MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mwanza leo imetoa hukumu na kutupiliambali
pingamizi la Chama Cha Demkrasia na Maendeleo (CHADEMA) la kupinga kufunguliwa
Kesi Namba 13/2012 ya kuwavua Uanachama Makada wake ambao ni Madiwani Mheshimiwa
Henry Matata (Kitangiri)na Mheshimiwa
Adamu Chagulani(Igoma) iliyofunguliwa na Makada hao kupinga Kamatiku ya CHADEMA
kuwavua uanachama.
Akisoma hukumu hiyo majira ya saa 3:30 asubuhi katika
Mahakama kuu hiyo Jaji A.N.M Sumari,Alisema kwamba katika pingamizi hilo
lililowasilishwa katika Mahakama hiyo na Wakili Kimomogoro aliyeteuliwa na
Chama hicho kuwasilisha kwa niaba ya Kamati Kuu Taifa ya CHADEMA chini ya Kiapo
cha Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya
Chama hicho na Mjumbe wa Kamati Kuu Slivestar Masinde aliyeteuliwa na Chama.
Utaratibu ulikiukwa kwa Wakili Methord Kimomogoro
kujiandalia Kiapo hicho bila kukipeleka kwa mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini
kukisaini na kula kiapo kisheria na badala yake kukiwasilisha Mahakamani hapo
bila kufuata taratibu hizo za kisheria ambalo ni kosa kwa wakili kutengeneza
kiapo na kukiwasilisha bila kumhusisha mtajwa katika kutengeneza kiapo hicho
kisheria.
Jaji Sumari alisema kuwa kutokana na Mapungufu yaliyoonekana
katika Kiapo hicho ambayo aliyaeleza kuwa ni pamoja na Kiapo alichoapa Masinde
kilionyesha sahihi tu na Muhuri bila kuonyesha Jina la aliyetoa Kiapo hicho na
kusema kwamba hilo ni pungufu la kwanza na kwa mujipu wa sheria hilo ni kosa na
pili Pingamizi hilo liliwasilishwa Desemba 29 mwaka 2012 tayari muda ukiwa
umepita wa kufanya hivyo.
Katika madai mengine katika pingamizi hlo yalidai kuwa
Walalamikaji Mhe. Matata ambaye kwa sasa ni Meya wa Manispaa mpya ya Ilemela na
mwenzake Mhe. Chagulani waliidanganya na kupotosha Mahakama hiyo juu ya kufutwa
Uanachama kwa madai kuwa taratibu zote zilifuatwa huku bila kuonyesha ushahidi
wa na utetezi wao zaidi ya Wakili wao
kusema pia hawakuwa na uhalali wa kufungua kesi hiyo.
Jaji Katika kunuku mifano ya kesi mbalimbali za aina hiyo na
mapingamizi kwenye kesi za ndani na nje kwenye Mataifa ya nje kama ya nchini
Uingereza na ile ya Mhe. Mkosamali
iliyokuwa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora aliyokuwa amewekewa pingamizi kama hilo alisema
kuwa halikuwa na uhalali na kuamua kulitupilia mbali shauri hilo la pingamizi
juu yake na hivyo linamhalalisha naye kufanya hivyo kama ilivyopendekezwa na
mawakili wa walalamikaji.
Mawakili watatu maarufu Jijini Mwanza Salum Magongo,
Boniphace Matata na Julius Mushobozi wanaowatetea walalamikaji katika kesi No.
13/2012 Mhe. Matata na Mhe. Chagulani walionekana kumzidi mbinu za kisheria
Wakili Methord Kimomogoro na kumbana kila kipengele na hatimaye Pingamizi zake
alizowasilisha kutupiliwa mbali na kuondolewa ili kutoa nafasi ya Kesi ya
Msingi kuanza kutajwa na kusikilizwa.
Awali CHADEMA kupitia kwa Wakili wake huyo Kimomogoro waliwasilisha madai ya mapingamizi mengine matatu ambapo katika dai la kwanza walidai kuwa walalamikaji waliofungua kesi moja katika Mahakama mbili tofauti na hiyo walikuwa na nafasi ya kukata rufaa kwenye Chombo cha Baraza kuu la wajumbe wa Chama hicho lakini waliamua kukimbilia Mahakamani
Dai la pili lilieleza kuwa CHADEMA ni Taasisi Binafisi
inayojiongoza na kusimamia Mamlaka ya Umma ambapo mtu yeyote anayejiunga nayo
ni lazima ukubaliwe na kudhaminiwa na Chama hicho kugombea nafasi ya uwakilishi
wa wananchi ukiwa mwanachama wa chama cha siasa na si vinginevyo kwa mujibu wa Katiba
ya Chama hicho.
Dai la Tatu Mahakama iliyofunguliwa kesi hiyo Haikuwa na
Mamlaka ya kisheria kuiwezesha kusikiliza kesi hiyo hivyo ni vyema ukatupiliwa
mbali na kufutwa kwa kuliondosha shauri hilo Mahakamani kwa kuwa waliofungua
hawakuwa na uhalali huo.
Maandamano ya hivi majuzi kutaka kumng'oa Meya Matata. |
Pili:-Mahakama hiyo inayo Haki ya Kisheria ya kuiwezesha
kusikiliza kesi iliyofunguliwa kwa kuwa taratibu za Taasisi ya CHADEMA
hazikufuatwa za kuwavua Uanachama na kufanyika Kibabe kwa mujibu wa Katiba ya
CHADEMA hivyo uhalali wa walalamikaji ni sawa kutafuta haki ambayo itapatikana
kwa taratibu za kisheria kwa mujibu wa madai yao na Katiba ya Chama na ile ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee.
Tatu:-Hati ya Kiapo cha Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini nayo
ilikuwa na mapungufu na iliwasilishwa nje ya muda wa kisheria uliokuwa unatoa
nafasi ya CHADEMA na Wakili wao Kimomogoro kuwasilisha kabla walalamikaji awajafuta
kesi hiyo waliyokuwa wameifungua katika Mahakama nyingine isiyokuwa na uwezo wa
kuisikiliza kwa mujibu wa taratibu za kisheria.
Kama ilivyodaiwa na wakili wao wa CHADEMA awali, lakini
walichelewa na tayari kesi hiyo ilikwisha ilifutwa katika Mahakama hiyo nyingine na
kuhamishiwa katika Mahakama hiyo ambayo inao uwezo wa kuisikiliza kisheria
katika hukumu iliyosomwa na kuamuliwa na Jaji A.N.Sumari mwezi Juni 31mwaka jana.
Kufatia hukumu hiyo ya leo Mahakama hiyo kupitia Jaji A.N.
Sumarikuwa Kesi ya Msingi na Mahakama hiyo
itaendelea sasa na taratibu za
kuipanga,kutajwa na kuanza kuisikiliza
baada ya kuwajulishwa Mawakili wote wa pande mbili kwa mujibu wa taratibu za
kisheria za Mahakama hiyo na kumaliza kusoma hukumu hiyo iliyosomwa kwa dakika
45.
Baada ya kusomwa hukumu hiyo wafuasi wa CHADEMA wakiongozwa
na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na Wilaya na Makada wa Chama hicho waliokuwa
wamejitokeza kwa wingi katika makundi walijikuta
wakitoka kimyakimya huku wengine wakidai kuwa Wakili wao Kimomogoro ameonyesha
udhaifu na hakuwa makini dhidi ya Mawakili wa walalamikaji hivyo wakidai ni
vyema akatafuwa wakili mwingine ambaye anaweza kuwasilisha upya pingamizi ndani
ya muda uliotolewa na Jaji kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Kijiwe Maarufu Cha KEMONDO kinachojulikana kuwana watu wa
kada tofauti na wenye ueledi mkubwa wa kuchambua mambo leo kilikuwa na watu
wenye nyuso za huzuni kutokana na kile kilichoshuhudiwa na kufatiliwa kwa
umakini Mahakamani wakati Jaji Sumari akisoma hukumu hiyo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.