ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 7, 2013

MBEZI WAIBUKA WASHINDI MICHUANO MPINGA CUP



Timu ya Mbezi inayohusisha waendasha pikipiki maarufu kama bodaboda ikishangilia ushindi mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza wa michuano ya Mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay police. Mbezi iliifunga makondeko mabao 7-6 na kuibuka washindi

Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga akibadilishana mawazo na  Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh.Pereira Silima ambaye  wakati wa fainali za michuano ya mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay police.

Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga akimtambulisha  Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh. Pereira Silima ambaye ni mgen rasmi  wakati wa fainali za michuano ya mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay police.

Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde akikabithi zawadi kwa captain wa timu ya makondeko Stanley Peter mara baada ya kuibuka washindi wa pili wa mashindanoo ya mpinga Cup yaliyohusisha waendasha pikipiki (bodaboda)  kwa muda wa wiki moja katika viwanja vya oyesterbay polisi. Kushoto pembeni ni kiongozi wa timu ya makondeko bwana Mneke S Mneke

Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh. Pereira Silima akikabithi mfano wa hundi ya shilingi millioni moja kwa captain wa timu ya Mbezi Ally Shila Kulola  baada ya timu yake kuibuka washindi wakwanza wa michuano ya mpinga Cup kwa kushinda Makondeko  mabao 7-6

Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh. Pereira Silima akikabithi kombe  captain wa timu ya Mbezi Ally Shila Kulola  baada ya timu yake kuibuka washindi wakwanza wa michuano ya mpinga Cup kwa kushinda Makondeko  mabao 7-6

Michuano ya mpinga Cup imemalizika rasmi jana baada ya mchezo wa fainali thidi ya timu ya Mbezi na makondeko ambapo, timu  hizo zilitoka sare ya bao 2 -2 na kuingia kwenye mkwaju wa penalti ambapo timu ya kawe iliibuka na ushindi wa mabao 7 -6  
Katika michuano hiyo iliyodumu kwa muda wa wiki nzima na kushirikisha timu nane kutoka katika mkoa wa kipolisi wa kinondoni timu ya  mikocheni  Iliibuka kuwa mshindi wa tatu wa michuano hiyo.

Mgeni rasmi Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh. Pereira Silima alisema” tunawashukuru waandalizi wa michuano hii na wadhamini ambao ni Airtel, Mr price, home shoping center na Rotary Club Dar es Saalam kwa ushirikiano wao mkubwa na mchangao wao katika kuhakikiksha mashindano haya yanafanyika kwa mafanikio.  Hii nijitahada ya pekee kuunganisha michezo na elimu ya usalama barabarani. Tumegundua vipaji vingi hapa tunawaasa wachezaji hawa wajiendeleze mbali na kuendesha  pikipiki kwa muda wa ziada wataweza kucheza mpira na kupata njia nyingine ya kipato kwa michezo ni ajira.

Naye Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga amewashukuru washiriki wote wa michuano hii na kusisitiza  wananchi na watanzania kwa ujumla kutii sheria bila shurutishi.

Akiongea kwa niaba ya wadhamini Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde alisema” mashindano haya yamekuwa ya mvuto mkubwa kwa washiriki na wadau wa michezo zaidi tumeshuhudia jinsi mafunzo ya elimu ya usalama barabarani yalivyoendesha na kuelimisha watumiaji wa barabara waliokuwa wakihudhuria hapa. 

Tunaamini kuendelea na  juhudi hizi tutaweza kupunguza idadi za ajali barabarani. Airtel tunaahidi kuendelea kushirikiana na jeshi la  polisi  usalama barabarani katika shughuli mbalimbali za uelimishaji umma juu ya sheria za barabarani

Michuano ya mpinga cup kwa wilaya ya kinondoni imefika tamati hapo jana na mpango ni kuwa na michuano hii pia katika mkoa wa ilala na temeke na kisha kuendelea na michuano hii nchini nzima.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.