ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 13, 2023

NACHINGWEA IMEPOKEA MIL.931 KWA AJILI YA MRADI WA BOOST

 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea akiwa kwenye moja ya majukumu ya kutoa elimu kwa wanachi namna gani ya kuunga mkono miradi inayoletwa na serikali kwenye maeneo 


Na Fredy Mgunda,Nachingwea.


HALMASHAURI ya wilaya ya Nachingwea imepokea kiasi cha shilingi millioni 931,500,000 kutoka serikali kuu kwa ajili ya Mradi wa kuboresha upatikanaji wa fursa sawa katika ujifuzanji bora wa elimu ya awali na msingi Tanzania bara (BOOST)

Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda Kawawa alisema kuwa wamepokea fedha kiasi cha shilingi millioni 931,500,00 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa,vyoo na nyumba za walimu.

Kawawa alisema kuwa fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa shule ya msingi mpya moja ya Kiegei, nyumba ya 2 in 1 moja katika kata ya Kiegei,ujenzi wa matundu matatu ya vyoo shule ya chimbendenga,shule ya msingi Kaloleni matundu matatu ya vyoo, Mchangani, Namatula,Namkula,Ntila na Tunduru ya Leo wote watajengewa matundu matatu vya vyoo kwa kila shule.

Alisema kuwa kutakuwa na ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Chimbendenga madarasa 6, Kaloleni madarasa 2, Mchangani madarasa 2, Ntila madarasa 2,Namkula madarasa 3, Tunduru ya Leo madarasa 2 na ujenzi wa madarasa ya mfano elimu ya awali katika shule ya msingi Chiwindi.

Aidha mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda Kawawa aliwaomba wananchi kujitokeza kujitolea nguvu kazi ili kuisaidia kumaliza mradi kwa wakati na ubora unaotakiwa.

Mhandisi Chionda Kawawa aliishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoka fedha katika Halmashauri hiyo kuboresha sekta ya elimu.

Friday, May 12, 2023

MRADI WA KUENDELEZA KILIMO NA UVUVI KUTATUA CHANGAMOTO ZA UFUGAJI VIUMBEMAJI CHATO.

 

Kulia Mratibu wa Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bw. Salim Mwinjaka, akizungumza wakati wa ujumbe huo ulipotembelea Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, ujumbe huo upo katika ziara maalum ya ukaguzi wa maeneo yanayotekeleza program hiyo ya AFDP.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Profesa Godius Kahyarara akizungumza na ujumbe na wataalam kutoka Program ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) haupo katika picha ulipotembelea ofisini kwake jana jioni. ujumbe huo upo katika ziara maalum ya ukaguzi wa maeneo yanayotekeleza program hiyo ya AFDP.


Kushoto Bi Jackline Motcho, Afisa wa Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi nchini (AFDP) akizungumza na baadhi ya wajumbe waliokuwepo katika ziara ya ukaguzi wa maeneo yanayotekeleza mradi huo katika kijiji cha Rubambagwe Wilayani Chato, Mkoani Geita.
Bi. SIFA Bujune, ni mfugaji wa viumbemaji katika kijiji cha Rubambagwe kilichopo Wilayani Chato, Mkoani Geita, akizungumzia baadhi ya changamoto wanazokutana nazo katika majukumu yao. 
Picha ikionesha moja ya jengo lililojengwa katika kijiji cha Rubambagwe  na Mradi wa kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) litakalo tumika wakati wa kutoa mafunzo kwa wafugaji wa viumbemaji 


Na; Mwandishi wetu - CHATO

Imeelezwa kuwa Mradi wa kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) unakwenda kutatua changamoto wanazokumbana nazo wafugaji VIUMBEMAJI katika kituo Cha Rubambagwe kilichopo Wilayani Chato,mkoani Geita.

 Hayo yameelezwa Leo na Dkt. Nazaeli Madala, Mkurugenzi wa ukuzaji viumbe Maji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Dkt. amesema kituo Cha Rubambagwe kipo katika UJENZI ambapo, Nia na madhuni ya kituo hiki ni kuhamasisha, kuendeleza na kusimamia ukuzaji viumbe Maji,Kwa maana Ufugaji wa samaki kwa mabwawa na vizimba katika ukanda wa ziwa Victoria.

Alisema kuwa, kituo kitakwenda kutoa mafunzo ya utengenezaji wa chakula cha samaki,Ufugaji na ulishaji sahihi wa samaki, wafugaji watafundishwa pia namna ya kutengeneza chakula Cha samaki Kwa kutumia malighafi za asili, kutakuwa na majengo ambayo yatawezesha wafugaji wanaotoka mbali kukaa hapo wakati wa mafunzo, sambamba na hilo, kutakuwa na kiwanda kidogo Cha kutengeneza chakula cha samaki.

Aliongeza kusema kuwa kituo pia kitazalisha vifaranga vya samaki ili kuweza kutatua changamoto ambazo wafugaji wanakutana nazo "kutakuwa na kitotoleshi ambacho kitakuwa na uwezo mkubwa sana wa kuzalisha vifaranga ambavyo vitakwenda kuwezesha vitotoleshi vya sekta binafsi kupata wazazi "Alifafanua

Akiongea na ujumbe huo, Bi. Sifa Buguni  mmoja wa wafugaji wa samaki Rubambagwe Chato alibainisha changamoto kubwa mbili  walizokumbana nazo kabla ya mradi huu kukamilika kuwa ni pamoja na uhaba wa upatikanaji wa mbegu na chakula cha kulisha samaki.

Awali, ujumbe huu wa IFAD ulifika ofisini Kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Prof. Godius Kahyarara ambapo alisema ni wakati sasa kwa wakazi wa Mkoa wa Geita kujikita katika katika shughuli za kilimo na ufugaji wa viumbemaji na kwa uwekezaji wa uhakika kuweza kuwekeza katika sekta hizo kama wanavyowekeza katika sekta ya madini.

Ujumbe kutoka IFAD, wataalam na Mratibu wa Programu hiyo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bw. Salim  Mwinjaka wapo katika ziara ya ukaguzi wa maeneo yanayotekelezwa mradi huo.

KWA UNDANI JUU YA MVUA ZA EL NINO ZINAZOTARAJIWA KUNYESHA NCHINI.

 Hivi karibuni Mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania (TMA) ilitoa taarifa juu ya uwepo wa kutokea kwa mvua za El Nino kwa asilimia 60.

Lakini je mpaka mvua hizi za El Nino kunyesha kuna viashiria gani na je athari ni zipi zinazoweza kujitokeza? Kwa upande wa Kanda ya Ziwa Mvua hizi zinazoendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo nizile zipo ndani ya msimu ama? na zitaendelea ama kuisha baada ya muda gani? Ikiwa tunashuhudia matukio ya vifo vinavyotoka na maji elimu elekezi inawafikiaje wahusika ikiwa ni pamoja na Wavuvi, nakwa njia ipi naje kuna gharama yoyote ya namna ya kupata taarifa za hali ya hewa lakini kuna tafadhali zozote na umuhimu wa kufatilia taarifa hizi MENEJA MAMLAKA YA HALI YA HEWA KANDA YA ZIWA AGUSTINO NDUGANDA ANAELEZA ZAIDI

ChopLife SoundSystem & Mr Eazi - Wena (feat. Ami Faku) [Official Music Video]

 

Lyrics

Hayi wena Bugijimi izolo (No you were running away not so long ago) Bheka nou Sewu’yandazi today (But look, today you act like you know me) Umama wayendiyala Wathi mntanami Uzulumkele (My mom warned me and said I should be careful) Hayi wena Bugijimi izolo (No you were running away not so long ago) Bheka nou Sewu’yandazi today (But look, today you act like you know me) Umama wayendiyala Wathi mntanami Uzulumkele (My mom warned me and said I should be careful) Ngoba Wena uyaz Akekho Ofana nawe Apha elizweni (Because you should know there’s nobody else like you in this entire world) Wena uyaz Akekho Ofana nawe Apha elizweni (You should know there’s nobody else like you in this entire world) I just wanna know what’s on your mind Baby I have been loving you long time (no no) Right now I’m ready to kick it down Sendakhetha ukuthula Ndibaleke Phela awundazi kahle (I’ve decided to be silent and run away cause you clearly don’t know me) Sendakhetha ukuthula Ndibaleke Phela awundazi kahle (I’ve decided to be silent and run away cause you clearly don’t know me) Sendakhetha ukuthula (sendakhetha ukuthula) Ndibaleke (sendakhetha) Phela awundazi kahle (Phela awundazi kahle) (I’ve decided to be silent and run away cause you clearly don’t know me) Sendakhetha ukuthula (sendakhetha ukuthula) Ndibaleke (sendakhetha) Phela awundazi kahle (Phela awundazi kahle) (I’ve decided to be silent and run away cause you clearly don’t know me) Ngoba Wena uyaz Akekho Ofana nawe Apha elizweni (Because you should know there’s nobody else like you in this entire world) Wena uyaz Akekho Ofana nawe Apha elizweni (You should know there’s nobody else like you in this entire world) I just wanna know what’s on your mind Baby I have been loving you long time (no no) Right now I’m ready to kick it down Ready to kick it down

TANZIA :- MEMBE AFARIKI

 

#𝗥𝗶𝗣𝗕𝗲𝗻𝗮𝗿𝗱𝗠𝗲𝗺𝗯𝗲 

#TANZIA: Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe, amefariki dunia muda mfupi uliopita katika Hospitali ya Kairuki, Dar es Salaam.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa alipata changamoto ya kifua na kupelekwa alfajiri ya leo Hospitalini hapo na baadaye  akaaga dunia.
𝕭𝖜𝖆𝖓𝖆 𝖆𝖒𝖊𝖙𝖔𝖆 𝖓𝖆 𝕭𝖜𝖆𝖓𝖆 𝖆𝖒𝖊𝖙𝖜𝖆𝖆 𝖏𝖎𝖓𝖆 𝖑𝖆 𝕭𝖜𝖆𝖓𝖆 𝖑𝖎𝖇𝖆𝖗𝖎𝖐𝖎𝖜𝖊.
.
.
.
.
.
.
#𝗥𝗶𝗣


MBUNGE KOKA ATOA MIFUKO 100 YA SARUJI KUBORESHA SHULE YA SEKONDARI VISIGA.

 

Na Victor Masangu,Kibaha

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka katika katika kuunga juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuboresha sekta ya elimu amechangia mifuko 100 ya sarufi kwa lengo la kukarabati miundombinu chakavu ya madarasa Saba katika shule ya sekondari Visiga.


Koka ametoa ahadi ya kuchangia mifuko hiyo wakati wa halfa inayojulikana Kama Visiga day ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kuweka mikakati ya kujadili namna ya kuongeza kiwango cha ufaulu pamoja na kukutana na wazazi ili kujadili changamoto zilizopo ili zitafutiwe ufumbuzi.

Aidha Mbunge huyo pamoja na kuchangia mifuko hiyo ya saruji ameahidi kuchangia madawati 50 kwa lengo la kuweza kusaidia Wanafunzi kuondokana na changamoto ya kusoma kwa mlundikano.


"Kikubwa natambua elimu ndio kila kitu kwa hivyo nimesikiliza risala ya mwalimu mkuu na nimegundua kuna mahitaji ambayo yanatakiwa katika kukuza kiwango cha ufaulu kwa Wanafunzi na kuondokana na adha ya kusoma katika mazingira ambayo sio rafiki,"alisema Koka.

Kadhalika Mbunge huyo aliongeza lengo lake kubwa ni Kuhakikisha anashirikiana bega kwa bega na wazazi,walezi pamoja na walimu katika kuwalinda Wanafunzi katika kuwa na nidhani ya kusoma kwa bidiii ili kuondokana kabisa na kupata alama mbaya.

"Kunatakiwa walimu,walezi na wazazi kwa pamoja tushirikiane katika kuwasaidia Wanafunzi wetu ili kutokomeza zero kabisa katika shule hii ya Visiga sekondari na kwamba anachukukizwa na shule za kata kuitwa kayumba,"alisema Koka.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Visiga Abasi Kikonyo katika risala yake amemshukuru Mbunge kwa sapoti yake ya kuisaidia shule hiyo pamoja na wadau wengine wa maendeleo wakiwemo wazazi sambamba na viongozi wa chama kwa kuchangia michango na vifaa vya ukarabati wa madarasa.


Naye Mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Mwajuma Nyamka amesema Mbunge huyo anatekeleza ilani ya chama kwa vitendo hivyo anastahili kuungwa mkono katika kuchochea maendeleo.


Nao baadhi ya Wanafunzi wa shule hiyo hawakusita kutoa pongezi zao za dhati katika kuona umuhimu mkubwa wa kusaidia ukarabati wa madarasa pamoja na kuchangia meza na viti ambavyo vitakuwa ni mkombozi mkubwa wa kusoma kwa mlundikano.

KOKA AJIPANGA KUWASAIDIA WANAFUNZI KUONDOKANA NA DIVISHENI ZERO.

 


Na Victor Masangu,Kibaha

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amewahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii na kuwa na nidhamu katika masomo ili kuongeza kiwango cha ufaulu na kuondokana kabisa  na changamoto ya kupata divisheni zero.

Koka ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanafunzi na walimu wa shule ya sekondari Visiga iliyopo katika halmashauri ya mji Kibaha wakati wa sherehe maalumu ya kuwakutanisha wadau wa elimu wakiwemo wazazi na walezi ijulikanayo Kama Visiga day.

Mbunge huyo alibainisha kwamba anachukizwa sana na baadhi ya watu kuziita shule za kata majina mabaya yasiyofaa kabisa wakati serikali inatenga kiasi kikubwa kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu hivyo kunahitajika juhudi za makusudi ili wanafunzi wafanye vizuri katika masomo yao.

"Kimsingi ndugu zangu Mimi Kama Mbunge wenu wa Jimbo la Kibaha mjini uwa nachukizwa sana shule zetu za kata kuitwa majina ya kayumba hii sio sawa kabisa kwa sababu uwezo wa kuwafanya wanafunzi wetu wafanye vizuri tunao na kuondokana kabisa na kupata alama ya divisheni zero kukibwa ni kuongeza juhudi,"alisema Koka.

Aidha aliwataka walimu na wazazi kuweka maazimio ya pamoja katika kuweka mikakati madhubuti ambayo itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kutokomeza kabisa divisheni zero kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Visiga pamoja na shule nyingine za kata zilizopo katika Jimbo lake.

Alifafanua kwamba katika kulifanikisha hilo ataendelea kutoa michango yake ya hali na mali ikiwemo kusaidia viti na meza pamoja na kuboresha miundombinu ya vyumba vya madarasa lengo ikiwa ni wanafunzi waweze kusoma katika mazingira rafiki.

Pia alisema kuwa ana Imani kubwa endapo wazazi,walezi pamoja na walimu wakishirikiana kwa pamoja wataweza kuwasaidia Wanafunzi hao kufanya vizuri katika masomo yao na kuondokana kabisa na kupata alama mbaya.

Abasi Kikonyo ambaye ni mkuu wa shule ya visiga alisema kwa sasa shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo uchakavu wa madarasa pamoja na mahitaji mengine ambayo yakifanyiwa kazi yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kiwango cha ufaulu.

Nao baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo ya Visiga waliahidi kuyafanyia kazi yale yote ambayo wameekekezwa kuyafanya na Mbunge huyo wa Jimbo la Kibaha mjini ili waondokane kabisa na kupata alama ya divisheni zero.

Thursday, May 11, 2023

CMC AUTOMOBILES SAO HILL FOREST RALLY OF IRINGA KUFANYIKA TAREHE 13/5/2023 HADI 14/5/2023

 

Kaimu muhifadhi mkuu wa shamba la miti Saohill PCO Tebby Yoramu akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mashindano ya mbio za magari zitakazofanyika Misitu ya asili Saohill.Mmoja ya magari ambayo yatashiriki Mashindano ya mbio za magari yatayofanyika Iringa yenye jina la CMC Automobile Saohill Forest Rally of Iringa yanatarajiwa kuanza tarehe 13na 15 mwezi wa tano katika Misitu ya asili Saohill .Mmoja ya magari ambayo yatashiriki Mashindano ya mbio za magari yatayofanyika Iringa yenye jina la CMC Automobile Saohill Forest Rally of Iringa yanatarajiwa kuanza tarehe 13na 15 mwezi wa tano katika Misitu ya asili Saohill .




Na Fredy Mgunda,Iringa.

 Mashindano ya mbio za magari yanayofahamika kwa jina la CMC Automobile Saohill Forest Rally of Iringa yanatarajiwa kuanza tarehe 13 mwezi wa tano katika Misitu ya asili Saohill .


Kwa mujibu wa Robert Maneno muandaaji mkuu wa mashindano hayo amesema kuwa wamedhamiria kufanya mashindano ya mbio za magari tarehe 14  mwezi wa Tano yanayohusisha washiriki kutoka Tanzania na nje ya Tanzania ikiwa ni pamoja na washiriki kutoka Tanzania ,Kenya ,Uganda na Zambia .

" Tarehe 13 kutakuwa na maonyesho pale uwanja wa Samora alafu tarehe 14 itakuwa ni kilele hapa katika shamba la Saohill na mashindano yamekamilika tunashukuru pia kwa muhifadhi kwa kufanya maandalizi mpaka saa hizi Kuna gari 12 na washiriki kadhaa mwingine kutoka Tanzania wengine kutoka nchi za jirani Kama Zambia,Kenya na mwingine kutoka Uganda na wameanza safari Yao kuja hapa Iringa na Kuna gari ambao nafikiri tunategemea italeta vionjo japo zote zitaleta vionjo Ila gari itakayokuwa Kali ni Fordfiesta R5 ambao itatumiwa na mtu kutoka Uganda " .

Alisema kuwa katika maandalizi ya mashindano hayo wanatarajia tarehe 13 kufanya maonyesho ya magari katika viwanja vya Samora huku kukiwa na magari yenye viwango vikubwa kulinganisha na mashindano yaliyopita .

Amjad Khan ni mwenyekiti wa mashindano ya mbio za magari zitakazofanyika Misitu ya Saohill alisema kuwa pamoja na mashindano hyao kufanyika wanatarajia kupokea ugeni mkubwa huku aliwataka washiriki kutumia vizuri sheria watakazopatiwa n mamlaka ya Misitu .

"Mpaka Sasa tumefikia asilimia 90 safari hii tunategemea kupata ugeni mkubwa Sana wanakujaniwa sababu sio mashindano tuu Bali wankauja kuangalia pia mashindano katika shamba kwa hiyo hiyo siku itatujengea jina kubwa tunashukuru kwa watu wa Saohill kwa kutupokea mashabiki wa gari karibuni Sana haya ni tofauti na Yale tuliyokuwa tukifanya zamani kikubwa tuzingatie sheria tutakazopewa ikiwemo sigara hapa marufuku mazingira tuache yakiwa safi ".

Naye PCO Tebby Yoramu Kaimu muhifadhi mkuu wa shamba la miti Saohill alisema kuwa mashindano hayo yatakuwa fursa ya kuonyesha utalii uliopo ndani ya shamba la miti Saohill ikiwa ni pamoja na utalii wa nyuki , uvuvi na maporomoko yaliyopo ndani ya Hifadhi ya shamba Hilo .

Alisema pamoja na kuwepo kwa mashindano hayo bado ni fursa kwa waandaji wa mashindano baiskeli ,mashindano ya riadha kwani Kuna kilomita nyingi zinazotoa fursa za ufanyikaji wa mashindano hayo .

"Tunashukuru na kufirahi kwa kuona Saohill inafaa kwa mashindano ya mbio za.magari hii ni fursa za vivutio kwa ajili ya utalii wa tiolojia kwa sababu ukitaka kuangalia hapa tunavyanzo vya utalii vingi ikiwamo tunamizinga ya nyuki ,Manzuki , na hapa Kuna uoto wa miti ya kupandwa ,wanyama pia mimea ,pia itakuwa chanzo Cha utalii kwa sababu Kuna maporomoko ya maji ,bwawa la ngwazi,uvuvi wa kurejesha pia utalii wa makasia na mashindano haya huenda yakafungua pia fursa ya mashindano mengine Kama mashindano ya baiskeli, marathon".

Shamba la miti Saohill sio tuu kwa ajili ya mashindano ya mbio za magari pia utalii wa uoto wa asili na usio wa asili ,utalii wa bwawa la ngwazi ,Uvuvi wa kurejesha ,utalii wa makasia na mto Ruaha huku ikiwa na fursa kwa wawekezaji wengine.

BENKI YA CRDB YAZINDUA MIKOPO MAALUM YA HAJJ NA UMRAH ISIYO NA DHAMANA KUSAIDIA MAHUJAJI KUTEKELEZA IBADA ZA HIJA NA UMRAH

 

Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Mikopo ya kuwawezesha mahujaji kwenda kwenye ibada za "Hajj na Umrah" ya Benki ya CRDB kupitia CRDB Al Barakah Banking, uliofanyika leo kwenye Makao Makuu ya Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam leo. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul (wapili kushoto), Mjumbe wa Baraza la Ulamaa na Naibu Kadhi, Sheikh Ally Hamis Ngeruko (wakwanza kushoto), na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha CRDB Al Barakah Banking, Muhsini Said (kulia).
 
Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Mikopo ya kuwawezesha mahujaji kwenda kwenye ibada za "Hajj na Umrah" ya Benki ya CRDB kupitia CRDB Al Barakah Banking, uliofanyika leo kwenye Makao Makuu ya Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam. Kulia ni Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally pamoja naye ni Mjumbe wa Baraza la Ulamaa na Naibu Kadhi, Sheikh Ally Hamis Ngeruko.
 
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha CRDB Al Barakah Banking, Muhsini Said (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Mikopo ya kuwawezesha mahujaji kwenda kwenye ibada za "Hajj na Umrah" ya Benki ya CRDB kupitia CRDB Al Barakah Banking, uliofanyika leo.

========    ========    ========

Dar es Salaam, 10 Mei 2023 - Dar es Salaam, Tanzania – Katika jitihada zake za kupanua wigo wa kuwahudumia wateja Benki ya CRDB leo imezindua mikopo maalum ya Hija na Umrah, ambao unalenga katika kuwawezesha waislamu kufikia malengo yao ya kufanya kwa gharama nafuu.

Mikopo hiyo ya Hija na Umrah imekuja kama suluhisho kwa waumini wa dini ya kiislam ambao wanataka kufanya safari ya hija lakini wanakabiliwa na changamoto za kifedha. Kupitia mikopo hiyo, Benki ya CRDB inatoa suluhisho rahisi na nafuu, ambayo inawawezesha wateja kulipia gharama zao za usafiri na malazi.

Uzinduzi wa bidhaa hii mpya umekuja wakati mwafaka  ambapo Waislamu kutoka sehemu mbalimbali duniani wanajiandaa kutekeleza wajibu wao wa kuhiji. Mwaka huu, Tanzania ina nafasi ya kupata hadi mahujaji 3,000, lakini wengi wao hawana fedha za kutosha kufadhili safari yao.

"Tunafurahi kuja na ubunifu huu wa mikopo Hajj na Umrah kama nyongeza kwenye bidhaa zetu za CRDB Al Barakah Banking. Mikopo hii inathibitisha dhamira yetu ya kutoa ufadhili nafuu za ufadhili kwa wateja wetu wote, hasa wale wanaotaka kutekeleza ibada ya Hijja na Umrah," alisema Bonaventura Paul.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha CRDB Al Barakah Banking, Muhsin Said alisema mikopo hiyo ya Hajj na Umrah inatolewa kwa masharti nafuu kwani haihitaji dhamana yoyote, hivyo kutoa fursa kwa Waislamu wote nchini kunufaika.

“Mikopo hii inatolewa hadi shilingi milioni 30. Kwa wateja wafanyakazi Benki inafanya uwezeshaji wa hadi asilimia 80 ya gharama zote za safari na kwa wafanyabiashara na wajasiriamali Benki inatoa uwezeshaji wa hadi asilimia 50 ya gharama zote za safari,” alisema Muhsin.

Katika hafla hiyo ya uzinduzi, Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir, aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuanzisha mikopo hiyo ya ufadhili wa Hija na Umrah, huku akiwahamasisha Waislam kote nchini kutumia fursa hiyo kutimiza ibada za Hija na Umrah.

"Huu ni mpango mzuri sana kutoka Benki ya CRDB, na nawapongeza kwa kuja na ubunifu huu. Ninahimiza Waislamu wote wa Tanzania kutumia fursa hii," alisema Sheikh Abubakar Zubeir huku akiiomba Benki ya CRDB pia kuziwezesha taasisi za mahujaji nchini.

Uzinduzi wa mikopo ya ufadhili wa ibada za Hija na Umrah unasisitiza zaidi dhamira ya Benki ya CRDB katika kutoa masuluhisho ya kifedha ya kibunifu na jumuishi kwa wateja wote. Kupata huduma za mikopo hiyo, wateja wanatembelea tawi lolote la Benki ya CRDB.

Benki ya CRDB ilizindua huduma zake za “CRDB Bank Al Barakah,” mwaka 2021 ambapo hadi sasa tayari imevutia wateja zaidi ya wateja 30,000 ambao wamenufaika na huduma mbalimbali zinazotolewa zikiwemo akaunti na mikopo.

Ripoti ya Benki hiyo inaonyesha kuwa Benki ya CRDB kupitia Al Barakah Banking imetoa zaidi ya Shilingi bilioni 73 kwa wateja tangu kuanzishwa kwake, jambo linaloonyesha ongezeko la mahitaji ya huduma za kibenki zinazofuata msingi ya kiislamu nchini Tanzania.

BAISKELI ZA UMEME, PIKIPIKI ZITAZUIA UCHAFUZI WA MAZINGIRA NA PUNGUZA GHARAMA ZA USAFIRI

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein kushoto akifuatilia vijana hao wakiendelea na utengenezaji wa pikipiki zinazotumia umeme


Vijana wakiendelea na utengenezaji wa pikipiki za umeme kama wanavyoonekana katika Shule ya Ufundi Tanga School

Vijana wakiendelea na matengenezo ya pikipiki zinazotumia umeme

Matengenezo ya Pikipi za kutumia Umeme yakiendeleaMkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya mafunzo hayo

Na Mwandishi Wetu,Tanga


VIJANA wanaopata mafunzo ya kutengeneza na kuunda Pikipiki na Baiskeli zinazotumia umeme Jijini Tanga wamesema kwamba zitasaidia kuzuia uchafu wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini. Pia, ma dereva haswa bodaboda wataweza kujiongezea kipato kwa kupunguza gharama ya mafuta na usafiri


Mafunzo hayo yanaendeshwa na Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization(TOIO) na Robotech Labs chini ya ufadhili wa Shirika la Botnar Fondation ambao wamedhamiria kutoa ujuzi kwa vijana ili kuweza kuutumia na kuweza kujikwamua kiuchumi


Akizungumza wakati mafunzo hayo yakiendelea ,Mwanafunzi wa kidato cha Pili wa shule ya Sekondari Tanga Ufundi Saidi Kasim alisema mafunzo hayo yanawapa mwanga mzuri wa mbeleni kutokana na kwamba ujuzi wanaoupata utawasaidia kuweza kujiajiri


Alisema kutokana na kwamba mbinu mbalimbali ambazo wamekuwa wakifundishwa siku hadi siku ikiwemo jinsi ya kutenegenza pikipiki za umeme na baiskeli kutokana kwa mkufunzi wao na hivyo kuwa njia nzuri ya kuweza kukabiliana na soko la ajira hapa nchini.


Aidha alisema kutokana na kwamba hivi sasa zipo changamoto mbalimbali zinazotokana na uchafuzi wa mazingira na hivyo wakati Serikali ikichukua jitihada za kukabiliana nayo mradi huo utakuwa ni wa manufaa kutokana na kujibu tatizo hilo.


“Mafunzo haya na pikipiki za umeme na baiskeli tunayojifunza hapa ni jinsi zinavyotengenezwa na namna ya kuweka fremu zanje na kuweka waya hakika mradi huu utatusaidia sana “Alisema


“Lakini pia utatusaidia kujiajiri pindi tunapomaliza shule na kwenda nje tunaweza kuanzisha mradi wa kubadilisha pikipiki za kawaida na zikawa zinatumia umeme kutokana na kwamba sio jambo gumu”Alisema


Haya hivyo alitoa wito kwa vijana wengine Jijini Tanga kuchangamkia mafunzo hayo kutokana na umuhimu wake wa kuweza kuwaandaa kujiajiri baadae na hivyo kujikwamua kiuchumi wao na jamii zao


Naye kwa upande wake Peter Sanga ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili alisema mafunzo ambayo wamefundishwa kwenye mradi huo yamewawezesha kufahamu namna ya kuzibadilisha pikipiki za umeme na baiskeli kutoka zilivyokuwa awali zikitumia mafuta.


Hata hivyo alisema pia wamefundishwa namna ya kutengeneza pikipiki na baiskeli hizo kutumia umeme na hilo ni jambo muhimu kutokana na kwamba kipindi hiki uchafuzi wa mazingira umekuwa mkubwa sana.


“Kwa sababu ukifuatilia vyombo vingi vya usafiri vimekuwa vikitumia mafuta na yamekuwa ni chanzo cha kuchafua mazingira hivyo vyombo hivyo ni muhimu kwa lengo la kutunza mazingira”Alisema


Aliongeza kwamba mradi huo una umuhimu mkubwa katika kutunza mazingira kwa sababu vitakapokuwepo hata vyombo vinavyotumia mafuta vitapungua na hivyo kuwa moja ya kutunza mazingira.


Awali akizungumza Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein alisema kwamba wameanza fursa ya mafunzo hayo kuanzia May 5 -10 kuhusu pikipiki na baiskeli za umeme lengo wanataka vijana kutoka kata mbalimbali wachangamkie fursa ya kusoma jinsi ya kuviunga,kuvirekebisha na kutenegenza baiskeli na pikipiki za umeme.


Alisema somo hilo lina vipindi viwili awamu ya kwanza ni kuanzia asubuhi saa nne mpaka saa sita na pili kuanzia saa nane mpaka saa kumi mpaka sasa wamepata vijana zaidi ya 30 huku akitoa shukrani za dhati kwa Jiji la Tanga na Taasisi ya Fondation Botnar ambao wamewezesha kutoa mafunzo hayo kwa vijana mbalimbali.

Wednesday, May 10, 2023

MASHABIKI MWANZA WAUZUNGUMZIA USHINDI WA YANGA IKIITANDIKA MARUMO 2-0, SHABIKI WA SIMBA ATIA FORA

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Baada ya mchezo kumalizika Jembe Fm ikiwa kibanda umiza ikateta na mashabiki wa soka, kwenye mic Jacob Mlay wa Sports Ripoti ya Jembe Fm Mwanza. ............................................................................................ MAGOLI. Ni Aziz Ki, kiungo wa Yanga alianza kutupia bao la ufunguzi dakika ya 63 kwa shuti akiwa ndani ya 18. Pamoja na kuanguka Morrison hakukata tamaa baada ya kuchezewa faulo na kipa pamoja na beki wa Marumo alikomaa akiamka chapchap akapiga mahesabu kujua goli liko wapi bila kuangalia kwa macho na kupachika bao la pili dakika ya 90 ya mchezo mpira ukitamatika kwa wenyeji #Yanga Sc 2-0 #Marumo Gallants. Hii inamaanisha YANGA kwa hivi sasa imetanguliza mguu mmoja hatua ya fainali. #samiasuluhuhassan

Tuesday, May 9, 2023

VITA YA FISTON MAYELE VS RANGA CHIVAVIRO


 FISTON MAYELE VS RANGA CHIVAVIRO 🔥


Wakati Young Africans wakijiwinda kukabiliana na Marumo Gallants kwenye mchezo wa nusu fainali CAFCC, vita nyingine itakuwa ni ya kuwania kiatu cha dhahabu kati ya Fiston Kalala Mayele na Ranga Chivaviro

Mpaka sasa kila mmoja amefunga magoli matano katika michezo 8 kuanzia hatua ya makundi mpaka robo fainali... Nani kung'aa kwa Mkapa Jumatano hii?

Ranga vs Al Akhdar ⚽️⚽️
Ranga vs FC Saint Eloi Lupopo ⚽️⚽️
Ranga vs Pyramids ⚽️

Mayele vs AS Real Bamako ⚽️
Mayele vs AS Real Bamako ⚽️
Mayele vs US Monastir ⚽️
Mayele vs Rivers ⚽️⚽️

MBUNGE WAITARA ALIA TENA, AZIMIWA KIPAZA SAUTI, ATOKA KWA HASIRA BUNGENI

Shuhudia namna Mbunge wa #Tarime Vijijini Mwita Waitara alivyocharuka bungeni baada ya kutoridhishwa na jibu la Serikali juu ya lini wananchi wa vijiji vya Komerera, Nyamichere na Murwambe vinavyozunguka mgodi wa Barrick Gold watalipwa fidia zao kama ilivyo haidiwa. #bungenidodoma

Monday, May 8, 2023

SHAMBA BOY AWEKA HISTORIA KUPACHIKA MIMBA MABINTI WATATU WA TAJIRI WAKE

 


Shamba boy mmoja Mkenya ambaye jina lake limehifadhiwa, ameweka historia ya kuwapachika mimba mabinti watatu wa tajiri wake.

Warembo hao watatu wana wazazi wakali ambao kwa kawaida waliwafungia ndani ya nyumba na kuwanyima nafasi ya kutangamana na marafiki.

Dada watatu wanaripotiwa kupachikwa mimba na mwanaume mmoja ambaye ni shamba boy wao

Inasemekana kuwa dada hao watatu kwa kawaida waliwekewa vikwazo na wazazi wao ambao walikuwa wagumu sana kwao na pia kuwazuia kufanya urafiki

 Wakati mama wa dada hao watatu alipogundua ukweli, alizimia papo hapo na mfanyakazi huyo alitimuliwa

Inaripotiwa kwamba mfanyakazi huyo pekee ndiye aliyekuwa akitangamana nao.

Kama ilivyoelezwa kwenye chapisho hilo, shamba boy huyo alianza kujamiana na dada wote watatu bila wazazi wao ambao ni Wakristo wenye itikadi kali kujua.

Imeelezwa  kwamba mfanyakazi huyo alianza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mzaliwa wa pili na alikamatwa katika tendo hilo na dada yake mkubwa.

Wakati huo huo, ili kifungua mimba aweze kuweka siri hiyo, alimwomba shamba boy huyo kutosheleza kiu yake ya ngono.

Wakiwa wanarushana roho, mzaliwa wa tatu naye aliwafumania katika kitendo hicho na pia alidai hamu yake ya mapenzi ili kujiridhisha ikiwa hawataki awaambie wazazi wao wakali.

Matokeo ya uhusiano wao na mfanyakazi huyo yaligeuka kuwa ujauzito na wote watatu wamejifungua.

 Baada ya kusikia habari hizo, wazazi hao walipigwa na butwaa kutokana na jinsi mambo yalivyobadilika licha ya jitihada zote za kuwaepusha kutangamana na wanaume.

 Walipoulizwa ni nani aliyehusika na ujauzito huo, walimwaga mtama na kumtaja shamba boy huyo, habari ambazo zilimfanya mama yao kuanguka chini na kuzirai papo hapo.

Wazazi hao sasa wamekubali matokeo baada ya kupewa ushauri nasaha na kujilaumu kwa kuwa wakali sana kwa binti zao.

Shamba boy naye alipigwa kalamu lakini dada hao bado humtumia pesa na kumpenda kama baba wa binti zao wawili na mtoto wa kiume.

POLISI: HAKUNA MTOTO ALIYEFUFUKA, WAZAZI WALITAKA KUMUIBA.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa

"Hakuna mtoto aliyefufuka" ndiyo kauli aliyoitumia Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa kuelezea majibu ya uchunguzi wa tukio la mtoto, Mabirika Wilson (8) kudaiwa kufariki, kuzikwa kisha kuonekana akizurura kwenye majaruba yaliyoko kijiji cha Mwangika Wilaya ya Kwimba mkoani humo. 

Mtoto huyo ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Salong'we Wilaya ya Magu mkoani Mwanza alifariki Aprili 16 mwaka huu nyumbani kwao baada ya kuugua maradhi yanayodhaniwa kuwa ni homa na kuzikwa nyumbani kwao Aprili 17 mwaka huu.

Siku 13 baada ya maziko ya mtoto huyo, Jeshi la Polisi mkoani humo lilitoa taarifa ya kuibuka sintofahamu kuhusu kifo cha mtoto huyo kufuatia wazazi wa Mabirika, Wilson Bulabo (35) na Helena Robert (32) kudai kwamba mtoto aliyeokotwa ni wao jambo lililoibua taharuki na kuwalazimu polisi kufukua kaburi ili kuchukua sampuli kwa ajili ya kipimo cha Vinasaba (DNA).

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jumamosi Mei 5, 2023 Kamanda Mutafungwa amesema uchunguzi wa awali wa vinasaba uliofanyika kwa watu wanne wakiwemo wazazi, babu wa marehemu na mtoto aliyeokotwa umeonyesha wazazi hao wa marehemu Mabirika hawana Unasaba (uhusiano) na mtoto aliyeokotwa katika kijiji cha Mwangika bali wazazi hao walitaka kumuiba. 

"Uchunguzi wa Vinasaba tulioufanya kwa mtoto aliyeokotwa tumebaini siyo mtoto wa wazazi hao badala yake mtoto wao ni aliyefariki. Hivyo, tunawashikilia wazazi hao ambao walidanganya na kuzua taharuki kuwa mtoto aliyeokotwa ni wa kwao amefufuka tukikamilisha uchunguzi tutawafikisha Mahakamani kwa tuhuma za kuibua taharuki na kutaka kuiba mtoto," amesema Mutafungwa

Kuhusu mtoto aliyeokotwa, Mutafungwa amesema baada ya kumfanyia mahojiano chini ya usimamizi wa Ofisi ya Ustawi wa Jamii amejitambulisha kwa jina moja la Mussa (8) huku akiwaomba wazazi ambao mtoto wao amepotea kufika Kituo Kikuu cha Polisi mkoani humo kwa ajili ya kumtambua mtoto huyo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Salong'we, Geremanus Masala amewataka wakazi wa mkoa huo kuacha kuzusha taarifa za imani potofu na kishirikina kuwa mtu akifa anaweza kufufuka jambo linaloweza kuzua taharuki kwa Umma.

"Nitawafikishia ujumbe wakazi wa kijiji changu cha Salong'we kuachana na imani potofu, watambue kuwa mtoto huyu siyo aliyefariki na pia tunaenda kukemea imani potofu," amesema Masala

Mtoto huyo ambaye aliokotwa anaendelea kuwa chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi na Ofisi ya Ustawi wa Jamii mkoani Mwanza wakati akisubiria utambuzi wa wazazi ama ndugu zake kujitokeza.

AJIKATA UUME WAKE AKIDAI KUCHOSHWA NA UGONJWA.

  

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa.

Mkazi wa kijiji cha Kibitilwa kata ya Ilula Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, Marko Samwel (32) anatibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi baada ya kujikata na kuondoa kabisa uume wake kwa kutumia kisu.

Samwel anadaiwa kujifanyia kitendo hicho cha kikatili Mei 3 mwaka huu Saa 7 usiku kwa madai kuwa amechoka kuuguza maradhi yanayomsumbua (yamehifadhiwa) kwa zaidi ya miaka mitano.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema mwanaume huyo alijikata kwa kutumia kisu kisha kuziondoa kabisa sehemu zake za siri jambo lililosababisha apoteze damu nyingi na kukimbizwa Hospitali ya Wilaya ya Kwimba kabla yakupatiwa rufaa ya kwenda Bugando anakoendelea na matibabu.

"Amekata uume wake kwa kisu kikali kwa madai kwamba amechoka kuugua, akakimbizwa Hospitali ya wilaya ya Kwimba lakini hali yake ikazidi kuwa mbaya akakimbizwa Bugando,"

"Hali yake inaendelea vizuri na sisi tunaendelea kumsubiria apone kabisa arejee kwenye utimamu wake ili atueleze kwa nini amekata sehemu zake za siri baada ya hapo tutamfikisha Mahakamani," amesema Mutafungwa

Mutafungwa ameitaka jamii kuepuka kuchukua maamuzi yanayoweza kuwaathiri kimwili na kisaikolojia akitolea mfano tukio hilo na kuwataka wenye changamoto kuwahusisha ndugu, wanasaikolojia na viongozi walioko katika maeneo yao.

BENKI YA CRDB, CARE INTERNATIONAL KUWAINUA WANAWAKE KUPITIA PROGRAMU YA IMBEJU

 

Benki ya CRDB imesaini makubaliano ya kushirikiana na Shirika la Care International kuwawezesha wanawake kupata mafunzo ya namna bora ya uendeshaji wa biashara, usimamizi wa fedha na mitaji, pamoja na kuwapatia mitaji wezeshi ya kujikwamua kiuchumi kupitia program ya IMBEJU.

Akizungumza kwenye hafla ya kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa amesema taasisi hiyo inafurahia kuingia mkataba wa ushirikiano na shirika la Care International kwani utakwenda kuwezesha programu ya IMBEJU kuwafikia wanawake wajasiriamali wengi zaidi nchini.
Tully amesema lengo ya programu ya IMBEJU ni kuongeza ujumuishi wa kiuchumi nchini, hivyo ushirikiano na Care International utakwenda kusaidia kufikia lengp hilo kwani shirika hilo limekuwa likijihusisha na uwezeshaji wa vikundi vya kiuchumi kote nchini kwa takribani miongo mitatu.

Tully amewakaribisha wabia wengine wa maendeleo nchini kushirikiana katika programu hiyo ya IMBEJU ili kuweza kuleta matokeo chanya zaidi na kuwezesha makundi ya vijana na wanawake.
“Benki yetu na taasisi yetu ya CRDB Bank Foundation ina amini katika ubia kama msingi wa kutatua changamoto zilizopo katika jamii yetu. Niwashukuru Care International kwa utayari wao wakushirikiana nasi kupitia programu ya wanawake. Tunawakaribisha na wadau wengine waje tuunganishe nguvu,” amesema.

Aidha, aliishukuru Serikali kupitia Tume ya Taifa Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Tume ya TEHAMA (ICTC) kwa ushirikiano ambao wanautoa kupitia programu biashara changa bunifu za vijana. Hivi karibuni Benki ya CRDB ili tangaza matokeo ya programu shindani ya vijana ambapo vijana 706 waliwasilisha maombi huku 106 wakichaguliwa kushiriki mafunzo kabla ya kupewa mitaji wezeshi.

“Programu ya wanawake kupitia IMBEJU bado dirisha lipo wazi, na tumeendelea kuongeza nguvu kwa kushirikiana na Care International ili tuwafikie wengi zaidi. Nitoe rai kwa wanawake wanawake wajasiriamali kuchngamkia fursa hii ili kuboresha shughuli zao,” aliongezea Tully akitoa hamasa kwa wanawake.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Care International, Bi Prudence Masako amesema CRDB Bank Foundation ni mbia muhimu kwao kwani juhudi zao za kukabiliana na umasikini zitafanikiwa kutokana na uhakika wa fedha za uwezeshaji kupitia programu ya IMBEJU.

Mkurugenzi huyo amesema shirika la wa Care International lilianzishwa miaka 78 iliyopita lakini lina miaka 29 tangu liingie nchini na katika mkakati wake wa kusaidia jamii kupambana na umasikini linafanya kazi na vikundi zaidi ya 50 vyenye wanachama wasiopungua 600,000.

“Moja ya malengo makuu ya Care International ni kusaidia jitihada za kupunguza umasikini. Hivyo tuliposikia kuhusu programu ya IMBEJU tulifurahi kwani hii ni fursa ya kuwafikia watu wengi ambao wameachwa nyuma katika shughuli za kiuchumi. Vilevile tunaamini katika usawa, hakuna jamii imeendelea kama mwanamke hajaendelea,” amesema Prudence huku akiwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kushiriki programu ya IMBEJU.

Kunufaika na uwezeshaji kupitia programu ya IMBEJU wanawake wanatakiwa kuwa katika vikundi na kisha kuwasilishwa maombi kupitia tawi lolote la Benki ya CRDB nchini, au kupitia mfumo wa uwezeshaji wa vikundi wa Care International.
Vikundi vitatakiwa kusaini makubaliano ya kushiriki programu ya IMBEJU, na kisha kupatiwa mafunzo na Shirika la Care International au maafisa uweshaji wa CRDB Bank Foundation. Mitaji wezeshi inatolewa kwa mwanachama mmoja mmoja wa vikundi baada ya kuhitimu mafunzo.

Program ya IMBEJU ilizinduliwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Machi 12 mwaka huu na kufungua dirisha la ufadhili kwa biashara changa za vijana na wanawake wajasiriamali. Zaidi ya Shilingi 5 bilioni zimetengwa kwa ajili ya kuwawezesha vijana na wanawake kupata mtaji wezeshi wa kuendesha biashara zao kupitia programu hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa (kulia)  akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa ushirikiano katika ya taasisi hizo kupitia programu ya IMBEJU unaolenga kuwawezeshawanawake wajasiriamali wengi zaidi kote nchini kupitia mafunzo na mitaji wezeshi iliyofanyika mwishoni mwa wiki makao makuu ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam.Wengine pichani ni na Mkurugenzi Mkazi wa Care International, Prudence Masako (katikati), na Mkurugenzi wa Miradi Care International, Haika Mtui.




--