ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 24, 2026

YANGA SC YATELEZA UGENINI, YACHAPWA 2-0 NA AHLY ALEXANDRIA

 


TIMU ya Yanga imeteleza ugenini baada ya kuchapwa mabao 2-0 na wenyeji, Al Ahly katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika usiku huu Uwanja wa Borg El Arab Jijini Alexandria, Misri. 

Mabao yaliyoizamisha Yanga SC jana yote yamefungwa na winga wa kushoto, Mahmoud Ahmed Ibrahim Hassan ‘Trézéguet’ moja kila kipindi, dakika ya 45’+3 na 75.

Kwa ushindi huo, Al Ahly inafikisha pointi saba kufuatia ushindi wa 4-1 dhidi ya JS Kabylie ya Algeria nyumbani na sare ya 1-1 ugenini dhidi ya wenyeji, AS FAR Rabat nchini Morocco.

Yanga wanabaki na pointi zao nne walizovuna kwenye mechi mbili za awali wakishinda 1-0 nyumbani dhidi ya FAR Rabat na sare ya bila mabao, 0-0 ugenini na JS Kabylie.

Mchezo mwingine wa Kundi B leo, JS Kabylie watawakaribisha AS FAR Rabat Uwanja wa Hocine Aït Ahmed mjini Tizi Ouzou.

Yanga wanarejea nyumbani kuwasubiri Al Ahly kwa mchezo wa marudiano Januari 31 Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

𝗦𝗘𝗥𝗜𝗞𝗔𝗟𝗜 𝗬𝗔𝗢𝗠𝗕𝗪𝗔 𝗞𝗨𝗣𝗨𝗡𝗚𝗨𝗭𝗔 𝗭𝗔𝗜𝗗𝗜 𝗚𝗛𝗔𝗥𝗔𝗠𝗔 𝗭𝗔 𝗨𝗦𝗔𝗝𝗜𝗟𝗜 𝗪𝗔 𝗢𝗡𝗟𝗜𝗡𝗘 𝗠𝗘𝗗𝗜𝗔.

Mwenyekiti wa MISATAN na MPC, Edwin Soko (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa BMG Media, George Binagi, tuzo maalum kutoka YouTube baada ya BMG Media kufikisha zaidi ya wafuasi (subscribers) laki moja.

Serikali imeombwa kuendelea kupunguza gharama za usajili wa vyombo vya habari mtandaoni (Online Media) ili kuongeza fursa za ajira na kujiajiri kwa vijana nchini.

.
Ombi hilo limetolewa Jumamosi Januari 24, 2026 na Mkurugenzi wa BMG Media, George Binagi, wakati wa hafla fupi ya kupokea tuzo maalum kutoka YouTube baada ya BMG Media kufikisha zaidi ya wafuasi (subscribers) laki moja.
.
Akizungumza katika hafla hiyo, Binagi amesema licha ya Serikali kupunguza gharama za usajili wa Online Media kutoka shilingi milioni moja hadi shilingi laki tano, bado kiwango hicho ni kikubwa kwa vijana wengi, hususan wahitimu wa taaluma ya uandishi wa habari na wabunifu wa maudhui, hivyo ameomba gharama hizo zishushwe hadi shilingi laki moja.
 

Ameeleza kuwa hatua hiyo itachochea vijana wengi zaidi kuanzisha vyombo vya habari mtandaoni na kujiajiri, jambo litakalosaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini.
.
Aidha, Binagi amesema kuanzia mwaka 2026, watengeneza maudhui mtandaoni wameanza kukatwa asilimia tano ya mapato yao na kuwasilishwa serikalini, huku wakiendelea kulipa kodi nyingine mbalimbali, hali ambayo imewaongezea mzigo wa kodi na kusababisha kile alichokitaja kama kulipa kodi mara mbili.
.
 Kutokana na hilo, ameomba Serikali kulitafutia ufumbuzi suala hilo.
.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa MISATAN na MPC, Edwin Soko, amesema mitandao ya kijamii imeendelea kuwa fursa muhimu kwa vijana katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira, hivyo amewahimiza vijana kutumia mitandao hiyo kwa njia sahihi na yenye tija.
.
Kuhusu gharama za usajili na masuala ya kodi, Soko amesema atayawasilisha kwa mamlaka husika kupitia vikao mbalimbali vya wadau wa habari ambavyo vinaendelea kufanyika kwa lengo la kuboresha na kukuza sekta ya habari nchini.
.
#YouTube 
#mwanza 
#Habari 
CC: @bmgonlinetv 

Wednesday, January 21, 2026

JKT YATANGAZA NASAFI MAFUNZO YA KUJITOLEA.

news
Mkuu wa Tawi la Utawala wa JKT, Brigedia Jeneral Hassan Mabena

 

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) imetangaza nafasi za kujiunga na mafunzo ya kujitolea kwa vijana wa Tanzania Bara na visiwani kwa mwaka 2026 huku likisisitiza nafasi hizo ni bure kwa vijana watakaoomba.

Akizungumza katika Makao Makuu ya JKT, Chamwino Dodoma, Mkuu wa Tawi la Utawala wa JKT, Brigedia Jeneral Hassan Mabena, amesema usahili wa vijana hao utaanza Januari 26 mwaka huu katika mikoa yote ya bara na visiwani.

Amesema utaratibu wa vijana kuomba mafunzo hayo unaratibiwa chini ya ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya na vijana wenye elimu ya kuanzia darasa la saba hadi chuo kikuu wanazo sifa za kuomba, akisema watakaochaguliwa wataanza kujiunga katika kambi mbalimbali za JKT kuanzia February 27 hadi Machi nne mwaka huu.

"Mafunzo haya ni bure wazazi au walezi wasikubali kurubuniwa kutoa fedha ili vijana wao wapate nafasi za kujiunga na mafunzo hayo," amesema Brigedia Jenerali Hassan Mabena.

Amezitaja kozi ambazo wanazipa kipaumbele ni zile za taaluma ya Stashahada ya Teknolojia ya Habari, Stashahada ya Mifumo ya Taarifa za Biashara, Stashahada ya Sayansi ya Kompyuta, Stashahada ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), Stashahada ya Usalama Mtandaoni.

Nyingine ni Shahada ya Sayansi katika Sayansi ya Kompyuta, Shahada ya Sayansi katika Teknolojia ya Habari, Shahada ya Sayansi katika Uhandisi wa Kompyuta, Shahada ya Sayansi katika Teknolojia ya Habari za Biashara,Shahada ya Sayansi katika Usalama wa Mtandao na Forensics ya kidigitali.

"Nitoe wito kwa Watanzania wenye sifa waende kwenye vijiji kata,tarafa zao ili waweze kujiandikisha, nasisitiza  nafasi hizi haziiuzwi ni fursa iliyotolewa bure kwa Watanzania wote," amesema Brigedia Jenerali Mabena 

Mabena amesema Vijana watakaopewa kipaumbele kuchanguliwa ni waliosoma kozi za masulala ya Sayansi pia akawatahadharisha wazazi kuepuka matapeli.

MBOWE: MZEE MTEI HAKUWA NA SHARI NA MTU.

Mbowe: Mtei hakuwa na shari na mtu

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe, amesema Hayati Mzee Edwin Mtei (94), alikuwa ni mtu aliyejenga uhusiano mwema na watu wakati wote.

Mbowe ameeleza hayo Jana Jumanne Januari 20 jijini Arusha, wakati akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa msibani.

Akisimulia namna alivyomfahamu Mzee Mtei, Mbowe, amesema hakuwa mtu wa shari, kila alikofanya kazi, alikuwa amejipanga na alikuwa hachagui rafiki ndani na nje ya chama.

Mtei, alifariki dunia usiku wa kuamkia Januari 19 mwaka huu, wakati akikimbizwa kupatiwa matibabu katika Hospitali  ya Selian Jijini Arusha, inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

"Hakuwa mtu mwenye njaa, alikuwa ni mtu anayejiweza, akifanya siasa za mageuzi katika mazingira yale...misingi mikuu ambayo mzee huyu ametuachia ni sera. Tulikuwa na waasisi 12 wa CHADEMA." amesema Mbowe.

Mbowe amesema Mtei aliwasaidi kupata uzoefu ndani ya chama husuani masuala ya kifedha.

Amesema alikuwa na ujuzi mkubwa wa masuala ya kodi na sera pamoja na uzoefu mkubwa wa masuala ya kidiplomasia.


Wakati wa uhai wake, Hayati Edwin Mtei aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Kanda ya Afrika, Katibu

Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Waziri wa Fedha wakati wa uongozi wa Hayati Julius Nyerere.

MWASISI WA SARAFU

Mbowe amesema: "Mzee Mtei, ndiye aliyekuwa mwasisi wa kwanza wa sarafu ya Tanzania, baada ya ile sarafu ya Afrika ya Mashariki baada ya sisi kuanzisha Benki Kuu ya Tanzania (BoT)".

KUUGUA

Mbowe amesema Mzee Mtei ameugua kwa muda mrefu na familia imepokea kwa uzito msiba huo kutokana na rekodi iliyotukuka, aliyoiweka ndani ya chama na Taifa.

Kwa mujibu wa Mbowe, Mzee Mtei alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali, ikiwemo Hospitali ya Nairobi-Kenya, Dar es Salaam na maeneo mengine kadha wa kadha.

Mbowe alisema: "Natambua CHADEMA  wametuma ujumbe katika msiba huu ili kuungana na familia kwa sababu mzee alikuwa ni mwasisi wa chama chetu. Ni kiongozi ambaye bado tulikuwa tunamuheshimu sana katika njia mbalimbali, kwa sababu misingi yote ya CHADEMA huyu ndiye aliyeianzisha"

ASKOFU ROSEMARY AMPONGEZA DKT. BITEKO

 

Na, Ernest Magashi

Askofu wa Kanisa la Ufunuo Jimbo la Geita, Rosemary Mashauri Bendera, amempongeza Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dkt. Doto Biteko, kwa juhudi zake za kuwaletea wananchi maendeleo, huku akiwahimiza wananchi kushirikiana kwa pamoja katika kuijenga na kuendeleza Wilaya ya Bukombe.Pongezi hizo zilitolewa Jumapili ya Tarehe 19 Jan 2026 wakati wa ibada ya shukrani kwa Mungu baada ya kuvuka mwaka 2025 na kuukaribisha mwaka 2026, iliyofanyika katika Kanisa la Ufunuo mjini Ushirombo, wilayani Bukombe.Katika ibada hiyo, Askofu Rosemary aliwaomba waumini kuendelea kuiombea Serikali na viongozi wake ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Alitaja baadhi ya miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa wilayani humo, ikiwemo ujenzi wa soko la kisasa, stendi ya mabasi na uwanja wa mpira wa miguu, kama vielelezo vya dhamira ya Serikali katika kuboresha maisha ya wananchi.Aidha, Askofu Rosemary aliwatunuku wachungaji 12 daraja la uchungaji kamili na kuwakabidhi vifaa vya kazi, akiwahimiza kumtumikia Mungu kwa uaminifu kwa kushirikiana na Serikali pamoja na jamii zinazowazunguka katika maeneo watakayopangiwa.Vilevile, aliwasisitiza wazazi na walezi kuwekeza katika elimu ya watoto wao kwa kuhakikisha watoto waliofikia umri wa kuandikishwa darasa la awali na kidato cha kwanza wanaandikishwa na kuhudhuria shule, sambamba na jitihada za Serikali za kuendelea kujenga na kuboresha miundombinu ya elimu.Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dkt. Doto Biteko, katika ziara zake za kikazi hivi karibuni amekuwa akihamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo kwa kuchangia nguvu kazi, hususan katika ujenzi wa zahanati na shule.Dkt. Biteko amesema Serikali inatarajia kukarabati shule 23 pamoja na miundombinu yake, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuboresha huduma za elimu wilayani Bukombe, huku akisisitiza kuwa jukumu la wazazi na walezi ni kuhakikisha watoto wote wanapelekwa shule kwa wakati.

Monday, January 19, 2026

NI SENEGAL BINGWA AFCON, MOROCCO YALALA NYUMBANI 1-0

 

TIMU ya Senegal ‘Simba wa Teranga’ imefanikiwa kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Morocco usiku huu Uwanja wa Prince Moulay Abdellah Jijini Rabat.


Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo wa ulinzi wa Villarreal ya Hispania, Pape Alassane Gueye dakika ya 94 katika mchezo uliodumu kwa dakika 120.


Hilo linakuwa taji la pili la AFCON kwa Senegal baada ya awali kulibeba mwaka 2021 nchini Cameroon Waliofunga Misri kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 0-0 Uwanja wa Olembe Yaoundé.


Nyota wa Senegal, Sadio Mane wa Senegal amechaguliwa Mchezaji Bora wa michuano hiyo (MVP), Mfungaji Bora Brahim Diaz wa Morocco mabao matano, Kipa Bora Yassine Bounou wa Morocco na Timu iliyoonyesha Mchezo wa Kiungwana, Morocco.