ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 24, 2013

SHUHUDIA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 MKOANI TABORA


Msanii machachari wa muziki wa bongofleva/filamu Shilole akiimba huku akiwa amebebwa na shabiki wake,huku shangwe na miluzi za mashabiki zikiwa zimetawala kila kona.
Baadhi ya mashabiki waliojitokeza kucheza jukwaani,wakionesha umahiri wao wa kukata nyonga mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Tabora na vitongoji vyake,waliojitokeza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi.


Anajiita Raisi wa Manzese,kutoka  kundi la Tip Top Connections,atambulikae kwa jina la Madee akiwaimbisha mashabiki wake wimbo wake wa NANI KAMWAGA POMBE YANGU, kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.

Mashabiki wakiitikia kwa pamoja huku mikono yao wakipunga hewani.

Mmoja wakali wa hip hop,Stamina akikamua jukwaani vilivyo usiku huu mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Tabora na vitongoji vyake waliojitokeza kushuhudia makamuzi ya wasanii mbalimbali wa tamasha la Serengeti Fiesta 2013.

bdul Kiba,msanii wa muziki wa bongofleva akiimba mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd kwa kushirikiana na Clouds FM,na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.


Sehemu ya  umati wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Neylee akiimba kwa hisia mbele ya wakazi wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd kwa kushirikiana na Clouds FM,na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.
Linah (katikati)
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Linah pichani kati akiwa na madensa wake wakitumbuiza jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu. 
Sehemu ya  umati wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.
Anaitwa Amin, mmoja wa wasanii mahiri akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu kwenye u kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu. Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd kwa kushirikiana na Clouds FM,na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.
Wenyewe mashabiki waki wanamuita Baba Levo na yeye kabaki Levo kwenye gemu ya muziki wa bongofleva,ndiye pichani Baba Levo akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani Tabora.
Ni shwangwe tu usiku huu kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani Tabora.
Wakali wa kudansi kutoka THT,wakijulikana kwa jina la Makomando wakionesha umahiri wao wa kucheza jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.

Wanamuita Mzee wa Masauti,Christian Bella akiwaimbisha mashabiki wake wa muziki wa dansi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta,liinalofanyika usiku huu kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi.
Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Tabora waliojitokeza usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 wakiwa wamewasha tochi za simu zao wakiashiria kushoo love ya pamoja
Msanii wa muziki wa bongofleva,Rachael akicheza jukwaani na mmoja wa madensa wake,huku mashabiki wake wakipiga mayowe ya shangwa kuonesha kukunwa vilivyo na msanii huyo.

Sehemu ya  umati wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd kwa kushirikiana na Clouds FM,na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.

JIJI LA MWANZA LIMEPIGA MARUFUKU KUPANGA BIDHAA NJE YA MADUKA

Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Alifa Hassan Hida (kushoto) akitoa tamko kwa waandishi wa Habari wengine wanaoonekana katika picha ni baadhi ya wadau wa kikosi kazi cha kutekeleza mpango kazi wa kuwapanga wamachinga na kuwaondoa maeneo yasiyoruhusiwa.
Na Peter Fabian
MWANZA.

HALMASHAURI ya Jiji la Mwanza imepiga marufuku na kuagiza wamiliki wa maduka makubwa na madogo kuacha kupanga bidhaa zao nje ya maduka yao na kuwataka wamachinga wote wanaofanya biashara kwenye njia za watembea kwa miguu kando ya barabara za Kenyata na Nyerere kupisha maeneo hayo.

Agizo hilo limetolewa jana na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Halifa Hida kwa waandishi wa habari ofisini kwake, alisema kwamba hatua hiyo inafuatia Jiji hilo kutoa muda wa miezi miwili ya kuwataka wafanyabiashara wadogo (Machinga) kufanya biashara zao kwenye maeneo waliyotengewa badala ya kuanza kuzagaa na kupanga bidhaa kiholela.

Mkurugenzi Hida alieleza kuwa kuanzia kesho wataanza kutekeleza sheria ndogo namba 8 ya Mipango Miji ya mwaka 2007 na sheria ndogo ya Usafi wa Mazingira ya mwaka 2010 pamoja na kuendelea kulinda na kulipatia Jiji la Mwanza Hadhi ya Kimataifa itakayoleta fursa mbalimbali za kiuchumi na kuendelea kuwanufaisha wananchi wake.

“Wananchi wetu kupitia sekta za Utalii,Biashara, Ujenzi wa vitega Uchumi na Uwekezaji katika Jiji letu ili kutuingizia mapato na kuboreshwa mazingira ya upatikanaji huduma kwa wananchi za kiwango cha kitaifa na kimataifa likiwa na mwonekano wenye Hadhi kuendana na kasi ya ukuaji wake.

Hida alifafanua kuwa katika utekelezaji huo ambao unaambatana na Mpango kazi unaozingatia suala la kuwapanga wamachinga ikiwa ni mwendelezo ulioanza tangu mwaka 2007/2008 ili kufanikisha zoezi hili na kuhakikisha Jiji linakuwa kwenye mpangilio mzuri na kila eneo la Mji linatumika kama ilivyokusudiwa.

“Jiji tayari limeisha boresha maeneo ya yaliyotengwa kwa ajili ya masoko ya wafanyabiashara wadogo (Machinga) kwa kuweka miundombinu mwafaka ya vyoo, maji na vituo vya daladala lakini masoko hayo yamekuwa hayatumiki na kutelekezwa jambo ambalo limewafanya vijana wengi kufanya biashara kiholela katikati ya Mji”alisema.

Alieleza kuwa Jiji lake litaendelea kubaini na kuyaendeleza maeneo yaliyoruhusiwa kwa wafanyabiashara wadogo, kuainisha maeneo yasiyoruhusiwa kwa shughuli za biashara za machinga, kuondoa kero nyingine na kuondosha huduma za chakula kwenye vichocholo vya wazi na magenge sehemu mbalimbali zisizoruhusiwa kuwepo huduma hiyo.

“Wamiliki wa maduka tumeisha wapatia muda wa kutosha na kuwatangazia kuwa wanatakiwa kupunguza kero za kutoweka bidhaa zao nje ya maduka, kuweka mapipa ya plasitiki ya kuhifadhia taka pamoja na kuhakikisha mitaro iliyo mbele ya maduka yao haichafuliwi kwa taka ngumu au maji kutuama”alisisitiza

Aliyataja maeneo yasiyoruhusiwa kwa shughuli za wafanyabiashra wadogo kuwa ni maeneo yote ya Mzunguko wa Mjini kati  karibu na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) barabara ya Nyerere hadi Nyamhongolo, Pamba kuanzia mzunguko wa mnara wa Nyerere, barabara kuelekea Kanisa Katoliki la Bugando hadi maungiyo ya barabara ya Kenyata.

Barabara zingine alizitaja ni Rwagasore, Lumumba, Karuta, Kenyata, Stesheni ya Reli, Soko kuu la Mjini kati, eneo la stendi ya zamani ya Tanganyika pamoja na maeneo yote ya watembea kwa miguu kwa barabara za Nyerere, Kenyata,Uwanja wa Ndege, Aghakan na kwenye nyumba za ibada za madhehebu mbalimbali.

Mkurugenzi Hida alisema kuwa maeneo yaliyotengwa yataendelea kutumiwa na wafanyabiashara wadogo kuwa ni maeneo ya Mirogo (Community Center), Makoroboi, Uchochoro wa Tanganyika,Stendi ya zamani ya Mkuyuni, barabara ya vitunguu soko kuu, Asante moto, barabara ya Pamba chini (Daraja-White Pub), Market Street na Stendi ya Nyegezi.

“Biashara ya samaki haitaruhusiwa kwenye maeneo hayo na watakao kwenda kinyume na maelekezo ya mpango huo wa kuwapanga wamachinga na wafanyabiashara wamiliki wa maduka makubwa na madogo Jiji litatumia sheria kuhakikisha taratibu hizo zinafuatwa na halitakuwa tayari kukubaliana na wanasiasa kutumia mwanya wa kuwarejesha kwa manufaa ya kujipatia umaarufu”alisisitiza.

Amewataka wananchi na wafanyabiashara wote wakiwemo machinga na mama lishe kutoa  ushirikano kwa wataalamu wa Idara ya Mipango Miji na askari Polisi na wale mgambo wa Jiji wakati wa kuhakikisha mpango wa zoezi hilo unatekelezwa kama ilivyokusudiwa ili Jiji liendelee kuwa safi na kunyakuwa tena tuzo ikiwemo usafi wa jumla wa kila jumamosi ya kwanza ya kila mwezi

Friday, August 23, 2013

KUMVUA UANACHAMA MEYA MATATA - CHADEMA YAANGUKA CHALI MAHAKAMANI, PINGAMIZI LAKE LATUPILIWA MBALI.Meya Henry Matata (katikati) wakati akiendesha moja kati ya vikao vya Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Ilemela, kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Zuberi Mbyana na kushoto ni Naibu Meya Dede Swila. PICHA NA MAKTABA G.sengo
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mwanza leo imetoa hukumu na kutupiliambali pingamizi la Chama Cha Demkrasia na Maendeleo (CHADEMA) la kupinga kufunguliwa Kesi Namba 13/2012 ya kuwavua Uanachama Makada wake ambao ni Madiwani Mheshimiwa Henry Matata  (Kitangiri)na Mheshimiwa Adamu Chagulani(Igoma) iliyofunguliwa na Makada hao kupinga Kamatiku ya CHADEMA kuwavua uanachama.

Akisoma hukumu hiyo majira ya saa 3:30 asubuhi katika Mahakama kuu hiyo Jaji A.N.M Sumari,Alisema kwamba katika pingamizi hilo lililowasilishwa katika Mahakama hiyo na Wakili Kimomogoro aliyeteuliwa na Chama hicho kuwasilisha kwa niaba ya Kamati Kuu Taifa ya CHADEMA chini ya Kiapo cha Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini  ya Chama hicho na Mjumbe wa Kamati Kuu Slivestar Masinde aliyeteuliwa na Chama.

Utaratibu ulikiukwa kwa Wakili Methord Kimomogoro kujiandalia Kiapo hicho bila kukipeleka kwa mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini kukisaini na kula kiapo kisheria na badala yake kukiwasilisha Mahakamani hapo bila kufuata taratibu hizo za kisheria ambalo ni kosa kwa wakili kutengeneza kiapo na kukiwasilisha bila kumhusisha mtajwa katika kutengeneza kiapo hicho kisheria.

Jaji Sumari alisema kuwa kutokana na Mapungufu yaliyoonekana katika Kiapo hicho ambayo aliyaeleza kuwa ni pamoja na Kiapo alichoapa Masinde kilionyesha sahihi tu na Muhuri bila kuonyesha Jina la aliyetoa Kiapo hicho na kusema kwamba hilo ni pungufu la kwanza na kwa mujipu wa sheria hilo ni kosa na pili Pingamizi hilo liliwasilishwa Desemba 29 mwaka 2012 tayari muda ukiwa umepita wa kufanya hivyo.

Katika madai mengine katika pingamizi hlo yalidai kuwa Walalamikaji Mhe. Matata ambaye kwa sasa ni Meya wa Manispaa mpya ya Ilemela na mwenzake Mhe. Chagulani waliidanganya na kupotosha Mahakama hiyo juu ya kufutwa Uanachama kwa madai kuwa taratibu zote zilifuatwa huku bila kuonyesha ushahidi wa na utetezi wao  zaidi ya Wakili wao kusema pia hawakuwa na uhalali wa kufungua kesi hiyo.

Jaji Katika kunuku mifano ya kesi mbalimbali za aina hiyo na mapingamizi kwenye kesi za ndani na nje kwenye Mataifa ya nje kama ya nchini Uingereza  na ile ya Mhe. Mkosamali iliyokuwa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora aliyokuwa amewekewa pingamizi kama hilo alisema kuwa halikuwa na uhalali na kuamua kulitupilia mbali shauri hilo la pingamizi juu yake na hivyo linamhalalisha naye kufanya hivyo kama ilivyopendekezwa na mawakili wa walalamikaji.

Mawakili watatu maarufu Jijini Mwanza Salum Magongo, Boniphace Matata na Julius Mushobozi wanaowatetea walalamikaji katika kesi No. 13/2012 Mhe. Matata na Mhe. Chagulani walionekana kumzidi mbinu za kisheria Wakili Methord Kimomogoro na kumbana kila kipengele na hatimaye Pingamizi zake alizowasilisha kutupiliwa mbali na kuondolewa ili kutoa nafasi ya Kesi ya Msingi kuanza kutajwa na kusikilizwa.

Awali  CHADEMA kupitia kwa Wakili wake huyo Kimomogoro waliwasilisha madai ya mapingamizi mengine matatu ambapo katika dai la kwanza walidai kuwa walalamikaji waliofungua kesi moja katika Mahakama mbili tofauti na hiyo walikuwa na nafasi ya kukata rufaa kwenye Chombo cha Baraza kuu la wajumbe wa Chama hicho lakini waliamua kukimbilia Mahakamani 

Dai la pili lilieleza kuwa CHADEMA ni Taasisi Binafisi inayojiongoza na kusimamia Mamlaka ya Umma ambapo mtu yeyote anayejiunga nayo ni lazima ukubaliwe na kudhaminiwa na Chama hicho kugombea nafasi ya uwakilishi wa wananchi ukiwa mwanachama wa chama cha siasa na si vinginevyo kwa mujibu wa Katiba ya Chama hicho.

Dai la Tatu Mahakama iliyofunguliwa kesi hiyo Haikuwa na Mamlaka ya kisheria kuiwezesha kusikiliza kesi hiyo hivyo ni vyema ukatupiliwa mbali na kufutwa kwa kuliondosha shauri hilo Mahakamani kwa kuwa waliofungua hawakuwa na uhalali huo.

Maandamano ya hivi majuzi kutaka kumng'oa Meya Matata.
Katika Majibu ya mapingamizi hayo yaliyowasilishwa na Mawakili hao watatu wanaowatetea Mhe.Matata na mwenzake Mhe.Chagulani  Kwanza:-majibu yake yalieleza kuwa Tayari shauri moja lilikuwa limeisha futwa na walalamikaji kabla ya Wakili wa CHADEMA kuwasilisha madai ya mapingamizi yake ya Chama na wateja wake na kunukuu kesi ya Mhe.Mkosamali iliyotolewa hukumu kama hiyo Mahakama kuu ya Tabora.

Pili:-Mahakama hiyo inayo Haki ya Kisheria ya kuiwezesha kusikiliza kesi iliyofunguliwa kwa kuwa taratibu za Taasisi ya CHADEMA hazikufuatwa za kuwavua Uanachama na kufanyika Kibabe kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA hivyo uhalali wa walalamikaji ni sawa kutafuta haki ambayo itapatikana kwa taratibu za kisheria kwa mujibu wa madai yao na Katiba ya Chama na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee.

Tatu:-Hati ya Kiapo cha Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini nayo ilikuwa na mapungufu na iliwasilishwa nje ya muda wa kisheria uliokuwa unatoa nafasi ya CHADEMA na Wakili wao Kimomogoro kuwasilisha kabla walalamikaji awajafuta kesi hiyo waliyokuwa wameifungua katika Mahakama nyingine isiyokuwa na uwezo wa kuisikiliza kwa mujibu wa taratibu za kisheria.

Kama ilivyodaiwa na wakili wao wa CHADEMA awali, lakini walichelewa na tayari kesi hiyo ilikwisha  ilifutwa katika Mahakama hiyo nyingine na kuhamishiwa katika Mahakama hiyo ambayo inao uwezo wa kuisikiliza kisheria katika hukumu iliyosomwa na kuamuliwa na Jaji A.N.Sumari mwezi Juni 31mwaka jana.

Kufatia hukumu hiyo ya leo Mahakama hiyo kupitia Jaji A.N. Sumarikuwa Kesi ya Msingi na Mahakama hiyo  itaendelea sasa  na taratibu za kuipanga,kutajwa  na kuanza kuisikiliza baada ya kuwajulishwa Mawakili wote wa pande mbili kwa mujibu wa taratibu za kisheria za Mahakama hiyo na kumaliza kusoma hukumu hiyo iliyosomwa kwa dakika 45.

Baada ya kusomwa hukumu hiyo wafuasi wa CHADEMA wakiongozwa na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na Wilaya na Makada wa Chama hicho waliokuwa wamejitokeza kwa wingi katika makundi  walijikuta wakitoka kimyakimya huku wengine wakidai kuwa Wakili wao Kimomogoro ameonyesha udhaifu na hakuwa makini dhidi ya Mawakili wa walalamikaji hivyo wakidai ni vyema akatafuwa wakili mwingine ambaye anaweza kuwasilisha upya pingamizi ndani ya muda uliotolewa na Jaji kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Kijiwe Maarufu Cha KEMONDO kinachojulikana kuwana watu wa kada tofauti na wenye ueledi mkubwa wa kuchambua mambo leo kilikuwa na watu wenye nyuso za huzuni kutokana na kile kilichoshuhudiwa na kufatiliwa kwa umakini Mahakamani wakati Jaji Sumari akisoma hukumu hiyo.

JIONEE YALIYOJIRI NDANI YA KUSANYIKO LA FURSA MKOA WA TABORA...!!

Mghani mahiri wa mashairi hapa nchini Mrisho Mpoto akizungumza kwa msisitizo,masuala ya fursa mbalimbali zinazopatikana katika suala zima la ujasiliamali mapema leo kwenye semina ya Fursa iliyofanyika katika ukumbi wa  Student's Center,uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora mapema leo.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil. 
 Baadhi ya Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakishiriki semina ya Fursa kwa vijana ililiyofanyika leo kwenye ukumbi wa Student's Center katikati ya mji wa mkoa wa Tabora mapema leo,kutoka kulia ni Msanii Godzilla,Baba Levo,Amin,Stamina na wengineo.
 Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya mafuta-Lake Oil,Bwa.Ben Temu akizungumza kwenye semina ya Fursa,ambapo yeye alielezea mambo mbalimbali ikiwemo suala la vijana kuwa wenye moyo wa kujituma na kutokata tamaa,alieleza kwa kuwataka vijana wawe wavumilivu na kutoka tamaa kwa kila fursa wanayokumbana nayo,badala yake waitumie vizuri katika suala zima la kujikwamua na kujiendeleza kimaisha. Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil. 

 Semina ya Fursa ikiendelea mapema leo ndani ya ukumbi wa Student's Center katikati ya mkoa wa Tabora mapema leo.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil. 

 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Mwasiti Almas akizungumzia baadhi ya fursa alizozipata mara baada ya kujiunga na shirika la NSSF,mbele ya Washiriki wa Semina ya Fursa (hawapo pichani),kulia kwake ni Mwakilishi wa NSSF-Makao Makuu Bwa,Salim Khalfan akimsikiliza kwa makini.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil. 
 Mwakilishi wa Shiriki la NSSF kutoka Makao Makuu jijini Dar,Bwa.Salim Khalfan akielezea fursa mbalimbali zinazopatika mara mtu yeyote anayejiunga ama amejiunga na NSSF,alifafanua zaidi kuwa mtu yeyeote atakayejiunga na shirika hilo atanufaika na mambo mengi,ikiwemo suala la matibabu,mikopo na mengineyo lukuki yanayopatikana ndani ya shirika hilo.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil. 

 Baadhi ya Wakazi wa Tabora wakifuatilia kwa makini semina ya ujasiliamali iliyokuwa ikiendelea ndani ya ukumbi wa Student's Center katikati ya mkoa wa Tabora mapema leo
Picha ya pamoja,kiukumbusho zaidi,Msanii Mrisho Mpoto akiwa amepozi na Diamond
 Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Diamond,akiwaimbisha washiriki wa semina ya Fursa waliojitokeza kwa wingi mapema leo kwenye  ukumbi wa Student's Center uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora,kushoto kwake ni Bwa.Marco Vingila kutoka shirika la TPSF. .
 Mmoja wa akina Mama wajasiliamali kutoka mkoa wa Tabora,Flora Zakaria akiwa na bidhaa zake alizozitengeneza yeye mwenyewe kama mjasiliamali,akiuza ndani ya semina ya Fursa.semina hiyo ambayo imewahusisha wadau mbalimbali wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya,wakazi mbalimbali wa mji wa Tabora,Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali.
 Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba,Mkuu wa Wilaya ya Igunga ( Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora),Mh. Elibariki Kingu wakitazama paketi ya sabuti iliyotengenezwa na mjasiliamali aliyehudhuria semina ya Fursa,iliyofanyika kwenye ukumbi Student's Center uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora.
 Wadau wajasiliamali wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo.
  Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba,akizungumza mbele ya washriki wa Semina ya Fursa ndani ya ukumbi  kwenye ukumbi Student's Center uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora.
 Sehemu ya Meza kuu.Kutoka kushoto ni Wawakilishi kutoka shirika la NSSF,Salim Khalfan (makao makuu),Alloys Banigwa (Meneja wa NSSF-Tabora),Mkuu wa Wilaya ya Iramba kutoka Mkoani Singida,Mkuu wa Wilaya ya Igunga,Mh.Elibarik Kingu,Ruge Mutahaba-Clouds Media Group, pamoja na Ben Temu kutoka kampuni ya Lake Oil
 Baadhi ya Wasanii mbalimbali wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye semina ya Fursa,mapema leo mkoani Tabora.

 Baadhi ya wakazi wa Tabora wakiwa kwenye semina ya Fursa ndani ya ukumbi  Student's Center mkoani  Tabora mapema leo,ambapo mada mbalimbali zimezungumzwa,ikiwemo mambo ya ujasiliamali kwa vijana,mikopo,akiba sambamba na namna ya kujiongezea thamani ya fursa unayoipata.