Meneja wa Mradi Kinyerezi II, Mhandisi Stephens S.A.Manda (wakwanza kulia), akimtembeza Naibu Mkurugenzi wa TANESCO (usambazaji) Mhandisi Raymond Seya, (wapili kulia), kujionea maendeleo ya mradi w aumeme wa Kinyerezi II jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Oktoba 12, 2018.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA
la Umeme Nchini TANESCO limesema liko tayari kupokea uwekezaji wa viwanda vya
aina zote kwani hivi sasa kuna umeme wa kutosha, bora na wa uhakika. Hayo
yamesemwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO (Ugawaji), Mhandisi Raymond
Seya, baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa umeme Kinyerezi II jijini Dar es Salaam, Ijumaa
Oktoba 12, 2018.
“Mradi
unafikia mwisho sasa, kwasababu mashine zote zimeshafungwa na uwezo wa mashine
hizi ni kuzalisha Megawati 240, tunamalizia
mambo madogo madogo kama ujenzi wa barabara na kupaka rangi lakini pia kujenga
ofisi za wafanyakazi.”
Alifafanua Mhandisi
Seya Tunataka
kuwahakikishia wananchi uwekezaji huu mkubwa wenye thamani ya zaidi ya shilingi
bilioni 750 zote zikiwa zimetolewa na serikali umekamilika na tayari umeingizwa
kwenye Gridi ya taifa.
“Tunapenda
kumshukuru sana Mhe. Rais wa serikali ya awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli
kwa kuridhia kufadhili mradi tunawahakikishia sera ya awamu ya tano ya kujenga
uchumi wa viwanda itatekeelezwa kikamilifu na sisi kama TANESCO tuko tayari
kupokea uwekezaji wa viwanda vya aina zote.” Alisema.
Alisema,
tayari umeme huo umeingizwa kwenye gridi ya taifa na hadi sasa kwa ujumla kuna
kiasi cha umeme kwenye gridi ya taifa Megawati 1500 na ukiangalia repoti za
matumizi ya umeme kila siku tunakiuwa na ziada ya Megawati 250 hadi 160,
Wikiendi inakuwa zaidi kwa sababu matumizi ya umeme yanapungua kwa hivyo
yunapoongeza vyanzo hivi vya uzalishaji umeme tuanzidi mkuwa na uwezo wa
kuunganisha wateja zaidi na kutoa huduma iliyo bora.” Alisema. Mhandisi
Seya pia alitembelea mradi mwingine wa upanuzi wa Kinyerezi I ambapo
miundombinu ya kusimika mashine iko tayari na kwamba zoezi la kufunga mashine
hizo litaanza wakati wowote luanzia sasa.
Akitoa
taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo, Meneja wa Mradi
Kinyerezi II, Mhandisi Stephens S.A.Manda Alisema miradi
yote miwili ni miradi ya kimkakati na kwamba wakati mradi wa Kinyerezi II
tayari umekamilika, mradi wa upanuzi wa Kinyerezi I, umefikia asilimia 70. “Mradi
wa upanuzi wa Kinyerezi I, utakuwa na Megawati 185 ambapo Kinyerezi I yenyewe
inazalisha umeme Megawati 150 na hivyo utafanya jumla ya Megawati 335 utakapokamilika
Agosti mwakani.
“Kwa
hiyo miradi yote hii itakapokamilika tunazungumzia jumla ya Megawati 575
zitakuwa zinazalishwa hapa Kinyerezi.” Alifafanua Mhandisi Mmanda. “Sasa hivi kwenye Gridi ya Taifa tunatosheleza
mahitaji yote na tuna ziada, kwa hiyo tunachosema kama Shirika la umeme tunao
umeme wa mkutosha na wawekezaji waje ili tuweze ili twende na falsafa ya Rais wetu
ya kuwa na nchi yenye uchumi wa kati lakini zaidi sana nchi yenye uchumi wa
viwanda.” Alsiema. Mhandisi
Mmanda alibainisha kuwa Mradi wa upanuzi wa Kinyerezi I utakamilika Agosti
mwakani.
Meneja wa Mradi Kinyerezi II, Mhandisi Stephens S.A.Manda (wapili kulia), akimpatia maelezo Naibu Mkurugenzi Mtedaji wa TANESCO (usambazaji), Mhandisi Raymond Seya, kuhusu namna mitambo katika chumba cha udhibiti (Control room) inavyofanya kazi
Meneja Miradi Mwandamizi TANESCO, Mhandisi Emmanuel Manirabona, akikagua mitambo kwenye chumba cha udhibiti (Control room) cha Kinyerezi II leo Ijumaa Oktoba 12, 2018.
Mhandisi Seya (kushoto), akiteta jambo na Mhandisi Mmanda.
Naibu Mkurugenzi Mtedaji Shirika la Umeme nchini TANESCO anayeshughulikia usambazaji, Mhandisi Raymond Seya, (katikati), kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, akitembelea mradi wa umeme wa Kinyerezi II kujionea maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo leo Ijumaa Oktoba 12, 2018. Kulia ni Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Stephenes S.A Mmanda (kulia) na Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika hilo, Bi. Leila Muhaji,.
Moja ya mitambo ambayo tayari imewasili ili kutekeleza mradi mwingine wa upanuzi wa Kinyerezi I.
Muonekano wa eneo itakapofungwa mitambo kwenye eneo la upanuzi wa mradi wa umeme Kinyerezi I hadi kufikia leo Ijumaa Oktoba 12, 2018.