ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 18, 2010

STONE CLUB WIKI HII UTAMU Tuuuu!!...!!....!!

MWISHO WA MWAKA MASIKUKU YAKO PARE-PARrrEEE!
RAHA TUJIPAGE'' WENYEWE LEO THE JIWE EI-KEI-EI' STONE CLUB
KWA ATAKAYE FUNIKA
KIMTOKO!
KUCHEZA!
NA KUJIACHIA ILE ILE!!
ATALAMBA ZAWADI

"USKOSE"

UHURU PEAK LAGER NDANI YA SENGEREMA.

KAMPUNI ya Bia ya Serengeti Breweriers jana iliendelea na zinduzi zake kuitambulisha bia yake mpya Uhuru Peak Lager kama hatua ya kuendelea kukuza soko la la bidhaa zake hapa nchini. Uzinduzi wa jana ulikuwa ni ktk Wilaya ya Sengerema mjini.

Sengerema ni moja ya wilaya zinazokua kwa kasi hapa nchini na hivyo Kampuni ya Serengeti imeona ni bora kuitambulisha bia hiyo kwa wakazi wa mji wa huo na vitongoji vyake ili nao wajivunie kwa kupata kile kilicho bora.

Bia hiyo yenye ujazo wa mililita 350 ikiwa na asilimia 5.8 ya kilevi, tayari imeshaanza kuuzwa katika mikoa mbalimbali ya Kanda ya Ziwa na wilaya zake; kwa mji wa Sengerema ni wiki ya pili sasa tangu bia hiyo iingie sokoni.

ABOU SEMHANDO AFARIKI DUNIA KWA AJALI.

ENZI ZA UHAI WAKE ABOU SEMHANDO.
Taarifa zilizopatikana asubuhi hii na kuthibitishwa na mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo zinamtaja mpiga drums maarufu nchini kutoka bendi ya African Stars wana wa kutwanga na kupepeta, Abou Semhando amefariki dunia usiku wa kuamkia leo maeneo ya Tangi bovu, Mbezi jijini Dar es salaam. Imeelezwa kuwa marehemu Abou Semhando alikuwa akiendesha pikipiki ghafla akakumbana na gari nalo likamgonga hivyo kufariki papo hapo.

PIKIPIKI ALIYOKUWA AKIENDESHA MAREHEMU ABOU SEMHANDO.

GARI LILILOMGONGA MAREHEMU NA MASHUHUDA WA AJALI HIYO WAKITATHMINI.
Kwa sasa msiba wa mwanamuziki huyo upo nyumbani kwake Mwananyamala.
Tutaendelea kupeana taarifa zaidi...

PICHA NA HABARI KWA HISANI YA MICHUZI JR.

Friday, December 17, 2010

WAR REVIEW WON'T CHANGE U.S. withdrawal plans

President Barack Obama meets the national security team during a monthly meeting on Afghanistan and Pakistan in the Situation Room of the White House.

A long-awaited U.S. military analysis of the war in Afghanistan is expected later this week, a year after President Obama ordered additional U.S. troops to the country as part of a strategy that could bring some forces home as soon as July 2011. Officials have said the goal is to end combat operations in Afghanistan in 2014.

MAELFU WAJITOKEZA MAZISHI YA DR. REMMY.

Hatimaye mwili wa gwiji wa muziki wa dansi nchini Ramazan Mtoro Ongalla maarufu kama Dr. Remmy Ongalla umezikwa jana katika makaburi ya sinza, Dar es salaam ambapo mamia ya wakazi walihudhuria mazishi hayo. Kabla ya kuzikwa mwili wa marehemu uliagwa katika viwanja vya Biafra vilivyopo Kinondoni, jijini Dar.
Mamia ya waombolezaji walilazimika kuvumilia adha ya kukanyagana wakati kila mhudhuliaji akijaribu kupata nafasi ya kumuaga mwanamuziki huyo aliyeacha watoto sita.


Waziri wa Habari, Vijana na Michezo Emmanuel Nchimbi alisema Taifa litaendelea kukumbuka mchango wa Dr. Remmy hasa kwa kuwa mkongo wa kwanza kupigania sanaa ya Tanzania miaka mingi iliyopita.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

Thursday, December 16, 2010

ILIKUWA CHEREKO CHEREKO HASWAAA..!.. HARUSI YA DR DICKSON NA NYAMIZI.

Hakika ilikuwa siku njema kwa dr. Dicky wa mwanza pale alipofunga pingu za maisha na bi. Nyamizi Mohamed.

Harusi ilifungwa katika kanisa la Nyakahoja jijini mwanza na kisha baadaye sherehe ya kufana kwenye ukumbi wa new mwanza hotel.

Bwana harusi Dr. Dicky akicheki kwa makiniz chuma chake wakati wakishuka kuingia ukumbini toka kwenye mchuma wa wazi.

Makaribisho yalikuwa supa ile hatari, mlangoni ilikuwa unakaribishwa na zawadi toka kwa maharusi, wahudhuriaji nao kama unavyomwona bi dada walipendeza ile mbaya'.

Hapa ni pozi la kufungua sherehe......MMMMMMMMMMMwaaaaaa!! UTEPE UKAKATIKA WENYEWE BILA MKASI.

Prince Baina Kamukulu wa kwanza kushoto akinyatia CHIAzz!

Mr. Gebbo na Ua lake.

Safu ya wanakamati na Maharusi.

Kila la kheri na furaha maishani kwa Dr. Dicky na Bi. Nyamizi.

EWE MTU WA MUNGU USIKOSE CCM KIRUMBA JUMAPILI HII!!

KUNDI LINALOTAMBA KATIKA MEDANI YA MUZIKI WA INJILI JERUSALEM BAND LA JIJINI MWANZA SIKU YA JUMAPILI YA TAREHE 19 DEC 2010 LINAKWENDA KUZINDUA ALBUM YAKE MPYA INAYOITWA MJUE SANA MUNGU. ALBUM HIYO NI YA TATU KWA KUNDI HILO IKITANGULIWA NA ALBUM YA KWANZA INAYOITWA 'UPENDO WA MUNGU HAUNA KIPIMO' NA ILE YA PILI 'SISI JE TUTAPATAJE KUPONA'. UZINDUZI WA ALBUM YA SASA KUSINDIKIZWA NA WAIMBAJI MAHIRI KAMA YUSTO ONESMO, MATHA RAMADHANI, EMMY LEMA NA REBEKA MAGABA, SI HAO TU! KWAYA MBALIMBALI NAZO KUMWAGA UPAKO:- VIJANA WA KEKUNDU (AIC MAKONGORO), AIC MUUNGANO, WANAKITAMBO, WWI WAKINA MAMA, MWANZA SINGERS, MWANZA GOSPEL, NA NYINGINE NYINGI.
UZINDUZI ALBUM YA TATU YA JERUSALEM BAND KUHUSISHA MAUZO YA ALBUM HIYO MPYA KWENYE MIFUMO YA CD, AUDIO TAPE, VCD, NA DVD.


MGENI RASMI WA UZINDUZI HUO ATAKUWA MH. MKUU WA MKOA WA MWANZA ABASS KANDORO. NAE KIONGOZI WA KUNDI HILO RUTH MUTASH AMESEMA KUWA KUNDI LAKE LIMEJIANDAA VYEMA KUHAKIKISHA KUWA LINAWASHA MOTO WA IMANI ILI KILA ATAKAYE FIKA UWANJA WA CCM KIRUMBA SIKU HIYO YA JUMAPILI KUONDOKA NA FURAHA YA UTAKASO.

CHANGIZO WAKUBWA NI SH. 2,000/= NA WATOTO NI SH. 1,000/=
KUMBUKA NI TAREHE 19.DEC.2010
MUDA KUANZIA SAA 8:00 MCHANA HADI 12:00 JIONI
NYOTE MNAKARIBISHWA.

Wednesday, December 15, 2010

TP MAZEMBE YAWEKA HISTORIA AFRIKA.

Mabingwa wa Afrika TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamefuzu kucheza fainali ya kuwania kombe la klabu bingwa duniani, baada ya kuwalaza mabingwa wa Amerika ya kusini- Internacional kutoka Brazil mabao 2-0 mjini Abu Dhabi.TP Mazembe inakuwa klabu ya kwanza barani Afrika kufikia hatua ya fainali ya Kombe la Dunia, na inasubiri kucheza fainali dhidi ya mshindi kati ya mabingwa wa ulaya Inter Milan ya Italia na mabingwa wa Asia, Seongnam IIhwa kutoka Korea Kusini, ambazo zinachuana leo Jumatano katika nusu fainali ya pili.

Bao la kwanza la TP Mazembe lilifungwa katika dakika ya 53 na mshambuliaji Mulota Kabangu, naye Dioko Kaluyituka akafunga la pili katika dakika ya 85. Internacional walipata nafasi nyingi katika kipindi cha kwanza lakini ngome imara ya ulinzi ya TP Mazembe ikayakomesha mashambulizi yote, na pia mlinda mlango Muteba Kidiaba akaokoa mikwaju mingi.

Fainali itachezwa siku ya Jumamosi tarehe 18.

CHEKSHIA HAPA NA KULEEEeee!!....!!>>>

Jarida namba moja la Burudani Tanzania KITANGOMA tayari limekwisha ingia kanda ya ziwa. Humo ndani kuna mastori kibao ya mastaa wa sasa na wazamani , pati zote kubwa duniani includi' FIESTA, kona ya KALI ZA MTONI, ENZI HIZO, CHUCHIZI na maelelezo kibao juu ya vipindi vya CLOUDS TV. Lipate sasa ujionee mwenyeweEEE Mautamu kama mdau hapo juu niliyemfuma langoni mwa Imalaseko supermarket Mwanza aki 'Utamutika'.

KAMBI POPOTE, 20 KALI ZA TOWN, MTVBASE,A to Z ya filamu za Bongo ndani ya TAKE ONE. Ebwanaee..! jarida la KITANGOMA ni mpango mzima ile kabaaa..,





Long time kidogo Mwanza hii ndiyo club iliyo tukaribisha wengi, ikiitwa 'RUMAZ CLUB' wajanja wote walikuwa hawakosi kuzama humu, ambapo kwa sasa eneo limezungushiwa uzio jengo likipigwa nyundo kupisha ujenzi wa mjengo mpya. Mara baada ya kuja mapinduzi ya viota vya burudani kama Villa park na Stone club watu kama waliambizana vile... Mmmmh Rumaz wakawa wanapiga disco, asubuhi zawadi bakuli la supu.. Wapi watu hawazuki!! mwisho wa siku ngoma kwishni'

Hivi karibuni lile wimbi la vibaka wakabaji na waporaji lilirejea Eneo la Nera hapa Rock city, sababu kuu ikiwa ni giza. Duh afadhali Nimekuta mafundi wakikamilisha ukarabati wa taa hizo eneo la mwisho kabisa town.

Anakuja!

Juu kwa juu Kirumba Mwanza.

Tuesday, December 14, 2010

ASKARI MAGEREZA MWANZA AJILIPUA KWA RISASI.

Askari magereza mwenye namba B50004 Elias Bukwima amekufa kwa kujifyatua risasi tatu kichwani kwa kutumia bunduki aina ya smg yenye namba za usajili D61220 aliyokuwa akiitumia kazini.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mapema leo kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Simon Sirro amesema kuwa tukio hilo lililotokea jana majira ya saa saba mchana wakati askari huyo akiwa eneo la lindo kwenye gereza la Butimba jijini Mwanza.

Maiti ya askari huyo imehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando huku polisi wakiendelea kufanya uchunguzi kubaini chanzo cha mauaji hayo.

MASHABIKI WA ARSENAL' MUPOoooooo!!...!!

JI-SUNG PARK.
Bao safi kwa kichwa la Ji-Sung Park katika kipindi cha kwanza, lilitosha kuipatia ushindi Manchester United dhidi ya Arsenal na kuwawezesha kushikilia usukani wa ligi kutoka kwa mahasimu wao hao.

Nafasi nzuri kwa Arsenal ilikuwa ni ya Marouane Chamakh, ambaye alikosa kufunga baada ya mpira wa kichwa alioupiga kuzuiwa na Nemanja Vidic.


WAYNE ROONEY.
Wayne Rooney angeweza kuongeza bao la pili, lakini mkwaju wake wa penalti baada ya Clichy kuunawa mpira, ukapaa juu ya lango la Arsenal.


Kwa matokeo hayo, Manchester United sasa wamefikisha pointi 34 wakiwa na mchezo mmoja mkononi, wakifuatiwa na Arsenal yenye pointi 32, sawa na Manchester City iliyo nafasi ya tatu na Chelsea watakaopambana na Manchester United siku ya Jumapili ijayo wapo nafasi ya nne na pointi 31.

WELCOME TO A TRUE WORLD OF SOCIAL NETWORK.

Welcome to a true world of social network, best of Tanzanian Entertainment. Chat, Forums, News, Video and the latest bongo flava.

Je, Unahitaji rafiki, unahitaji kujumuika na marafiki wengine sehemu mbalimbali duniani? Je, unahitaji watu kwa ajili kubadilishana nao mawazo? Unahitaji kutumiwa na kupokea barua toka kwa marafiki zako waliozagaa sehemu mbalimbali? Kuupload muziki katika profile yako. Kuchati, Kushare picha, Video na marafiki zako. Je, umechoshwa na utitiri wa mitandao ya marafiki ambayo imekuwa ikiasisiwa na wenzetu walioko Ulaya tu na sasa unataka ku-feel kitu cha nyumbani?

Kama majibu ya maswali yote hayo ni ndio, basi huna haja ya kubabaika zaidi maana kwa heshima na taadhima tunakuletea kwenu
www.gongamx.com…. tovuti yenye lengo la kukukutanisha na marafiki (well…hata maadui zetu si huwa wanakuwemo bwana), watu kwa ajili ya kubadilishiana mawazo, na mambo kibao.

wwww.gongamx.com, tovuti ya Watanzania, iliyoanzishwa na Mtanzania kwa ajili ya Watanzania. Dah!! nisimalize uhondo….hebu shuka mwenyewe katika maskani hiyo ujiunge na tuanze kulisongesha ndani ya www.gongamx.com

--
Michael Carter Mlingwa | Product Manager

MWANZA YAONDOKEWA NA MSANII: NI HAMAD SALEHE WA BWV.

MAREHEMU HAMAD SALEHE KATIKA FIESTA 2004 CCM KIRUMBA MWANZA.
Kama waijua vyema historia ya muziki wa Bongo Fleva kwa mkoa wa Mwanza hakika utakuwa unawafahamu wasaii kama Jontwa Jokeli, Jose Kashushura, Phantom Lanks, Shija Rweymamu, jingo Man, Jet Man, Jitah Man, Kid Bway na wengine wengi waliokuwa wakitikisa katika muziki huo wa kizazi kipya miaka ya tisini na mwanzoni mwa millennium mpya katika kona ya muziki wa Ragga. Na katika hip hop kuna wengi Fid Q ‘Ngosha the Don’ anayetamba hadi sasa, Dr KB na bila kusahau kundi la BWV ambapo humo nina tuama nikiwa na Inshu ya kuzungumzia.
WAKIWA CITY CABANA MWANZA KUTOKA KUSHOTO WALIO CHINI NI BAVON, AMBWENE YESAYA 'AY' NA PHILBERT KABAGO NA WALIOSIMAMA KUTOKA SHOTO NI MAREHEMU HAMAD SALEHE, DR LIFE NA HAYATI COMPLEX.
BWV au BOYS WITH VOICES ni kundi lililoundwa na vijana wawili Filbert Kabago na Hamad Salehe waliochangia harakati za Maendeleo ya jiji la Mwanza pale walipopakuwa singo iitwayo ‘barabara’ ikichambua uhalali wa Mwanza kuitwa jiji ile hali Barabara zikiwa tope na mahandaki kibao, changamoto hiyo iliigusa serikali hata ikafanya mambo hatimaye miaka ya sasa twaziona barabara za jiji la mwanza zikiwa full mikeka.
MWENYE KIPAZA MBELE NI MAREHEMU HAMAD SALEHE KWENYE UZINDUZI WA ALBUM YAO BWV CCM KIRUMBA SEPTEMBER 14/2003 ULIOANDALIWA NA ZIZOU FASHION (TIPPO) ENZI HIZO H.BABA AKIWA DENSA.
BWVWalijali pia maslahi ya wafanyakazi pale walipoiweka hewani singo ‘Bosi nipe mshahara wangu’ track iliyo bamba na kushika wengi, kwa wafanyakazi wakiitumia kama mkombozi wa haki zao huku waajiri wasio zingatia majukumu yao wakizima radio kutokana na madongo yaliyokuwa yakielekezwa kwao.
Nazungumza YOTE haya kukupa TU! historia ujue japo kwa muhtasari muziki wa kizazi kipya mkoa wa Mwanza ambao ni moja kati ya mikoa iliyotia changamoto kwa muziki Bongo fleva kukuwa nchini Tanzania. Nayatanguliza maelezo hayo nikiwa na masikitiko kutangaza kifo cha Hamad Salehe mmoja kati ya vijana waliounda kundi la BWV.

STUDIO ZA MWANZA RECORDS KWA ENRICO FEGWERADO: KUTOKA SHOTO NI SOGGY DOGGY, PHILBERT KABAGO NA HAMAD SALEHE NA SISTER P (PALE KATI).
Baada ya kuugua kwa muda mrefu Hamad Salehe amefariki dunia mwishoni mwa juma siku ya jumapili ya Tarehe 12 dec 2010 saa 8 mchana na kuzikwa jumatatu ya tarehe 13 dec 2010 kabla ya adhuhuri katika makaburi ya kirumba jijini Mwanza. Akizungumzia kuhusu msiba huo msanii mwenzake katika kundi Philbert kabago anayetamba na singo Wivu aliomshirikisha mwanadada Farida anasema kuwa ingawa kwa kipindi kirefu amekuwa akifanya muziki kama solo kutokana na msanii mwenzie kuugua pengo alikuwa analiona lakini kwasababu hakuwa na jinsi ilimbidi kupigana hivyo hivyo. Marehemu Hamad Salehe alizaliwa juni 23 1982 Nyakalilo wilayani Sengerema, akianza muziki mwishoni mwa 1996 akiwa darasa la sita shule ya Victoria Internation. Marehemu ameacha mtoto mmoja wakiume(6).

MABALOZI WA SWEDEN NA NORWAY WAWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS KIKWETE.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi wa Sweden na Norway katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam. Waliowasilisha hati zao ni Balozi Lennarth Hjelmaker wa Sweden na Balozi Bi.Ingunn Klepsvik wa Norway. Pichani Balozi Ingunn Klepsvik wa Norway akiwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete.
Picha na Freddy Maro - Ikulu

Monday, December 13, 2010

BREAKING NEWS: REMMY ONGALA AFARIKI DUNIA.

MWANAMUZIKI MAARUFU DR. REMMY ONGARA AMEFARIKI DUNIA ALFAJIRI YA KUAMKIA LEO KATIKA HARAKATI ZA KUMKIMBIZA HOSPITALI TOKA NYUMBANI KWAKE SINZA JIJINI DAR ES SALAAM.
Alipotoa kwa mara ya kwanza kibao kinachoitwa Siku ya Kufa, mwanamuziki Ramadhan Mtoro Ongala ‘Dk Remmy’, akiwa na bendi ya Orchestra Makassy, wengi walihisi anajichulia kifo chake kiko karibu. La hasha mara baada ya hapo maisha yaliendelea akaishi miaka ishirini naushee.... na hatimaye miaka ya 2004-2005 mzee mzima aliamua kuokoka mara baada kupona toka kuugua sana na hata kupooza.
Mwenyewe katika mahojiano nami aliwahi kukiri kuwa Mungu ndiye alimpigania akarejea katika hali nzuri, Remmy aliachana na muziki wa dunia na kuingia ktk fani ya kuhubiri neno la Mungu kwa kutoa album ya nyimbo za injili 'KWA YESU KUNA FURAHA' iliyotumika kubadili wengi. Lakini ndiyo hivyo tena tumeandikiwa kwamba kila kilichozaliwa na mwanadamu hakina budi kufa, hatimaye usiku wa kuamkia leo majira ya saa nane Remmy Ongala Akaaga dunia wakati akikimbizwa hospitali mara baada ya kuzidiwa akiwa nyumbani.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

KILI STARS: MERRY CHRISTIMAS TANZANIA.

Kocha mkuu wa Kilimanjaro Stars,Jan Poulsen akimshika mwari pamoja na nahodha wake Shadrick Nsajigwa.Kikosi kizima cha Kilimanjaro Stars bingwa mpya kombe la Tusker Challenge 2010 katika picha ya pamoja.Stars wameibuka na kombe na kitita cha US$ 30000/= -hongera Kilimanjaro Stars,Hongera Tanzania.

KIKOSI BINGWA CHA Kilimanjaro stars. Stars iliwakilishwa na Juma Kaseja, Shadrack Nsajigwa, Stephano Mwasyika, Kelvin Yondani, Juma Nyosso, Jabir Aziz, Shaban Nditi, Nurdin Bakari, Idrissa Rajab/Kigi Makasi/ Haruna Shamte na John Bocco/Henry Joseph.

KIKOSI CHA Ivory Coast, Kiliwakilishwa na Sangare Badra, Goua Mahan/Kouadio Konan, Wawa Serge, Kouame Desire, Bile Georges, N’goran Kouassi, Coulibaly Tiecoura, Kone Mahamadou/Kipre Tchetche, Kipre Balou na Dion Sede/Guy Herve.

Nahodha wa Kili Stars,Shadrack Nsajigwa akifunga Bao la ushindi lililopatikana kwa njia ya penati nara baada ya .

Waziri wa habari, vijana utamaduni na michezo dr emmanuel nchimbi akikabidhi nahodha wa timu ya Kilimanjaro stars, shadrack nsajigwa mfano wa hundi mara baada ya kuibuka washindi katika michuano hiyo na hatimaye kunyakua kombe la cecafa pia.

Kipa wa Kilimanjaro Stars Juma Kaseja akionesha tuzo yake ya kipa bora wa Tusker challenge 2010. Kuhusu kupewa jezi na shabiki wakati mchezo ukiendelea, alisema hiyo inaonyesha ni jinsi gani mashabiki wanavyomkubali hadi wanamfuata uwanjani na kumtunza jezi.

Tupo pamoja tukikirudi 'kiduku na Malewa style' licha ya kutocheza kwa kuwa na kadi mbili za njano Mrisho Ngasa alijumuika kunyimwaga na wenzake.