ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 18, 2022

KARSAN ATANGAZA KUSTAAFU UKURUGENZI UTPC.

 AFUNGUKA MENGI:- NILIWAHI KUFUKUZA MTU KAZI KISHA BAADA YA MUDA AKAFARIKI DUNIA, ILINIUMA SANA, HATA UKINIKOSEA VIPI SIWEZI KUKUFUKUZA.

NA ALBERT G. SENGO /MWANZA Mkurugenzi wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan amesema anatarajia kustaafu kazi hiyo ifikapo Desemba mwaka huu baada ya kuitumika kwa muda wa miaka 19. Karsan aliyekuwa akizungumza wakati akifungua mkutano wa kuthibitisha kanuni za maadili ya uandishi wa habari mtandaoni na vyombo vya habari vya kawaida leo Juni 17 2022, Karsan amesema amechukua uamzi huo toka mwaka jana na tayari taratibu za kumpata mkurugenzi mpya atakayeiongoza taasisi hiyo umeshafanyika. Amesema uamuzi wa kustaafu ameuchukua toka mwaka jana na hajasurutishwa na mtu na kwamba anawaachia vijana kuendesha taasisi hiyo ambayo imeanzishwa mwaka 2003. “Nilichukua uamuzi wa kustaafu toka mwaka jana ambapo nilishirikisha viongozi kutoka bodi ya wakurugenzi ambao baada ya kuwaeleza matakwa yangu walinitaka niendelee kuwepo hadi mwishoni mwa mwaka huu, na baada ya kustaafu nitakuwepo nikimwangalia mkurugenzi mpya kwa takribani miezi mitatu,” amesema Karsan huku akiwataka waandishi wa habari kutoa ushirikiano kwa mkurugenzi huyo ambaye tayari ameshapatikana.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.