ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 25, 2009

SANA TUUU WADAU

KUNA KIWANJA KIPYA KIMEZALIWA MWANZA CHAITWA MALAIKA MITA KADHAA TOKA AIR PORT MZ, KINA KILA SIFA. PICHANI HILI NI ENEO LA NDANI LA MJENGO WA STAREHE.

SWIMMING POOL YA AINA YAKE AMBAYO IKO JUU YA ZIWA (NAJUA UTAKUWA NA MASWALI KAA MKAO WA KULA)

CHEKI SMILE ZA WATOTO CEDRICK A.G.SENGO NA RAFIKIYE.
NI YA KWAKO SI YA MWINGINE

Thursday, December 24, 2009

MERRY X MASS AND HAPPY NEW YEAR.


MR. EDGAR JONAS MAPANDE WA DAR ES SALAAM ANAWATAKIA KILA LA KHERI NA FANAKA MARAFIKI WOTE KATIKA KUSHEREHEKEA X.MASS NA MWAKA MPYA 2010 UPENDO NA BURUDANI VIENDELEE.

Wednesday, December 23, 2009

PATA JARIDA LA KUPERUZ KIPINDI CHA CHRISTMAS.LIKIWA LIMESHEHENI ISHU KIBAO NYINGINE ZA KI MWANZA MWANZA JARIDA LAKO SHEAR BEAUTY MAGAZINE LIKO MTAANI SASA.

Tuesday, December 22, 2009

TASWIRA YA TAIFA

MARA NYINGI TUMEKUWA TUKILAUMU TU NA KUKEMEA BILA KUPIMA SUALA LA AJIRA KWA WATOTO, SWALI NI JE! TUMESHAWAHI KUFANYA UTAFITI KUTAMBUA NINI KINACHOPELEKEA HALI HII?
GHARAMA ZA MAISHA NI KUBWA ZIKIPANDA KILA KUKICHA, MAHITAJI NI MENGI CHAKULA, KODI YA NYUMBA, MATIBABU, KARO ZA SHULE. WENGI FAMILIA ZAO HAZIJIWEZI KIFEDHA HIVYO NGUVU YA KILA MMOJA HATA MTOTO INAHITAJIKA. BIASHARA YENYEWE FAIDA SH. 300/= HADI SH.800/= TUTAFIKA?
WATOTO WENGINE WAZAZI WAO WALISHA FARIKI DUNIA WANAISHI NA BABU NA BIBI WASIOJIWEZA NAO WAMEGEUKA KUWA WALEZI JE WAWEVIBAKA, OMBAOMBA AU WATAFUTE RIZIKI KUPITIA BIASHARA NDOGO NDOGO?

Monday, December 21, 2009

X. MASS TUBANANE HAPA.

NI MWENDO WA VIDOLE JUU NA KULISAKATA RUMBA LA KIJANA WA KISASA USIKOSEEE!

TANZIA

ILIKUWA NI TAREHE 19DEC2009 BINAFSI KIBINADAMU ILIKUWA KAZI KUAMINI LAKINI MARA BAADA YA KUFIKA HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO SIKUWA NA JINSI. ASUBUHI HIYO HIYO KIASI CHA SAA MOJA NA DK KADHAA MAMA ADVENTINA TEGA ALIKUWA AMEAGA DUNIA. NI MAMA WA MFANYAKAZI MWENZETU CLOUDS FM MWANZA (HUMPHREY SIMON). BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE. pichani ni ndani ya kanisa la RC. kirumba Mwanza ibada ya kumwombea marehmu.

SEHEMU YA UMATI KATIKA IBADA HIYO.

PICHA NJE YA KANISA KUTOKA KUSHOTO BW. HUMPHREY SIMON (mtoto wa marehemu), DEUS KATAHIGWA NA OLIVER SENGO (my wife)

TUMEROGWA?


IMEKUWA NI POA TU KWA MAGARI YA KUBEBA TAKA YA MANISPAA YA JIJI LA MWANZA KUSOMBA TAKA HUKU YAKITIRIRISHA UCHAFU BARABARANI.

KIPINDI KIREFU SASA WATANZANIA WAMEKUWA WAKIHIMIZANA KUTUNZA MAZINGIRA HUKU SUALA LA USAFI NALO LIKIPEWA KIPAUMBELE, NAO WADAU NA MAKAMPUNI MBALIMBALI WAMEKUWA MSTARI WA MBELE KUBUNI JINSI YA USHIRIKI WAO KTK SUALA ZIMA LA USAFI (mfano TIZAMA PICHA JUU) SERIKALI NAYO HAIJABAKI NYUMA IMEKUWA IKITUMIA MBINU MBALIMBALI KUSHINDANISHA MIJI KTK SUALA LA USAFI SAMBAMBA NA UTOAJI TUZO KWA MSHINDI.
KWA KIPINDI SASA MFULULIZO MKOA WA MWANZA UMEKUWA UKIIBUKA MSHINDI KTK TUZO YA USAFI. LAKINI KAMA WAHENGA WASEMAVYO "MGEMA UKIMSIFIA TEMBO HULITIA MAJI"MAGARI YA UBEBAJI TAKA HUSUSANI MAGARI YA MABAKI YA SAMAKI TOKA VIWANDANI MWANZA HAYANA USTAARABU
KERO SI TAKA PEKEE BALI HARUFU MBAYA TOKA TAKA HIZI.