ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 5, 2024

KOKA KUIPIGA JEKI SHULE YA MSINGI TUMBI KATIKA KUBORESHA MIUNDOMBINU

 


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 


Shule ya msingi Tumbi iliyopo katika Halmashauri  Kibaha mji kwa sasa bado inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo kutokuwa na bwalo la kulia chakula,uhaba wa kompyuta  pamoja na upungufu mkubwa wa matundu ya vyoo 21.

Hayo yamebainika wakati wa halfa ya mahafali ya 53 kwa wanafunzi wa darasa la saba waliohitimu  katika shule ya msingi Tumbi na kuhudhuliwa na viongozi mbali wa chama,serikali pamoja na wazazi na walezi wa wanafunzi.

Katika kuliona hilo Mbunge Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe.Silvestry Koka ameamua kulivalia njuga suala hilo la kuahidi kulitafutia ufumbuzi suala hilo ili kuwawekea wanafunzi mazingira mazuri ya kujisomea.

Koka amebainisha kwamba lengo lake kubwa ni kuboresha kiwango cha elimu na kwamba atatumia fedha za mfumo wa Jimbo kwa ajili ya kutatua changamoto hiyo ya matundu ya vyoo katika shule hiyo.

"Nimesikiliza  risala yenu kuhusiana na suala la changamoto ya uhaba wa matundu ya vyoo na mm kama Mbunge wenu nitatumia fedha za mfuko wa Jimbo kwa lengo la kuweza  kukabiliana na changamoto zilizopo katika shule hii,"alisema Mhe.Koka 

Alisema kwamba pamoja na kupambania suala la miundombinu ya vyoo pia ataisaidia shule hiyo kuwatafutia wadau mbali mbali wa maendeleo katika kuwasaidia kuwapatia kompyuta ili wanafunzi kupata fursa ya kujifunza zaidi.

Mbunge huyo pia alimshukuru Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza  kutenga fedha ambazo zimekwenda kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo.

Aidha alisema kwa kipindi cha kipindi cha miaka mitatu katika Jimbo la Kibaha mjini limeweza kupata fedha ambazo zimeza kufanikisha ujenzi wa shule mpya saba zikiwemo za Sekondari na msingi.

Katika hatua nyingine Koka amewahimiza wazazi na walezi kuwalinda watoto wao katika suala zima la malezi ikiwa sambamba na  kuchangia suala la chakula cha mchana kwa wanafunzi.

Kwa upande wake mkuu wa shule ya Tumbi Jane Moses  ametoa pongezi kwa Mbunge kwa kuweza kuonyesha ushirikiano wa kutosha katika suala zima la kuboresha sekta ya elimu.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la elimu Kibaha Robert Shiringi amempongeza Rais Samia pamoja na Mbunge kwa kuweza kutekeleza ilani  ya chama kwa vitendo katika nyanja mbali mbali.

Shiringi amebainisha kwamba katika kipindi cha miaka mitatu kuna hatua kubwa ya kimaendeleo ambayo imefanyika katika Halmashauri ya mji Kibaha ikiwemo sekta ya afya,maji,elimu pamoja na miundombinu ya barabara.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.