ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 9, 2017

DIAMOND PLATNUMZ ft RICK ROSS - WAKA (Official Video)Hii ngoma unaweza kula diamond karanga ukashushia na chibu perfyum nishawaka niacheni tuu.

MCT WATOA TAMKO KUHUSU MWANDISHI ALIYEPOTEA.

Kufuatia kupotea kwa mwandishi wa Gazeti la Mwananchi, Azory Gwanda, Ambaye leo Desemba 9, 2017, ametimiza siku 18 tangu apoteee huko wilayani Kibiti mkoani Pwani, Baraza la Habari Tanzania (MTL), limetoa tamkoa la kulaani kitendo hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu mtendaji wa baraza hilo, Kajubi Mukajanga, amesema kuwa wamefanya mahojiano na mke pamoja na watu wa karibu na Azory, ambao kwa maelezo yao inaonekana mwandishi huyo yupo katika mikono salama.

“Ndugu Azory kwa asilimia kubwa kilichomfanya kupotea ni kazi zake, amekuwa akifanya kazi ya kuripoti matukio mbalimbali ya mauaji, tumejiridhisha kwamba ameshikiliwa na watu wasiojulikana kwa sababu ya kazi zake za uandishi, hasa ukizingatia mazingira ya Kibiti yalivyo” amesema Ndugu Mukajanga.

ASKOFU OSCA MNUNGU, WA KANISA LA ANGLIKANA DAYOSISI YA NEWALA,ANGOZA IBADA YA KIPAIMARA JIJINI MWANZA


TAREHE 09.12.2017
NA ZEPHANIA MANDIA WA G.SENGO TV
ASKOFU OSCA MNUNGU, WA KANISA LA ANGLIKANA DAYOSISI YA NEWALA,AMEWAPA KIPAIMARA WAKISTO ZAIDI YA 40 KATIKA KANISA LA ANGLIKANA TANZANIA,PARISHI YA AMANI NYAKATO DAYOSISI VICTORIA JIJINI MWANZA.

AIDHA ASKOFU MNUNGU, AMEONGOZA IBADA HIYO YA KIPAIMARA NAKUWAOMBA WAUMINI HAO KUWA NA HOFU YA MUNGU KUBADILI TABIA NAKUMPENDEZA.

KATIKA IBADA HIYO ALIAMBATANA MAASKO MBALIMBALI AKIWEMO ASKOFU MBELWA WA DAYOSISI YA KAGERA,MWENYEKITI WA KANISA LA ANGLIKANA TANZANZIA NAKUONGOZA IBADA ILIYO HUZURIWA NA MAMIA YA WAKRITO JIJINI HAPO.

ASKOFU MNUNGU AMEWAPONGEZA WAKRISTO WA KANISA HILO KWA JUHUDI NA MIPANGO MIZURI YA UJENZI WA KANISA NA KUHUDUMIA KANISA LA MUNGU.

MAGUFULI AWAACHIA HURU BABU SEYA NA MWANAE PAPI KOCHADecember 9, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ametangaza msamaha kwa Familia ya Babu Seya, msamaha huo ameutoa wakati wa Maadhimisho ya Miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania bara Mjini Dodoma wakati akihutubia.

Friday, December 8, 2017

VIDEO:- WASICHANA WALIOVISHANA PETE ZA UCHUMBA WAPANDISHWA MAHAKAMANI.Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limewafikisha  katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi mkoa  wa Mwanza washtakiwa  wanne wa makosa ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja pamoja na makosa ya kimtandao na kuwasomea mashtaka matatu.

Wakisomewa Mashtaka  hayo mahakamani hapo leo, mbele ya Hakimu  Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya  ya Nyamagana, Greyson Sumaye   kwa niaba ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu MkaziMkoa waMwanza, Wilbert Chuma, Wakili wa Serikali, Emmanueli Luvinga,aliieleza mahakama hiyo kuwa watuhumiwa hao wanakabiliwa na makosa matatu tofauti.

Alisema  Washtakiwa Milembe Suleiman(36) maarufu kwa jina la Kim The Don, Janeth Julius(25),  na Aneth William(24) wanadaiwa kufanya makosa yanayoashiria kufanya mapenzi ya jinsia  moja kinyume na  sheria   namba 138 A ya  kanuni ya adhabu sura ya 16  kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

“Mnamo mwezi Agosti, mwaka huu   washtakiwa  Milembe Suleiman  na Janeth Julius walitenda makosa  ya kugusanisha ndimi zao hadharani na kuvalishana pete  katika Hotel Pentagon makosa yanayoashiria kufanya mapenzi ya jinsia  moja huku Aneth William  akiwa mshereheshaji katika shughuli hiyo,” alisema Luvinga.

Alisema mshtakiwa Richard Fabian(28) maarufu kwa jina la Rich Mavoko  anakabiliwa na kosa la kuwapiga picha washtakiwa hao watatu na kuzisambaza katika mitandao ya kijamii kinyume na sheria ya makosa ya mitandao  ya mwaka 2015.

“Kati ya Agosti  na Septemba mwaka huu  mshtakiwa Fabian akiwa maeneo ya Buzuruga wilayani Nyamagana alisambaza picha za video za washtakiwa  Milembe Suleiman na Janeth Julius  wakinyonyana  mate hadharani na kuvalishana pete hadharani katika Hotel ya Pentagon,” alisema Luvinga.


Baada ya kusomewa mashtaka hayo watuhumiwa wote walikana mashtaka ambapo  Hakimu Sumaye  aliwaeleza  watuhumiwa hao hawezi kuwapatia dhamana kwa kuwa hakimu  aliyepaswa kusikiliza kesi  hiyo kuwa na shughuli nyingine  ila dhamana yao ipo wazi na kesi hiyo imeahirishwa mpaka Desemba 13, mwaka huu.