NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Adam Malima, leo amefanya uzinduzi wa ujenzi wa vivuko vipya vitatu vitakavyotumika kutoa huduma katika maeneo ya Nyakaliro -Kome, Bwiru-Bukondo na Ijinga-Kahangala, ili kuondoa kero za usafiri kwa wananchi
Naibu katibu mkuu wa wizara ya ujenzi na uchukuzi (sekta ya ujenzi) Ludovick Nduhiye, amesema uzinduzi wa ujenzi wa vivuko 3 ambavyo vimezinduliwa jijini Mwanza, ni hitaji kubwa kwa wananchi wanaoishi maeneo ambayo vivuko hivyo vitatoa huduma, baada ya ujenzi wake kukamilika.
Mkurugenzi wa kampuni ya Songoro Marine Transport Major Songoro, amesema vivuko 3, vinajengwa kwa kuzingatia viwango vya kitaifa (TASAC) na kimataifa (IMO, na kuwa wamejipanga kikamilifu kuhakikisha vivuko hivyo vinakamilika kwa muda uliopangwa. Uzinduzi wa ujenzi umefanyika leo
Kwa mujibu wa Mtendaji mkuu wa wakala wa ufundi na umeme Tanzania (TEMESA) Lazaro Kilahala, ujenzi wa vivuko vitatu uliozinduliwa jijini hapa, umefanywa na kampuni hiyo ya kizalendo ya Songoro Marine Transport baada ya kushinda zabuni ya kazi hiyo, ambapo utagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 15.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.