Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limewafikisha katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza washtakiwa wanne wa makosa ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja pamoja na makosa ya kimtandao na kuwasomea mashtaka matatu.
Wakisomewa Mashtaka
hayo mahakamani hapo leo, mbele ya Hakimu Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana, Greyson Sumaye kwa niaba ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa
Mahakama ya Hakimu MkaziMkoa waMwanza, Wilbert Chuma, Wakili wa Serikali,
Emmanueli Luvinga,aliieleza mahakama hiyo kuwa watuhumiwa hao wanakabiliwa na
makosa matatu tofauti.
Alisema Washtakiwa
Milembe Suleiman(36) maarufu kwa jina la Kim The Don, Janeth Julius(25), na Aneth William(24) wanadaiwa kufanya makosa
yanayoashiria kufanya mapenzi ya jinsia
moja kinyume na sheria namba 138 A ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
“Mnamo mwezi Agosti, mwaka huu washtakiwa
Milembe Suleiman na Janeth Julius
walitenda makosa ya kugusanisha ndimi
zao hadharani na kuvalishana pete katika
Hotel Pentagon makosa yanayoashiria kufanya mapenzi ya jinsia moja huku Aneth William akiwa mshereheshaji katika shughuli hiyo,”
alisema Luvinga.
Alisema mshtakiwa Richard Fabian(28) maarufu kwa jina la
Rich Mavoko anakabiliwa na kosa la
kuwapiga picha washtakiwa hao watatu na kuzisambaza katika mitandao ya kijamii
kinyume na sheria ya makosa ya mitandao
ya mwaka 2015.
“Kati ya Agosti na
Septemba mwaka huu mshtakiwa Fabian akiwa
maeneo ya Buzuruga wilayani Nyamagana alisambaza picha za video za washtakiwa Milembe Suleiman na Janeth Julius wakinyonyana
mate hadharani na kuvalishana pete hadharani katika Hotel ya Pentagon,”
alisema Luvinga.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo watuhumiwa wote walikana
mashtaka ambapo Hakimu Sumaye aliwaeleza
watuhumiwa hao hawezi kuwapatia dhamana kwa kuwa hakimu aliyepaswa kusikiliza kesi hiyo kuwa na shughuli nyingine ila dhamana yao ipo wazi na kesi hiyo
imeahirishwa mpaka Desemba 13, mwaka huu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.