela wanapaswa kupewa habari zaidi kuhusu afya ya rais wao.

Ujumbe wa Jeshi
Bwana Chavez amekua uongozini nchini Venezuela kwa tangumaradhi yake yamzidie ambapo alipelekwa hospitali ya kijeshi kuendelea miaka 14 na anatazamiwa kuleta mageuzi makubwa yaliyolenga zaidi kuimarisha maisha ya raia wa pato la chini.
Taarifa kutoka kwa jeshi imesema kuwa wataendelea kuilinda hadhi ya nchi na kuimarisha usalama. Pia jeshi limeahidi kuendelea kuwa waaminifu kwa makamu wa rais Nicholas Marduro na wakatoa wito kwa raia kuwa watulivu.
Chavez - wasifu
Hugo Chavez alijitosa katika siasa za Venezuela mnamo Februari 1992 akiwa luteni katika jeshi. Aliongoza mapinduzi dhidi ya rais wa wakati huo Carlos Andres Perez.
Lakini kutokana na kukosa usaidizi wa kutosha wa kijeshi, Chavez na wanamgambo wenzake walishindwa kunyakua madaraka hayo. Alikiri kushindwa na aliwekwa korokoroni.
Aliingia uongozini baada ya ushindi mkubwa ulioviondosha vyama vya kisiasa wakati huo. Katika kuapishwa kwake mnamo February 1999, Hugo Chavez alitangaza wazi kwamba mipango yake ya mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi sio kampeni tu. Alitimiza ahadi yake na kuiongoza nchi hiyo katika mabadiliko ambayo hayakuwahi kushuhudiwa katika muda wa miongo kadhaa. Alibadili muundo wa bunge na kulifanya kuwa la kikatiba, ambalo liliiunda katiba mpya baada ya kura ya maoni iliyoidhinishwa na 88% ya wapiga kura.
Rais Chavez alitaifisha rasilmali ukiwemo utajiri wake mkubwa wa mafuta. Sera kama hizi zilimfanya azozane na kampuni za kimataifa za mafuta, lakini alipata uungwaji mkono mkubwa wa watu maskini.
Chavez na jamii ya kimtaifa
Kutokana na urafiki wake na viongozi wa mrengo wa kushoto kama vile rais wa Cuba, Fidel Castro, ambaye walikuwa na uhusiano wa karibu aligongana kidiplomasia na Marekani, ambayo ni mshirika wake mkuu wa kibiashara.
Chavez alipendwa nyumbani na wafuasi wake lakini alipingwa na baadhi ya watu nchini humo na katika nchi za nje. Alionekana sio tu kama bingwa wa jamii maskini lakini pia kama muingiliaji wa siasa za nchi jirani. Katika miaka ya hivi karibuni alilenga kukabiliana na masuala ya ndani ya Venezuela, kama uhalifu, kuinua uchumi wa nchi na kukabiliana na rushwa.
 Hisani ya BBC SWAHILI

Tuesday, March 5, 2013

MKALI WA WIMBO WA 'ZUNGUKA' NA MKALI WA WIMBO WA 'RAHA JIPE MWENYEWE' KUZINDUA KAMPUNI YA KUTENGENEZA MUZIKI NA VIPINDI PASAKA HII CCM KIRUMBA MWANZA

Meneja wa kampuni mpya ya kurekodi muziki, vipindi na video ya COSU Entertainment Albert G. Sengo (kushoto) akitoa taarifa juu ya uzinduzi utakao kwenda kufanyika Sikukuu ya Pasaka tarehe 31/03/2013 ambapo waimbaji Enock Jonas anayetamba na wimbo wake wa Zunguka pamoja na Neema Mwaipopo maarufu kwa wimbo wa Raha Jipe Mwenyewe na wengine wengi watashuka jijini Mwanza kuupamba uzinduzi huo kulia kwake ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Fabian Fanuel. Sikiliza hapo juu.


Mkurugenzi wa kampuni mpya ya kurekodi muziki, vipindi na video ya COSU Entertainment Fabian Fanuel akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari hii leo kwenye ofisi za kampuni hiyo zilizoko nyegezi jijini Mwanza.

Mkurugenzi wa kampuni mpya ya kurekodi muziki, vipindi na video ya COSU Entertainment Fabian Fanuel akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari  kwenye ofisi za kampuni hiyo zilizoko nyegezi jijini Mwanza, nyuma ni timu ya baadhi ya wafanyakazi wa idara mbalimbali za utayarishaji muziki na makamera mana wa kampuni hiyo walio tambulishwa leo.


Msikilize hapa..


Meneja wa kampuni mpya ya kurekodi muziki, vipindi na video ya COSU Entertainment Albert G. Sengo (kushoto) akitoa taarifa juu ya uzinduzi utakao kwenda kufanyika katika Sikukuu ya Pasaka tarehe 31/03/2013 ambapo waimbaji Enock Jonas anayetamba na wimbo wake wa Zunguka pamoja na Neema Mwaipopo maarufu kwa wimbo wa Raha Jipe Mwenyewe na wengine wengi watashuka jijini Mwanza kuupamba uzinduzi huo.  


Meneja wa kampuni ya COSU Entertainment Albert G. Sengo akitoa wazo la jinsi ya kuboresha moja ya kazi za video za muziki kwa  mtayarishaji makini David Kimario ambaye yuko mtamboni, kulia kwake ni Mkurugenzi Fabian Fanuel,  shughuli nyingine zinazofanywa na kampuni hiyo ni pamoja na kumiliki jukwaa la vipaji mbalimbali kama wanamitindo, sarakasi, waigizaji filamu na utoaji huduma za matangazo ya barabarani.


Shughuli ya usanifu ikiendelea chumba cha madaktari wa video.


Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakipata maelezo toka kwenye chumba cha mtayarishaji wa Muziki wa kampuni ya COSU Entertainment jijini Mwanza.


Mkurugenzi wa COSU Entertainment hapa alipata fursa ya kuimba pamoja na wanahabari toka kulia ni Mashaka Bartazar wa Jambo leo na Majira na kushoto ni Sheilah Sezy wa Gazeti lililokuja na mabadiliko makubwa sokoni hivi sasa la Mwananchi.


Hapa kazi iliyokuwa ikisubiriwa ni Sheilah Sezy wa Gazeti lililokuja na mabadiliko makubwa sokoni hivi sasa la Mwananchi kukaanga chips aka kupiga drums.
Ndipo chips zikakaangika...


Hili ndilo gari la PA (matangazo ya barabarani) la Great Zone iliyo ndani ya COSU Entertainment.


Mjengo wa COSU Entertainment ulioko Nyegezi jijii Mwanza.

UZINDUZI WA KAMPUNI ILIYONUIA KULETA MAPINDUZI KWENYE SOKO LA DIGITALI MWANZA COSU ENTERTAINMENT UTAKAOFANYIKA TAREHE 31/03/2013 SIKU YA PASAKA UWANJA WA CCM KIRUMBA MWANZA .
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ndugu zangu wanahabari.
Ujio wa COSU Intertainment unakuja wakati Tanzania ikishuhudia Media zake zikiingia katika mfumo wa digitali ambao unahitaji kulishwa ipaswavyo ili kuvutia wadau na wafanyabishara kuweza kushawishika kununua muda wa vipindi husika (kuwa wadhamini) jambo ambalo huchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya utoaji huduma kwa media mbalimbali hapa nchini.

Ikumbukwe kuwa awali Taifa letu lilikuwa kwenye mfumo wa Analojia ambao ilikuwa ukiwa na Luninga yako na nishati na antenna yako ya waya basi mawasiliano utayapata utatizama Tv yoyote hata vipindi visivyokuwa na ubora  au usivyokuwa na mpango navyo alimuradi tu umetizama TV, sasa hizo zama zinatoweka taratibu mikoa baada ya mikoa.

Walianza Dar es salaam, Dodoma, Tanga sasa Mwanza nayo imeingia kwenye mfumo wa digitali mwisho wa siku wilayani, vijijini na Taifa kwa ujumla litakuwa digitali.

Kwa hali ya sasa ndani ya mfumo wa digitali ili upate mawasiliano ya televisheni lazima uwe na king’amuzi ambacho unalipia, sasa wamiliki wa ving’amuzi tulivyonavyo (vi 3 sasa) ili kuvutia wateja kwa malengo ya kupata soko kubwa wanalazimika kuweka channel zenye mvuto na zenye ubora ili kukidhi soko la ushindani.
Kupitia ushindani itafika kipindi ndani ya king’amuzi kimoja kutakuwa na chanel  200 hivi za ndani na nje hapa tutashuhudia tukishindanishwa na televisheni za kimataifa, kwa mfumo huu vituo vingi vitakuwa vikishindana kwa kuwa na maudhui nzuri na kuwa na vipindi vya kipekee  ili vipate matangazo na wadhamini wa kutosha.

Ni suala lililo wazi kuwa wenye matangazo yao hukimbilia vituo vinavyotizamwa.

Media kwa sasa ziko kwenye mahitaji ya kiushindani, hivyo zina mahitaji na mahitaji, kwa mtindo huu basi COSU Entertainment tumeona kuwa kuna mwanya hapo, nasi ni vijana wakongwe katika tasnia ya media tuko kwaajili ya kuuziba mwanya huo, na hizi ndizo juhudi sasa za kuitikia wito wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA kuzifanyia kazi zile ajira ambazo tumeelekezwa zipo nasi kushuhudia kweli zipo.

COSU Entertainmen tuliojikita zaidi katika uandaaji na utayarishaji kuanzia vipindi, Audio music, Video za muziki pamoja na kujenga jukwaa la vipaji mbalimbali nchini Tanzania tumeliona soko hilo la ajira na sasa tunataka kuudhihirishia umma wa Watanzania kuwa mapinduzi yatafanyika kupitia sisi.

Hatujaishaia hapo pia tumeliona soko jingine la ajira lililopo vijijini na wilayani hapa tunazungumzia Muziki wa Asili, huu ni muziki ambao kwa sasa vionjo vyake vinakuja kwa kasi na kuboresha muziki wa kisasa na muziki huo wa asili ukionyesha kuwa na dira ya maisha marefu sokoni.

Tizama marafiki zetu Afrika Magharibi, Afrika ya kati, Afrika ya kusini wote hao vionjo vya muziki asili vimechangia kuubeba sana muziki wao kutamba katika soko la kimataifa na sasa ndiyo wameiteka dunia.
Mifano iko mingi – akina Werason, Koffi  Olomide, Fally Ipupa, J. Martins na wengine wengi wote hawa style zote mpya wanazokuja nazo nyingi zinatoka vijijini, ambako hufanya mashindano ya vipaji mbalimbali iwe waimbaji, wapigaji muziki hadi wachezaji na kuubebea muziki huo kwenye soko hatimaye makubwa mapinduzi tunayashuhudia.

Sasa kwa hili tukirejea nchini na kuanzia hapa Kanda ya ziwa, Kanda inayosifika sana kwa vipaji vya nyimbo asili tena za kuchezeka, anzia Kagera kwa akina Saida Karoli, Maua, Papaa Kishaju wote muziki wao unadumu, Ingia Shinyanga kuna ngoma asili pale kama Bolaboka, Wigashe, Bogobogobo, rudi Mwanza na wilaya zake nenda Ukerewe na Kadogoli, Dungu, ngoma nyingi za kuchezeka tena za kusisimua na hata tumeshuhudia mara nyingine zikitumika kwenye  maharusi na dhifa mbalimbali na kadhalika.

Hivyo basi nina uhakika tukitumia vyema muziki huu mengi yatafanyika.

Katika project tutakazozifanya kuna watu wakajkuja kwetu kurekodi kwa fedha na kuna watu tutawasaka nao warekodi kwa gharama zetu hawa ote tutashirikiana nao kutengeneza matirio zenye maudhui ya kuuzika, zenye Ushawishi.

Ndugu zangu waandishi wa habari huduma zetu ingawa zimeanza kufanya kazi kwa kurekodi baadhi ya vipindi kwaajili ya vituo vya televisheni mbalimbali, pamoja na kurekodi video za kwaya na bendi mbalimbali kwa sasa, uzinduzi rasmi tutaufanya mnamo tarehe 31/03/2013 katika sherehe ya sikukuu ya Pasaka uwanja wa CCM Kirumba ambapo tutatoa burudani ya Muziki wa Injili tuliyoipa jina la PASAKA GOSPEL FESTIVAL ambapo wakazi wa Mwanza watashuhudia burudani ililoandaliwa kwa ubunifu wa hali ya juu ikishirikisha waimbaji wakubwa kama Enock Jonas (ZUNGUKA), na Neema Mwaipopo (RAHA JIPE MWENYEWE).

Wengine ni Nesta Sanga (JIANDAENI), Danni Safari, John Shahban, Jeska Julius, Isaya Msangi (SHETANI IMEKULA KWAKO), Danny Sanga kutoka Iringa, Tumaini Mbembela  kutoka Mbeya na mkoa wa Arusha utawakilishwa na Neema Munisi.

Kwaya za mkoa wa Mwanza ni nyingi za kutosha Anglican Vijana kwaya, EAGT City Centre kiufupi kwa zote zitaweka kambi kwenye shughuli yetu ya Uzinduzi Pasaka hii.

Jumatatu ya pasaka tutakuwa Geita uwanja wa CCM Katoro
Kiingilio kwa maeneo yote kitakuwa ni shilingi. 2000/= tu
Hivyo tunawakaribisha wote kwenye uzinduzi huo.

Nanyi ndugu zangu wanahabari twawaomba mtusambazie habari hizi kwani hili linatoka kwa watu wenu na msishangae waandishi nanyi kupitia vipaji vyenu mkapata fursa katika soko la ajira la COSU Entertainment, tukawa tukiwakodisha mara kadhaa kutokana na either kuzidiwa na mahitaji hivyo tunawasihi msisite kufungua milango ya ushirikiano ili tujenge Tanzania yetu.

Zidumu fikra za Maendeleo!
Aksanteni kwa kutusikiliza.