Uongozi na wafanyazi wa Jembe Media Limited Tunasikitika Kutangaza Kifo cha Mpenda wetu JIMMY KAGARUGI maarufu JIMMY K kilichotokea asubuhi ya Jumatatu ya tarehe 20/06/2022 wakati akiwa njiani kukimbizwa Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana (Butimba).
Jimmy Kagaruki ambaye alisikika Kupitia Kipindi cha MCHAKAMCHAKA Jumatatu hadi Ijumaa Saa 12 asubuhi hadi Saa 3 na SANTURI kinachoruka hewani kila Jumapili Saa 4 hadi Saa 6 mchana, alisifika kwa umahiri wake wa kuwasilisha taarifa na kufafanua masuala mbalimbali ya kijamii, burudani, siasa na uongozi.
Hakika huu ni mstuko mkubwa kwetu lakini kama maandiko yasemavyo 'shukuruni kwa kila jambo' nasi hatunabudi.....!
Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa Jina lake lihimidiwe🙏🏼🌱🕊
#RIPJIMMYK
#RIPFBI
CC:- @jembefmtz
@jembenijembe
@kikotifred
@gijegije
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.