Askari magereza mwenye namba B50004 Elias Bukwima amekufa kwa kujifyatua risasi tatu kichwani kwa kutumia bunduki aina ya smg yenye namba za usajili D61220 aliyokuwa akiitumia kazini.Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mapema leo kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Simon Sirro amesema kuwa tukio hilo lililotokea jana majira ya saa saba mchana wakati askari huyo akiwa eneo la lindo kwenye gereza la Butimba jijini Mwanza.
Maiti ya askari huyo imehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando huku polisi wakiendelea kufanya uchunguzi kubaini chanzo cha mauaji hayo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment