Shamba boy mmoja Mkenya ambaye jina lake limehifadhiwa, ameweka historia ya kuwapachika mimba mabinti watatu wa tajiri wake.
Warembo
hao watatu wana wazazi wakali ambao kwa kawaida waliwafungia ndani ya nyumba na
kuwanyima nafasi ya kutangamana na marafiki.
Dada
watatu wanaripotiwa kupachikwa mimba na mwanaume mmoja ambaye ni shamba boy wao
Inasemekana
kuwa dada hao watatu kwa kawaida waliwekewa vikwazo na wazazi wao ambao
walikuwa wagumu sana kwao na pia kuwazuia kufanya urafiki
Wakati mama wa dada hao watatu alipogundua
ukweli, alizimia papo hapo na mfanyakazi huyo alitimuliwa
Inaripotiwa
kwamba mfanyakazi huyo pekee ndiye aliyekuwa akitangamana nao.
Kama
ilivyoelezwa kwenye chapisho hilo, shamba boy huyo alianza kujamiana na dada
wote watatu bila wazazi wao ambao ni Wakristo wenye itikadi kali kujua.
Imeelezwa
kwamba mfanyakazi huyo alianza kuwa na
uhusiano wa kimapenzi na mzaliwa wa pili na alikamatwa katika tendo hilo na
dada yake mkubwa.
Wakati
huo huo, ili kifungua mimba aweze kuweka siri hiyo, alimwomba shamba boy huyo
kutosheleza kiu yake ya ngono.
Wakiwa
wanarushana roho, mzaliwa wa tatu naye aliwafumania katika kitendo hicho na pia
alidai hamu yake ya mapenzi ili kujiridhisha ikiwa hawataki awaambie wazazi wao
wakali.
Matokeo
ya uhusiano wao na mfanyakazi huyo yaligeuka kuwa ujauzito na wote watatu
wamejifungua.
Baada ya kusikia habari hizo, wazazi hao
walipigwa na butwaa kutokana na jinsi mambo yalivyobadilika licha ya jitihada
zote za kuwaepusha kutangamana na wanaume.
Walipoulizwa ni nani aliyehusika na ujauzito
huo, walimwaga mtama na kumtaja shamba boy huyo, habari ambazo zilimfanya mama
yao kuanguka chini na kuzirai papo hapo.
Wazazi
hao sasa wamekubali matokeo baada ya kupewa ushauri nasaha na kujilaumu kwa
kuwa wakali sana kwa binti zao.
Shamba
boy naye alipigwa kalamu lakini dada hao bado humtumia pesa na kumpenda kama
baba wa binti zao wawili na mtoto wa kiume.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.