NA ALBERT G.SENGO/MWANZA
Afisa uhusiano wa kampuni ya huduma za meli nchini (MSCL), Edmond Rutajama amekutana na kufanya kikao kazi na waandishi wa habari wa mkoa wa Mwanza kutoa taarifa za miradi inayoendelea kutekelezwa na kampuni hiyo ikiwemo ujenzi wa meli ya Mv. Mwanza Hapa Kazi Tu.
Pamoja na hayo afisa huyo ametumia muda huo kujibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari likiwemo lile la muda mrefu ambalo kwa kipindi fulani lilizua gumzo mitandaoni na kuleta sintofahamu iliyokosa majibu, kwamba moja ya meli zake Mv Victoria imekuwa mazalio ya kunguni mende na viroboto nao abiria wakijiuliza , uchafu huo unasababishwa na nini? Jeh wahusika, hawalioni hilo? Na jeh hatua zipi zimechukuliwa mpaka hivi sasa kudhibiti hali hiyo?
Rutajama
amesema, Mwaka wa fedha 2022/2023 serikali imetenga shilingi bilioni
113,706,822,200 kwa ajili ya kutekeleza miradi
12 ya meli, miradi 4 ikiwa mipya, 5 ikikarabatiwa na
miradi 3 ikitekelezwa.
Ziwa
Tanganyika zitatumika bilioni 53 kutekeleza miradi 7, na bilioni 57 zitatumika kutekeleza mirdi 5 ndani ya
ziwa Victoria huku bilioni 2 zitatumika kuendesha meli 3 zilizopokelewa kutoka
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA). Edmond Rutajama Afisa Uhusiano (MSCL )
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.