ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 15, 2010

PATATOSHA TU!

MASHABIKI WA SOKA WAKIWA NJE YA UWANJA WA CCM KIRUMBA MWANZA, WAKISUBIRI UWANJA UFUNGULIWE WAPATE KUONA MAZOEZI YA TIMU ZAO SIMBA AU YANGA KULINGANA NA RATIBA YA MAZOEZI. MAJIRA YA SAA 11 JIONI KWA SIKU YA JANA MPAKA NAONDOKA ENEO HILO UWANJA KATU HAUKUFUNGULIWA.

ILE HALI TIKETI ZIMEKWISHA ANZA KUUZWA TANGU MAJIRA YA MCHANA WA LEO, MILANGO 6 KUWA WAZI SIKU YA KESHO KUTOA NAFASI KWA MASHABIKI KUINGIA BILA BUGHUDHA KUSHUHUDIA MTANANGE HUO WA WATANI WA JADI.

MAHOTELI NA NYUMBA NYINGI ZA WAGENI ZIMEJAA WAGENI WA UKWELI SIYO WAGENI WENYEJI. PICHANI MASHABIKI WA YANGA AFRIKA NDO WANAINGIA JIONI HII MWANZA.

SIMBA WAO CCM KIRUMBA NDICHO KIWANJA CHAO CHA NYUMBANI HIVYO KUWAKARIBISHA YANGA HIYO KESHO.

MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA NA HALI YA MAZINGIRA YA KAMANGA MWANZA, PICHANI NI MOJA YA WACHUUZI WA SAMAKI AKIOSHA NDOO ZA KUSAFIRISHIA SAMAKI MIKOANI.
ATHARI ZA MVUA NA MIUNDO MBINU YA KUSAFIRISHA MAJI TAKA KITAANI KWETU. MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAJI TAKA JIJINI MWANZA (MWAUWASA) MMELIONA HILI? AU MPAKA....

Thursday, October 14, 2010

WAKAZI WA MUSOMA SAHANI MOJA NA AKUDO.

WIKENDI ILIYOISHA AKUDO IMPACT WALIKUWEPO KANDA YA ZIWA HUKU SHOW YAO YA MWISHO IKISABABISHWA PALE MARA KATIKA MJI WA MUSOMA.

ENDELEA NA MACHO YAKO MDAU..

HAPO JEH!

JIBEBE UKISHINDWA KURONGA NAMI PIGA *120#.

TOTO ZE BINGWA NA FLOWERZ ZA MUSOMA.

NIAJE!

SI NDO HAWA SASA!

WATU JUST KWA KONA PALE KATI' WALIJIACHIAJEEEEeee!

SHUKURANI KWA MDAU WA BLOG HII ESTER aka KADADAA NAKATI YA MS.

TUMUENZI BABA WA TAIFA KWA VITENDO.


TAIFA LA TANZANIA LEO LINATIMIZA MIAKA 11 TOKA KIFO CHA MUASISI WAKE BABA WA TAIFA HAYATI JULIUS KAMBARAGE NYERERE KILICHOTOKEA KATIKA HOSPITALI YA MT THOMAS LONDON, UINGEREZA AMBAPO WATANZANIA WANAADHIMISHA SIKU HII IKIWA BADO SIKU KUMI NA SABA KUFIKIA UCHAGUZI MKUU OCT 31/2010.

VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI VIMEENDELEA KUKUMBUSHA HOTUBA ZA MWALIMU, MOJA KATI YA HOTUBA HIZO NI ILE INAYO TUASA JUU YA KIONGOZI GANI BORA KUMCHAGUA SIKU YA KUPIGA KURA. KARIBU MANENO MENGI KWENYE HOTUBA ZINAZORUSHWA HEWANI NA VYOMBO VYA HABARI VYA KIELEKTRONIKI YAMETENDEKA NA NDIYO MAMBO YANAYOZUA GUMZO KTK JAMII YA WATANZANIA KWA SASA.TUKIO LA LEO LINAKWENDA SAMBAMBA NA HITIMISHO LA MBIO ZA MWENGE WA UHURU.
JUHUDI ZA MAENDELEO ZINAANZIA PALE ULIPO NA KWA KILE KIDOGO ULICHONACHO.“Tanzania inatakiwa kufahamu kuwa misingi sahihi ya nchi yetu imejengwa kwa nguvu kubwa na waasisi wa taifa letu hivyo wale wote wanaotaka kuibomoa wanakosea na wanafanya dhambi kubwa na ipo siku watahukumiwa kwa kuwa hakuna anayependa kuona nchi inagawanywa kwa sababu wachache wanataka kuona wanapata furaha huku wengi wakiumia.”

MIUJIZA YATENDEKA CHILE, HATIMAYE WACHIMBAJI WOTE 33 WALIONASA WAOKOKA.

ILE NDOTO YA KUTISHA ILIYOCHUKUWA SIKU SABINI KUMALIZIKA HATIMAYE IMEFIKIA TAMATI KWA HARAKA TOFAUTI NA WENGI TULIVYODHANI HUKU IKISALIMISHA ROHO ZA WATU WOTE 33 WALIFUKIWA NA KIFUSI HUKO KATIKA MIGODI YA SAN JOSE NCHINI CHILELUIS URZUA MCHIMBAJI WA MWISHO KUOKOLEWA AKISHEREHEKEA MBELE YA RAIS WA CHILE SEBASTIAN PINERA MARA TU BAADA YA KUOPOLEWA TOKA KIFUSINI.

Rais wa Chile amesema kamwe nchi yake haitarejea hali iliyokuwa nayo awali baada ya kukamilika kwa shughuli ya uokoaji wa wachimba migodi 33 waliokuwa wamenaswa chini ya ardhi kwa siku 69. Sebastian Pinera amesema anahisi wananchi wa Chile sasa "wana umoja zaidi na imara kuliko wakati mwingine wowote" na wanaothaminika kote duniani.

MCHIMBAJI WA 21 KUOKOLEWA YONNI BARIRIOS AKIPOKEA BUSU MOTO MOTO MARA TU ALIPOIKANYAGA ARDHI.

Kulikuwa na kila hali ya ushangiliaji wakati Luis Urzua, mwenye umri wa miaka 54, mchimbaji wa mwisho alipotolewa nje ya mgodi huo.

WANANCHI WA CHILE WAKISHEREHEKEA WAKATI MTU WA MWISHO ALIYE NASA AKITOLEWA.

Baadhi yao wamebainika kuwa na matatizo ya meno, na wengine wanasumbuliwa na macho kutokana na kuishi katika vumbi na giza mgodini humo. Mmoja wao amegundulika kuwa na kichomi, ingawa hali yake inaelezewa kuwa si mbaya sana.
Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Jaime Manalich, alisisitiza kuwa wachimbaji wote wanaonekana kuwa katika afya njema kuliko ilivyokuwa ikitarajiwa. Haijawahi kutokea binadamu aliyenaswa chini ya ardhi kwa muda mrefu kiasi hicho kusalimika.
Wachimbaji hao walikuwa wamesalia na chakula cha kutosheleza kwa saa 48 wakati sehemu ya mgodi wa shaba na dhahabu wa San Jose nchini Chile katika jangwa la Atacama ulipoanguka tarehe 5 Agosti. Baada ya siku 17 za kuchimba kuwatafuta, hatimaye waokoaji walifanikiwa kuwasiliana nao.

Wednesday, October 13, 2010

UOKOAJI ULIOWEKA HISTORIA.

SHANGWE ZIMEENDELEA KULIPUKA LEO KATIKA MACHIMBO YA HUKO SAN JOSE NCHINI CHILE MARA BAADA YA JUHUDI ZA KUWAOKOA WACHIMBAJI WALIOKUWA WAKIISHI KATIKA GIZA LA KIFUSI KWA TAKRIBAN MIEZI MIWILI KUZAA MATUNDA HATIMAYE MMOJA BAADA YA MWINGINE KUOKOLEWA AKIWA HAI.

MWANDISHI WA HABARI AMBAYE NI MPIGA PICHA AKIWA AMEUCHAPA USINGIZI KUSUBIRI MATUKIO YA UOPOAJI KWENYE MIGODI HUKO SAN JOSE MJINI COPIAPO.

MCHIMBAJI MARIO GOMEZ (63) JAMAA MWENYE UMRI MKUBWA KULIKO WACHIMBAJI 33 WALIOTEKWA NA+KIFUSI CHA MGODI AKISALI KUMSHUKURU MUNGU MARA BAADA YA KUIKANYAGA ARDHI KWA MARA NYINGINE.

SHANGWE..!!

RAIS WA CHILE SEBASTIAN PINERA KUONESHA FURAHA HAPA AKIMKUMBATIA MCHIMBAJI WA KWANZA KUOPOLEWA BW FLORENCIO ANTONIO SILVA.

JIMMY SANCHEZ AKIWASILI HOSPITALINI KWA AJILI YA UCHUNGUZI BAADA YA KUOKOLEWA LEO.

SHANGWE MARA BAADA YA UOKOZI TAARIFA MPAKA BLYAKO INAKWENDA HEWANI MIDA HII WATU TISA TAYARI WAMEOKOLEWA.
TAARIFA ZAIDI NITAENDELEA KUKUMWAGIA.

Tuesday, October 12, 2010

FM ACADEMIA KUISHIKA MWANZA SIKU MOJA KABLA YA MECHI YA WATANI WA JADI (SIMBA NA YANGA)


UTAMBULISHO WA ALBUM MPYA VUTA NIKUVUTE KWA WAKAZI WA MWANZA SIKU MOJA KABLA YA KIPUTE CHA WATANI WA JADI SIMBA NA YANGA, FM KUANGUSHA KAZI IJUMAA HII.