Ibrahim Kamwe akiwa na rais wa WBF Howard Goldsberg. |
Ibrahim akiwa na maofisa wenzake,Sakwe Mtulia, Fidel Hynes na Lucas Msomba wakirekebisha jambo. |
Emmanuel Saleh, Ibrahim Kamwe, Emmanuel Mlundwa. |
HABARI KAMILI.
Siku ya terehe 1 ya mwezi wa pili katika ukumbi wa vijana hall kinondoni KUANZIA SAA TATU NA NUSU ,kutakuwepo na mkutano mkubwa wa wanamasumbwi wote ulioitishwa na orgnaizesheni ya ngumiza kulipwa Tanzania (TPBO) kwa lengo la kuwakutanisha mapromota wote,mabondia na makocha wa ngumi wote kwa lengo la kujadili ngumi za kulipwa zinapoelekewa,kujuana na kuelimishana sheria za ngumi za kulipwa zinavyotumika kinyume na sasa ,sheria nyingi zinafungiwa macho na kutumia uzoefu zaidi kuendesha mgumi nchini. Mkutano huo ulioitishwa na Rais wa TPBO bw Yasin Abdallah akishirikiana na Ibrahim kamwe na Mapromota wa ngumi chini ya ufadhili wa kitwe Traders unatarajiwa kuwa mkutano wa kwanza kuwakutanisha mapromota wote pamoja na mabondia wa ngumi za kulipwa wa hapa nchini ili kuboresha ngumi na kuhamasisha wadhamini na makampuni wajitokeze kuudhamini mchezo huo ,ambao ndio mchezo unaoliletea mataji na sifa Tanzania katika medani za kimataifa lakini hauna udhamini wowote ,mpaka sasa ni mchezo ambao unaojiendesha wenyewe kwa nguvu za wadau wachache wachovu na mabondia wenyewe ambao uwezo wao ni mdogo sana kukikidhi matakwa kamili ya mchezo wenyewekam ilivyo kwa wenzetu,ni mchezo ambao una huduma nyingi zinazohitaji nguvu ya wadhamini ili uendelee kuboreka zaidi.
Akizungumza na vyombo vya habari katibu wa ngumi za kulipwa nchini bw Ibrahim kamwe , amesema imewaalika viongozi wa baraza la michezo (BMT), na viongozi wengine wote wa ngumi za kulipwa watakuwepo kama vile Emmanuel mlundwa,names kavishe, makaranga,Onesmo ngowi,kinyogoli, matumla, Zuwena kibena(mama zugo) na viongozi wadau wa karibu na ngumi wamealikwa kuhudhulia mkutano huo ambao utafanyika Siku ya terehe moja ya mwezi wa pili katika ukumbi wa vijana hall kinondoni. hivyo kamwe alimaliza kwa kuwaomba kila anaejijua kuwa yeye ni bondia wa ngumi za kulipwa na promota wangumi ahudhurie bila kukosa mkutano huu muhimu sana kwa wamasumbwi ya nchi yetu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.