ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 1, 2013

LOWASSA AZINDUA VIKOBA KWA AKINA MAMA MWANZA

Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa (wapili kutoka kulia) akikata utepe wa kuashiria uzinduzi wa Vikoba vya umoja wa wanawake wa madhehebu ya Kikristo Mwanza, kulia ni askofu wa Kanisa la Anglican Diosisi ya Nyanza (DVN) Boniface Kwangu akiwa ameshikilia kiasi cha shilingi millioni 40 zilizochangwa ikiwa ni pamoja na hudhi na ahadi zilizowekwa kutunisha Vikoba, Mkuu wa mkoa wa Simiyu Paschal Mabiti pia anaonekana pichani wa pili kushoto .
Na Albert  Sengo.
WAZIRI Mkuu Mstaafu Edward Lowassa amewapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Serikali ya Zanzibar Dkt.Mohamed Sheni kwa njisi ambavyo wamekuwa wakikazia suala la kudumisha amani nchini, wakiwemo viongozi wa Taasisi za kidini Kalidinali, Askofu Mkuu Polycarp Pengo (Romani),Askofu Alex Malasusa (KKKT), Mufti Shekhe Mkuu wa Tanzania  Simba Bin Simba na viongozi wengine wakiwemo wachungaji wa madhehebu mbalimbali nchini.

Lowassa alitoa pongezi hizo leo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Vikoba vya umoja wa wanawake wa Madhehebu ya Kikristo Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela uliofanyika katika Kanisa la D.V.N Angilikana lililopo Nyamanoro Wilayani Ilemela  na kueleza kwamba viongozi hao wamekuwa wakikemea udini na kutaka watanzania kuendelea kuilinda amani ya nchini kama mboni ya jicho kwani kuipoteza Amani tuliyonayo nchini itatugharimu maisha kuirejesha hivyo amewasihi watanzania wasichoke na Amani ambayo ni kama hewa ikitoweka haiwezi kurudi tena kamwe.
Lowassa amewataka watanzania wote kuwasikiliza viongozi hao na kuwaunga mkono katika kukemea watu wanaotaka kuwatumia na kusababisha vurugu ili amani tuliyonayo nchini iweze kupotea kwa masilahi yao. 
Sikiliza alichosema.... Maandamano yalifanyika kutoka viwanja vya furahisha hadi Kanisa la D.V.N Angilikana lililopo Nyamanoro Wilayani Ilemela kwaajili ya uzinduzi wa Vikoba vya umoja wa wanawake wa Madhehebu ya Kikristo Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela. 
Hatimaye maandamano yalifika katika Kanisa la D.V.N Angilikana lililopo Nyamanoro Wilayani Ilemela.


Ilikuwa ni majira ya saa 3:45 asubuhi na hii ni sehemu ya kusanyiko lililofika kanisani hapa  kwaajili ya kushuhudia uzinduzi wa Vikoba vya umoja wa wanawake wa Madhehebu ya Kikristo Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.


Kwaya ya Anglican Nyamanoro Mwanza nayo ilihudumu kwenye ya uzinduzi wa Vikoba vya umoja wa wanawake wa Madhehebu ya Kikristo Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.


Watu wa mataifa mbalimbali nao wamekuja katika kusanyiko hili Kanisa la D.V.N Angilikana lililopo Nyamanoro Wilayani Ilemela kwaajili ya uzinduzi wa Vikoba vya umoja wa wanawake wa Madhehebu ya Kikristo Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.


Sambamba na tukio la uzinduzi wa vikoba lililofanyika kanisani hapa vilevile ikumbukwe kuwa siku hii ni sehemu ya Maadhimisho ya Maombezi ya kinamama duniani hivyo akinamama walifanya maombezi hayo kisha baadaye ukafuata uzinduzi uliosimamiwa vyema na mh. Lowassa.


Ibada ya maombezi ikiendelea kanisani.


Umoja wa akinamama wa Madhehebu ya Kikristo Mwanza ukimkabidhi zawadi Mh. Lowassa kwaajili ya mkewe ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maombezi ya Kinamama Duniani katika Kanisa la D.V.N Angilikana lililopo Nyamanoro Wilayani Ilemela. 


Umoja wa akinamama wa Madhehebu ya Kikristo Mwanza pia ulimkabidhi zawadi ya Biblia Mh. Lowassa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maombezi ya Kinamama Duniani katika Kanisa la D.V.N Angilikana lililopo Nyamanoro Wilayani Ilemela. 


Umoja wa akinamama wa Madhehebu ya Kikristo Mwanza pia ulimkabidhi zawadi ya Biblia Mh. Lowassa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maombezi ya Kinamama Duniani katika Kanisa la D.V.N Angilikana lililopo Nyamanoro Wilayani Ilemela.


Aidha Mbunge huyo wa Jimbo la Monduli na Mjumbe wa NEC CCM Taifa wa Wilaya ya Monduli amewataka wanasiasa wote nchini kumuunga mkono kuiomba serikali kurudisha fedha za Mabilioni ya JK na kuhakikisha yanapelekwa moja kwa moja kwa wanawake wa vijijini walioanzisha VICOBA ili kuwasaidia kujikwamua kiuchumi hali ambayo itawawezesha wanawake wengi kuondokana na umasikini. 

Sikiliza alichosema..

Utaifa zaidi ndani ya kwaya ya kanisa la DVN.

Aidha amewataka watanzania wote kuwasikiliza viongozi hao na kuwaunga mkono katika kukemea watu wanaotaka kuwatuawa  na kusababisha vurugu ili amani tuliyonayo nchini iweze kupotea kwa masilahi yao kamwe wasikubali hivyo ni vyema wakaungana kuwakataa kwa nguvu zote kwani hadi sasa wagombea Urais wan chi ya Kenya wanawataka wakenya kuwa kama watanzania hivyo hivyo na Waganda wamekuwa wakihubiliwa kutuiga kutokana na umoja na amani tuliyonayo hapa nchini.


Furaha ya mchungaji na mwanae.


Katika kuuzindua mfuko wa Vikoba vya umoja wa wanawake wa Madhehebu ya Kikristo Jiji la Mwanza, Mfanyabiasha ambaye ni mkurugenzi wa Gold Crest Hotel, Bw. Mathias Manga alitoa cheki yenye thamani ya shilingi millioni 5.


Waziri mkuu mstaafu Mh. Edward Lowassa akimpa mkono wa pongezi MNEC wa Busega Bw. Raphael Chegeni mara baada ya kuwasilisha mchango wake wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Vikoba vya umoja wa wanawake wa Madhehebu ya Kikristo Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela uliofanyika katika Kanisa la D.V.N 


Furaha. 


Saa 6:30 mchana shughuli ya uzinduzi inamalizika na Mh. Lowassa anaondoka eneo la tukio huku akipeana mkono na waumini. 

BONDIA ALBERT MENSAH KUWA NA WAKATI MGUMI ULINGONI TAREHE 30, MACHI


FOR IMMEDIATE RELEASE – Friday, March 1st, 2013 -Dar-Es-Salaam, TANZANIA- Bondia wa IBF aliye na kiwango cha namba 11 duniani katika uzito Jr. Welter, Albert Mensah wa Ghana atakuwa kwenye wakati mgumu atakapombana na bondia mkongwe ulingoni na asiye na huruma na ngumi zake Mghana Ben Odamettey katika mpambano wao wa kugombea mkanda wa “IBF Africa uzito wa jr. Welter”.
Pambano hili linalowafanya Waghana wengi kuwa na roho juu juu kuhusu ni nani haswa mbabe kati ya wawili hao litafanyika jijini Accra, Ghana tarehe 30 Machi 2013 na linaandaliwa na kampuni kubwa ya kupromoti ngumi ya “GoldenMike Boxing Promotions Syndicate” inayomilikiwa na bwana Michael Tetteh andHenry Many-Spain.
Albert Mensah (kulia) akifanya anachokipenda sana  “Kuwaadhibu wapinzani wake”

Huu ni wakati ambao Waghana wengi kutoka kila kona ya nchi waliokuwa wanaungojea na wawili hao hawajaacha kugeuza hata jiwe moja kwa namna wanavyojifua kwa mazoezi yao ya mpambano huu!

Albert Mensah, ni bondia mtulivu na anayetumia akili nyingi ulingoni ambaye mabondia wengi waliokutana naye wanakiri kuwa huwezi kujua anachokifikiri ukingoni na hata ni ngumi gani atairusha kwako na wakati gani. Ni bondia aliyepewa nafasi kubwa sana ya kuchukua umaarufu wa bondia bingwa wa zamani wa dunia wa Ghana Profesa Azumah Nelson.
Naye bondia mwenye madaha na majivuno mengi Ben Odamettey, huu ni wakati wa ukweli umewadia kwani atatakiwa kuwahakikishia wapenzi wake kuwa hana wasiwasi na mpambano huu na kwamba yuko tayari kukumbana na adui wake mkubwa ambaye ni “Hasira”
Wakati ambao Waghana wa kila umri na rika zote waliokuwa wanaungojea na hawatangoja zaidi ya tarehe 30 Machi, 2013.
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA

LOWASSA ATUA JIJINI MWANZA KUZINDUA VIKOBA KWA WAAKINA MAMA MKOANI MWANZA

Mh Waziri Mkuu mstahafu ambaye ni Mbunge wa Monduli Edward Lowasa akisalimiana na mmoja wa wawakilishi wa wazee wa Mwanza Ally Zagamba ikiwa ni sehemu ya makaribisho kwenye uwanja wa ndege wa jiji la Mwanza jana, ambapo leo anategemewa kufanya uzinduzi wa Vikoba Kanisa la Anglican Nyamanoro  pia siku ya leo inatambulika kimataifa kuwa ni Siku ya Maombezi ya Wanawake Duniani.  


Mh Waziri Mkuu mstahafu ambaye ni Mbunge wa Monduli Edward Lowasa akisalimiana na Kemylembe kwenye uwanja wa ndege wa jiji la Mwanza jana, ambapo leo anategemewa kufanya uzinduzi wa Vikoba Kanisa la Anglican Nyamanoro  pia siku ya leo inatambulika kimataifa kuwa ni Siku ya Maombezi ya Wanawake Duniani. 


Mh Waziri Mkuu mstahafu ambaye ni Mbunge wa Monduli Edward Lowasa akisalimiana kada wa CCM Bi. Flora Magabe kwenye makaribisho uwanja wa ndege wa jiji la Mwanza jana, ambapo leo anategemewa kufanya uzinduzi wa Vikoba Kanisa la Anglican Nyamanoro  pia siku ya leo inatambulika kimataifa kuwa ni Siku ya Maombezi ya Wanawake Duniani. 


Mh Waziri Mkuu mstahafu ambaye ni Mbunge wa Monduli Edward Lowasa akisalimiana na Kada namba moja wa CCM mkoani Mwanza Emmanuel Nzungu akiwa sehemu ya watu waliojitokeza kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa jiji la Mwanza jana, ambapo leo anategemewa kufanya uzinduzi wa Vikoba Kanisa la Anglican Nyamanoro  pia siku ya leo inatambulika kimataifa kuwa ni Siku ya Maombezi ya Wanawake Duniani.


Mh Waziri Mkuu mstahafu ambaye ni Mbunge wa Monduli Edward Lowasa akisalimiana na Mama Rugaco kwenye uwanja wa ndege wa jiji la Mwanza jana, ambapo leo anategemewa kufanya uzinduzi wa Vikoba Kanisa la Anglican Nyamanoro  pia siku ya leo inatambulika kimataifa kuwa ni Siku ya Maombezi ya Wanawake Duniani.


Mh Waziri Mkuu mstahafu ambaye ni Mbunge wa Monduli Edward Lowasa akisalimiana na MNEC wa jimbola Busega Mh. Chegeni katika makaribisho ya mapokezi uwanja wa ndege wa jiji la Mwanza jana, ambapo leo anategemewa kufanya uzinduzi wa Vikoba Kanisa la Anglican Nyamanoro  pia siku ya leo inatambulika kimataifa kuwa ni Siku ya Maombezi ya Wanawake Duniani.


Mh Waziri Mkuu mstahafu ambaye ni Mbunge wa Monduli Edward Lowasa akisalimiana na mdau mwingine wa Mwanza Mr. Eddo Masama ikiwa ni sehemu ya makaribisho ya mbunge huyo kwenye uwanja wa ndege wa jiji la Mwanza jana.


Mh Waziri Mkuu mstahafu ambaye ni Mbunge wa Monduli Edward Lowasa akisalimiana na mfanyabiashara wa Mwanza Mr. Eddo Masama ikiwa ni sehemu ya makaribisho ya mbunge huyo kwenye uwanja wa ndege wa jiji la Mwanza jana.


Msafara wa viongozi mbalimbali pamoja na wananchi kutoka uwanja wa ndege Mwanza kwa mapokezi ya Mh Waziri Mkuu mstahafu ambaye ni Mbunge wa Monduli Edward Lowasa , ambapo leo anategemewa kufanya uzinduzi wa Vikoba Kanisa la Anglican Nyamanoro , ulioandaliwa na wanawake  toka madhehebu ya kikristo jiji la Mwanza, pia siku ya leo inatambulika kimataifa kuwa ni Siku ya Maombezi ya Wanawake Duniani.


Msafara wa viongozi mbalimbali pamoja na wananchi kutoka uwanja wa ndege Mwanza kwa mapokezi ya Mh Waziri Mkuu mstahafu ambaye ni Mbunge wa Monduli Edward Lowasa , ambapo leo anategemewa kufanya uzinduzi wa Vikoba Kanisa la Anglican Nyamanoro , ulioandaliwa na wanawake  toka madhehebu ya kikristo jiji la Mwanza, pia siku ya leo inatambulika kimataifa kuwa ni Siku ya Maombezi ya Wanawake Duniani.


Makaribisho zaidi, shughuli ya uzinduzi wa Vikoba  inatarajiwa kuanza rasmi saa 2:00 asubuhi na kukamilika saa 6:00 mchana katika Kanisa la Anglican Nyamanoro Ilemela jijini Mwanza.

SONGI JIPYA LA CHID BENZ FT BARNABA - NAFURAHI

Ile ngoma iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kutoka kwa rapper Chidi Beenz akiwa na amemshirikisha mwanamuziki kutoka Tanzania House Of Talent (THT), Barnaba sasa imeachiwa rasmi.
 Sikiliza sasa

MICHUANO YA MPINGA CUP YAANZA RASMI LEO

Kanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Saalam Suleiman Kova akijiandaa kudaka mpira ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa michuano ya Mpinga Cup inayowahusisha waendesha pikipiki maarufu kama Bodabado inayoanza rasmi leo kwa muda wa wiki moja. Mpinga cup imedhaminiwa na  Airtel , Rotary Club, Mr price na Shoprite  ikiwa na lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikipiki na kupunguza ajali barabarani . akishuhudia kushoto ni  Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Seleman Kova akidaka mpira ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa michuano ya Mpinga Cup inayowahusisha waendesha pikipiki maarufu kama Bodabado inayoanza rasmi leo kwa muda wa wiki moja. Mpinga cup imedhaminiwa na  Airtel , Rotary Club, Mr price na Shoprite  ikiwa na lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikipiki na kupunguza ajali barabarani . akishuhudia kushoto ni  Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Seleman Kova akikagua timu wakati wa uzinduzi wa  michuano ya Mpinga Cup inayowahusisha waendesha pikipiki maarufu kama Bodabado inayoanza rasmi leo kwa muda wa wiki moja. Michuano hii imeanza rasmi kwa mechi kati ya Kawe Tiptop na Manzese anayefata pichani ni Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga


Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga akikagua timu kabla ya mechi kati ya  Kawe Tiptop na Manzese leo wakati wa uzinduzi wa michuano ya Mpinga Cup, anayefata pichani ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando

Kikosi cha timu ya Kawe Tiptop katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa mashindano ya mpinga Cup yaliyofanyika leo katika viwanja vya polisi oyesterbay , katikati pichani ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Seleman Kova akifatiwa na Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga

Kikosi cha timu ya Manzese  katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa mashindano ya mpinga Cup yaliyofanyika leo katika viwanja vya polisi oyesterbay , katikati pichani ni Kanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Saalam Suleiman Kova akifatiwa na Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga

Thursday, February 28, 2013

MWANZA DIGITALI RASMI IFIKAPO SAA 6 KAMILI USIKU WA LEO

Mtangazaji wa Passion Fm Philbert Kabago akizungumza katika kipindi maalum na Mkurugenzi Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Habbi Gunze (kushoto) pamoja na Innocent Mungi (Kulia) ambaye ni Meneja wa Mawasiliano wa mamlaka hiyo leo asubuhi wakati walipo fika kwenye kituo hicho kutoa taarifa zaidi kuhusiana na uzimwaji wa mitambo ya analogia na kuingia digitali, unaokusudiwa kufanyika leo usiku ifikapo saa 6:00.  
Kwamujibu wa Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya hiyo Habbi Gunze amesema kuwa maandalizi ya kuzima mitambo ya analojia ya Utangazaji wa televisheni kwa jiji la Mwanza na vitongoji vyake, yamekamilika kwa kuwashirikisha wadau wa sekta ya utangazaji hapa Mwanza ambapo mitambo hiyo itazimwa saa 6 kamili usiku wa leo tarehe 28 Februari 2013.

Elimu kwa umma kupitia mbinu mbalimbali kuhusu mchakato wa kuhamia katika teknolojia ya mfumo wa utangazaji wa digitali imekuwa ikitolewa kwa kiwango cha kuridhisha. Matangazo ya digitali yanawafikia watu asilimia zaidi ya 22% kati ya asilimia 24% ya wanaopata matangazo ya televisheni ya analojia. 
Mtangazaji wa Passion Fm Philbert Kabago (katikati) katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Habbi Gunze (kushoto) pamoja na Innocent Mungi (Kulia) ambaye ni Meneja wa Mawasiliano wa mamlaka hiyo leo asubuhi wakati walipo fika kwenye kituo hicho kutoa taarifa zaidi kuhusiana na uzimwaji wa mitambo ya analogia na kuingia digitali, unaokusudiwa kufanyika leo usiku ifikapo saa 6:00.  
Mamlaka ya Mawasiliano imeendelea kutoa agizo kwa watoa huduma za kusambaza ving'amuzi walioko Mwanza kuhakikisha kuwa kunakuwa na stoku ya kutosha ya ving'amuzi,  pia mamlaka hiyo imefanya ukaguzi katika jiji la Mwanza na kugunda kuwa kuna ving'amuzi vya kutosha huku vingine vikiwa njiani kuwasili madukani kwaajili ya kukidhi mahitaji ya wengi.
Mtangazaji wa Passion Fm Devota Soteli (katikati) katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Habbi Gunze (kushoto) pamoja na Innocent Mungi (Kulia) ambaye ni Meneja wa Mawasiliano wa mamlaka hiyo leo asubuhi wakati walipo fika kwenye kituo hicho kutoa taarifa zaidi kuhusiana na uzimwaji wa mitambo ya analogia na kuingia digitali, unaokusudiwa kufanyika leo usiku ifikapo saa 6:00.
Mamlaka hiyo imeshukuru kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa wadau wa sekta ya utangazaji na wananchi kwa ujumla katika kipindi cha uzimaji wa mitambo ya utangazaji wa televisheni ili kufanikisha zoezi la uzimaji wa mitambo ya utangazaji ya taknolojia ifikapo tarehe 28 Februari 2013.

ZAWADI ZA MASHINDANO YA MPINGA CUP ZATANGAZWA

Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga akionyesha moja ya jezi zitakazotumika katika michuano  ya mpinga cup itakayoanza leo jijini Dar es saalam chini ya udhamini wa Airtel, Rotary club, Mr.Price, Home Shopping Center  pamoja na Baraza la Taifa la Usalama BarabaraniZawadi za Mashindano ya Mping Cup zatangazwa
Kiongozi mkuu  maandalizi ya Mashindano ya Mpinga Cup ametangaza zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwa timu zitakazoshiriki katika michuano ya Mpinga Cup inayoshirikisha waendesha pikipiki maarufu kama bodabado wa jijini dar esa saalam yanayotegemea kufanyika leo katika viwanja vya Oysterbay police kwa muda wa wiki moja.

Akitangaza zawadi hizo ASP Emilian Kamwanda ambaye ni msaidizi Mwandamizi wa polisi na Kiongozi wa maandalizi ya michuano ya mpinga cup alisema” leo tunayo furaha kutangaza zawadi mbalimbali za washindi katika mashindano hayo ambayo yana lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikiki (bodaboda). Na zawadi hizi ziko kama ifuatavyo:-
Mshindi wa kwanza atapata Kombe, Pesa taslimu shilingi million moja, jezi  set moja, kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1, mshindi wa pili atapata pesa taslimu shilingi laki tano, jezi seti moja , kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1 na mshindi wa tatu atapata  pesa taslimu shilingi laki tatu, , kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1,
Aidha zawadi zitatolewa kwa Mchezaji bora na Goalkeeper bora ambapo  kila mmoja atapata  pesa taslimu shilingi laki moja,  vocha za kufanya manunuzi Mr Price zenye thamani ya Laki moja na kofia ngumu (helmet) 1

Timu tano zitakazoshindwa pia hazitaondoka hivihivi , zitazawadiwa kila moja mipra na kofia ngumu Helmet.

Mashindano ya Mpinga Cup yameandaliwa na Jeshi la polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani na kudhaminiwa na Airtel, Rotary club,Mr.Price, Home Shopping Center  pamoja na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ili kutoa elimu kwa waendesha pikipiki juu ya sheria mbalimbali za usalama , kuimarisha uelewa wao wa matumizi ya barabara kwa lengo la kuendelea kudhibiti  ajali za barabarani pamoja na elimu ya Polisi jamii.

Mashindano haya yanatarajiwa kutimua mbio kuanzia tarehe leo katika viwanja vya Polisi Oysterbey   kwa kushirikisha timu 8 za waendesha pikipiki. Mpinga Cup itaendelea katika mikoa ya Kipolisi ya Ilala na Temeke na hatimaye kutafuta mshindi wa mkoa wa Dsm.

CLOUDS FM YAIBUKA NA TUZO YA UBORA (SUPERBRANDS) KWA MARA YA TATU MFULULIZO.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk Mary Nagu (kati) pamoja na Mkurugenzi wa Mradi wa Superbrands Afrika Mashariki, Bw Jawad Jaffer kwa pamoja wakimkabidhi cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga kwa Couds Fm redio kuibuka na tuzo hiyo ya ubora kwa mara ya tatu mfululizo. Tukio hilo lilifanyika hivi karibuni katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Mradi Superbrands Afrika Mashariki, Bw Jawad Jaffer akimkabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Bwa. Joseph Kusaga mara baada ya Clouds Fm Radio kuibuka na tuzo hiyo ya Superbrand kwa mara ya tatu mfululizo. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Wednesday, February 27, 2013

MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI WENGINE WAWILI WASAKWA KWA UCHOCHEZI WA VURUGU ZA KIDINI

Kamanda Ernest Mangu akitoa taarifa kwa waandishi wa habari.
Jeshi la polisi mkoani Mwanza linamshikilia mtu mmoja na kuwasaka wengine wawili wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya kueneza na kuchochea vurugu za kidini.


Akizungumza na vyombo vya habari leo katika ukumbi wa mikutano wa jeshi la polisi mkoani Mwanza Kamanda  Ernest Mangu, amemtaja mtu huyo anayeshikiliwa kuwa ni Imam Hamza.

Watuhumiwa wengine wanaosakwa ni pamoja na Shekhe Ilunga Hassan Kapunga, ambaye yuko nchini India akipatiwa matibabu pamoja na Askofu Agustino Mpemba wa kanisa la Tanzania Field Evangelist ambaye vilevile ni Mkurugenzi wa kituo cha redio Kwaneema Fm cha jijini Mwanza ambaye anatajwa kuwa kwa sasa yupo jijini Dar es salaam. Bofya play kumsikiliza Kamanda.Baadhi ya CD zinazotajwa kuwa mali ya watuhumiwa hao wa makosa ya uchochezi wa kidini.
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunakuja kufuatia vurugu zilizotokea Zanzibar na Geita ambapo jeshi hilo liliamua kufanya operesheni maalum kuwasaka watu wanaoeneza uchochezi wa vurugu za kidini. 

Mtuhumiwa Imam Hamza ambaye amekwisha kamatwa na tayari mapema leo amefikishwa mahakamani mkoani  Mwanza anatuhumiwa kuandaa CD inayoitwa 'NDEGE WOTE WALIE AKILIA BUNDI UCHURO' ambapo ndani yake imetajwa kuwa na maudhui ya Uchochezi wa vurugu. 
Kamanda Ernest Mangu akitoa taarifa.
Mwingine ni Shekhe Ilunga Hassan Kapunga anayetuhumiwa kuandaa CD zenye maudhui ya Uchochezi ya kwanza ikiwa na jina la Mauaji ya kinyama ya Shekhe Aboud Rogo wa Mombasa ambayo ameipa jina la 'UNAFIKI KATIKA SENSA' ya pili 'KADHIA YA MUUNGANO WATANGANYIKA NA ZANZIBAR' na ya tatu ameipa jina la 'UADUI WA MAKAFIRI'.

Shekhe Ilunga kwa sasa anatajwa kuwa yuko nchini India ambapo jeshi la polisi nchini kupitia interpol inafanya juhudi ya kumkamata na kumrejesha nchini apate kujibu mashitaka.

Mtuhumiwa wa tatu Askofu Agustino Mpemba wa kanisa la Tanzania Field Evangelist ambaye vilevile ni Mkurugenzi wa kituo cha redio Kwaneema Fm cha jijini Mwanza yeye anatuhumiwa kusambaza CD yenye jina 'INUKA CHINJA ULE' inayotajwa kuwa na maudhui ya kuchochea vurugu huyu anatajwa kuwa kwa sasa yupo jijini Dar es salaam.