ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 12, 2015

VIDEO ZA SHUGHULI NZIMA YA KUAPISHWA KWA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI.

Fuatilia hafla ya kuapisha baraza la mawaziri inayoendelea katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaa.
Mawaziri wapya wakishiriki katika zoezi la kula kiapo mbele ya rais Magufuli jijini Dar es Salaam.

Ni baraza lililosheheni watendaji watiifu na waadilifu ambao watajiunga pamoja na Rais Magufuli kutumikia wananchi.
Ni kiapo kinachojumuisha umanifu na utunzaji wa siri za baraza la mawaziri sanjari na utendaji mzuri wa kazi za Taifa.

TRAFFIC MWANZA ATUMBUKIZA BAJAJI DEREVA WA BODABODA MTARONI ....JEH UNARIDHIKA NA UTENDAJI KAZI WA TRAFFIC WAPYA MKOANI PAKO?

Kupitia kipindi cha KAZI NA NGOMA ya JEMBE FM Mwanza stori ya Traffic aliyetumbukia mtaroni akiendesha bajaji ya mizigo aliyoikamata kutoka kwa dereva wa bodaboda imesikika, nini kisa na mkasa kwa ufupi ni kwamba> Mara baada ya kumkamata mwendeshaji Hamisi Omary kwa kusa la kupakia mzigo mkubwa wa mbao alimwamuru kulipa faini ya shilingi elfu 30, naye Hamisi akamwomba msamaha kwa Traffic huyo kwamba ni fedha nyingi sana ambayo hawezi kuilipa kwa hata kipato anachokipata toka kwa tajiri aliye mpa mzigo kuusafirisha toka eneo moja hadi jingine.

Traffic huyo akauliza kuhusu leseni, dereva huyo akaonyesha,....leseni ya biashara akaonyesha....

Traffic huyo alipoona hakuna kosa jingine akarudi kwenye kosa la kwanza, akitumia kauli ya "Siwezi kukusamehe, nakulipua huku nacheka"   
Mwendeshaji Hamisi Omary akizungumza nasi kilichotokea.
BOFYA PLAY. Ili kujua kisa na mkasa hatimaye Traffic huyo mwenye namba (Zimehifadhiwa) kuitumbukiza bajaji hiyo mtaroni.
Wananchi wakisaidiana kuitoa bajaji hiyo mtaroni mara baada ya mvutano wa mabishano kutaka michoro ya usalama barabarani ifanywe na matraffic waliokuwa zamu kutokea na hatimaye kufanyika.
Bajaji yenye namba....
Eneo la ajali ni kiunganishi cha barabara ya Makongoro Airport na kushuka Uwanja wa CCM Kirumba, karibu na Mwanza City Mall, lilizungukwa na wadau wa bodaboda.

Kwa sasa mkoani Mwanza na maeneo mbalimbali nchini kuna baadhi ya sura mpya za wanausalama wa vyombo vya usafiri barabarani ambapo licha ya wale wakongwe waliohamishwa toka mkoa mmoja kwenda mwingine pia kuna wapya waliotoka vyuo vya jeshi nchini. 

Swali kuu ni>Jeh baadhi ya wadau hawa wa usimamizi wa usalama wa vyombo vya usafiri barabarani wanazisimamia kweli sheria ipaswavyo, Jeh wanafanya kazi zao vipi na kwa hali gani, kwa nia ya kuonya, kuelimisha au kukomoa?

Friday, December 11, 2015

MANCHESTER UNITED YATUPWA NJE MICHUANO YA KLABU BINGWA ULAYA.

 Machester United imeaga michuano ya klabu bingwa Ulaya baada ya kukubali kipigo cha bao 3 kwa 2 dhidi ya Wolfsburg ya Ujerumani.   

ALIYEKUWA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SUMVE AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUGUSHI NA UTAPELI.

Thursday, December 10, 2015

JINSI WAFANYAKAZI WA TIGO WALIVYOSHIRIKI ZOEZI LA USAFI 9 DEC 2015

Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Mawasiliano ya simu Tigo Bwa. Edgar Mapande akifanya usafi katika moja ya mitaro sugu ipitishayo maji barabara inayoingia katika moja ya mitaa inayounganisha Soko la Mwaloni Kirumba jijini Mwanza, katika kuadhimisha sherehe za Uhuru wa Tanganyika ambapo safari hii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufu aliamuru maadhimisho hayo kuadhimishwa kwa style ya kufanya usafi.
Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Mawasiliano ya simu Tigo Bwa. Edgar Mapande akiongoza wafanyakazi wenzake kuondosha uchafu ulioziba katika moja ya mitaro sugu ipitishayo maji barabara inayoingia katika moja ya mitaa inayounganisha Soko la Mwaloni Kirumba jijini Mwanza, katika kuadhimisha sherehe za Uhuru wa Tanganyika ambapo safari hii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufu aliamuru maadhimisho hayo kuadhimishwa kwa style ya kufanya usafi.
Hali safi ya uhai katika usafi imeanza kuonekana.
Hapa ndipo eneo korofi zaidi kuliko maeneo yote.
Uhuru na usafi.
Zoezi hili lilifanyika kwa ushirikiano wa aina yake kwani hata majirani walio karibu na eneo hilo waliungana na wafanyakazi wa Tigo kukamilisha majukumu ya usafi.
Zoezi la hili la usafi lililofanywa na wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya simu za mkononi Tigo tawi la Mwanza lilihamasisha wadau mbalimbali wa maeneo yote karibu na soko la Mwalo wa Kirumba kufanya usafi kwa jitihada ya kupata mazingira yenye mwonekano sahihi....

CCM YAMSIMAMISHA JAMES BWIRE KUWANIA NAFASI YA MEYA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu CCM wilaya ya Nyamagana katika uchaguzi wa kumsaka diwani atakaye simama kwa tiketi ya chama hicho kuwania nafasi ya Meya wa Halmashauri ya jiji la Mwanza uliofanyika leo jijini hapa.
Diwani wa Kata ya Nyamagana mjini akitoa shukurani zake mbele ya wajumbe wa mkutano wa uchaguzi mara baada ya kuinyakuwa tiketi ya CCM kuwania nafasi ya unaibu Meya wa Halmashauri ya jiji la Mwanza.
Diwani wa Kata ya Mahina, James Bwire, akitoa shukurani kwa wajumbe mara baada ya kuitwaa tiketi ya kuwania U'Meya wa  Halamashauri ya Jiji la Mwanza kupitia CCM.


Kutoka kushoto ni Charles Nyamasiriri, Yahya Shalia ambaye ni mchumi CCM Wilaya ya Nyamagana na Kaimu Katibu wa UWT wilaya ya Nyamagana.
Sehemu ya wajumbe wa mkutano.
Kutoka kushoto wadau meza kuu Katibu msaidizi CCM (W) Iddi Mkowa, Katibu wa UVCCM Mkoa Philipo Elieza, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga na Katibu Mwenezi  Mustapha Banigwa.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nyamagana Raphael Shilatu akitoa maelekezo kwa wajumbe wa uchaguzi huo.
Pongezi.
Shangwe na pongezi.

NA PETER FABIAN, MWANZA.

MADIWANI wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya na Jimbo la Nyamagana LEO wamewachagua, Diwani wa Kata ya Mahina, James Bwire, kuwa mgombea nafasi ya Meya wa  Halamashauri ya Jiji la Mwanza na Diwani wa Kata ya Nyamagana, Bikhu Kotecha, kuwania nafasi ya Naibu Meya.

Bwire alichaguliwa kugombea nafasi ya Meya kwenye kikao cha madiwani wa chama hicho kilichoketi leo katika ofisi za CCM Wilaya ya Nyamagana na Kotecha kuwania nafasi ya Naibu Meya baada ya majina kurejeshwa na Kamati Kuu ya CCM Taifa ili kumpata mshindi ambaye atachuana na wagombea wa nafasi hizo kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Msimamizi wa Uchaguzi huo, Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Idd Mkowa, kabla ya kutangaza matokeo hayo alisema kwamba wagombea watatu ambao ni madiwani, James Bwire (Mahina) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shule ya Alliance ya jijini mwanza inayomiliki pia Kituo cha michezo cha Alliance, John Minja (Igogo) na Dismas Ritte (Mkolani) majina yao yaliteuliwa na Kamati kuu ya CCM taifa ili kufanya uchaguzi ndani ya Chama na kupata mshindi.

Mkowa alisema kuwa Kamati Kuu ya CCM taifa pia iliwateuwa madiwani wawili, Bikhu Kotecha (Nyamagana) na Edithy Mdogo (Nyegezi) kuwania nafasi ya Naibu Meya na Katibu wa madiwani wa Chama hicho waliteuliwa diwani Donatha Gapi (Mkuyuni) na Mahamod Jama (Mbugani) ili kumpata mmoja atakayekuwa Katibu kwenye vikao vya madiwani wa Chama hicho Jimbo la Nyamagana.
Katibu huyo msaidizi anayekayimu nafasi ya Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana  akitangaza matokeo hayo alisema kwamba nafasi ya Meya Diwani Bwire amepata kura15 na kuibuka mshindi dhidi ya wapizani wake, Minja aliyepata kura 4 na Ritte aliyeambulia kura moja ya kwake pekee,nafasi ya Naibu Meya, Diwani Kotecha ameibuka mshindi kwa kura 16 na mpinzani wake Mdogo akipata kura 4.

Mkowa alimtangaza Gapi kushinda nafasi ya Katibu wa Madiwani wa Chama hicho kwa kupata kura 11 dhidi ya Jama aliyepata kura 9, pia aliwapongeza wagombea na madiwani kwa kutumia demokrasia ya kuwachagua viongozi hao ili kuhakikisha wanashirikiana kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Nyamagana.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akizungumza na wajumbe wa mkutano wa baraza la madiwani wilaya ya Nyamagana katika uchaguzi uliofanyika leo jijini hapa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga, aliwataka viongozi hao na madiwani kuweka pembeni tofauti zao na badala yake wajikite kuwatumikia wananchi kama walivyowaahidi wananchi wakati wa kampeni pia kuendana na kasi ya Rais Dk John Magufuli, kuhakikisha Halmashauri ya Jiji haipati hati Chafu na iweke mipango ya maendeleo.


Kwa upande wake Meya aliyemaliza muda wake ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (CCM) amewapongeza viongozi hao waliochaguliwa na madiwani wenzake na kuwaomba ushirikiano ili kutekeleza mahitaji ya wananchi bila kuwabagua kwa namna yoyote ile zaidi ya kuwaunganisha katika jitihada za maendeleo katika Mitaa, Kata na Jimbo hilo.

Madiwani, James Bwire (kushoto) aliyechaguliwa kugombea nafasi ya Meya wa Jiji la Mwanza, Diwani Donatha Gapi (katikati) aliyechaguliwa kuwa Katibu wa Madiwani wa CCM na kulia ni Diwani, Bikhu Kotecha aliyechaguliwa kugombea nafasi ya Naibu Meya jana kwenyekikao cha madiwani wa chama hicho.
Kesho Ijumaa utakuwa uzinduzi wa baraza la madiwani wa Jiji hilo ambao kikao cha uzinduzi kitaanza majira ya saa 3.00 asubuhi kwa kuapishwa madiwani wote wa Kata 18 za Jiji hilo pamoja na madiwani wa Vitimaalum kutoka vyama vya CCM na CHADEMA waliochaguliwa kabla ya uchaguzi wa Meya na Naibu Meya ambapo vyama hivyo vitawashindanisha wagombea wake waliochaguliwa na vikao vya madiwani ndani ya vyama hivyo.

CCM inao madiwani walioshinda katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu kutoka Kata 14 kati ya 18 na CHADEMA wakiwa na madiwani Kata 4 huku CCM ikipata madiwani wa Vitimaalum 5 na CHADEMA wakiwa na Vitimaalum 1 hivyo kwa uchaguzi wa Meya na Naibu Meya CCM wakiwa na nafasi kubwa kutwa uongozi wa Jiji hilo.

BARAZA LA HALAMSHAURI YA WILAYA YA MOSHI LAMCHAGUA MICHAEL KILAWILA KUWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI.

Wajumbe wa baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,wakiwa ukumbini hapo kabla ya kuapishwa.
Baadhi ya wajumbe wa baraza hilo kabla ya kuapishwa.
Wajumbe wa baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,wakiapishwa kuwa madiwani rasmi.
Katibu tawala wilaya ya Moshi,Remida Ibrahim akiongoza zoezi la upigaji kura kwa ajili yakumpata Mwenyekiti na Makamu wake wa Halmashauri hiyo.
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akiteta jambo na Diwani wa kata ya Kahe ,Rodrick Mmanyi wakati wa kikao cha baraza hilo.
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akipiga kura wakazi wa zoezi hilo.
Wajumbe wakishiriki zoezi la upigaji kura.
Diwani wa kata ya Mabogini Emanuel Mzava akimpongeza Diwani wa kata ya Kindi,Michael Kilawila baada ya kutangazwa mshindi kwa kupigiwa kura 36 .
Madiwani wakifurahia mara baada ya kuvaa joho rasmi kwa ajili ya uzinduzi wa baraza hilo.
Mwenyekiti mpya wa baraza la Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila akiongozana na Makamu wake ,Exaud Mamuya wakati wakiingia katika ukumbi wa baraza hilo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Fulgence Mponji akitoa muongozo wakati wa uzinduzi rasmi wa baraza hilo.
Mwenyekiti wa baraza la Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila akitoa hotuba yake ya kwanza wakati wa uzinduzi rasmi wa baraza hilo.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza la Halmashauri ya wilaya ya Moshi.
Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro ,Severine Kahitwa akitoa maelekezo mbalimbali ya uendeshaji wa baraza hilo kwa Madiwani na uongozi mpya wa baraza hilo.
Menyekiti wa Chadema wilaya ya Moshi vijijini Ekarist Kiwia pia alikuwa ni miongoni mwa mashuhuda wa mchakato wa kumpata Mwenyekiti wa Halmashauri.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi ,Michael Kilawila.
Ndugu wa madiwani wakifurahia nje ya ukumbi wa Hlamshauri ya wilaya ya Moshi mara baada ya Madiwani kuapishwa.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kakskazini (0755659929).