Friday, September 6, 2024
Darassa & Harmonize - Mazoea (Visualiser)
Music by Darassa & Harmonize performing "MAZOEA", Conveys a powerful message about the strength of love and the memories it leaves behind in a relationship. The chorus reminds us that while love may fade, the habits and memories shared by lovers remain, often becoming the source of true sorrow. The song is filled with a sense of regret and carries a message of seeking forgiveness in the hope of rekindling the relationship. Audio produced by Abbah process & Visual shot by Mbongo.
MAMA KOKA AUNGANA NA RAIS SAMIA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU SHULE YA MSINGI BOKO TIMIZA
NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Thursday, September 5, 2024
WAHAMASISHWA KUTUMIA NISHATI SAFI ZA KUPIKIA
Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inaendelea kuhamasisha wananchi kutumia Nishati Safi za Kupikia kwa lengo la kuwezesha utunzaji wa mazingira, kuboresha afya na ustawi wa jamii sambamba na kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Mhandisi wa Miradi kutoka REA, Mhandisi Kelvin Tarimo amesema hayo hivi leo Septemba 04, 2024 Jijini Dodoma alipokuwa akiwasilisha mada ya Nishati Safi ya Kupikia kwa wanawake zaidi ya 650 katika Mkutano Mkuu wa kwanza wa Mtandao wa Wanawake wa Jeshi la Magereza.
“Matumizi ya Nishati Safi za Kupikia ni ajenda inayolenga kukabiliana na ongezeko la uharibifu wa mazingira pamoja na athari za kimabadiliko ya tabianchi pamoja na athari za kiafya zinazotokana na matumizi ya nishati zisiyo safi za kupikia,” amesema Mhandisi Tarimo.
Alifafanua kuwa matumizi ya Nishati zisizo safi na salama za kupikia huchangia uharibifu wa mazingira ambapo alibainisha kuwa inakadiriwa zaidi hekari zipatazo Laki Nne za misitu hukatwa kila mwaka kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwemo matumizi ya kuni na mkaa jambo ambalo alisema limekua likisababisha madhara mbalimbali ya kimazingira ikiwemo uharibifu wa vyanzo vya maji na ikolojia kwa ujumla.
Mhandisi Tarimo alisema katika kukabiliana na hali hiyo, Wakala kama moja ya mdau mkuu wa masuala ya Nishati Vijijini itaendelea kuhakikisha inatimiza vyema lengo kuu la utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao umelenga hadi kufikia Mwaka 2034 asilimia 80 ya wananchi wawe wanatumia Nishati Safi za Kupikia.
Amesema REA imejipanga kuhakikisha adhma hiyo inafikiwa kikamilifu kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Nishati Safi ya Kupikia na amewasisitiza wananchi hususan wanawake kuendelea kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo kwenye mnyororo mzima wa thamani wa masuala ya Nishati Safi ya Kupikia.
“Hatua tunazoendelea nazo sasa ni pamoja na kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu umuhimu wa matumizi ya Nishati Safi za Kupikia; kuhakikisha upatikanaji wa Nishati Safi, nafuu, endelevu na za uhakika za Kupikia kote nchini haswa maeneo ya vijijini na kuhamasisha Uwekezaji katika Sekta Ndogo ya Nishati Safi ya Kupikia,” amefafanua Mhandisi Tarimo.
KOKA KUIPIGA JEKI SHULE YA MSINGI TUMBI KATIKA KUBORESHA MIUNDOMBINU
NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Wednesday, September 4, 2024
Monday, September 2, 2024
MBUNGE KOKA APANIA KUWAINUA KIUCHUMI UVCCM KUPITIA MRADI WA KAMPUNI
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka katika kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo amepania kuwainua vijana na kuwaondoa katika wimbi la umasikini kwa kuwachangia gharama mbali mbali kwa ajili ya kuanzisha kampuni ya umoja wa vijana wa (UVCCM) Wilaya ya Kibaha mjni ambayo itawasaidia katika kujikwamua kiuchumi.
Koka ametoa kauli hiyo wakati wa kikao cha baraza la UVCCM Wilaya ya Kibaha mjini na kusema kwamba amekubali kwa moyo mmoja kuwaunga mkono juhudi ambazo zinafanywa na vijana hao ya kutaka kuanzisha kampuni ambayo itakuwa ikijikita zaidi katika shughuli mbali mbali.
Alibainiwa kwamba lengo lake kubwa ni kuhakikisha anaweka mipango madhubuti kwa vijaana hao kuweza kuwa na miradi mbali mbali ya kimaendeleo hivyo atachangia gharama mbali mbali ambazo zitahitajika ikiwemo kufanya usajili wa kampuni hiyo ambayo itaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa vijana hao.
"Vijana mimi kama mbunge wenu nipo pamoja na nyinyi na Risala yenu nimeisikia ya kutaka kuwa na kampuni ambayo itakuwa ikifanya shughuli mbali mbali kwa hiyo mimi nitachangia gharama mbali mbali ikiwemo kampuni hiyo kupata usajili na nina imani kwamba taratibu zote zikikamilika kampuni hiyo itaanza kufanya kazi kwa maslahi mapana ya vijana wa jimbo la Kibaha mjini,"alisema Koka
Aidha Mbunge huyo aliwataka vijana hao kuhakikisha wanakuwa kitu kimoja na kuachana kabisa na kuwa na makundi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unatarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu kwani lengo ni kuweza kushinda katika mitaa yote 73.
Kadhalika Mbunge Koka amewasihi vijana kufanya kazi zao kwa ushirikiano ikiwa pamoja na kuheshimu viongozi mbali mbali wa chama na serikali walioko madarakani kwa ngazi zote za kiutawala na kutengeneza misingi imara ya kuwa karibu na jamii kwa makundi yote bila ya kuwa na ubaguzi wowote.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kibaha mjini Ramadhani Kazembe amesema kwamba malengo ambayo wamejiwekea ni kubuni miradi mbali mbali ya kimaendeleoambayo itaweza kuwasaidia vijana kuondokana na umasikini ikiwa pamoja na kujiongezea kipato.
Kazembe alisema kwamba ana imani kubwa kampuni hiyo pindi itakapokamilika itakuwa ni moja ya fursa ya kipekee kwa vijana wa UVCCM kuweza kupata fursa za ajili kutokana na shughuli mbali mbali ambazo zitakuwa zikifanyika na kuwahimiza vijana waweze kuwa na umoja na mshikamano katika kukijenga chama pamoja na jumuiya zake zote.
Sunday, September 1, 2024
CRDB Bank Foundation yazindua Kampeni ya Kuwaunganisha Wajasiriamali Wadogowadogo nchini na programu ya IMBEJU
Akizungumza Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Bonaventura Paul, ambaye aliipongeza CRDB Bank Foundation kwa kuja na kampeni hiyo iliyopewa jina la ‘IMBEJU Uwezeshaji’ ambayo inalenga kuwafikia wajasirimiali wadogo wadogo kote nchini hususani wale walio maeneo ya pembezoni na vijijini jambo ambalo litasaidia si tu kukuza ujumuishi wa kifedha bali pia kukuza sekta ya ujasiriamali na uchumi wa Taifa kwa ujumla.
"Malengo yetu ni kuwa baada ya kuhitimu programu hii, wataweza Kuunganishwa na uwezeshaji kupitia Benki yao ya CRDB ambapo kupitia Idara yetu ya Wateja Wadogo na Wakati wataweza kukopeshwa hadi shilingi bilioni 3 kulingana na uwezo wa ulipaji wa biashara zao," aliongeza.
"Programu ya IMBEJU imeleta mapinduzi makubwa katika kuchochea ujumuishi wa kifedha, ambapo zaidi ya wanawake na vijana wajasiriamali 600,000 wamefikiwa na mitaji wezeshi ya zaidi ya shilingi bilioni 11 imetolewa," alisema Bushagama.
“Timu yetu kutoka Makao Makuu kwa kushirikiana na matawi ya Benki yetu ya CRDB katika mikoa hiyo, pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii tutashirikiana kwa pamoja kutoa elimu ya fedha, mafunzo ya biashara na ujasirimali. Baada ya kanda hiyo tutakwenda Kanda ya Kusini na Kanda ya Kati,” aliongezea Bushagama.
MATI SUPER BRANDS LTD YAPEWA TUZO MAALUMU NA CHUO CHA UKAMANDA NA UNADHIMU (CSC) CHA JWTZ
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Kampuni ya Mati Super Brands Limited inayozalisha vinywaji changamshi yenye makao yake Makuu Mjini Babati Mkoani Manyara imepewa tuzo ya maalumu kutoka Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (CSC) cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kusaidia jamii inayowazunguka pamoja na kushirikiana na taasisi mbali mbali za kiserikali.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (CSC) chenye makao yake Mkoani Arusha, Colonel Verus Chrysostom Mbuzi katika ziara maalumu ya kimafunzo iliyofanywa na Maafisa hao wa ngazi za juu wa Kijeshi kutoka mataifa mbali mbali katika kampuni ya Mati Super Brands Ltd.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited, David Mulokozi ametoa shukrani zake kwa Chuo hicho cha kijeshi kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo katika masuala mbali mbali ikiwemo kurudisha sehemu ya faida wanayoipata kwa jamii inayowazunguka.
Mulokozi amesema kuwa Tuzo hiyo inawapa chachu ya kuendelea kufanya vizuri kuendelea kushirikiana na taasisi za umma pamoja na kuzalisha bidhaa bora zinazozingatia ubora na usalama wa mtumiaji.
Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (CSC) , Colonel Verus Chrysostom Mbuzi amepongeza Kiwanda kwa kuwa karibu na jamii na taasisi za serikali pamoja na kutoa fursa wa mafunzo kwa vitendo vya Maafisa wa Kijeshi juu ya masuala mbali mbali ikiwemo usalama wa chakula .