ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 16, 2024

TAKUKURU MWANZA YAOKOA ZAIDI YA MILIONI 290 KATIKA KODI

 NA ALBERT G. SENGO/ MWANZA

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza James Ruge amesema,Taasisi hiyo kupitia kazi ya Uchambuzi wa mfumo wa ukataji na uwasilishaji wa kodi ya zuio imewezesha zaidi ya shilingi milioni mia mbili kukusanywa na Halmashauri za Mkoa wa Mwanza na kuwasilishwa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA ) ikiwa ni makusanyo ya kodi ya zuio kazi hiyo ilifanyika kwa lengo la kuboresha na kuimarisha matumizi ya stakabadhi na EFD na ukataji wa kodi ya zuio kwenye manunuzi ya vifaa na huduma katika Halmashauri za Mkoa wa Mwanza ili kuwezesha Serikali Kuu kukusanya mapato yake. "Mpaka wakati huu tunawasilisha ripoti yetu mbele ya waandishi wa habari TAKUKURU Mwanza imefuatilia utekelezaji miradi 17 ya maendeleo ya thamani ya zaidi ya Bilioni 6 na nusu, miradi 7 ya thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 2imekutwa na mapungufu na kwa miradi yenye mapungufu madogo madogo maboresho yamefanyika vilevile miradi iliyobainika kuwa na mapungufu makubwa uchunguzi umeanzishwa" amesema Mkuu huyo wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.