ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 24, 2014

HUU NDO UKWELI KUHUSU USAJILI WA OKWI

CHANZO: Shaffih Dauda.

NJOO UPUNGUZE STRESS ZA WIKI NZIMA NA BURUDANI YA SKYLIGHT BAND NDANI YA THAI VILLAGE MASAKI LEO.

DSC_0010
Kikosi kazi cha Skylight Band kikiongozwa na Rappa Joniko Flower kikitoa burudani kwa mashabiki wao ndani ya kiwanja chao cha Thai Village, Masaki jijini Dar Ijumaa iliyopita. Kutoka kulia ni Winfrida Richard, Sam Mapenzi, Aneth Kushaba AK 47 pamoja na Digna Mbepera.
DSC_0061
Mashabiki wa Skylight Band mdogo mdogo wakijimuvuzisha kwa Dancing Floor.
DSC_0012
Am not a Gold Digger...Njagala Mukwano..... ni Winfrida Richard, Hashim Donode na Digna Mbepera wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band.
DSC_0048
Joshua Ndege akimwaga mifwedha kwa Mary Lucos.
DSC_0088
Digna Mbepera akikonga nyoyo za mashabiki wa Skylight Band.
DSC_0127
Tuwapo Skylight Band tunatupa shida chini tunaweka mikono juu......Mashabiki wakijiachia kwa raha zao.
DSC_0130
Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa wa Bongo akiwapagawisha mashabiki wa Skylight Band.
DSC_0134
Full kuchizika yani usipime itumie Ijumaa yako ya leo vizuriiiiii na Skylight Band.
DSC_0030
Aneth Kushaba AK74 na Mary Lucos wakifanya yao jukwaani.
DSC_0116
Shazi la mashabiki wa Skylight Band wakijimwaga kwenye dancing floor.
DSC_0050
Sam Mapenzi sambamba na Sony Masamba wakitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band.
DSC_0128
DSC_0153
Mheshimiwa Bundala Backstage na Digna Mbepera wa Skylight Band.
DSC_0152
Lubea wa Skylight Band na Ukodak
DSC_0149
Wadau Donny pamoja na Martin Tanrose wakishow love.
DSC_0148
Sisi Dugu moja.... Aba Billdard na Mdogo wake Cliff Seduu wakipata Ukodak.
DSC_0037
Backstage ya wasanii wa Skylight Band.

Thursday, January 23, 2014

MKUTANO MKUU WA NGUMI ZA KULIPWA

Ibrahim Kamwe akiwa na rais wa WBF Howard Goldsberg.
Ibrahim akiwa na maofisa wenzake,Sakwe Mtulia, Fidel Hynes na Lucas Msomba wakirekebisha jambo.
Emmanuel Saleh, Ibrahim Kamwe, Emmanuel Mlundwa.

HABARI KAMILI.

Siku ya terehe 1 ya mwezi wa pili katika ukumbi wa vijana hall kinondoni KUANZIA SAA TATU NA NUSU ,kutakuwepo na mkutano mkubwa wa wanamasumbwi wote ulioitishwa na orgnaizesheni ya ngumiza kulipwa Tanzania (TPBO) kwa lengo la kuwakutanisha mapromota wote,mabondia na makocha  wa ngumi wote kwa lengo la kujadili ngumi za kulipwa zinapoelekewa,kujuana na kuelimishana sheria za ngumi za kulipwa  zinavyotumika kinyume na sasa ,sheria nyingi zinafungiwa macho na kutumia uzoefu zaidi kuendesha mgumi nchini.  Mkutano huo ulioitishwa na Rais wa TPBO bw  Yasin Abdallah akishirikiana  na Ibrahim kamwe na Mapromota wa ngumi chini ya ufadhili wa kitwe Traders unatarajiwa  kuwa mkutano wa kwanza  kuwakutanisha mapromota wote pamoja na  mabondia wa ngumi  za kulipwa wa hapa nchini ili kuboresha ngumi na kuhamasisha wadhamini na makampuni wajitokeze kuudhamini mchezo huo ,ambao ndio mchezo unaoliletea mataji na  sifa Tanzania katika medani za kimataifa lakini hauna udhamini  wowote ,mpaka sasa ni mchezo  ambao unaojiendesha wenyewe kwa nguvu za  wadau wachache wachovu  na mabondia wenyewe ambao uwezo wao ni mdogo sana kukikidhi matakwa kamili ya mchezo wenyewekam ilivyo kwa wenzetu,ni mchezo  ambao una huduma nyingi zinazohitaji nguvu ya wadhamini ili  uendelee kuboreka zaidi.

Akizungumza na vyombo vya habari katibu wa ngumi za kulipwa nchini bw Ibrahim kamwe , amesema imewaalika viongozi wa baraza la michezo (BMT), na viongozi wengine wote wa ngumi za kulipwa watakuwepo kama vile Emmanuel mlundwa,names kavishe,  makaranga,Onesmo ngowi,kinyogoli, matumla, Zuwena kibena(mama zugo) na viongozi wadau wa karibu na ngumi wamealikwa kuhudhulia mkutano huo ambao utafanyika Siku ya terehe moja ya mwezi wa pili katika ukumbi wa vijana hall kinondoni. hivyo kamwe alimaliza kwa kuwaomba kila anaejijua kuwa yeye ni bondia wa ngumi za kulipwa na promota wangumi  ahudhurie bila kukosa mkutano huu muhimu sana kwa wamasumbwi ya nchi  yetu.

WAZIRI MKUU MSTAAFU SUMAYE ATEMBELEA CLOUDS MEDIA GROUP LEO

Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akimkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye alipowasili mapema leo kwenye makao makuu ya ofisi hizo zilizopo Mikocheni jijini Dar,pichani kati anaeshuhudia ni Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group,Simon Simalenga.
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye kwenye moja ya Ofisi za kampuni hiyo,alipofanya ziara fupi mjengoni humo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo zikiwemo  na urushaji wa matangazo ya redio na Televisheni kwa ujumla. pichani kati anaeshuhudia ni Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group,Simon Simalenga.
Mkuu wa Kitengo cha Habari Clouds FM,Joyce Shebe akitoa ufafanuzi mfupi  kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye alipotembelea kitengo hicho cha habari na kujionea uandaaji wa habari ya televisheni na redio unavyofanyika.
Mmoja wa Watangazaji kipindii cha Michezo Clouds FM,kiitwacho Sports Extra, Ibrahim Masoud a.k.a Maestro akifanya mahojiano mafupi na Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye kuhusiana ushabiki wake mkubwa kwa timu ya Simba sambamba na migogoro iliyoikumba club hiyo ya Msimbazi
Ruge Mutahaba akitoa ufafanu mfupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye,kuhusiana na Kifaa maalum na cha kisasa cha kurushia matangazo ya biashara,pichani nyuma ni Mkuu wa Kitengo cha Habari Clouds FM,Joyce Shebe akisikiliza.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye akiwa kwenye chumba cha kurekodia mahojiano mbalimbali,akiwa amekutana na wadau wa Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT),pichani kulia ni Afisa Masoko Mwandamizi wa UTT,Mfaume Kimario na Afisa Masoko na Uhusiano,Bwa.Rahim Mwanga
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye kuhusiana na urushaji wa matangazo kwa njia ya kisasa ndani ya studio kuu ya redio Clouds FM,Sumaye amefanya ziara fupi mjengoni humo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo zikiwemo  na urushaji wa matangazo ya redio na Televisheni kwa ujumla.
Ruge Mutahaba akimtambulisha Mkurugenzi mwanzake wa Maendeleo ya Biashara,Sheba Kussaga kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye
Mkuu wa Kitengo cha uzalishaji vipindi wa Clouds TV,Bwa Kanyopa akitoa ufafanuzi mfupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye namna ya kuandaa na kuhariri vipindi vya televisheni.
Ruhe Mutahaba akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye kuhusiana na mitambo ya kisasa ya kurushia matangazo ya televisheni na ubora wa picha za televisheni unaotoka kwenye mitambo hiyo ya kisasa. PICHA ZOTE NA MICHUZIJR WA MICHUZI MEDIA GROUP

MH. LOWASSA AMFARIJI MZEE MAKAMBA ALIEFIWA NA MAMA YAKE MZAZI

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM,Mzee Yusuph Makamba (wa pili kushoto) wakati alipokuwa akimtambulisha dada zake,wakati Mh Lowassa alipokwenda kumpa pole Mzee Makamba aliepatwa na msiba wa kufiwa na mama yake mzazi huko kijijini kwake Maezangula wilaya ya Korogwe,Mkoani Tanga jana.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (katikati) na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM,Mzee Yusuph Makamba wakimsikiliza Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia,Mh. January Makamba wakati wa mazungumzo yao.Mh Lowassa aliitembelea Familia ya Mzee Makamba kwa  kumpa pole kwa kupatwa na msiba wa kufiwa na mama yake mzazi huko kijijini kwake Maezangula wilaya ya Korogwe,Mkoani Tanga jana.

CHADEMA YAIONYA CCM.

Ruvuma/Songea/Tanga. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema kuwa chama hicho kitachukua uamuzi mgumu ikiwa wabunge wa CCM watajikita katika kulinda masilahi yao kwenye Bunge Maalumu la Katiba kinyume na maoni ya wananchi.

Alisema hayo jana katika Wilaya ya Nyasa na Mbinga kwenye siku ya kwanza ya Operesheni Pamoja Daima. Katika operesheni hiyo, ambapo aliruka kwa helikopta katika sehemu mbalimbali, alihutubia mikutano katika maeneo ya Mbamba Bay, Mbinga, Peramiho, Namtumbo na Songea Mjini.
Akiongozana na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Dk Slaa aliwaonya wabunge wa CCM kutotumia wingi wao bungeni kutetea masilahi ya chama chao. “Kamwe wasithubutu kwani Chadema itachukua uamuzi mgumu ambao kwa sasa si vizuri kuutaja,” alisema Slaa.
Alionya akisema ni lazima wabunge watoe maoni ambayo yana masilahi ya wananchi wote na siyo vyama.
Daftari la wapigakura
Katika hatua nyingine, alisema Chadema itasusia kura ya maoni iwapo daftari la wapiga kura halitaboreshwa kwa ajili ya mchakato wa Katiba.
Alisema kwa sasa chama hicho kinasambaza fomu maalumu nchi nzima kwa ajili ya watu wasio na vitambulisho vya kupiga kura wajiorodheshe.
“Kuna maelfu ya watu waliopoteza vitambulisho vyao vya kupigia kura na wengine wamefikia umri wa kupiga kura lakini Serikali haioni suala hilo kuwa ni muhimu,” alisema.
Alisema uchunguzi wa chama hicho umebaini watu zaidi ya 5,000,000 hawana vitambulisho vya kupigia kura japokuwa tayari wamefikia umri wa kupiga kura.
Ili kuhakikisha Bunge la Katiba linakuwa na manufaa, Dk Slaa aliwataka wananchi kufuatilia mjadala juu ya Katiba Mpya kwa makini ili kuwabaini wabunge wasioitakia nchi hii mema.
Alisema wabunge wa namna hiyo wamepanga kutengeneza Katiba ya viongozi badala ya katiba ya wananchi.
Baadaye katika mkutano uliofanyika katika Uwanja wa Matarawe mjini Songea mvua kubwa ilinyesha, lakini wananchi waliofurika hawakujali kunyeshewa badala yake walionyesha shauku ya kuendelea kumsikiliza Dk Slaa. 

Wednesday, January 22, 2014

AIRTEL ‘MIMI NI BINGWA’ YAZIDI KUWAPA WATANZANIA WENGI FARAJA

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mmbando (kulia) akisisitiza jambo wakati akiwatangaza washindi wa droo ya wiki ya tisa ya promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa iliyochezeshwa jana na kuwapata washindi wa pesa taslimu ya zaidi ya Shilingi milioni 22 na kumpata Edwin Edmund Kajimbo kutoka Iringa aliyejishindia tiketi mbili ya safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda kuangalia mechi ya ligi kuu ya Uingereza moja kwa moja ‘live’ kwenye uwanja wa Old Trafford. Kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania Mrisho Millao.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mmbando (kulia) akimpigia simu Bw. Edwin Edmund Kajimbo mkazi wa Iringa aliejishindia tiketi mbili ya safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda kuangalia mechi ya ligi kuu ya Uingereza moja kwa moja ‘live’ kwenye uwanja wa Old Trafford, katika droo ya tisa ya promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa. Wakati wa droo hiyo iliyochezeshwa jana, washindi 14 wa pesa taslimu ya zaidi ya Shilingi milioni 22 walipatikana. Kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania Mrisho Millao.
Airtel ‘Mimi ni Bingwa’ yazidi kuwapa watanzania wengi faraja
  • Yatoa zaidi ya shilingi milioni 194 kwa washindi
  • Tiketi 18 za kwenda Old Trafford zatolewa
Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya mawasiliano ya Airtel Tanzania imeendelea kuwapa faraja washindi wake wa promosheni ya ‘Mimi ni Bingwa’ kwa kuwazawadia zaidi ya pesa taslim shilingi milioni 194 na kutoa tiketi 18 za safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda Old Trafford nchini Uingereza.

Kampuni hiyo ya mawasiliano jana imetoa shilingi milioni 22 pesa taslim kwa washindi 14 na tiketi mbili za kwenda Old Trafford kuangalia mechi ya ligi kuu ya Uingereza moja kwa moja ‘live’, kwa mshindi mmoja wa kila wiki katika wiki ya tisa ya promosheni ya Mimi ni Bingwa iliyochezeshwa katika ofizi ya makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya droo, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema promosheni ya Mimi ni Bingwa imekuwa ikiwapa faraja watanzania wengi ambao wamekuwa wakionyesha furaha zao za ushindi wa pesa taslim au safari inayogharamiwa kila kitu ya kwenda Old Trafford.

“Tumekuwa tukipokea maoni kutoka kwa washindi wetu, hususani wale waliojishindia pesa taslim, wakisema pesa waliojishindia toka promosheni ya Mimi ni Bingwa wameipata wakati muafaka wakihitaji zaidi msaada wa kifedha.

“Wanasema miezi iliyochaguliwa kwa ajili ya promosheni na pesa walizopokea bila jasho kutoka Mimi ni Bingwa promosheni, zimeweza kuwaongezea uwezo wa kifedha ili kupambana na hali ngumu ya kiuchumi katika miezi hii migumu inayohitaji fedha nyingi. Tumekuwa tukituma milioni moja (1m/-) kwa washindi wetu mara tu baada ya kuwatangaza kupitia Airtel money na kuweka shilingi milioni tano (5m/-) katika akaunti za washindi baada ya kupata taarifa zao za benki,” alisema Mmbando.

Aliongeza kuwa promosheni hiyo ya Mimi ni Bingwa iliyoanza mwishoni mwa mwezi wa Novemba mwaka jana, imelenga kurudisha sehemu ya pato la kampuni kwa jamii inayoizunguka na kuwaunganisha mashabiki wa soka na michezo ya kimataifa.
Alimtangaza Edwin Edmund Kajimbo kutoka Iringa kuwa ni mshindi wa wiki hii wa tiketi mbili wa safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda kuangalia mechi za klabu ya Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford.

Bw. Kajimbo anakuwa ni mshindi wa tisa wa tiketi toka promosheni ilipoanza baada ya Michael Joseph Shirima kutoka Kinondoni jijini Dar es Salaam, Bw. Shaibu Rashid Dege, Mwenyekiti wa Kijiji cha  Nang’olo katika wilaya ya Kilwa - Mkoani Lindi, Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Joseph Steven Mambo kutoka Kawe jijini Dar es Salaam, Emmanuel Mahenge Jacob kutoka Njiro mkoani Arusha, Rashid Jacob Kagombola kutoka Bukoba mkoani Kagera, Harrison Wilson Mwambogolo kutoka Kigogo jijini Dar es Salaam na Salma Juma Mughery kutoka Dar es Salaam, waliojishindia tiketi katika droo za kila wiki zilizopita.

Mmbando pia aliwatangaza washindi wawili wa shilingi milioni 5 kila mmoja wa wiki kuwa ni Bw. Uruma Samwel Mkongwa kutoka Usa River mkoani Arusha na Filemon Nathaniel Mgaya kutoka Dar es Salaam pamoja na washindi wengine 10 waliojishindia shilingi milioni 1 kila mmoja.  

“Zaidi ya shilingi milioni 324 zilitengwa kama zawadi ya pesa taslim kwa ajili ya promosheni ya Airtel ya Mimi ni Bingwa, inayowapa fursa washiriki wa Mimi ni Bingwa kushinda kila siku na kila wiki,” alisema.

Mmbando alisema kuwa mwenendo wa washiriki wa Mimi ni Bingwa kuendelea kujikusanyia pointi unazidi kutoa amasa.

“Bado kuna zawadi nyingi zaidi kushindaniwa, ikiwa ni pamoja na zawadi kubwa ya shilingi milioni 50. Nawaasa wateja wa Airtel ambao bado hawajajisajili katika promosheni hii kuwa hawajachelewa; bado kuna zawadi nyingi zaidi kushindaniwa. Ili kuingia katika promosheni hii mteja anatakiwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neno “BNGWA” kwenda namba 15656, kwa kujibu maswali mengi iwezekanavyo, unaweza kuwa mshindi wa milioni 50 au zawadi nyinginezo nyingi,” alisema.

KITUKO MAHAKAMANI LEO: MAHABUSU MWANZA AJIPAKA KINYESI AKIJARIBU KUTOROKA.

Askari akiwa amemnasa mahabusu aliye kimbia mara baada ya kujipaka kinyesi katika mahabusu ya mahakama ya wilaya ya Nyamagana na Mahakama ya Mwanza.
 HUWA YANASIKIKA KUTOKEA LAKINI LEO NI LAIVU BILA CHENGA...... Mahabusu mmoja aliyekuwa mahabusu ya mahakama ya wilaya ya Nyamagana na Mahakama ya Mwanzo iliyopo eneo la jirani na Mamlaka ya maji safi na Hifadhi ya Mazingira (MWAUWASA) jijini Mwanza alitoa kioja cha mwaka kwa kujaribu kutoroka kwa kujipaka kinyesi ili asiguswe wala kukamatwa.

Mtuhumiwa huyo ambaye jina lake halikufahamika alijimwagia kinyesi kilichokuwa kwenye ndoo iliyokuwa ndani ya sero ya Mahakamani hapo na askari alipokwenda kufungua ili kuwapeleka watuhumiwa kwenye chumba cha Mahakama kusomewa kesi yake baada ya kutajwa na karani wa Mahakama ya mwanzo, baada ya kutajwa ndipo mahabusu huyo alipopata mwanya wa kukimbia na kutoa tahadhari kwa atakaye mgusa au kumshika atakumbana na kadhia ya kuchafuliwa kwa kupakwa kinyesi.

Askari mwingine mwenye cheo cha sajenti, ambaye alikuwa akihushughulika na huduma nyingine mahakamani hapo, kwa kuwa alikuwa na uzoefu wa kupambana na mikasa na vioja kama hivyo vya mahabusu wanao kula njama za kutaka kutoroka aliamua kula naye sahani moja kwa kumkimbiza na kufanikiwa kumkamata.
 Baada ya kumkamata na kumrejesha katika chumba cha mahabusu mahakamani hapo, kwanza mtuhumiwa huyo aliamriwa kuzoa mtondoro wa kinyesi cha binadamu alichokuwa amejimwagia na kutapakaa chini na mara baada ya kumaliza kuzoa uchafu huo, alipelekwa kwa hakimu ambapo alisomewa kosa la kula njama za kutoroka na kukumbana na adhabu nyingine ya kuhukumiwa kifungo cha miezi sita (6) jela, huku kesi yake iliyokuwa ikimkabili awali ikiahirishwa.
"Kama alivyojipaka ndivyo alivyo yazoa..."
Moja baada ya jingine.
Hatua kwa hatua chini ya ulinzi mkali wa askari shupavu.
Huku akiweka kinyesi hicho kwenye ndoo mahabusu huyo alilazimika kukizoa kwa mikono kama muuza mkaa apimavyo mkaa kwenye kopo kuwauzia wateja wake. 
Mchafuzi wa mazingira akiadabishwa kabla ya kwenda kusomewa kesi nyingine ya kula njama za kutaka kutoroka.
Hatari....

WIMBO UNAONIFARIJI SIKU ZOTE.

Ni wimbo wenye video iliyo chukuliwa katika mazingira ya kawaida kwenye location tofauti tofauti na kama ilivyo kawaida kwa Pharrell Williams naye ame-act na mavazi simple tu bila mingaro mingi kama wengine wafanyavyo.... Oh men this song make me Happy. Enjoy.

Tuesday, January 21, 2014

WAFANYAKAZI WA KAMAGA FERY WAGOMA KUSHINIKIZA BAADHI YA VIONGOZI KUTOLEWA NA HUDUMA YASIMAMA KWA MASAA KADHAA.

Afisa Mfawidhi SUMATRA Kanda ya Ziwa Japhet Leisimaye Ole akiwatuliza abiria ambao walikuwa wakihitaji kusafiri katika eneo la Kamanga kufuatia mgomo wa wafanyakazi wa kivuko cha MV. Orion.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kamanga Ferry wilayani Sengerema wakiwa na mabango yao katika mgomo wao wakitaka haki itendeke kufuatia kuondolewa kazini kwa watumishi wenzao katika hali ambayo waliitaja kuwa ilikuwa ya kiuonevu..
'Abiria wetu tunawaomba mtuvumilie, tunahitaji haki zetu' Lilisomeka moja ya bango la waaandamanaji hao.
Mkurugenzi wa Orion Bi. Wiebke Gaetye ambaye pia inatajwa na moja kati ya wafanyakazi wa MV. Orion kuwa alikuwa akitishiwa na Meneja wake Renatus Manyanda kuwa akimfukuza kazi naye ataondolewa nchini akitumia vibaya Jina la Mama Salma kikwete kumtishia Mkurugrnzi huyo.
Safari ilisitishwa kwa muda mpaka kieleweke.
Mv. Orion
Kapteni wa MV. ORION Adam Yusuph akiongoza meli yake huku Afisa Mfawidhi wa SUMATRA Kanda ya Ziwa Japhet Leisimaye Ole akijiridhisha juu ya ubora wa usafiri huo katika utoaji huduma. 
Safari inasonga.
Ratiba.
Mfanyakazi wa Kamanga Ferry akitoa maelekezo kwa abiria jinsi ya kuvaa jaketi la kujiokoa wakati wa ajali.
Safari imefikia ukingoni.
Mahojiano na wananchi.
Hatimaye mgomo umepatiwa utatuzi nacho chombo kinaendelea na utoaji huduma. 
Na Peter Fabian.
G. Sengo blog.
MWANZA.
WATUMISHI wa Kampuni ya Kamanga Fery ya Wilayani Sengerema leo wameweka mgomo ukishinikiza kuondolewea kwa watumishi wenzao wawaili na kusimamisha utowaji huduma ya usafiri wa abiria na magari Jijini hapa.

Hatua hiyo ilielezwa na Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi Adamu Yusufu ambaye pia ni Kepteni wa kivuko cha MV Orion cha Kampuni ya Kamanga Fery Ltd. kinachotoa huduma kati ya Kamanga Wilayani Sengerema na Kamanga Jijini Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za kampuni hiyo Mwenyekiti Kapteni Yusufu alisema kwamba wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa ujumla wao wameamua kugoma kutoa huduma ili kushinikiza Mkurugenzi Wiebke Gaetye kuwaondoa watumishi Renatus Manyanda (Meneja rasilimali watu) na Anna Malapa (Mhasibu matumizi) kutokana na kuwanyanyasa wafanyakazi wa Kampuni hiyo.

Mwenyekiti huyo alitaja sababu za mgomo huo kuwa ni pamoja na Manyanda kuwafukuza watumishi bila kosa, kushindwa kulipa makato ya mishahara yao kwenye Mfuko wa Jamii (NSSF), kushindwa kulipa mishahara zao kwa wakati ambapo wanadai tangu mwezi Novemba mwaka jana na kushindwa kufanya matengenezo ya vivuko vya kampuni hiyo kwa wakati.

“Bila Mkurugenzi kuyashughulikia haya tunayolalamikia ikiwa ni pamoja na kutuondolea watumishi hawa wanaolalamikiwa na wenzao, nasi hatuko tayari kufanya kazi na tutaendelea na mgomo hadi kilio chetu kitakaposikilizwa na kutolewa majibu” alisisitiza.

Kwa upande wa Mhasibu Malapa alisema kwamba amekuwa akiwanyima malipo yanayoizinishwa na Mkurugenzi ama uongozi wa Kampuni hiyo na hata amekuwa akitoa kauli za kuwakejeli watumishi wenzake jambo ambalo wamedai kuchoshwa nalo.

Kufatia mgomo huo uliodumu kwa masaa kadhaa na kupelekea Mkurugenzi Gaetye kuchukua jukumu la kukaa na wafanyakazi ili kusikiliza hoja na malalamiko yao ambapo aliamua kumfukuza kazi kwanza Manyanda kisha kusikiliza malalamiko mengine ili kupoza hasira za wafanyakazi hao.
Akizungumza madai ya wafanyakazi hao Mkurugenzi huyo alisema kwamba tayari amemfukuza kazi huku hoja za malipo ya mishahara yao ataifanyia kazi haraka na ile ya NSSF huku Mhasibu Malapa akisimamishwa kwanza kuchunguzwa na uamuzi wake ukisubili kikao cha uongozi wa Kampuni.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi (Cotwu) tawi la Kampuni hiyo Kapteni Jorwa Magesa (MV Orion) alisema kwamba kufatia kikao na Mkurugenzi wao wamelidhika na hatua alizochukua na wamempatia muda kushughulikia mambo mengine yaliyosalia ikiwa ni malalamiko yao ya msingi.

Hatua ya kuondolewa kwa Manyanda imepongezwa na wafanyakazi na wananchi wa Kijiji cha Kamanga Wilayani Sengerema ambao juzi majira ya jioni waliandamana na mabango kumpinga kuendelea kuwa mfanyakazi wa Kampuni hiyo hali hiyo ilipelekea jana kuwepo mgomo mkali kwa wafanyakazi hao nao wakipinga kuendelea kuwepo kwa watu hao katika Kampuni hiyo.

Manyanda pia amelalamikiwa na baadhi ya wafanyakazi waliokataa kutajwa majina yao hadharani kwa madai kuwa Manyanda alikuwa akitumia pia Jina la Mama Salma Kikwete kumtishia Mkurugenzi huyo raia wa Taifa moja la Ulaya kuwa akimfukuza naye ataondolewa nchini.

Hadi tunakwenda mitamboni hali ya eneo la Kamanga fery ilikuwa shwari baada ya Mkurugenzi na wafanyakazi wake kukubaliana kuendelee kutolewa huduma ya usafiri wa abiria na magari wakati madai yao mengine yakishughulikiwa na kuchukuliwa hatua za haraka kama walivyokubaliana.