ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, January 25, 2023

MBOWE, LISSU WAKUTANA TEMEKE WALIWEKA JIJI LA DAR MTEGONI.


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema mageuzi ya siasa za Tanzania yanapaswa kuanzia Dar es Salaam kwa kuwa ndilo jiji lenye idadi kubwa ya watu kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini.


Mbowe ambaye ni aliwahi kuwa Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni na mbunge wa Hai, amesema nchi zote zinazojitambua kidemokrasia, majiji ndiyo huongoza kwa mageuzi hivyo Dar es Salaam inapaswa kuwa kitovu cha mageuzi.


Kauli hiyo ameitoa leo Jumatano Januari 25, 2025 katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika viwanja vya Bulyaga wilayani Temeke jijini Dar es Salaam ambapo pia ni wa kumpokea Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu aliyekuwapo nchini Ubelgiji.


"Kutokana na idadi kubwa ya watu waliopo Dar es Salaam kama wakiamua kudai Katiba mpya kwa kushirikiana utafika wakati Katiba mpya itapatikana. Mwaka huu tumefungua mikutano, tumerejea leo Dar es Salaam kumpokea Makamu, tutapiga jaramba, huku tunazungumza na kuwaamsha wananchi,"


"Inashangaza kuona Tanzania inaongozwa na chama kimoja katika kipindi cha miaka 30 ya vyama vya siasa, leo Rais ameteua wakuu wa wilaya mnaambiwa leo huyu ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke hamumjui hajawahi kuomba kura," amesema.


Mbowe pia amesema kama Chadema ikipata fursa ya kuongoza Tanzania watahakikisha kiongozi yeyote wa kisiasa hatopewa wajibu  kwa kuteuliwa bali atachaguliwa na wananchi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.