NA PETER FABIAN, MWANZA.
MKURUGENZI na Mmiliki wa shule binafisi ya Ntunduru,
Richard Mchele na mwanamke mmoja wamekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kugushi
Hati ya nyumba na Nyaraka ili kujipatia nyumba moja kwa utapeli Mjini Sengerema
na kutaka kuiuza kwa mtu mwingine Wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Taarifa za kukamatwa kwa Mchele ambaye
aliyekuwa mgombea Ubunge Jimbo la Sumve kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF)
katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu walikamatwa na Polisi baada ya
kuwepo taarifa za yeye na mwanamke mmoja anayedaiwa kuwa na mahusiano naye ya
kimapenzi kula njama za kugushi Hati ya nyumba na nyaraka ili kujipatia nyumba
mali ya Mkama Magesa wa mkazi wa Sengerema.
Mchele alikuwa akitafutwa kwa muda na
mlalamikaji Mkama na Polisi na kufanikiwa kukamatwa mjini Sengerema akiwa na
mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina lake na kisha kusafilishwa hadi jijini
Mwanza ambako alifunguliwa jarada la uchunguzi RB MW/IR/750/2015 lililofunguliwa Kituo cha
Polisi Kati Nyamagana na Mkama.
Habari zilizothibitishwa na Kaimu Kamanda wa
Polisi mkoani Mwanza, Augustino Senga, alikili kuwepo taarifa za kukamatwa watuhumiwa
hao ambao walikuwa wakisakwa kwa muda mrefu na mlalamikaji kwa kushirikiana na
Polisi ili kukabiliana na tuhuma zinazomkabili yeye na wenzake walifunguliwa jarada la uchunguzi katika kituo
cha Polisi mjini Kati.
“Ni kweli Mchele na mwenzake tumewakamata,
wakati wowote watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kughushi hati na nyaraka
za nyumba isiyokuwa yao na kutaka kuiuza kitapeli kwa mtu mwingine,” alisema
Senga bila kumtaja mnunuzi huyo.
Senga ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi Makosa
ya Jinai (RCO) mkoani Mwanza, alieleza kwamba watuhumiwa hao akiwemo mwanamke
mmoja ambaye anadaiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mchele, walikamatiwa
wilayani Sengerema na kusafirishwa hadi jijini Mwanza.
Alifafanua kuwa Mkama alipata taarifa za
kutaka kuuzwa kwa nyumba yake kutoka kwa wasamilia wema ambao walidai hati ya
nyumba hiyo imeandikwa jina la mwanamke huyo ambaye ana mahusiano naye badala
ya mtu aliyemuuzia Magesa, sasa Polisi inaendelea na upelelezi na wakati wowote
itawafikisha Mahakamani kujibu tuhuma za kosa linalowakabili.
Mchele aligombea ubunge wa jimbo la Sumve
katika uchaguzi Mkuu uliopita wa Oktoba 25 mwaka huu kupitia CUF akitokea CCM akishindana
na Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (CCM) katika mchakato wa kura za maoni ndani
ya CCM kabla ya kushindwa kwenye uchaguzi mkuu tena uliopita.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.