ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 30, 2012

MBUNGE WENJE AINGIA MATATANI NA SHIRIKA LA UMOJA WA MACHINGA MWANZA LA MURUKA JUU YA KAULI YAKE YAMPA SIKU 14 KUKANUSHA.


SHIRIKA la Umoja wa Machinga Jijini Mwanza (SHIUMA) leo limetoa tamko la kumpinga Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Bw.Ezekial Wenje kutumia jina la umoja huo kupotoshwa umma na wananchi kwa madai kuwa wamemuandikia tamko la Barua na kumpatia siku 14 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mhe.Mizengo Pinda za kumtaka amwondoshe Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Bw. Wilson Kabwe.
 Mh. Wenje alisoma tamko alilodai kuwa linatoka Kwa umoja huo wa Wamachinga kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa Sahara Jumanne ya wiki hili Jijini Mwanza.

 Akizungumza na vyombo vya habari leo Mwenyekiti wa Shirika la SHIUMA Bw.Ernest Matondo sehemu ya taarifa yake iliyosainiwa na viongozi wenzake imesema kuwa SHIUMA imesikitishwa na kufedheheshwa na taarifa iliyotolewa na Mbunge Bw. Wenje na kurushwa na baadhi ya vyombo vya habari wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara kwa kusoma barua hiyo siku ya Novemba 28 mwaka huu akiitaja kuwa ni ya uongo iliyolenga kuleta uchonganishi kati ya SHIUMA, Serikali, Machinga na Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikiwemo wakazi wa Jiji hilo 

Aidha Shirika hilo limelaani vikali kitendo cha Mbunge huyo kutumia Jukwaa la Kisiasa kutoa taarifa ya uongo kwa wananchi hali akitambua kuwa SHIUMA si Chama cha Kisiasa na hakuwa na mazungumzo yoyote na Uongozi mzima kwa kipindi hicho ambacho alitoa kauli hiyo katika mkutano wake wa hadhara.

 SHIUMA imepiga marufuku kwa mtu yoyote ama kikundi cha watu au wanasiasa kutumia SHIUMA kama daraja la kujiongezea umaarufu wa kisiasa kwa umma na mara nyingi wanasiasa wa aina hii wamekuwa ndio chanzo cha mpasuko na mgawanyiko kwa wamachinga kwa kuwa kauli zao ni ndumilakuwili zilizojaa chuki,husuda na tama za madaraka ikiwemo kujitafutia umaarufu wa kisiasa.

Bw.Matondo amewataka wamachinga na wanachama kuendelea na shughuli zao halali na kujiepusha na lugha za wanasiasa wa aina hiyo na badala yake wafuate sheria zilizopo ili kuepusha vurugu na ugomvi na halmashauri ya jiji na kuwaomba machinga wenzetu kuendelea kufanya biashara katika maeneo yaliyoruhusiwa na jiji na tushiriki katika suala la utunzaji mazingira katika maeneo hayo.

Sikiliza kauliya mwenyekiti wa walezi wa wamachinga kwa Kubofya play....


Tupe maoni yako

2 comments:

  1. Wenje cku zote utafuta umaarufu kwa kutumia machinga nashukuru kwa kuling'amua hilo

    ReplyDelete
  2. Tulianza vizuri lakini huyu jamaa ametuvuruga sana, kwa upande wa mz tuko mbioni kupoteza wenye hekima chamani kwasababu ya papara zake

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.