ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 1, 2012

MH. WAZIRI MKUU PINDA NDIYE MGENI RASMI SERENGETI MARATHON ITAKAYO TIMUA VUMBI DEC 11/2012

Taasisi ya Serengeti Sports Centre ya jimbo la Busega mkoani Simiyu imeandaa mashindano ya mbio za nyika yatakayotambulika kama Serengeti Marathon yanayotaraji kuanza kutimua vumbi mnamo tarehe 11/12/2012.

Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Kayanza Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa mashindano hayo ambayo si washiriki kutoka mkoa wa Simiyu pekee watashiriki, bali  pia Serengeti Marathon itashirikisha wafukuza upepo wa mikoa yote kwani tayari taarifa zimefika kwenye vilabu vya vyama vyote nchini vilevile balozi za nchi zote ukanda wa Maziwa Makuu na nchi zote za kimataifa zimepata mialiko, hivyo tutegemee kuona washiriki kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni.  

Bofya Play ili upate taarifa kamili, 


Zawadi kwa washindi wa michuano hiyo itakayoshirikisha makundi mawili yaliyotengwa kwa wanaume na wanawake wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea:

Washindi wa kwanza shilingi.....500,000/=
Washindi wa pili shilingi .............400,000/=
Washindi wa tatu shilingi............300,000/=
Washindi wa nne shilingi............200,000/=
Washindi wa tano shilingi...........100,000/=
Nao Washindi wa 6 hadi 10 kwa kila upande (wanawake na wanaume)  kuondoka na kifutajasho cha shilingi 20,000/= kila mmoja....

TANZANIA BARA YATINGA HATUA YA ROBO FAINALI KWA KISHINDOCECAFA LIVE;
SOMALIA vs TANZANIA BARA. 
Wakati timu hizo zinaingia mapumziko, Kilimanjaro Stars 5, Somalia 0. 
Ngasa akitupia 3 na John Boco zake 2.

Vijana wamecheza soka zuri la kuonana wakitawala mchezo kwa asilimia kubwa hata kuwatishia wahabeshi hao.

Picha lilionekana wazi kwamba kipindi cha pili magoli yataongezeka...
Yap yap, yooo... kipindi cha pili kikatinga timu zikazama dimbani, hadi dakika ya 58 magoli yale yale.

Mabadiliko ya; Boco nje, Edward Christropher ndani na Damayo nje, Chuji ndani yanafanyika ile hali Somalia walishamaliza sub toka kipindi cha kwanza. 

Dakika 90 za mchezo zinamalizika Somalia inalala 7-0 dhidi ya Tanzania bara, Khalfan Ngasa akiondoka na magoli matano.

SASA NI WAKATI WA KUANZISHA SHULE ZA MICHEZO - MH. LOWASSA

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (wa pili kushoto) akijumuika pamoja na Baadhi ya Wabunge wanaounda timu ya Bunge Sports inayoundwa na wabunge kutoka Baraza la Wawakilishi na Bunge la Jamhuri,wakati wa Chakula cha Mchana alichowaandalia Nyumbani kwake,Ngarashi Wilayani Monduli jana.Wengine pichani kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo,Mh. Amos Makalla,Mbunge wa Jimbo la Kinondoni,Mh. Iddi Azzan pamoja na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Monduli, Reuben ole Kunai.

Chakula cha Mchana mahala hapa.
Wakipata Chakula cha Mchana..na mazungumzo.
Wabunge wanaounda timu ya Bunge Sports inayoundwa na wabunge kutoka Baraza la Wawakilishi na Bunge la Jamhuri wakipata Chakula cha Mchana kilichoandaliwa na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa Nyumbani kwake, Ngarashi Wilayani Monduli jana.Mh. Lowassa alikutana na Wabunge hao ili kujadili maswala mbali mbali yahusuyo Michezo hapa nchin,wakati timu hiyo ikiwa Kambini jijini Arusha,kujiandaa kwenye Jijini Nairobi kwenye Mashindano ya Afrika Mashariki.


WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa amewashauri wabunge wa timu ya Bunge Sports kufikiri juu ya kutunga sera ya michezo itakayoruhusu kuanzishwa kwa Shule za Michezo (Sports Academy) hapa nchini.

Lowassa ameyasema hayo jana,baada ya kuialika nyumbani kwake timu hiyo iliyopiga kambi ya jijini Arusha tayari kwa mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki jijini Nairobi.

“Nilisikitika kweli Timu ya Taifa ya Kilimanjaro Stars ilipofungwa na Burundi kwenye mchezo wa pili wa Mashindano ya CECAFA huni Uganda, pamoja na juhudi za Rais Jakaya Kikwete kuleta makocha bado tumefungwa na Burundi iliyotoka kwenye vita juzi!.

“Nyinyi ni watunga Sera, ni wachezaji mnajua changamoto zinazofanya tusifike juu, umefika wakati wa kuwa na Shule za Michezo zinazotambuliwa na Sera zetu.

“Mpira ni chakula cha Watanzania, wanapenda mpira sana. Napendekeza baada ya kurejea anzeni kufikiria juu ya kutunga Sera ya kuwa na Shule za Michezo. Kipingu amejitahidi kuwa na kitu kama hiki lakini amebakia peke yake hakuna anayemuunga mkono,” alisema Lowassa.

Alisema kuwapo kwa Timu ya Bunge Sports kutasaidia kufikiria juu ya mafanikio ya mchezo wa mpira wa miguu, pete na michezo mingine.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Amos Makalla aliyeongozana na timu hiyo alimwambia Mh. Lowassa kwamba serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha Sera za michezo.

“Sera na sheria za sasa za michezo kweli haziendani kabisa na wakat,zote ni za zamani. Serikali imejipanga kuzifanyia kazi.

“Changamoto uliyoitoa ya kuanzisha Shule za Michezo na kuendeleza michezo nchini tunaipokea na tutaifanyia kazi.

“Nilipoteuliwa kuwa Naibu Waziri kwenye Wizara hii niliwaambia watu na binafsi namshukuru Rais Kikwete, kwamba upele ulipata mkunaji kwani mimi ni mwanamichezo na uwanjani ni kiungo mchezeshaji,” alisema Makala.

Naye Mwenyekiti wa Timu hiyo ya Bunge Sports inayoundwa na wabunge kutoka Baraza la Wawakilishi na Bunge la Jamhuri, Iddi Azan alimshukuru Mh. Lowassa kwa mawazo yake na kuahidi kuyafanyia kazi.

“Kwanza tunaahidi ushindi kwa nchi, Bunge letu na haya uliyoyasema tunaahidi kuendelea kuyafanyia kazi kwani tunatambua sheria na Sera za michezo zimepitwa na wakati,” alisema Azan.

Timu hiyo ya Bunge Sports ilikuwa na wachezaji wake wote waliopo kwenye kambi jijini Arusha wanaounda timu ya Mpira wa miguu na Pete.

BREAKING NEWS: MENGI ASHINDWA KESI YAKE NA SARAH HERMITAGE NA KUAMULIWA KUMLIPA 1.2 million £


Press Release
 Date:  30 November 2012
Sarah Hermitage Libel Defence Upheld

 Silverdale Farm Blog Justified
At the High Court in London today, Mr Justice Bean delivered Judgment in favour of Sarah Hermitage, who had been sued for libel by the wealthy Tanzanian businessman, Reginald Mengi, the Executive Chairman of IPP Ltd, a company which holds major newspaper and broadcasting interests in Tanzania.

Reginald Mengi sued in respect of five postings on Sarah Hermitage’s Silverdale Farm blog and two emails she had sent, which Mr Mengi claimed to be false and defamatory of him. 

During the trial, the Court heard unchallenged evidence from Sarah Hermitage and her husband, Stewart Middleton, as to how they were by threats, intimidation and corruption driven from Tanzania and forced to abandon the investment they had made in their farm, Silverdale, of which Reginald Mengi’s younger brother, Benjamin, then took possession.  The Court was told that a major factor in the ordeal they suffered was the hostile and defamatory coverage their case received from the IPP-owned English language Guardian and the Swahili Nipashe newspapers.  Reginald Mengi, in the course of his evidence, repeatedly stated that he“was not responsible, not accountable and not answerable” for the editorial content of IPP publications.

In giving Judgment, Mr Justice Bean ruled:
I find that the campaign in the Guardian and Nipashe facilitated Benjamin’s corruption of local officials and intimidation of the Middletons and thus helped Benjamin to destroy their investments and grab their properties; and that Mr [Reginald] Mengi, since he either encouraged or knowingly permitted the campaign, was in that sense complicit in Benjamin’s corruption and intimidation.  The allegation is thus substantially true, and justified at common law.

Following the handing down of the Judgment, Sarah Hermitage said today:
I set up my Silverdale Farm blog in 2009 to document our horrific experience in Tanzania, and to expose as a warning for others the corruption we encountered and our helplessness with no protection from the local Courts and officials.  As the Judge has found, my response to the campaign waged against us in IPP publications was reasonable, proportionate, relevant and without malice. To find myself then sued for libel in my own country, facing a claim of  legal costs of £300,000 from Mr Mengi before the proceedings had even started, was itself frightening and oppressive.  

I am relieved that, with the support of my legal team who were prepared to risk getting paid nothing at all under a “no win, no fee” agreement, justice has in the end prevailed in this case. I also must thank the brave and honest Tanzanian journalists who either openly or privately assisted in the preparation of our defence. I will continue to use my blog, my voice, to do all I can to fight against the corruption I have seen first hand in Tanzania, not least in the hope that it may in the end help the very good people, not least our loyal staff, who have stood by us throughout.

After handing down judgment Mr Justice Bean ordered that Reginald Mengi should pay the defence costs at the higher “indemnity” rate. In reaching this decision, the factors cited by the Judge included that Counsel for Sarah Hermitage had “rightly described the litigation as “oppressive”, that “enormous costs had been thrown at the case from the beginning, indeed before the issue of proceedings” and that the evidence of the Claimant and his witnesses had in a number of respects been “misleading and untrue.”


Mr Justice Bean ordered that Reginald Mengi should pay £1.2million on account of Sarah Hermitage’s legal costs, which will be subject to detailed assessment by the court in due course.

D-Malick - Mama mwenye Nyumba [Official Video].


Eyooo...Chekshia mzigo mpya wa kiooni wa mtoto wa nyumbani home sweet home 'Rock City' Mwanza-Mwanza..

Friday, November 30, 2012

MBUNGE WENJE AINGIA MATATANI NA SHIRIKA LA UMOJA WA MACHINGA MWANZA LA MURUKA JUU YA KAULI YAKE YAMPA SIKU 14 KUKANUSHA.


SHIRIKA la Umoja wa Machinga Jijini Mwanza (SHIUMA) leo limetoa tamko la kumpinga Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Bw.Ezekial Wenje kutumia jina la umoja huo kupotoshwa umma na wananchi kwa madai kuwa wamemuandikia tamko la Barua na kumpatia siku 14 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mhe.Mizengo Pinda za kumtaka amwondoshe Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Bw. Wilson Kabwe.
 Mh. Wenje alisoma tamko alilodai kuwa linatoka Kwa umoja huo wa Wamachinga kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa Sahara Jumanne ya wiki hili Jijini Mwanza.

 Akizungumza na vyombo vya habari leo Mwenyekiti wa Shirika la SHIUMA Bw.Ernest Matondo sehemu ya taarifa yake iliyosainiwa na viongozi wenzake imesema kuwa SHIUMA imesikitishwa na kufedheheshwa na taarifa iliyotolewa na Mbunge Bw. Wenje na kurushwa na baadhi ya vyombo vya habari wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara kwa kusoma barua hiyo siku ya Novemba 28 mwaka huu akiitaja kuwa ni ya uongo iliyolenga kuleta uchonganishi kati ya SHIUMA, Serikali, Machinga na Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikiwemo wakazi wa Jiji hilo 

Aidha Shirika hilo limelaani vikali kitendo cha Mbunge huyo kutumia Jukwaa la Kisiasa kutoa taarifa ya uongo kwa wananchi hali akitambua kuwa SHIUMA si Chama cha Kisiasa na hakuwa na mazungumzo yoyote na Uongozi mzima kwa kipindi hicho ambacho alitoa kauli hiyo katika mkutano wake wa hadhara.

 SHIUMA imepiga marufuku kwa mtu yoyote ama kikundi cha watu au wanasiasa kutumia SHIUMA kama daraja la kujiongezea umaarufu wa kisiasa kwa umma na mara nyingi wanasiasa wa aina hii wamekuwa ndio chanzo cha mpasuko na mgawanyiko kwa wamachinga kwa kuwa kauli zao ni ndumilakuwili zilizojaa chuki,husuda na tama za madaraka ikiwemo kujitafutia umaarufu wa kisiasa.

Bw.Matondo amewataka wamachinga na wanachama kuendelea na shughuli zao halali na kujiepusha na lugha za wanasiasa wa aina hiyo na badala yake wafuate sheria zilizopo ili kuepusha vurugu na ugomvi na halmashauri ya jiji na kuwaomba machinga wenzetu kuendelea kufanya biashara katika maeneo yaliyoruhusiwa na jiji na tushiriki katika suala la utunzaji mazingira katika maeneo hayo.

Sikiliza kauliya mwenyekiti wa walezi wa wamachinga kwa Kubofya play....


POLE BROTHER EDGAR MAPANDE KWA KUFIWA NA BIBI MZAA BABA, MAZISHI KUFANYIKA JUMAPILI MAMBA WILAYA YA SAME MKOANI KILIMANJARO


Leo kuanzia majira ya saa 7:30 mchana hadi saa 8 mwili wa Bibi Eva E. Mapande umeagwa nyumbani kwa mwanae eneo la Nyakato jijini Mwanza ambapo pia ibada maalum kumwombea marehemu ilifanyika kabla ya kusafirishwa kuelekea Mamba wilayani Same mkoani Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa risala iliyosomwa na Edgar Mapande ambaye ni mjukuu wa marehemu bibi Eva E. Mapande alizaliwa mnamo mwaka 1920 na kufariki dunia tarehe 28 nov 2012, katika zama za mwisho marehemu pamoja na uzee alikuwa akisumbuliwa na macho hali iliyomsababisha kushindwa kuona kabisa hadi mauti inamchukuwa.


Mchungaji wa kanisa la Sabato akiendesha ibada kabla ya heshima za mwisho kwa marehemu kutolewa.


Sehemu tu ya watoto wa marehemu kwenye ibada hiyo iliyofanyika nyumbani.


Mr. Hamza akiongoza hatua ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu.


Majonzi yametawala  katika kuuaga mwili wa marehemu bibi Eva E. Mapande.


Majirani, ndugu jamaa na marafiki wameshiriki ibada hii ya kuuaga mwili wa marehemu bibi Eva E. Mapande


Ibada hii ya kuuaga mwili wa marehemu bibi Eva E. Mapande imehudhuriwa pia na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Mwanza, Sixbeth Reuben.


Ibada ya kuuaga mwili wa marehemu ikiendelea.


Ndugu na marafiki wameshirikiana pamoja kupeana moyo.
Marafiki na ndugu eneo la tukio.


Jipe moyo.


Mara baada ya kukamilika kwa ibada maalum kumwombea marehemu ilifanyika Nyakato jijini Mwanza, safari ikawekwa sawa kuelekea Mamba wilayani Same mkoani Kilimanjaro kwaajili ya mazishi yatakayofanyika jumapili hii ya kesho kutwa.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

AIRTEL TANZANIA TAANDAA PART YA KUMPONGEZA BALOZI WAKE AMBWENE YESAYA "AY" NYUMBANI LOUNGE LEO..

Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde na Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava) kwa pamoja wakionyesha tuzo ya  Channel O  aliyoipata Mwanamuzi huyo nchini Afrika Kusini. Tukio hilo limefanyika leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo Airtel imempongeza AY kwa ushindi alioupa pamoja na kumwandalia sherehe ya kumpongeza itakayofanyika leo usiku nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam 


Afisa Uhusiano wa Airtel akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo Airtel imempongeza AY balozi wake kwa kupata tuzo ya chanel O ya video bora, Katikati ni AY  akifatiwa na DJ wake Athur Baraka

Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava)  na Balozi wa Ambwene Yessaya 'AY'

Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava)  na Balozi wa Ambwene Yessaya 'AY' akiwashukuru watanzania kwa kumpigia kura na kumwezesha kupata tuzo hiyo kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde na kushoto ni  DJ wake Athur Baraka

Airtel Tanzania yaanda Part ya kumpongeza  Balozi wake AY Nyumbani Lounge

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakiwa na balozi wake Ambwene Yessaya “AY” leo wamewashukuru watanzania kwa kumpigia kura msaani maarufu wa kizazi kipya Ambwene Yessaya  “ AY “  na kumwezesha kuibuka mshindi wa tuzo ya kwanza katika kipengele cha Most Gifted East African video of the Year kupitia kibao chake kipya kijulikanacho kama “   I don’t wanna be alone”
Akiongea na wandishi wa habari katika Ofisi za Airtel leo AY amechukua fulsa kuwashukuru watanzania kwa kumpigia kura na kuweza kumwezesha kuibuka na ushindi. Aidha alivishukuru vyombo vya habari kwa kuendelea kushirikiana naye katika kufikisha habari na kumsaidia kupata tuzo hiyo.
Naye Afisa uhusino wa Airtel Jane Matinde alisema” tunafurahi kuona msanii AY ambaye ni balozi wetu kuibuka na tuzo iliyoshirikisha wasanii mbalimbali toka  Afrika, sisi tunasikia furaha kuona mafanikio ya wasanii wetu nchini yakiendelea kukua na ndio sababu leo tuko hapa kusherehekea ushindi  huu kwa pamoja na kuwashukuru watanzania kwa kumuwezesha AY kupata tuzo hii kwa kura zenu.
Tunapenda pia kuchukua fulsa hii kuwaalika watanzani na wateja wetu leo pale nyumbani lounge usiku kuanzi saa tatu tuweze kujumuika na AY na kumpongeza kupata tuzo hii. Tutakuwa na wasanii wengi pamoja na wadau mbalimbali wa Musiki na pia utapata muda kupiga picha na msanii huyo na Tuzo yake.

KAMPUNI YA WELLNESS TANZANIA YAENDESHA SEMINA JUU YA USTAWI WA MWAJIRIWA JIJINI DAR

Mtaalamu wa Ustawi wa mwajiriwa Bw. Doug Bramsem akitoa somo katika semina juu ya Ustawi wa Mwajiriwa iliyofanyika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam. Semina hiyo ilikuwa na lengo la kuwawezesha washiriki kujua nini maana ya Ustawi wa Mwajiriwa, jinsi ya kuendesha kampuni na kupata faida na kujua historia ya Ustawi wa Mwajiriwa nchini Tanzania na kumjenga mfanyakaziwako kuwa bora na kutatua ustawi wake katika kampuni zao

Mtaalamu wa Ustawi wa mwajiriwa Bw. Doug Bramsem akikazia neno.
Washiriki wakifuatilia semina.

Mtaalamu wa magonjwa ya akili kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha magonjwa ya akili, Prof. Gad Kilonzo akizungumzia Ustawi wa Mwajiriwa.

Mtaalamu wa mambo ya Saikolojia, Bi. Lisa Finke kutoka GIZ akitoa somo katika semina hiyo.
Mtaalamu wa Ustawi wa mwajiriwa, Dkt. Hilde Basstanie kutoka GIN akitoa somo la ugonjwa wa Ukimwi jinsi ya kujilinda makazini.
 Washikiri wakifuatilia kwa makini semina hiyo.

Mmoja ya washiriki wa semina hiyo, Bw. James Lwanga kutoka hospitali ya Kadic iliyopo Bukoto, Uganda akielezea mambo mbali mbali yanayofanyika katika jamii nchini kwao.

 Washiriki wakifuatilia kwa makini semina.

Washiriki wakiwa makini kupata somo.
Mtaalamu wa Ustawi wa mwajiriwa,  Dkt. Hilde Basstanie (kwanza kulia) kutoka GIN akiwa na washiriki wengine wakifuatilia kwa makini.
  
Washiriki wakiwa makini kupata somo.

Thursday, November 29, 2012

DAKIKA 90 ZIMEISHA ZANZIBAR 2-1 DHIDI YA RWANDA.

Zanzibar humbled Rwanda 2-1 as last year's runners-up suffered their first defeat of the 2012 Cecafa Senior Challenge Cup in the Ugandan capital Kampala.
Wakicheza kwenye dimba lenye pitch za kutereza mara baada ya mvua kubwa kunyesha, timu ya Zanzibar walionekana kuchukulia poa na wakiwa fresh zaidi juu ya hali hiyo ya hewa na walihitaji dakika nane tu kuzungumza na nyavu za wana wa Amavubi kwani makosa ya golikipa Jean Claude Ndoli yalimzawadia Khamis Mcha Khamis kuipa Zanzibar bao la kwanza la uzinduzi kuelekea ushindi.
Khamis grabbed his second when finishing off Kassim Sulyeman's curving pass as a Rwanda side that had poured on the pressure suffered from a communication lapse in defence.
Late on, Dady Birori pulled one back for Rwanda with a well-taken header from a Haruna Niyonzima cross but it was too little too late.

After two rounds of matches, Zanzibar are unexpected Group C leaders with four points, while second-place Rwanda boast three - the same asMalawi, who narrowly beat Eritrea 3-2 earlier in the day.
"My boys failed to master how to play on a wet pitch and also made some terrible mistakes," said Rwanda's Serb coach Sredejovic Micho. "But we shall fight back in our last group game."
Meanwhile, Zanzibar coach Salum Nassor was an understandably delighted man after the encounter.
"Beating Rwanda has always proved difficult for us, but we have done it today," he said.
Zanzibar's victory throws the group open but Malawi know they will qualify for certain with victory in their final group game against the islanders on Monday.
Kinnah Phiri is a man under pressure after Malawi minister of sports Enock Chihana warned that the Flames coach faces the axe should he fail to reach the quarter-finals.
"We have given them enough time to prepare and this is the tournament where they have to show that indeed they can do something," he said.
"In other matches they had excuses which we could understand but not Cecafa.
"If they qualify for the quarter-finals, it's completely a different matter. If they don't, it means my ministry, the council for sports and Football Association will sit down and make a decision," Chihana added.
Malawi beat Eritrea thanks to a brace from Chiukepo Msowoya and a strike from Miciam Mhone, with the hungry Eritreans piling on late pressure through Yosief Ghide and a Hermon Tecleab penalty.
"I am very bitter with my players for giving the opponents space to score such goals," Phiri said afterwards. "This is a game we should have won comfortably, but we ended up struggling."


BI ANASTAZIA ANATAKIWA KUKATWA MGUU WAKE WA KUSHOTO


Natumia nafasi hii kuwashukuru  Watanzania wote walioguswa na Ugonjwa  wa Bi Annastazia ambaye amekuwa akisumbuliwa na Kuvimba kwa Mguu wake wa Kushoto,kuna watu mbalimbali ambao walipiga simu wakielezea kuguswa na hali hiyo lakini wapo wengine walioenda mbali zaidi na kutoa pesa kidogo ambazo zitaweza kumsaidia  Bi Annastazia.

Mpaka sasa tayri kuna watanzania wawili ambao wametoa fedha  ambazo kwanjia moja zitamsaidia Bi Annastazia,kwa vile nilitumia mtandao huu kuwaomba wamsaidie pia napenda kutumia mtandao huu kutoa shukrani lakini pia kuwaomba wengine ambao hawajafanya hivyo kumsaidia Bi Annastazia. 

Waliotoa ni pamoja na
1.       Mama Abduweli wa Mamlaka ya Bandari Dar es Salaama - Sh 10,000.00
2.       2. Dada Edna Lwanji  kutoka nchini Uingereza -                  Sh 137,555.30

Pamoja na kupokea fedha hizo leo nimeongea na mama yake Annastazia na kusema kuwa Mtoto wake anatakiwa kupelekwa jijini Mwanza kwaajili ya kukatwa mguu huo kutokana na vpimo vilivyopatikana baada ya kupigwa X ray.

Hivyo basi watanzania tuendelee kumsaidia Annastazia kwani Mpaka sasa Mama yake hana fedha na hana msaada wowote kwani ni Mjane ,kama utahitaji kumsaidia Bi Annastazia kutuma kwa M Pesa katika namba  0756 035 825

www.mwanawaafrika.blogspot.com

MTOTO ALIYEZALIWA KIBOFU CHA MKOJO KIKIWA NJE AOMBA WASAMALIA WEMA KUMCHANGIA AKAPATIWE MATIBABU NCHINI INDIA.

 DICKSON VEDASTUS WASIWASI ALIZALIWA 7/07/1996 KATIKA HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO MWANZA, KIBOFU CHA MKOJO KIKIWA NJE (KIKIONEKANA WAZIWAZI), MADAKTARI WAMEMFANYIA MATIBABU KUPITIA OPARESHENI MARA TATU BILA MAFANIKIO.

OPARESHENI YA KWANZA ILIFANYIWA AKIWA NA MIEZI MIWILI, OPERESHENI YA PILI IKAFUATIA NA YA TATU IKAFANYIKA MWAKA 2000 HAPO HAPO HOSPITALI YA BUGANDO, LAKINI KWA BAHATI MBAYA ZOTE HAZIKUZAA MATUNDA.


KWA MUJIBU WA MZAZI WA KIJANA DICKSON, BW. VEDASTUS WASIWASI AMBAYE NI MKAZI WA MTAA WA SONGAMBELE, MAGOMENI KIRUMBA KATIKA  JIJINI MWANZA AMESEMA KUWA ALIPEWA USHAURI NA MADAKTARI WA HOSPITALI HIYO KUMPELEKA NCHINI INDIA KWA MATIBABU ZAIDI.

GHARAMA ZA MATIBABU NI SHILINGI MILIONI 20, NAYE HANA UWEZO HIVYO AMEOMBA WASAMALIA WEMA KUMSAIDIA KUNUSURU ADHA NA MATESO AYAPATAYO MTOTO WAKE.

 CHANGIA KUPITIA AKAUNTI ZIFUATAZO:-
CRDB     0152457709500
AZANIA 003003005102370001

SIMU 0762324527 OR 0683580004

 LEO tulipata fursa ya kuzungumza na mzazi wa mtoto anayehitaji upasuaji (Dickson) Bw. Vedastus Wasiwasi kujua usumbufu na adha aipatayo mtoto naye kwa ufupi alikuwa na haya ya kuongea.. Bofya play.