Saturday, August 17, 2024
ALI KAMWE "HALI HII CHAMA ANAFUNGA NA KU-ASISTI LAKINI BADO ANASIKITIKA"
NA ALBERT G.SENGO
MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wametanguliza mguu mmoja hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Vital'O ya Burundi katika mchezo wa kwanza Raundi ya Awali jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga leo yamefungwa na mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya sita, kiungo Clatous Chotta Chama dakika ya 68, msambuliaji mzawa, Clement Francis Mzize dakika ya 74 na kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki kwa penalti dakika ya 90'+1. Timu hizo zitarudiana Jumamosi ya Agosti 24 Uwanja wa Benjamn Mkapa, Dar es Salaam – na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati Sports Club Villa ya Uganda na Commercial Bank ya Ethiopia.
Friday, August 16, 2024
TAKUKURU MWANZA YAOKOA ZAIDI YA MILIONI 290 KATIKA KODI
NA ALBERT G. SENGO/ MWANZA
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza James Ruge amesema,Taasisi hiyo kupitia kazi ya Uchambuzi wa mfumo wa ukataji na uwasilishaji wa kodi ya zuio imewezesha zaidi ya shilingi milioni mia mbili kukusanywa na Halmashauri za Mkoa wa Mwanza na kuwasilishwa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA ) ikiwa ni makusanyo ya kodi ya zuio kazi hiyo ilifanyika kwa lengo la kuboresha na kuimarisha matumizi ya stakabadhi na EFD na ukataji wa kodi ya zuio kwenye manunuzi ya vifaa na huduma katika Halmashauri za Mkoa wa Mwanza ili kuwezesha Serikali Kuu kukusanya mapato yake. "Mpaka wakati huu tunawasilisha ripoti yetu mbele ya waandishi wa habari TAKUKURU Mwanza imefuatilia utekelezaji miradi 17 ya maendeleo ya thamani ya zaidi ya Bilioni 6 na nusu, miradi 7 ya thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 2imekutwa na mapungufu na kwa miradi yenye mapungufu madogo madogo maboresho yamefanyika vilevile miradi iliyobainika kuwa na mapungufu makubwa uchunguzi umeanzishwa" amesema Mkuu huyo wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza.UGANDA YAANZA KUSAFIRISHA MAFUTA KUPITIA BANDARI YA DAR ES SALAAM
Shirika la Mafuta la Uganda (UNOC) limetangaza kuanza kutumia Bandari ya Dar es Salaam katika kupakia bidhaa hiyo kwa ajili ya kupeleka nchini kwao.
Awali UNOC ilikuwa ikitumia bandari ya Mombasa nchini Kenya katika kuchukua bidhaa hizo huku ikisafirisha kwa kutumia Shirika la Bomba la Kenya (KPC).
“Uganda imepanga kusafirisha takriban lita milioni 36 za mafuta kila mwezi (mizigo 1,028 ya lori) kupitia bandari ya Dar es salaam, “imeeleza taarifa hiyo ya UNOC iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Proscovia Nabbanja
Hata hivyo, UNOC imesema kiasi hicho kinatarajiwa kuongezeka kadri siku zinavyoenda.
“Kundi la kwanza la lita milioni 18 (malori 520 ya lori) za mafuta zilianza kupakiwa wiki hii jijini Dar es Salaam na litawasili Kampala siku zijazo,”imesema taarifa hiyo.
Thursday, August 15, 2024
KUELEKEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA TAKUKURU MKOA WA MWANZA YAWAPIGA MSASA WAANDISHI WA HABARI
NA ALBERT G. SENGO/ MWANZA
James Ruge ni Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Mwanza.TASAF MKOA WA PWANI KUCHELE YAVIWEZESHA MITAJI YA FEDHA VIKUNDI 1,309
NA VICTOR MASANGU,PWANI
Mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF) Mkoa wa Pwani imeweka mipango madhubuti ya kuendelea kuhakikisha kwamba inapunguza kwa kiasi kikubwa kiwango cha umaskini hapa nchini kwa kuwawezesha wananchi mbali mbali kuweza kupata mahitaji muhimu na kuboresha maisha ya kaya kwa mtu mmojammoja.
Hayo yamebainishwa na mratibu wa Tasaf Rose Kimaro wakati wa kikao maalumu cha mwaka utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini ambapo amesema kwamba lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanatoa fedha taslimu kwa kila kaya na kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii.
Mratibu huyo alibainisha kwmaba kwa sasa maeneo ya utekelezaji katikampango wao katika Mkoa wa Pwani yamegusa katika halmashauri zote tisa ambapo jumla ya kata zipatazzo 133,vijiji 417,na mitaa 73 hadi kufikia mwezi juni 2024 kaya zilizonufaika na mpango huo zilikuwa 18,403 zimehitimu ambapo kaya 17,761 zinaendelea kunufaika zikiwa ni kaya katika vijiji vipya kwa asilimia 30.
Kadhalika mratibu huyo aliongeza kwamba mpango huo unatekelezwa katika sehemu nne ambazo ni utoaji wa ruzuku za msingi na masharti pamoja na miradi ya muda (PWP) lingine ni kuweka akiba na kukuza uchumi wa kaya (LE).
Pia alifafanua kwamba jukumu lingine la Mkoa katika utekelezaji wa mpango huo ni kuhakikisha lengo la serikali la kupunguza kiwango cha umasikini linatimia kama inavyoelekezwa katika ilani ya chama cha mapinduzi ibara ya 25 (n).
Kadhalika alisema kwamba jukumu lingine ni kendelea kuboresha kasi ya utekelezaji ya awamu ya tatu ya Tasaf ilikuwafikia wananchi masikini katika vijiji pamoja na mitaa yote
kwa kutekeleza miradi ya kutoa fursa za ajira za muda, kukuza uchumi wa kaya na kuendeleza rasilimali watu.
Mratibu huyo akizungumzia katika upande wa mafanikio amesema kwamba Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amewapatia kiasi cha fedha zaidi ya bilioni 40 ambazo zimeweza kutumika katika kukuza uchumi wa kaya kwa ruzuku za elimu na afya ,ikiwa sambamba na upatikanaji wa chakula na uboreshaji wa miundombinu ya elimu afya, soko pamoja na ujuzi na stadi za maisha.
Pia alisema kwamba jumla ya miradi ya miundombinu ya afya,maji na elimu 13 yenye thamnai ya kiasi cha shilingi bilioni 2.2 imetekelezwa katika ngazi za Wilaya ambapo jumla ya miradi 6 tayari imeshaanza kutoa huduma pamoja na ajira za muda (PWP) zipatazo 647 yenyethamani ya shilingi bilioni 4.5.
Katika hatua nyingine alibainisha kamba hadi kufikia juni 2024 jumla ya wanufaika wapatao 15,740 sawa na kiwango cha asilimia 50 ya wanufaika 31,697 wameweza kujiunga na mfumo wa upokeaji wa ruzuku kwa njia ya mtandao (Simu banki) ambapo pia wanafunzi 96 wameweza kujiunga na vyuo vikuu wakiwemo wasichana 50 pamoja na wavulana 46.
MHE. RAIS DKT. SAMIA AKIWAAPISHA VIONGOZI WATEULE IKULU DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Viongozi Wateule Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 15 Agosti, 2024.
Sunday, August 11, 2024
MBUNGE KOKA KUANZISHA KLINIKI MAALUMU YA KUKUZA VIPAJI KWA WASANII
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka katika kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kukuza na kuibua vipaji vya wasanii wa fani mbali mbali ameweka mikakati kabambe kwa ajili ya kuanzisha kliniki maalumu ambayo itaweza kuwapa fursa vijana waweze kuonyesha vipaji walivyonavyo ili waweze kutambulika zaidi kutokana na kazi wanazozifanya.
Koka ameyasema hayo wakati wa semina elekezi ambayo imewakutanisha wasanii mbalimbali wa Halmashauri ya mji wa Kibaha kwa lengo la kuweza kukutana kwa pamoja ikiwa pamoja na kubadilishana mawazo na kupeana uwezo, ujuzi ,mahalifa na mbinu ambazo zitaweza kuwasaidia kufika mbali katika sanaa ambayo wanaifanya.
Koka alisema kwamba lengo lake kubwa ni kuona namna ya kuendelea kuwakutanisha kwa pamoja wasanii mbali mbali wa Jimbo lake na kuwaweka katika Kliniki ya pamoja ambayo itaweza kuwapa fursa ya kuonyeha uwezo na vipaji walivyonavyo.
“Nafahammu katika Jimbo langu kuna vijana wengi ambao wana vipaji vya aina mbali mbali kwa hivyo nitashirikiana bega kwa bega na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha katika kuanzisha Kliniki maalumu ambayo itaweza kuwapa fursa zaidi vijana kuweza kuonyesha uwezo ambao walionao na kikubwa zaidi lengo ni kuweza kuwafanya vijana wetu waweze kufika mbali zaidi,”alisema Koka.
Kadhalika Koka aliongeza kwamba mbali na kuanzisha Kliniki hiyo maalumu ya kukuza vipaji hivyo vya wasanii amewaahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha kwa kuwasaidia baadhi ya vifaa mbali mbali ambayo vitaweza kuwasaidia kuwa na studio yao ya kisasa ambayo itakuwa ni mkombozi katika kufanya kazi zao mbali mbali za mziki.
Kwa wake Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon amesema kwamba lengo lake kubwa ni kushirikiana bega kwa bega na wasanii wa Wilaya ya Kibaha kuwatengenezea mfumo mzuri ambao utawasaidia katika kuwatangaza zaidi ikiwa pamoja na kwenda nao katika vituo mbali mbali kwa ajili ya kuweza kufanya mahojiano.
Naye Mwenyekiti wa wasanii waigizaji Wilaya Jumanne Kambi amempongeza kwa dhati Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kwa maamuzi yake ya kuweza kuanzisha Kliniki hiyo ya wasanii ambayo itawasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza vipaji vyao.