ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 28, 2023

BENKI YA CRDB YAKABIDHI MADARASA MAWILI SHULE YA MSINGI CHUDA, JIJINI TANGA

 

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Hawa Msuya (wapili kushoto) kwa pamoja na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Tanga, January Kilambata (wapili kulia) wakibadilishana hati ya makabidhino ya madarasa mawili kwa ajili ya wanafunzi wenye uhitaji maalumu wa Shule ya Msingi Chuda, jijini Tanga leo. Madarasa hayo yaliyo pamoja na ofisi ya Walimu yamejengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB kwa thamani ya Shilingi Milioni 41. Kushoto ni Afisa Elimu ya Awali na Msingi, Kassim Kaoneka pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Mbwana Hassan.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Hawa Msuya (wapili kushoto) kwa pamoja na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Tanga, January Kilambata (wapili kulia) wakisaini hali ya makabidhino ya madarasa mawili kwa ajili ya wanafunzi wenye uhitaji maalumu wa Shule ya Msingi Chuda, jijini Tanga leo. Madarasa hayo yaliyo pamoja na ofisi ya Walimu yamejengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB kwa thamani ya Shilingi Milioni 41. Kushoto ni Afisa Elimu ya Awali na Msingi, Kassim Kaoneka pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Mbwana Hassan.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Hawa Msuya (wapili kushoto) akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhino ya madarasa mawili kwa ajili ya wanafunzi wenye uhitaji maalumu wa Shule ya Msingi Chuda, jijini Tanga leo. Madarasa hayo yaliyo pamoja na ofisi ya Walimu yamejengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB kwa thamani ya Shilingi Milioni 41.

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Hawa Msuya (wapili kushoto) kwa pamoja na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Tanga, January Kilambata (wapili kulia) wakisaini hati ya makabidhino ya madarasa mawili kwa ajili ya wanafunzi wenye uhitaji maalumu wa Shule ya Msingi Chuda, jijini Tanga leo. Madarasa hayo yaliyo pamoja na ofisi ya Walimu yamejengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB kwa thamani ya Shilingi Milioni 41.
Muonekano wa Madarasa hayo yaliyokabidhiwa leo kwa Shule ya Msingi Chuda, Tanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Hawa Msuya (wapili kushoto), Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Tanga, January Kilambata pamoja na Afisa Elimu ya Awali na Msingi, Kassim Kaoneka (walioketi katikati) wakiungana na wanafunzi wenye uhitaji maalumu na walimu kuipongeza Benki ya CRDB kwa msaada wa madarasa mawili kwa ajili ya wanafunzi wenye uhitaji maalumu wa Shule ya Msingi Chuda, jijini Tanga leo. Madarasa hayo yaliyo pamoja na ofisi ya Walimu yamejengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB kwa thamani ya Shilingi Milioni 41.

Friday, January 27, 2023

HATUA ZA KISHERIA KUCHUKULIWA DHIDI YA WAHALIFU NA WATUHUMIWA WA MAKOSA YA UHAMIAJI

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Onyo limetolewa kwa wale wote wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu wa makosa ya kiuhamiaji kwa kushirikiana na wahamiaji haramu, au kusaidia wahamiaji haramu hatua kali za kisheria zitachukuliwa juu yao. Peter Mbaku ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza, ametoa kauli hiyo hii leo akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake wakati akitoa ripoti ya mwaka wa utekelezaji 2022-2023 ambayo pia aliambatanisha na mipango mikakati iliyowekwa na idara hiyo. Watuhumiwa waliokamatwa kwa makosa mbalimbali ya kiuhamiaji yakiwemo makosa ya uhamiaji haramu na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa mwaka uliopita 2022 ni watu 783 ambao wanatoka katika mataifa 23. Hatua za kisheria zimechukuliwa dhidi ya wahalifu na watuhumiwa hao wa makosa ya uhamiaji ikiwemo kufikishwa mahakamani, kuondoshwa nchini, wakimbizi kurudishwa makambini, kupewa onyo kali huku wengine wakiamriwa kushughulikia vibali stahiki na kufanya kazi kulingana na sharia na taratibu za kiuhamiaji. Jeh kwanini wahamiaji hao hupitia mkoani Mwanza? Na nini kinachosababisha watu hao kutoka mataifa mengine kukimbilia nchini Tanzania huku idadi yao ikiongezeka kila uchwao? #mwanza #uhamiaji #wahamiajiharamu

HIZI HAPA SALAMU ZA MKUU WA MKOA WA MWANZA "HERI YA KUZALIWA RAIS SAMIA"

NA. ALBERT G.SENGO/MWANZA KWA NINI MWANZA INAKILA SABABU KUADHIMISHA KUMBUKUMBU SIKU YA KUZALIWA SAMIA? RC MALIMA AFUNGUKA.

Thursday, January 26, 2023

RC MWANZA AZINDUA VIVUKO VITATU KWA MPIGO VINAJENGWA NA KAMPUNI YA MTANZANIA SHIGONGO JIMBO LIMEPONA.

NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

 Mkuu wa mkoa wa Mwanza Adam Malima, leo amefanya uzinduzi wa ujenzi wa vivuko vipya vitatu vitakavyotumika kutoa huduma katika maeneo ya Nyakaliro -Kome, Bwiru-Bukondo na Ijinga-Kahangala, ili kuondoa kero za usafiri kwa wananchi


Naibu katibu mkuu wa wizara ya ujenzi na uchukuzi (sekta ya ujenzi) Ludovick Nduhiye, amesema uzinduzi wa ujenzi wa vivuko 3 ambavyo vimezinduliwa jijini Mwanza, ni hitaji kubwa kwa wananchi wanaoishi maeneo ambayo vivuko hivyo vitatoa huduma, baada ya ujenzi wake kukamilika.


Mkurugenzi wa kampuni ya Songoro Marine Transport Major Songoro, amesema vivuko 3, vinajengwa kwa kuzingatia viwango vya kitaifa (TASAC) na kimataifa (IMO, na kuwa wamejipanga kikamilifu kuhakikisha vivuko hivyo vinakamilika kwa muda uliopangwa. Uzinduzi wa ujenzi umefanyika leo


Kwa mujibu wa Mtendaji mkuu wa wakala wa ufundi na umeme Tanzania  (TEMESA) Lazaro Kilahala, ujenzi wa vivuko vitatu uliozinduliwa jijini hapa, umefanywa na kampuni hiyo ya kizalendo ya Songoro Marine Transport baada ya kushinda zabuni ya kazi hiyo, ambapo utagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 15.

Wednesday, January 25, 2023

MBOWE, LISSU WAKUTANA TEMEKE WALIWEKA JIJI LA DAR MTEGONI.


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema mageuzi ya siasa za Tanzania yanapaswa kuanzia Dar es Salaam kwa kuwa ndilo jiji lenye idadi kubwa ya watu kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini.


Mbowe ambaye ni aliwahi kuwa Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni na mbunge wa Hai, amesema nchi zote zinazojitambua kidemokrasia, majiji ndiyo huongoza kwa mageuzi hivyo Dar es Salaam inapaswa kuwa kitovu cha mageuzi.


Kauli hiyo ameitoa leo Jumatano Januari 25, 2025 katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika viwanja vya Bulyaga wilayani Temeke jijini Dar es Salaam ambapo pia ni wa kumpokea Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu aliyekuwapo nchini Ubelgiji.


"Kutokana na idadi kubwa ya watu waliopo Dar es Salaam kama wakiamua kudai Katiba mpya kwa kushirikiana utafika wakati Katiba mpya itapatikana. Mwaka huu tumefungua mikutano, tumerejea leo Dar es Salaam kumpokea Makamu, tutapiga jaramba, huku tunazungumza na kuwaamsha wananchi,"


"Inashangaza kuona Tanzania inaongozwa na chama kimoja katika kipindi cha miaka 30 ya vyama vya siasa, leo Rais ameteua wakuu wa wilaya mnaambiwa leo huyu ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke hamumjui hajawahi kuomba kura," amesema.


Mbowe pia amesema kama Chadema ikipata fursa ya kuongoza Tanzania watahakikisha kiongozi yeyote wa kisiasa hatopewa wajibu  kwa kuteuliwa bali atachaguliwa na wananchi.

KUNGUNI WADHIBITIWA MV VICTORIA 'SASA KUNA KITENGO MAALUM CHENYE WATAALAM WA AFYA'

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Afisa uhusiano wa kampuni ya huduma za meli nchini (MSCL), Edmond Rutajama amekutana na kufanya kikao kazi na waandishi wa habari wa mkoa wa Mwanza kutoa taarifa za miradi inayoendelea kutekelezwa na kampuni hiyo ikiwemo ujenzi wa meli ya Mv. Mwanza Hapa Kazi Tu.


Pamoja na hayo afisa huyo ametumia muda huo kujibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari likiwemo lile la muda mrefu ambalo kwa kipindi fulani lilizua gumzo mitandaoni na kuleta sintofahamu iliyokosa majibu, kwamba moja ya meli zake Mv Victoria imekuwa mazalio ya kunguni mende na viroboto nao abiria wakijiuliza , uchafu huo unasababishwa na nini?  Jeh wahusika, hawalioni hilo? Na jeh hatua zipi zimechukuliwa mpaka hivi sasa kudhibiti hali hiyo?


Rutajama amesema, Mwaka wa fedha 2022/2023 serikali imetenga shilingi bilioni 113,706,822,200 kwa ajili ya kutekeleza miradi  12 ya meli, miradi 4 ikiwa mipya, 5 ikikarabatiwa  na  miradi 3 ikitekelezwa.


Ziwa Tanganyika zitatumika bilioni 53 kutekeleza miradi 7, na bilioni  57 zitatumika kutekeleza mirdi 5 ndani ya ziwa Victoria huku bilioni 2 zitatumika kuendesha meli 3 zilizopokelewa kutoka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA). Edmond Rutajama  Afisa Uhusiano (MSCL )

IRINGA WAGAWA VISHIKWAMBI 30 KWA MADIWANI NA WAALAM

 

Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwanda akimkabidhi kishikwambi mmoja ya madiwani wa Manispaa hiyo
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwanda akimkabidhi kishikwambi mmoja ya madiwani wa Manispaa hiyo.


Na Fredy Mgunda, Iringa.


HALMASHAURI ya Manispaa ya Iringa imegawa vishikwambi kwa madiwani na wakuu wa idara kwa lengo la kurahisisha utenda wa kazi na kuendana na teknolojia.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vishikwambi hiyo, Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwanda alisema kuwa mabaraza na madiwani wa Manispaa hiyo waliazimia kununua vishikwambi na kuachana na matumizi ya taarifa za kwenye makaratasi.

Ngwanda alisema kuwa kununulia kwa vishikwambi hivyo kutapunguza matumizi makubwa ya fedha za vikao kwa ajili ya kuchapisha taarifa hizo.

Alisema kuwa jumla ya vishikwambi 30 vimenunuliwa kwa gharama ya shilingi millioni 18 ambapo vishikwambi hivyo vitatumika kwa miaka mingi.

Aliwataka madiwani na wataalam waliopata vishikwambi hivyo kuvitunza kwa kuwa hiyo ni ofisi na hayupo tayari kusikia taarifa kuwa vishikwambi hivyo vimeibiwa.

Ngwanda alisema kuwa kununulia kwa vishikwambi hivyo kutawarahishia utendaji wa kazi wa madiwani na wataalam kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia hapa nchini.

Alimalizia kwa kuupongeza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa kufanikisha kwa kununuliwa kwa vishikwambi hivyo.

Kwa upande wao baadhi ya madiwani na wataalam walisema wanampongeza Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwanda kwa kusimamia maazimio ya madiwani kwa wakati.


Walisema kuwa kupatikana kwa vishikwambi hivyo kutasaidia kufanya kazi kwa wakati na kutapunguza matumizi makubwa ya fedha za Serikali wakati wa vikao vya madiwani na matukio mengine ambayo yatakuwa yanahitaji kutolewa taarifa.

Tuesday, January 24, 2023

MSANII HUYU NDANI YA MWANZA VALENTINE HII

 Ruby Africa - Tai Chi (Official Music Video)

Monday, January 23, 2023

SAMIA NA FUMBO LA MKAKATI WA MANENO MANNE.

 NA ALBERT G. SENGO

RAIS Samia Suluhu Hassan akiwa DC nchini Marekani ameainisha mkakati wake wenye maneno manne tu. (4R's) 1. Reconciliation 2.Resillience 3. Reforms 4.Rebuilding of the Nation ( Tanzania) Kuna mtanzania ambae ana hataki Mambo manne muhimu Sana kwa nchi yetu huyo tumuombea dua mapepo kichwani kwake yatoke . Jamani Nani huyo mwenye kuhitaji Masada tumsaidie aachiwe huru na mapepo kichwani kwake

SAMIA AONGOZA KIKAO BARAZA LA MAWAZIRI.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Jumatatu Januqru 23, 2023 ameongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

POLISI WAFUKUA KABURI LA KIJANA ALIYEONEKANA MTAANI.


JESHI la Polisi kwa kushirikiana na wananchi na wataalamu wa afya, wamefukua kaburi la kijana Henry James (28), aliyedaiwa kufariki Aprili 20, 2022 na kupatikana akiwa hai Desemba 22,2022.


Tukio hilo la ufukuaji wa kaburi umefanyika katika Kijiji cha Kandaga, wilayani Uvinza mkoani Kigoma leo Januari 22, 2023 na kukutwa mwili huo ambapo wamechukua sampuli na kupelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali kwa ajili ya uchunguzi wa vina saba.

Lengo la ufukuaji huo wa kaburi linalodaiwa la kijana Henry ni kupata sampuli za vinasaba vya mwili huo na kulinganisha na sampuni za kijana huyo huyo anayedaiwa kuonekana uraiani akiwa hai mwishoni mwa mwaka jana.

POLISI WAUWA MAJAMBAZI WAWILI, WAKUTWA NA MABOMU.

 


WATU wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wenye umri kati ya miaka 25 hadi 30 wameuawa na Jeshi la Polisi mkoani Kagera na kisha kukutwa na bunduki moja aina ya AK 47, risasi 25 na mabomu mawili ya kurusha kwa mkono.


Watu hao bado hawajafahamika, waliuawa Januari 21, 2023 na miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Nyamiyaga wilayani Ngara kwa ajili ya kutambuliwa na kwa uchunguzi zaidi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, William Mwampaghale amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Januari 21, 2023 saa 3:35 usiku katika maeneo ya Barabara ya Kumunazi kwenda Relenge, Wilaya ya Ngara.

'RUKSA YA RAIS MIKUTANO YA HADHARA KWA VYAMA VYA SIASA IMEKUJA MUDA MUAFAKA INGECHELEWA INGETUKOSTI'

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Mshauri wa Kamati ya Amani Mkoa wa Mwanza Mchungaji Dkt. Jacob Mutash wa Kanisa la EAGT Kiloleli anasema kuendelea kuwa na zuio hilo baadaye ingetugharimu, kwani yangetokea mambo makubwa ya hovyo ambayo huenda yangeichafua nchi na sifa zake kutambulika kama kimbilio la amani. "Sito shangaa kuona viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa wakimpongeza Mhe. Rais Dkt Samia kwa kuwa hili lina busara yenye heri kwa taifa" "Kinachotakiwa hapo ni kupokea heshima hiyo aliyotupa Mhe. rais kwa moyo wa shukurani na kumuenzi kwa kufanya siasa za amani kwani kama angenyamaza nani angefanya chochote?" amehoji Mchungaji Mutash na kisha akaongeza. "Hatuzuii wasibishane, Hatuzuii wasipingane bali wapingane kwa hoja na wapingane wasibigane" #MikutanoYaHadhara #Siasa #tanzania

Sunday, January 22, 2023

LIVE:- Matchday Live | Man City v Wolves | Premier League

 Join Cel Spellman with guests Paul Dickov & Shaun Goater for our matchday live pre match show for our fixture against Wolves in the Premier League.

https://www.mancity.com/citytv/city-p... http://www.mancity.com http://www.facebook.com/mancity http://www.twitter.com/mancity http://www.instagram.com/mancity https://www.tiktok.com/@mancity About the Official Man City YouTube Channel: Here you will find all the latest videos from Manchester City, including, all Premier League goals, highlights, behind-the-scenes footage, training and much more. Get closer to the likes of Jack Grealish, Kevin De Bruyne, Erling Haaland, Riyad Mahrez, Phil Foden, Joao Cancelo and the rest of Pep Guardiola's team.

NIMEKUSOGEZEA WIMBO HUU WA INJILI TOKA MWIMBAJI WA A-TOWN - Elizabeth Mayengoh - Sema Nami Bwana (Official Video Music)

 BWANA akaja, akasimama, akaita vile vile kama kwanza, Samweli! Samweli! Ndipo Samweli akasema, Nena, BWANA; kwa kuwa mtumishi wako anasikia. 1Samweli 3:10

Shauku yetu na maombi yetu ni kusikia BWANA anasema nin #ElizabethMayengoh #MusicVideo #SemaNami

DIWANI KIMAYA AWATAKA WAZAZI,WALEZI KUWAPELEKA WATOTO WAO KITUO CHA SAYANSI STEM PARK CHA JIJINI TANGA

 


Na Oscar Assenga.Tanga

DIWANI wa Kata ya Chumbageni (CCM) Ernest Kimaya amewataka Wazazi na Walezi Jijini Tanga kukitumia kituo hicho cha Sayansi STEM PARK kwa kuwapeleka watoto wao ili waweze kujifunza na kupata Ubunifu wa mambo ya Kisayansi ili baadae waweze kuwa wabunifu wazuri na wenye vipaji kwenye maisha yao.

Aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kambi hiyo  Meneja wa Kituo Cha Sayansi STEM PARK TANGA wakati wa ufunguzi wa kambi maalumu ya kuwamejengewa Uwezo juu ya Sayansi ya Kilimo Cha Kisasa Maarufu kama Kilimo "Janja

Kambi hiyo  maalumu ambayo iliyofadhiliwa na Mashirika ya Club Rotary clubs Tanga , Robotech Labs na Tanzania Open Innovation(TOIO) kwa Ushirikiano wa Jenga Hub chini ya usimamizi wa Project Inspire ambao ndio wasimamizi wa Kituo Cha Sayansi Nchini STEM PARK kilichopo mkoani Tanga.
Alisema uwepo wa kituo hicho katika eneo lake umekuwa na tija kubwa kwani kimekuwa kikitumiwa na wanafunzi na Walimu kujifunza kwa vitendo masomo ya sayansi hivyo kusaidia wanafunzi wanapokuwa wakisoma kwa nadharia shuleni baadae wanapokwenda kwenye kituo hicho wanasoma kwa vitendo na hivyo kuwasaidia kuwa na uelewa mzuri wa mambo wanayofundishwa wakiwa darasani.

“Kwa kweli kituo hiki kinafanya kazi kubwa na nzuri sana hivyo niwapongeze kwani mafunzo mnayotoa vijana wetu ni mazuri na yanawasaidia namna ya kutumia ujuzi walioupata na hivyo kuepukana na kukaa vijiweni ambako wengine wanajikuta wakitumia dawa za kulevya “Alisema

Aidha alisema kwamba kazi inayofanywa na kituo hicho ni kubwa kwa sababu mafunzo waliyoyapata yanakwenda kuwasaidia kuwa wabunifu wazuri zaidi huku akiwataka pia kuyatumia vizuri kwa ajili ya tija zaidi.

Alisema kwamba mazoezi ambayo wamewafundishwa vijana hao watengeneze utaratibu mzuri baada ya wa kutoka hapo baadae waende kwenye uhalisi wakiondoka wanaondoka watakuwa kitu ambacho wanacho baada ya hapo vijana watakuwa na ujuzi mkubwa wa kuwatoa kwenye fikra.

Alieleza kwamba itawatoa kwenye fikra ambazo sio nzuri na badala yake watakuwa wabunifu na kuondokana na vijana wavuta bangi, madawa ya kulevya maana watakuwa wamejitambua na wanaamini wanafunzi wanashika sana wakiwa na umri mdogo.

Awali akielezea kambi hiyo Meneja wa Kituo cha Meneja wa Kituo Cha Sayansi STEM PARK TANGA  Max George alisema  Kituo hicho kimekuwa na utaratibu wa kuweka Kambi kwaajili ya kupata Mafunzo juu ya namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwakutumia Sayansi,

Alisema kituo hicho kimekuwa na  utaratibu maalumu wa kuweka kambi kwaajili ya kupata mafunzo ya mada husika, kwa mfano Kambi hii tumeifanya kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi Jijini Tanga kwaajili ya kujifunza Kilimo cha Kisasa changamoto mbalimbali za Kilimo Cha Kisasa Maarufu kama Kilimo Janja.

Aidha alisema lakini pia changamoto za kilimo kwa nyakati hizi sote tunafahamu kuwa ni mabadiliko ya Tabia Nchi ambayo yameperekea upungufu wa Mvua maeneo mengi, hivyo kwakupitia Kambi hii Wanafunzi wameweza kujifunza namna ya kulima Kilimo ambacho hakitahitaji maji mengi, wamejifunza jinsi ya kumwagilia mbegu lakini jinsi ya Kutumia mfumo wa mbolea na Umeme katika Kilimo" Alisema George

Alisema Kituo hicho kitaendelea kuwafundisha Wanafunzi masuala mbalimbali kisayansi nakuwataka Wazazi kuwaruhusu Watoto Wanapokuwa wanahitajika kituoni hapo,

"Kituo chetu kinafundisha Sayansi kwa ujumla na tutaendelea kuandaa Kambi kama hizi, Niwaombe Wazazi muwaruhusu Watoto wenu pale wanapohitajika lakini pia hata pale hatuwahiji ni vizuri Watoto mkawapatia utaratibu maalumu wa kumwezesha kufika kituoni kwaajili ya kujifunza Sayansi, hapa mwanafunzi anaruhusiwa kuja muda wote kujifunza na Walimu wapo muda wote " Alisisitiza George

MADIWANI MUFINDI WALIOKULA FEDHA ZA VIKUNDI KUKIONA CHA MTEMA KUNI

 

Katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi, Dikson lutevele (VILA) akiongea na wanachama wa chama hicho kata ya Mapanda juu ya umuhimu wa nidhamu ya uongozi.
Baadhi ya a wajumbe wa Halmashauri kuu ya kata ya Mapanda.


Na Fredy Mgunda, Iringa.


CHAMA cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi kimesema hakipo tayari kiwavumilia madiwani waliotumia vibaya mikopo ya vikundi ya asilimia 10 inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Akizungumza na mwandishi wa habari wa blog hii, katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi, Dikson lutevele (VILA) alisema kuwa lengo la serikali kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani ni kwa ajili ya kukuza mitaji ya vikundi na sio madiwani.

Lutevele alisema kuwa haiwezekani chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi kikamvumilia diwani anayezichezea fedha za Serikali ambazo zimetakiwa kupelekwa kwa vikundi kwa ajili ya kukuza mitaji ya vikundi kwa maendeleo ya wananchi wa Halmashauri husika.

Alisema kuwa hivi karibuni kumetokea kashfa kwa baadhi ya madiwani kuandikisha vikundi hewa na kupewa mikopo kutoka Halmashauri kwa manufaa ya diwani ambao sio walengwa wa mikopo hiyo na kuwakosesha fursa wananchi wenye sifa ambao walistahili kupata mikopo hiyo.

Lutevele alisema kuwa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi kimeanza vikao kwa ajili ya kuwachukulia hatua kali madiwani wote waliobainika kuunda vikundi hewa vya mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri kutokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri husika.

Alisema kuwa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi hakipo tayari kiwavumilia madiwani wote ambao wanakichafua chama kwa kuanzisha vikundi hewa na kuchukua mikopo ya asilimia 10 kutoka Halmashauri.

Lutevele alisema kuwa anampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Taifa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kukijenga nchi na chama kwa ujumla

Lutevele alimazia kwa kusema kuwa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi kipo kwa ajili ya kusimamia serikali na kukijenga chama hicho kutokana na ilani ya uchaguzi wa chama cha mapinduzi ya mwaka 2020/2025.