ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 18, 2022

KARSAN ATANGAZA KUSTAAFU UKURUGENZI UTPC.

 AFUNGUKA MENGI:- NILIWAHI KUFUKUZA MTU KAZI KISHA BAADA YA MUDA AKAFARIKI DUNIA, ILINIUMA SANA, HATA UKINIKOSEA VIPI SIWEZI KUKUFUKUZA.

NA ALBERT G. SENGO /MWANZA Mkurugenzi wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan amesema anatarajia kustaafu kazi hiyo ifikapo Desemba mwaka huu baada ya kuitumika kwa muda wa miaka 19. Karsan aliyekuwa akizungumza wakati akifungua mkutano wa kuthibitisha kanuni za maadili ya uandishi wa habari mtandaoni na vyombo vya habari vya kawaida leo Juni 17 2022, Karsan amesema amechukua uamzi huo toka mwaka jana na tayari taratibu za kumpata mkurugenzi mpya atakayeiongoza taasisi hiyo umeshafanyika. Amesema uamuzi wa kustaafu ameuchukua toka mwaka jana na hajasurutishwa na mtu na kwamba anawaachia vijana kuendesha taasisi hiyo ambayo imeanzishwa mwaka 2003. “Nilichukua uamuzi wa kustaafu toka mwaka jana ambapo nilishirikisha viongozi kutoka bodi ya wakurugenzi ambao baada ya kuwaeleza matakwa yangu walinitaka niendelee kuwepo hadi mwishoni mwa mwaka huu, na baada ya kustaafu nitakuwepo nikimwangalia mkurugenzi mpya kwa takribani miezi mitatu,” amesema Karsan huku akiwataka waandishi wa habari kutoa ushirikiano kwa mkurugenzi huyo ambaye tayari ameshapatikana.

'SENENE WAANGUSHA MTI BUKOBA'

 MZEE SENETI NA SENENE WALIOANGUSHA MITI NA MAJUBA BUKOBA / AFUNGUKA HAYA SEHEMU YA 1

Friday, June 17, 2022

"NATAMANI KUWA DAKTARI"

 WOMEN ROUND TABLE TANZANIA NA GEWOMA WATOA MSAADA WA MAGODORO 80 KWA WATOTO WENYE UHITAJI GEITA

NA ALBERT G SENGO/ GEITA Taasisi ya Women Round Table, Ikishirikiana na Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake Mkoani Geita, Mapema wiki hii imekabidhi magodoro Yenye thamani ya zaidi ya Shilingi 4 kwa Shule ya Msingi ya watoto wenye uhitaji maalum ya Mbugani.

KANUNI ZA MAADILI YA UANDISHI WA HABARI MTANDAONI ZAPITIWA NA KUTHIBITISHWA.

  Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania (UTPC) umekutana na Waandishi wa Habari Mtandaoni (Bloggers/Youtubers) kwa ajili ya kupitia na kuthibitisha Kanuni za Maadili ya Uandishi wa Habari Mtandaoni na Vyombo vya Habari vya kawaida.

Mkutano huo umefanyika leo Ijumaa Juni 17,2022 katika ukumbi wa Adden Palace Jijini Mwanza na kuhudhuriwa na waandishi wa habari wa mitandao ya Kijamii kutoka mikoa mbalimbali. Akifungua Mkutano huo, Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan amesema Kanuni za Maadili ya Uandishi wa Habari Mtandaoni zitasaidia kupunguza wimbi la habari za uongo mtandaoni hivyo kupunguza malalamiko mbalimbali.

Mshauri Mwelekezi wa Kutengeneza Kanuni za Maadili ya Uandishi wa Habari Mtandaoni, Pili Mtambalike akizungumza kwenye Mkutano wa Kupitia na Kuthibitisha Kanuni  za Maadili ya Uandishi wa Habari Mtandaoni.
Mshauri Mwelekezi wa Kutengeneza Kanuni za Maadili ya Uandishi wa Habari Mtandaoni, Pili Mtambalike akizungumza kwenye Mkutano wa Kupitia na Kuthibitisha Kanuni  za Maadili ya Uandishi wa Habari Mtandaoni 
Waandishi wa habari wa mitandao ya Kijamii wakiwa kwenye Mkutano wa Kupitia na Kuthibitisha Kanuni  za Maadili ya Uandishi wa Habari Mtandaoni 
Waandishi wa habari wa mitandao ya Kijamii wakipitia na Kuthibitisha Kanuni  za Maadili ya Uandishi wa Habari Mtandaoni 
Waandishi wa habari wa mitandao ya Kijamii wakipitia na Kuthibitisha Kanuni  za Maadili ya Uandishi wa Habari Mtandaoni 
Waandishi wa habari wa mitandao ya Kijamii wakipitia na Kuthibitisha Kanuni  za Maadili ya Uandishi wa Habari Mtandaoni 

MNDOLWA AONGOZA MAPITIO YA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO WA TUME YA TAIFAYA UMWAGILIAJI

 

MkurugenziMkuu, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Raymond Mndolwa akifungua kikao kazi cha mapitio ya mpango mkakati wa miaka mitano wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Jijini Dodoma.

Mhandisi wa Umwagiliaji wa Mkoa wa Singida William Kadinda akielezea namna mpango mkakati utakavyorahisisha utekelezaji kiutendaji katika maeneo husika.


Baadhi ya Wataalam wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakijadiliana kwa lengo la kuboresha Mpango Mkakati wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

Picha ya pamoja kati ya Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na Wahandisi wa Umwagiliaji wa Mikoa.


Na; MwandishiWetu - Dodoma

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Raymond Mndolwa, ameongoza kikao kazi cha mapitio ya mpango mkakati wa miaka mitano wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji, uliohusisha wataalam na wahandisi wa Umwagiliaji nchini, mapema leo Jijini Dodoma.

Bw. Mndolwa alisema kuwa,kuna umuhimu wakufanya mapitio ya mpango mkakati huo kwa pamoja tofauti kwa kuwa Mpango mkakati huo ni Dira ya Taasisi hivyo ni muhimu kila mtumishi katika taasisi anatakiwa kuifahamu kwani ndiyo zana inayotumika katika utekelezaji wa kazi za kila siku.

“Nimeona kuna Umuhimu wa kupitia kwa pamoja ili pale ambapo patakuwa na marekebisho turekebishe kwa pamoja, na kuwe na ushiriki kwa hoja katika kazi hii.” AlifafanuaMndolwa.

Kwa upande wake Mhandisi wa Umwagiliaji wa Mkoa wa Singida William Kadinda amesema, kikao kazi hiki kinatoa fursa ya mpango wa miaka mitano ambao unajumuisha shughuli zinazofanyika, pia kinaangalia maslahi ya watumishi katika upande wa mafunzo na kuona mahitaji yao, nakuweza kuwaongezea uwezo kiutendaji.

Kukamilika kwa mpango mkakati huo ni hatua muhimu kwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakati huu,ikiwa na jukumu kubwa la ukarabati na ujenzi wa Skimu za umwagiliaji pamoja na Mabwawa kwa ajili ya umwagiliaji. Lengola serikalini kufikia Hekta 1,200,000 za umwagiliaji mwaka 2025.

SOUTHAMPTON KUWANOA MAKOCHA WA TANZANIA -WAZIRI MCHENGERWA

 


Na John Mapepele.


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema  Tanzania inakwenda  kushirikiana na klabu ya Soka ya Southampton  kuwandaa makocha wa soka ili wawe kwenye kiwango cha kimataifa.

Mhe. Mchengerwa amesema haya leo juni 17, 2022 ofisini kwake akiambatana na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Dk. Hassan Abbasi wakati alipokutana na ujumbe wa Klabu hiyo ulioongozwa na Afisa Biashara  Mkuu wa Klabu hiyo David Thomas. 


Amesema dhamira ya Serikali ni kuona kuwa michezo mbalimbali inasimamiwa  kisayansi ili kuleta tija ikiwa ni pamoja na kuwa na makocha ambao watasaidia kufundisha  timu za micherzo ili kufuka kwenye kiwango cha kimataifa.


Katika kikao hicho  wamekubalina kuwa Timu ya soka  ya ya Wanawake chini ya Miaka 17 (Serengeti Girls)  itakwenda kupatiwa mafunzo maalum   kwenye Klabu hiyo ikiwa ni maandalizi ya kwenda kwenye  mashindano ya kombe la dunia nchini India.

Katika tukio hilo ujumbe wa timu hiyo ulimzawadia jezi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Samia Suluhu Hassan ikiwa ni kuthamini mchango wake mkubwa anaoutoa kuendeleza michezo nchini.

SHIRIKA LA BRAC TANZANIA LAWEZESHA WASICHANA 900 TANGA KUPATA ELIMU YA SEKONDARI MKOANI TANGA

 

MKURUGENZI wa Jiji la Tanga Sipora Liana akizungumza wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika kiwilaya kwenye viwanja vya Urithi Jijini Tanga

Meneja Mradi wa EELAY wa Shirika la Brac Tanzania Hope Jasson akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika kiwilaya kwenye viwanja vya Urithi Jijini Tanga  ambapo alielezea namna Shirika hilo lilovyowezesha zaidi wasichana 900 kupata fursa ya kumaliza elimu ya sekondari kupitia mpango wa muda mfupi chini ya taasisi ya Elimu ya Watu Wazima
 
Diwani wa Viti Maalumu (CCM) akizungumza wakati wa maadhimisho hayo

Na Oscar Assenga,TANGA.

SHIRIKA la Brac Maendeleo Tanzania limewawezesha zaidi ya Wasichana 900 walio na umri kati ya miaka 15-24 kupata fursa ya kumaliza elimu ya Sekondari kupitia mpango wa muda mfupi chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.

Hayo yalibainishwa leo na Meneja Mradi wa EELAY wa Shirika la Brac Tanzania Hope Jasson wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika kiwilaya kwenye viwanja vya Urithi Jijini Tanga.

Alisema Shirika hilo kwa msaada wa kifedha kutoka NORAD (Norwegian Agency For Development Cooperation) inatekeleza mradi wa miaka minne unaoitwa (Education Empowerment and Life Skills For Adolescent na Young Children –EELAY).

Mradi huo unatoa elimu ya Elimu,Uwezeshaji na Stadi za Maisha katika Halmashauri ya Jiji la Tanga na wilaya ya Korogwe tokea mwezi June mwaka 2018 hadi Desemba 2022 ambapo mpango huo ulikuwa ni wa muda mfupi yenye matokeo chanya (ALP) kuwasaidia katika kukamilisha miaka minne ndani ya miaka miwili .

Akieleza mafanikio makubwa ya mradi huku akieleza kwa sasa wanaendelea kutoa huduma kwenye vituo 30 vya masomo chini ya usimamizi wa Jamii,kati ya hivyo 20 viko Halmashauri ya Jiji la Tanga na 10 katika wilaya ya Korogwe.

“Lakini asilimia 86.8 ya wasichana walioko kwenye rika balehe wamefaulu na kupewa cheti cha Elimu ya Sekondari tangu 2017 hadi 2021 kati yao 51 wamejiunga na masomo ngazi za juu katika shule za Serikali na shule binafsi,wanafunzi 10 kutoka kundi la mwaka 2016 walijuunga na vyuo vikuu katika kozi za shahada ya kwanza”Alisema

Alisema takribani watoto 1670 kati ya umri wa miaka 3-5 walipata elimu ya makuzi,malezi na maendeleo ya awali ,madarasa mapya 22 yamejengwa na madarasa 13 yamekarabatiwa katika shule za Serikali na kutumia kama vituo vya kusomea vya watoto vijana.

“Walimu 41 wa elimu ya awali kutoka shule za Serikali walipatiwa mafunzo juu ya mtaala wa elimu ya awali na kutoa msaada wa rasilimali kwa ajili ya kutengeneza vifaa vya kufundishia”Alisema

“Lakini pia ni matumaini yetu kama Shirika baada ya Desemba 2022 Halmashauri ya Jiji la Tanga itaendelea na kazi ya Usimamizi na uangalizi huku jamii husika ziliendelea kutekeleza mradi hivyo mafanikio yataendelea kuonekana”Alisema

Awali akizungumza katika Maadhimisho hayo Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Sipora Liana alisema wakati wanaadhimisho siku ya mtoto wa Afrika ni vema kuimarisha ulinzi wa mtoto ili kuepusha ukatili dhidi yake na kutafakari kupata nafasi ya kuelimisha jamii juu kujenga taifa lenye uwasa na kutokokemeza matukio ya ukatili wa kijisia na ukatili dhidi yao

“Mkiona mnafanyiwa vitendo vya ukatili toeni ripoti waambieni walimu,mama,baba njoo pia kwangu mje mniembie lengo ni kufikia maendeleo endelevu kuongeza ushiriki wa watoto wa kike kwenye uongozi na kubadiliusha uzoefu kwenye masuala kichumi,kijamii na kiutamaduni”Alisema

Alisema zipo changamoto ambalimbali ambazo zinawakabili watoto na kusababisha kuzorotesha maendeleo yao ikiwemo ukatili huku akitoa wito kwao kuache kwenda mahali ambapo ni hatarishi.

“Bado Jamii na watoto wanajukumu la kufanya kuimarisha ulinzi hususani mtoto endapo matukio ya ukatili au dalili za kufanyiwa ukatili zinapotokea ili kuweza kuepukana na kadhia hizo”Alisema

“Naomba niwatie shime watoto wa kike ni kitovu cha maendeleo na wana wajibu wa kushiriki katika shughuli zote za maendeleo na kusoma kwa bidii pia mzitambue haki zenu ili kupunguza matukio ya ukatili wa kijisnia dhidi yenu”Alisema

Hata hivyo alisema pamoja na changamoto wanazopitia watoto Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu bado

Naye kwa upande wake akisoma risala ya siku hiyo Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mkwakwani Sumaiya Ally alisema katika siku ya mtoto wa Afrika wanatoa ombi kwa familia,Jamii na Serikali kwa ujumla kuungana kwa pamoja katika kuhakikisha ulinzi kwa mtoto unaimarishwa na matendo ya ukatili yanatokomezwa ili kujenga kizazi kilicho bora.

“Kwa kufanya hivyo tutakuwa tunatekeleza haki za mtoto zinazoanishwa kwenye sera ya mtoto ya mwaka 2008 ambazo ni haki ya kuishi, kuendelezwa,kushiriki,kulindwa na kutokubaguliwa”Alisema Sumaiya

Hata hivyo alitoa ombi kwa Serikali ,Mashirika yasiyoya kiserikali pamoja na wakazi wa Jiji la Tanga kutambua na kutafuta ufumbuzi wa matatizo wanayoyapata watoto wenzao wenye ulemavu,yatima na wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.

“Kwani watoto hao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi katika maisha kwa mfano unyanyasaji ,kokosa malezi mazuri kutoka kwa wazazi na walezi na hivyo kukosa haki zao za Msingi “Alisema


WALEMAVU IRINGA WATAKA ELIMU JUMUISHI

 

Makamu Mwenyekiti Chama cha Walemavu Tanzania (CHAWATA) mkoa wa Iringa Leo Sambala akiongea wakati wa mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali uliondaliwa na shirika lisilo la kiserikali la IDYDC na kufadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali linalotekeleza mradi wa Inclusive Media Project unaofadhiliwa na Internews Tanzania
Moja ya washiriki wa mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali uliondaliwa na shirika lisilo la kiserikali la IDYDC na kufadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali linalotekeleza mradi wa Inclusive Media Project unaofadhiliwa na Internews Tanzania akichangia mada wakati wa mkutano huo
Picha ya pamoja ya washiriki wa Mkutano huo.


Na Fredy Mgunda,Iringa.

CHAMA cha watu wenye ulemavu Tanzania (CHAWATA) mkoa wa Iringa wameiomba serikali kuweka mfumo wa elimu jumuishi kwa walemavu ili kutatua changamoto ambazo wanazokabiliana licha kuwa bado kunachangamoto kubwa ya miundombinu ya elimu hiyo.

Akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali uliondaliwa na shirika lisilo la kiserikali la IDYDC na kufadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali linalotekeleza mradi wa Inclusive Media Project unaofadhiliwa na Internews Tanzania  katika mkoa wa Iringa, Makamu Mwenyekiti Chama cha Walemavu Tanzania (CHAWATA) mkoa wa Iringa, Rukia Makweta alisema kuwa watoto wenye mahitaji maalumu kuchanganyikana na wengine inatengeneza umoja na kuondoa unyanyapaa kwa kuwa tayari wamezoeana na kupendana pamoja na kupewa ushirikiano kutoka kwa wenzao..

Makweta alisema kuwa kwa mujibu wa Sheria namba tisa ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010, inataka haki sawa kwa watu wenye ulemavu ikiwamo elimu, ajira, nafasi za uongozi na kuboresha miundombinu na kwa mujibu wa jarida ya Shirika la Kuhudumia watoto Duniani (Unicef), kati ya watoto watano ni wawili tu wapo shuleni hali ambayo inahitaji elimu jumuishi kuwavutia wengi zaidi.

Aliongeza kuwa katika suala la elimu walemavu wengi wanakabiliana na miundombinu isiyo rafiki ambayo ni kikwazo katika upataji wa elimu kwa walemavu waliowengi nchini.

Mmoja ya wanafunzi wenye ulemavu wa kuona, Kephason alisema shule jumuishi anayosoma bado ina changamoto za kimiundombinu  na kupelekea kuwa na ugumu kutoka sehemu moja hadi nyingine awapo kwenye  mazingira ya shule na kupelekea kukosa ari ya kuendelea na masomo kama wanafunzi wengine na kuitaka serikali kufanya jitihada madhubuti kurekebisha hili kwani kwa mwenendo huu wanafunzi wengi wenye ulemavu wanaamua kuacha shule ili kuepukana na changamoto za kimiundombinu wanazokutana nzao mashuleni kwani huwaathiri kisaikolojia pia.

“Elimu jumuishi imepewa kipaumbele zaidi kuliko aina nyinginena inachukuliwa kama njia bora” alisema.

Aidha Makweta alisema kuwa sehemu kubwa ya jamii nchini imeendelea kukumbatia utamaduni wa kuwafungia ndani watoto wenye ulemavu kwa madai mbalimbali ikiwamo ya kuhofia aibu au kuwaona hawatakuwa na uwezo wa kushiriki shughuli za kijamii ikiwamo elimu.

Naye Katibu wa Shirika la watu wenye Ulemavu, (SHIVYAWATA), Leo Sambala alisema kuwa moja ya changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni miundo mbinu isiyo rafiki kwenye shule nyingi za msingi na sekondari ni kati ya vikwazo vinavyoikabili elimu hiyo mkoani hapo  na kuongeza kuwa kama suala la miundombinu halitapewa uzito, watoto hao watashindwa kujifunza ipasavyo.

“Ni kweli shule zetu zinakabiliwa na miundombinu isiyo rafiki, hakuna vifaa vya kujifunzia hasa kwa walemavu wasioona, hapa hakuna kujifunza kwani walemavu wa kutoona wanahitaji vifaa maalum ambavyo sio kila shule inavyo, kwa hiyo huyu hatajifunza kama ataingia darasani na kukosa vifaa hivyo.” Alisema Sambala.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Elimu Jumuishi kutoka shirika lisilo la kiserikali la  Iringa Development of Youth Disabled and Children Care (IDYDC)linalotekeleza mradi wa Inclusive Media Project mkoa wa Iringa na kufadhiliwa na Internews Tanzania  , Reuben Magayane alisema kuwa lengo la mradi ni kutumia vyombo vya habari  kupaza sauti juu ya elimu jumuishi na kuibua maswala ya makundi maalumu na walemavu kupitia vyombo vya habari.

Alisema kuwa jambo ambalo limekuwa halipewi kipaumbele kwenye vyombo vya habari huku ikiiasa jitihada jumuishi kutoka kwa waandishi wa habari,jamii na serikai ili kufikia lengo la elimu kwani Msingi wa mafunzo mbalimbali katika jamii ni chachu ya kuondoa mawazo mgando juu ya watu wenye mahitaji maalumu kuwa hawawezi, hivyo ni jukumu la kila Mtanzania kutoa ushirikiano hitajika kwa watu wenye mahitaji maalumu hasa katika upande wa elimu.

Alisema kuwa katika kikao hicho moja ya changamoto ambayo imejitokeza ni ukosefu wa miundombinu rafiki ya kujifunzia katika shule jumuishi nchini hivyo ni moja ya njia ambazo zinaathiri kwa kiasi kikubwa maendeleo ya wanafunzi na  watu wenye ulemavu.Wilaya ya IringaKwa muda mrefu kumekuwa na kampeni mbalimbali kuhusu watu wenye ulemavu hasa juu ya haki zao za msingi ikiwamo elimu.

Magayane alisema kuwa kumekuwa na kampeni mbalimbali juu ya watu wenye ulemavu kupata miundombinu rafiki lakini bado kilio cha watu wenye ulemavu kupata mahitaji yao muhimu ili waishi kama makundi mengine kwenye jamii hakikomi.

Aliongeza kuwa changamoto lukuki ikiwamo miundombinu isiyo rafiki kwa wanafunzi wanaoishi na ulemavu, ni moja ya vilio vinavyowafanya baadhi kushindwa kupata elimu na mkoa Iringa ni kati ya mikoa inayokabiliwa na changamoto nyingi katika utoaji wa elimu jumuishi kubwa ikiwa miundombinu isiyo rafiki.

Thursday, June 16, 2022

MTUME BONIFACE MWAMPOSA AFIKA NYUMBANI KWA MBUNGE WA KISESA, LUHAGA MPINA KUHANI MSIBA MAMA YAKE NA KUMBUKUMBU YA MZEE MPINA

 

Mtume Boniface Mwamposa Bulldoza (kulia) akiendesha maombi maalum ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kufariki kwa Baba mzazi wa Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina (kushoto), Marehemu Mpina Gabisi Samweli Luchemba na kuhani msiba wa Mama yake, Marehemu Kephrine Kabula Masaga katika Kijiji cha Isangijo Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu leo Juni 15, 2022

 

Mtume Boniface Mwamposa Bulldoza  akiendesha maombi maalum  kwa wazazi wa Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Joelson Mpina, Marehemu Mpina Gabisi Samweli Luchemba na Marehemu Kephrine Kabula Masaga alipofika katika Kijiji cha Isangijo Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu Juni 15, 2022. Marehemu Mzee Mpina alifariki Juni 14, 2021 na Mama alifariki Juni 1, 2022.
Mtume Boniface Mwamposa Bulldoza akiendesha maombi ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kufariki kwa Baba mzazi wa Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Joelson Mpina, Marehemu Mzee Mpina Gabisi Samweli Luchemba na kuhani msiba wa Mama yake Mpina, Marehemu Kephrine Kabula Masaga aliyezikwa Juni 8, 2022. Hafla hii imefanyika Kijiji cha Isangijo Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu Juni 15, 2022.

Mtume Boniface Mwamposa Bulldoza akimbariki Diwani wa Kata ya Lubiga, Mhe. Juma Isack Mpina ambaye ni Kaka wa Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Joelson Mpina wakati wa ibada maalum ya kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha Mzee Mpina Gabisi Samweli Luchemba na kuhani msiba wa Mama yake Mpina, Marehemu Kephrine Kabula Masaga Kijiji cha Isangijo Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu, Juni 15,2022
Mtume Boniface Mwamposa Bulldoza akiwapaka mafuta ya upako wananchi wa Jimbo la Kisesa walifika nyumbani kwa Mbunge wa Kisesa Mhe. Luhaga Joelson Mpina wakati wa ibada maalum ya kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha Mzee Mpina Gabisi Samweli Luchemba na kuhani msiba wa Mama yake Mpina, Marehemu Kephrine Kabula Masaga katika Kijiji cha Isangijo Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu Juni 15,2022

Tuesday, June 14, 2022

TFS NA WADAU WAWEKA MKAKATI WA KUPAMBANA NA MOTO KWENYE MAZAO YA MISITU

 


Kamishna wa Uhifadhi - TFS Prof. Dos Santos Silayo akizungumza na wadau na wakulima wa mazao ya misiti juu ya madhara yanayotokana na moto na athari zake kwa uchumi wa jamii
Kamishna wa Uhifadhi - TFS Prof. Dos Santos Silayo akizungumza jambo na Dr Goliama wakati wa kikao cha kupambana na moto kwa wakulima wa mazao ya misitu 

 Na Fredy mgunda,Iringa.


SERIKALI na wadau wa mazao ya misitu  wamejipanga kuhakikisha wanazuia na kuyamaliza matukio ya moto kwa kuunda mkakakati ambao utasaidia kupambana na matukio ya moto kwa wakulima wa zao hili katika wilaya ya Mufindi na wilaya nyingine zinazopakana na mkoa wa Iringa.

 

 

Kumekuwa na matukio ya moto ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara hasa katika msimu wa kiangazi ambapo mojawapo ya vyanzo vinavyotajwa na usafishaji wa mashamba kwaajili ya kuandaa mashamba.

 

Akizungumza wakati wa kikao hicho Kamishna wa Uhifadhi - TFS Prof. Dos Santos Silayo alisema kuwa ni wakati sasa umefika kila mmoja kutambua wajibu wake katika kuhifadhi misitu iliyopo ili ilete manufaa makubwa katika jamii yote.

 

"Tunashukuru nchi yetu imejaliwa kuwa na misitu yenye ikolojia mbalimbali ambayo kuna mtawanyiko kuanzia maeneo ya chini ya usawa wa bahari ambapo kuna misitu ya mikoko hadi milimani ambapo kuna misitu asili  na ile ya kupandwa inayotupa faida kiuchumi na kimazingira." Prof. Dos Santos Silayo

 

Hata hivyo Kamishna wa Uhifadhi ameongeza kuwa uwepo wa misitu unafaida nyingi na hivyo kila mwananchi anatakiwa kusimamia sheria zilizopo na kuona manufaa makubwa yanayopatikana kutoka katika misitu kwa kuilinda misitu iliyopo ili kuritisha vizazi vijavyo.

 

"Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alitoa maelekezo 15 ya kusimamia mazingira nchini na maelekezo hayo mengi yalikuwa yanahusu misitu na kwasababu hii sekta ya misitu ni sekta ambayo inasaidia sekta nyingine kukua na kuwepo kama vile upatikanaji wa maji na malighafi zitokanazo na mazao ya misitu."Prof. Dos Santos Silayo

 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Saad Mtambule amewataka wananchi wa Wilaya ya Mufindi kuacha kuchoma moto hovyo katika misitu kwani kwa kufanya hivyo kunaleta madhara makubwa katika uchumi na mazingira kwa ujumla.

 

"Wilaya ya Mufindi tumejipanga vilivyo na hakuna mtu yoyote atakayeturudisha nyuma  katika mapambano haya ya kujikinga na matukio ya moto ili kulinda misitu yetu."Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Saad Mtambule

 

"Tumeona tuna adui ambaye ni mkubwa , adui moto ambaye anakatisha tamaa na kutuathiri katika jitihada zinazofanywa na wananchi kwa kupanda miti hivyo umefika mwisho wa matukio haya ya moto wilayani Mufindi na hivyo jitihada zinahitajika kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake katika kulinda misitu yetu" Mhe.Saad Mtambule

 

Kikao hicho kinajumuisha viongozi wote wa Wilaya, Tarafa,kata na vijiji kutoka Wilaya ya Mufindi wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Saad Mtambule.

 

Kikao hicho pia kinajumuisha maeneo ya yanayopakana na Shamba la Miti la Sao Hill  na wadau mbalimbali wa mazao ya misitu waliopo Wilayani Mufindi na Wilaya ya Kilombero- Morogoro na Kilolo-Iringa

 

Kwa upande baadhi ya Wadau walisema kongamano hilo litakuwa na manufaa makubwaa kutokana na wakulima walikuwa wanapata hasara baada ya miti yao kuungua na moto

RC MALIMA AIPONGEZA REA KWA KAZI NZURI WANAYOFANYA

 

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akizungumza na Bodi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijini (REA) Julius Kalolo wa pili kulia na Watendaji wa Wakala huo waliofika ofisini kwake kabla ya kuanza ziara ya kuelekea Kijiji cha Msomera kata ya Misima wilayani Handeni kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Manyema

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Julius Kalolo akieleza mpango wa wakala huo katika Kijiji cha Msomera Kata ya Misima wilayanai Handeni mara baada ya kumaliza ziara ya kukitembelea kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Handeni Mashaka Mgeta na kulia ni Mbunge wa Jimbo la  Handeni Vijijini John Salu
Mkurugenzi wa REA Mhandisi Hassan Saidi akizungumza jambo wakati wa ziara hiyo kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Handeni Mashaka Mgeta
Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini (CCM) John Salu akizungumza wakati wa ziara hiyo
KATIBU Tawala wa wilaya ya Handeni Mashaka Mgeta akizungumza wakati wa ziara hiy o kulia ni Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini John Salu


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Julius Kalolo akitoka kwenye moja ya makazi wa wananchi wa Msomera waliotoka Ngorongoro wakati wa ziara yake  wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Handeni Mashaka Mgeta


NA OSCAR ASSENGA,HANDENI

MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima amempongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Julius Kalolo na Watendaji wa Wakala huo kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa sababu imekuwa ni sekta inayotolewa mfano kwa Afria nzima kutokana na utendaji wao.

RC Malima aliyasema hayo wakati Mwenyekiti huyo wa Bodi ,Mkurugenzi wa REA na watendaji wengine walipofika kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Tanga kabla ya kuanza ziara ya kutembelea Kijiji cha Msomera kilichopo wilayani Handeni ili kujionea maendeleo na hali halisi na ili kupata taarifa zitakazoiwezesha bodi kukaa na kuiridhisha mambo muhimu na ya msingi ambayo yatafanya mazingira ya makazi kuwa na mazuri.

Alisema kwamba kutokana na kazi nzuri inayofanywa na wakala huo na kuwa mfano kwa Afrika Nzima zipo taasisi zinatamani kuja kujifunza kazi nzuri mlivyofanya hivyo nitumie fursa hii kuwapongeza sana huku akiwataka kuendeleza kasi hiyo.

“Lakini nichukue ahadi kwamba hao wakandarasi mnaofanya kazi na gharama za vifaa vinavyotumika sio ndogo huu ni uwekezaji mkubwa ambao unafanywa na serikali faida ni wananchi kupata umeme,niwapongeza isipokuwa miradi hiyo ina kipindi cha miwezi 18 wamepewa niwaambie kwamba Serikali ya Mkoa itaendelea kushirikiana nayi kusimamia miradi hii”Alisema

“Katika kikao chetu cha leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Mtendaji Mkuu wa Rea na wakandarasi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na REA mkoa huo tumepata muda wa kukaa na kushauriana nasuala mbalimbali ya utekelezaji bora wa miradi ya hii kwenye mkoa huo “Alisema

Aidha alisema wapo wanahabari hivyo niwaambie kwenye kazi mbalimbali zinazoendelea hakuna wilaya ilitakayokosa mradi wa rea hilo ndio kubwa na wanamshukuru Rais Samia Suluhu,Wizara ya Nishati na REA kwa kazi kubwa wanayofanya kuhakikisha nchi nzima huduma ya umeme inafika kwa wananchi.

Awali akizungumza wakati akiwa eneo la Msomera wilayani Handeni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Wakili Julius Julius Kalolo alisema kwamba Serikali wa kuomba baadhi ya watu wa Ngorongoro kuhamia eneo hilo kwa vyoyote mahitaji ya nishati vijijini yamekuwa makubwa kuliko ambavyo walivyokuwa wametengeneza kwenye bajeti yao.

Alisema hivi sasa wataweze kupitisha bajeti ya nyongeza kuhakikisha miundombinu ya nishati katika eneo la Msomera inakwenda vziuri kwa kuzingatia mfumuko wa wakazi wa eneo hilo ilikuwa lazima yeye na Mkurugenzi wa REA na watendaji wafika waone hali halisi na kupata taarifa kamili ili kuiwezesha bodi kwenye kukaa na kuiridhisha mambo muhimu na ya Msingi.

“Tutafanya mazingira ya makazi kuwa na mazuri na hawatawapa shida kwani wakazi walioamua wenyewe kuhamia eneo hili ili wasione kama wametengwa kilio cha muda mrefu maeneo yake mengi hayana huduma ya nishati vijijiji kwa kuwa hili lilijitokeza wakaona huu ndio wakati wake waende wajione ili waweze kutimiza azma ya kueneza nishati vijijini.

“RC ametupa maagizo ambayo tutakuwenda kuyafanyia kazi kuhakikisha nishati ya umeme inafika Kijiji cha Msomera na maeneo mengine hapa na hii ni hatua ya kwanza lakini bado kuna hatua nyengine ikiwemo mpango mwengine wa kuleta nishati mbadala kwa ajili ya kupikia ili kurahisisha maisha ya waakzi wa eneo hilo”Alisema

Naye kwa upande Mkurugenzi wa REA Mhandisi Hassan Saidi alisema wamefika eneo la Msomera ambacho kimetengwa kwa watanzania kutoka Ngorongoro Arusha na Taasisi mbalimbali zipo hapo kwa ajili ya kutoa huduma na wao wameona wahusike kuboresha huduma ya umeme kutoka kila kilomita 30 na tayari kilomita 15 zimeshakamilika na tano za hapa zimekamilika na Transoma ipo tayari kuwashwa na mradi utaendelea katika maeneo hayo ya msomera.

Mhandisi Hassan alisema mradi ambao wameufanyia kazi ni wa awamu ya tatu mzunguko wa pili kama alivyosema Mwenyekiti huo mradi upo kila kijiji kilipewa kilomita 1 ukiangalia hiyo haitoshi lakini azma yao ni kufikisha huduma ya umeme kwenye vijiji.

Alisema mpango wake ni kuhakikisha vijiji vyote vya Tanzania Bara vinafikishiwa umeme azma ya kwanza ni kufikisha umeme kwenye vituo vikubwa na kusambaza umeme kwenye majumbani wanafanyia kaz.

Hata hivyo alisema serikali imehaidi kuwapatia fedha hivyo wananchi wasiwe na hofu kila kijiji kitapata umeme na wanatarajia kufikia wateja wengi zaidi na kwa mkoa wa Tanga zaidi ya mradi wa Rea 111 ,11 wana mradi wa ujazilizi.

WAZIRI AWESO ATOA MAAGIZO KWA WAKUU WA TAASISI SEKTA YA MAJI

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wakaguzi wa ndani Sekta ya Maji.


WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewataka wakuu wote wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maji kuhakikisha Wakaguzi wa Ndani wanapata rasimali zote muhimu zitakazowawezesha kutekeleza wajibu wao kwa uhuru na ufanisi.

Waziri Aweso ametoa maelekezo hayo Juni 13, 2022 Jijini Mwanza alipokuwa akifungua kikao kazi cha siku sita cha Wakaguzi wa Ndani wa taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Maji.

Mwenyekiti wa Wakaguzi wa Ndani wa Sekta ya Maji Tanzania, CPA. Beatus Gulabaganira akizungumza kabla ya kufunguliwa kwa kikao kazi cha wakaguzi wa ndani Sekta ya Maji.
Baadhi ya wakaguzi wa ndani kutoka taasisi mbalimbali katika Sekta ya Maji wakimsikiliza Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao kazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Leonard Msenyele (aliyesimama) akizungumza kwa niaba ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Maji nchini wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wakaguzi wa ndani Sekta ya Maji.
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Maji, CPA Paul Temba akizungumza kabla ya ufunguzi wa kikao kazi cha wakaguzi wa ndani Sekta ya Maji.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na sekretarieti ya kikao kazi cha wakaguzi wa ndani Sekta ya Maji.

 Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na sekretarieti ya kikao kazi cha wakaguzi wa ndani Sekta ya Maji.

Awali akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Mwenyekiti wa Wakaguzi wa Ndani wa Sekta ya Maji Tanzania, CPA. Beatus Gulabaganira alibainisha changamoto mbalimbali zinazowakabili wakaguzi wa ndani wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ili kuzipatia ufumbuzi.

CPA. Beatus alieleza kuwa Wakaguzi wa Ndani wa Mamlaka nyingi za Maji wamewekwa katika nafasi ya chini kimuundo ikilinganishwa na wakuu wa idara jambo ambalo linasababisha wasiwe huru pindi wanapokuwa na wajibu wa kumkagua Mkuu wa idara ambaye yupo juu kimamlaka.

Changamoto nyingine zilizowasilishwa na wakaguzi wa ndani katika kikao hicho mbele ya Waziri Aweso ni kutokuwa na vitendea kazi muhimu ikiwemo usafiri, kutokuwa na uelewa wa matumizi ya mifumo ya kielektroniki pamoja na miongozo mbalimbali kutokana na kutopewa mafunzo na kutopata fursa ya kushiriki vikao vikuu vya maamuzi vya taasisi suala ambalo linawasababishia kushindwa kutoa ushauri kabla maamuzi hayajafanyika.

Waziri Aweso alizipokea changamoto hizo na kuahidi kuzifanyia kazi ambapo aliwaelekeza wakuu wote wa taasisi za maji kutengeneza mazingira rafiki yatakayowezesha ofisi za wakaguzi wa ndani kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ili kuleta tija iliyokusudiwa. 

Akizungumzia suala la usimamizi wa miradi ya maji, Waziri Aweso aliwaelekeza wakaguzi wa ndani wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maji kuhakikisha fedha za miradi zinatumika kama ilivyokusudiwa ili kuleta matokeo chanya.

Alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan  ameonyesha imani kubwa kwa Wizara ya Maji na kwamba ni jukumu la kila mtumishi katika Sekta ya Maji wakiwemo wakaguzi wa ndani kuhakikisha imani hiyo ya Mhe. Rais haipotei.

“Mmeshuhudia namna ambavyo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, alivyotuamini kwa kutupatia fedha nyingi za ujenzi wa miradi, ni wajibu wetu kuhakikisha hatuipotezi imani hiyo kwake kwa kuhakikisha tunatekeleza majukumu yetu kwa weledi kwa kusimamia vyema ujenzi wa miradi,” alielekeza Waziri Aweso.  

Aliwaelekeza kutumia ujuzi na uzoefu wao kujiuliza na kufuatilia endapo fedha iliyotengwa kwa dhumuni la kutekeleza miradi imetumika ilivyokusudiwa na kama inaleta matokeo chanya.

Waziri Aweso alisema kuwa wakaguzi wa ndani ni jicho la Wizara kwani kupitia wao hatua mbalimbali za utekelezwaji wa miradi na matumizi ya fedha kwenye ujenzi wa miradi unakuwa bayana na hivyo aliwataka kutambua jukumu lao la msingi bila kumuonea mtu.

“Mkaguzi wa ndani ni jicho la taasisi, sasa hakikisheni jicho hilo sio chongo; mnapaswa kumulika viashiria vyoyote vya matumizi mabaya ya fedha za miradi na kuishauri taasisi nini kifanyike sio kusubiri hadi mambo yaharibike,” alisisitiza Waziri Aweso.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Leonard Msenyele akizungumza kwa niaba ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Maji nchini, aliwaasa wakaguzi wa ndani kuhakikisha wanatimiza majukumu yao kwa weledi.

“Kwa niaba ya wenzangu tunaahidi kuendelea kushirikiana nanyi, kama alivyosema Mhe. Waziri Aweso ninyi ndio jicho letu msituangushe nasi hatutawaangusha tunatambua umuhimu wenu,” alisema Mhandisi Msenyele.

Kwa upande wake Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Maji, CPA Paul Temba alimshukuru Waziri Aweso kwa kutenga muda wake kuja kuzungumza na wakaguzi wa Ndani wa taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Maji licha ya kuwa na majukumu mengine mengi ya kitaifa.