Saturday, June 25, 2011
HABARI
Mwanamke wa kwanza kushtakiwa kwenye mahakama ya kimataifa kufuatia mauaji ya kimbari nchini Rwanda amehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Waziri huyo wa zamani wa masuala ya Familia, Pauline Nyiramasuhuko, amepatikana na hatia ya kupanga mauaji hayo na kuratibu ubakaji wa wanawake na wasichana wakati wa mauaji yaliotokea mwaka 1994.
Bi Nyiramasuhuko mwenye umri wa miaka 65, alifika katika mahakama ya uhalifu wa kivita nchini Rwanda (ICTR), ilioko mjini Arusha Tanzania leo.
Waziri huyo wa zamani na mtoto wake wa kiume Arsene Shalom Ntahobali, walikuwa wanakabiliwa na mashtaka kumi na moja, yakiwemo mauaji, ubakaji na kuwatesa watutsi na wahutu wenye msimamo wa wastani. Mashtaka ya dhidi yake kuhusu ubakaji yalikubalika kwa kuwa korti iliridhika kuwa alijua wasaidizi wake walikuwa wanafanya vitendo hivyo lakini hakuchukua hatua kuwazuia.
Mahakama hiyo imeambiwa kuwa waziri huyo wa zamani na familia yake alishiriki kuunda vikundi vya wanamgambo waliotekeleza mauaji hayo. Mahakama hiyo ilielezewa kuwa alihusika na mauaji yaliotokea maeneo ya kusini mwa jimbo la Butare.
Mahakama ya ICTR ilibuniwa mwaka wa 1994 kufuatia mauaji hayo ya kimbari ambapo inakadiriwa kuwa watu 800,000 waliuawa.
Shughuli ndiyo hivyoo imeiva na wageni mbalimbali sambamba na washereheshaji wanazidi kumiminika jijini Mwanza pichani mkali wa hip hop bongo Mwanafalsafa akitinga Mwanza tayari kwa Show ya Serengeti Fiesta itakayo fanyika jumapili hii kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, Nasi tukitinga kwa kiingilio cha shilingi 5,000 tu.
Chiddy Benz nae huyoo akiwa na mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho Clouds Fm Lovenes love.
Mwana hip-hop Prof J nae ameonekana akiwa mwenye furaha mara baada ya kutua uwanja wa ndege Mwanza kutokea jijini Dar es salaam kwaajili ya shughuli za Fiesta.
Sakafu ya jukwaa.
Wasanii wengine wanaotarajiwa kuperform siku hiyo ni pamoja na Mataluma, Barnaba, Linah, Godzillah, Sajna, Diamond, Recho, Makomandoo, Chriss Wamalya, Fid Q na mkali wa muziki wa Dancehall, Ragga & Reggae - Shaggy.
NB: Kuanzia saa sita kamili mchana kila nusu saa droo itachezeshwa na mshindi kujinyakulia kitita cha shilingi laki tano taslimu, zoezi hilo la zawadi litadumu hadi itakapotimu saa nane mchana "CHANGAMKIA MZIGO HUO MWANAWANE"
Thursday, June 23, 2011
FIESTA
Hatimaye Zawadi za washindi wa Vodacom Miss Mwanza 2011, zimetangazwa leo katika ukumbi wa Hoteli mpya ya Gold Crest iliyopo katikati ya jiji la Mwanza. Akitangaza zawadi hizo Katibu wa Sisi Entertainment Mukhsin Mambo maarufu Mc Stopper ameeleza, kifuta jasho kwa washiriki nafasi ya sita hadi ya kumi na nne watapata Tsh. 100,000/=
Nafasi ya Tano- 200,000/= Nafasi ya Nne- 200,000/= nafasi ya Tatu- 300,000/= Nafasi ya Pili- 500,000/= na Vodacom Miss Mwanza 2011- 1,000,000/=
Matembezi na elimu ya Vodacom.
Wakipata maelezo Idara kwa idara..
Hii ni kwa mara ya kwanza kwa Miss Mwanza kuzawadiwa donge nono la Tshs. 1,000,000/=
Mara baada ya warembo hao kupata fursa ya kutembelea ofisi za Vodacom Mwanza kushuhudia shughuli zinazofanywa katika ofisi hizo walipiga picha ya pamoja nje ya ofisi za Vodacom Mwanza.
(Msanii kutoka nchini Zimbabwe, Oliver 'Tuku' Mtukudzi akiwa katika picha ya pamoja na mlogishaji, Cathbert Angelo).
Msanii nguli barani afrika anayetokea nchini Zimbabwe Oliver 'Tuku' Mtukudzi anatarajia kuachia albamu yake ya 56 ifikapo mwezi wa saba.
Akizungumza na blog hii alipokuwa ametembelea nchini kwa ajili ya ufunguzi wa tamasha la Zanzibar filamu lijulikanalo kama 'ZIFF' lililozinduliwa June 18, na kuendelea mpaka tarehe June 24, 2011, msanii huyo alisema kuwa mpaka sasa anaalbamu zipatazo 55.
'Nimeshatoa albamu zipatazo 55 na zote zipo sokoni na zinafanya vizuri japo sikumbuki nyimbo zake zote, albamu ambazo ninazo mpaka sasa ni 1978 Ndipeiwo Zano (re-released 2000), 1979 Chokwadi Chichabuda, 1979 Muroi Ndiani?, 1980 Africa (re-released 2000), 1981 Shanje, 1981 Pfambi, 1982 Maungira, 1982 Please Ndapota, 1983 Nzara, 1983 Oliver's Greatest Hits, 1984 Hwema Handirase, 1985 Mhaka, 1986 Gona. Nyingine ni 1986 Zvauya Sei?, 1987 Wawona, 1988 Nyanga Yenzou, 1988 Strange, Isn't It?, 1988 Sugar Pie, 1989 Grandpa Story, 1990 Chikonzi, 1990 Pss Pss Hallo!, 1990 Shoko, 1991 Mutorwa, 1992 , 1992 Rumbidzai Jehova, 1992 Neria Soundtrack, 1993 Son of Africa, 1994 Ziwere MuKobenhavn, 1995 Was My Child, 1996 Svovi yangu.
Aliongeza albamu nyingine ni 1995 The Other Side: Live in Switzerland, 1997 Ndega Zvangu (re-released 2001), 1998 Dzangu Dziye, 1999 Tuku Music, 2000 Paivepo, 2001 Neria, 2001 Bvuma (Tolerance), 2002 Shanda soundtrack, 2002 Vhunze Moto, 2003 Shanda (Alula Records), 2003 Tsivo (Revenge), 2004 Greatest Hits Tuku Years, 2004 Mtukudzi Collection 1991-1997, 2004 Mtukudzi Collection 1984-1991, 2005 Nhava, 2006 Wonai, 2007 Tsimba Itsoka, 2008 Dairai (Believe), 2010 Rudaviro, 2010 Kutsi Kwemoyo (compilation) na 2011 Rudaviro. Nilipomuuliza ni tuzo ngapi ambazo amezipata tokea ameanza muziki? msanii huyu alisema kuwa yeye huwa haesabu na wala hana takwimu yoyote, kwa vile ni nyingi na huwa hajali kwa vile yeye anachojali ni kuchaguliwa kwani hiyo ndiyo heshima kwake.
'Wasanii wengi huwa wanajali sana tuzo bila kujali suala la kuchaguliwa, ni heshima tosha maana inaonyesha ni jinsi gani watu waliweza kukuthamini,' alisema Oliver Mtukudzi.
Oliver "Tuku" Mtukudzi (amezaliwa mnamo 22 Septemba, 1952 mjini Highfield, Harare) ni mwanamuziki wa Kizimbabwe. Oliver ni miongoni mwa wanamuziki walio maarufu kwa muda mrefu sana katika nchi hiyo ya Zimbabwe. Na alianza shughuli za muziki kunako miaka ya 1977 pale alipojiunga na bendi ya Wagon Wheels, ambayo pia alikuwemo na mwanamuziki wa zamani Bw. Thomas Mapfumo.
Nyimbo ya kwanza ilikuwa "Dzandimomotera" iliyoheshimika sana, na hapo ndipo Tuku alipotoa albamu yake ya kwanza, nayo pia ilileta mafanikio makubwa kabisa. Mtukudzi nae pia ni mmoja wa wanakundi la Mahube, kundi la muziki la nchi za Afrika ya Kusini.
Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Tigo Jackson Mmbando (kulia) wakati wa kuchezesha droo ya kwanza ya kumpata mshindi wa promosheni ya Endesha Pikipiki na Tigo jana jijini Dar es Salaam. Wengine ni Catherine Kasimbazi wa Solid Ltd, Pamela Shelukindo kutoka Tigo na Humudi Abdulhussein kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya washiriki wa mkutano wa Utumishi wa Umma kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Tuesday, June 21, 2011
BANGO