ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 11, 2018

KATIBU MKUU SUSAN MLAWI ATOA MAELEKEZO KWA VIONGOZI WA BODI WA FILAMU.


Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Susan Mlawi (kulia) akitoa maelekezo na ufafanuzi kwa wajumbe wa Bodi ya Filamu Tanzania kuhusu suala la Sera ya Bodi ya Filamu hatua iliyofikia walipofanya walipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dodoma,kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Prof.Frowin Nyoni.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Prof.Frowin Nyoni (katikati) akimweleza Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Susan Mlawi (wa kwanza kulia)namna uongozi wa bodi hiyo umejipanga kutatua changamoto ya upungufu wa watumishi katika kada mbalimbali ,kushoto ni Mjumbe wa Bodi hiyo Bw.Raymond Kwohelera.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi.Joyce Fissoo akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Susan Mlawi (hayupo pichani) ya kazi za filamu haramu zilizokamatwa mwaka 2016 na kushikiliwa na TRA zenye thamani ya Bilioni 6 kuwa wakati umefika wa kufanyiwa utaratibu stahiki kwa mujibu wa sheria walipomtembelea leo ofisini kwake Jijini Dodoma na baadhi ya wajumbe wa Bodi wa ofisi yake,wa kwanza kulia wajumbe wa Bodi hiyo ambao ni Bw.Raymond Kwohelera na wapili kulia  ni Bi.Anuciatha Leopold.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Susan Mlawi (wapili kulia)akiwa katika picha ya pamoja baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Filamu Tanzania walipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dodoma,watatu kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Prof.Frowin Nyoni,na kutoka kushoto watatu ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi.Joyce Fissoo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.