ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 26, 2014

KARIBU TENA HII LEO BOXING DAY, BAADHI YA PICHA ZA XMASS NDANI YA JEMBE BEACH 25 DEC 2014

'PAMOJA SANA' Mkurugenzi wa Jembe ni Jembe ambaye pia mmiliki wa 93.7 Jembe Fm Dr. Ndege akimtambulisha mwanamuziki Kidumu na bendi yake ya Bodaboda kwaajili ya kutumbuiza wakazi wa Mwanza katika sherehe ya Krismasi ndani ya Jembe Beach jijini Mwanza.
Aksante sana wana Mwanza kwa kujitokeza.
Usiku huu pia ulitumika kuitambulisha JJ Band aka Jembe ni Jembe Band ambayo kuanzia sasa itakuwa ikitumbuiza hapa.
Kiongozi wa JJ Band mbeleeeee.....!!
Muziki umekolea.....!!
Lady singer....!!
Hatariiii....!!
Kimenuka sasa mwendo ni Kusebenuka...!!
Hapa ndipo mziki unapikwa...!!
Hatariii....!!!
Ze nyomizzzz....!!
Penye kinu cha muziki 'Super sound master' Oxxy.
"The area na zile chomeX'
Karibu sana hii leo tufungue mazawadi.

ASKOFU BUNANGWA AWATAKA WATANZANIA KULIKABIDHI TAIFA KWA MUNGU

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la African Inland Charch Tanzania (AICT),Dayosisi ya Mwanza John Bunangwa, amewataka waumini kuliombea Taifa la Tanzania kwa Bwana Yesu ili kuliepusha kuingia kwenye dhambi na machafuko yanayoweza kuliangamiza.

Askofu Bunangwa akizungumza jana na waumini wa kanisa la AICT Makongoro Dayosisi ya Mwanza, alisema waumini na watanzania wote kwa ujumla bila kujali madhehebu yao na itikadi zao bali wanao wajibu mkubwa wa kuliombea Taifa kwa Bawana Yesu ili kuliepusha kuingia kwenye machafuko na dhambi ambayo inaweza kuleta vurugu na kutoweka kwa amani na utulivu uliopo sasa.

"Kuna baadhi ya watu wamekuwa waongo na wamewaiga Adamu na Eva waliomdanganya mungu na kutumbukia kuchuma dhambi ambazo leo hii wamejitumbukidha na kumsahau Bwana Yesu na kufanya vitendo vinavyomchukiza Mungu,"alisema.

Askofu, amewataka watanzania kuendelea na maombi na sala za kuliombea Taifa ili kuepuka kufika mwaka 2015 tukiwa tumejitumbukiza kwenye dhambi ya Adamu na Eva na kupelekea kuingia taifa kuwa kwenye machafuko na kusababisha amani na utulivu kutoweka na kuanza kusambaratika, hivyo ni vyema tukaendelea kuomba na kusali katika makanisa na majumbani kwetu.

"Niombe wenye dhambi mlioko humu kanisani mpite mbele ili kutubu na kuomba kusamehewa dhambi kwani dhambi ni usaliti kama wa Adamu na Eva ili msiende majumbani mwenu kusherehekea Chrismas mkiwa na dhambi bali muende mkiwa wasafi na wenye matumaini makubwa,"alisisitiza

Amwataka waumini kuwa na utaratibu wa kutubu  kwani ni kubadilika kifikira na kuwa na mwenendo mzuri kwa kila muumini na mwananchi wa taifa hili jambo ambalo kwa kila mmoja akilitekeleza kwa vitendo kutasaidia kuwa Taifa lenye kumpendeza mungu siku zote.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAAGA WATOTO WENYE MATATIZO YA MOYO KWENDA KUTIBIWA INDIA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ya kuwaaga jumla ya watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, waliofadhiliwa na Lions Club ya jijini, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ya kuwaaga jumla ya watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, waliofadhiliwa na Lions Club ya jijini, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Rais wa Lions (Host) Club ya Dar es Salaam, Mathew Levi, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mmoja kati ya watoto wanaokwenda kutibiwa nchini India, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa ya moyo iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mtoto, Nabil Hahya (4) kutoka Jijini Dar es Salaam, mmoja kati ya watoto 55 wa awamu ya kwanza kati ya 104 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo wanaokwenda kutibiwa nchini India, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto hao iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mama wa motto huyo, Amina Yahya. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mtoto, Hyria Ally (miezi 9) Kutoka Zanzibar, mmoja kati ya watoto 55 wa awamu ya kwanza kati ya 104 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo wanaokwenda kutibiwa nchini India, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto hao iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mama wa motto huyo, Zulekha Said. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa Beji ya miaka 50 ya Lions Club na Makamu wa Gavana wa Club hiyo, kwa nchi za Tanzania na Uganda, Hyderali Gangji, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo wanaokwenda nchini India kutibiwa. Hafla hiyo ilifanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Rais wa Lions (Host) Club ya Dar es Salaam, Mathew Levi, akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo. Picha na OMR
Badhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, wakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo. Picha na OMR
Badhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, wakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo. Picha na OMR
Badhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, wakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo. Picha na OMR
Baadhi ya wadau waliohudhuria hafla hiyo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wadau wa Lions Club, baada ya hafla fupi ya kuwaaga watoto hao. Picha na OMR

Thursday, December 25, 2014

SKYLIGHT BAND YATOA RATIBA YAKE YA WIKI TUKIANZA NA MKESHA WA X-MASS HADI MWAKA MPYA

10675565_408778115946839_5013196848087740184_n
24.12.14 Mkesha wa XMASS tutakua ESCAPE1, show itaanzaa saa mbili usiku, kiingilio buku 7000/= tu: tukutane ESCAPE1 tuikaribishe XMASS
Vile vile tunapenda kutoa taarifa na kuwaomba radhi wadau wetu kutokana na safari yetu ya kanda ya ziwa XMASS hii, show zetu za ijumaa tarehe 26.12.14 thai village na jumapili 28.12.14 ESCAPE1 hazitofanyika.
Ila tukutane tena kwenye mkesha wa mwaka mpya 31.12.14 ndani ya ESCAPE1. .. Burudika na bendi yako katika msimu huu wa siku kuu...Skylight Band...just follow the light ♫

TAMASHA LA TUONANE JANUARY (TUO8JANUARY) LAFANA MJINI MOROGORO

 Wasanii wa Hip hop katika anga ya muziki wa Bongofleva,Faridi Kubanda a.k.a Fid Q pamoja na Stamina wakilishambulia jukwaa kwenye tamasha la wazi la Tuo8January,hapo jana katika viwanja vya sabasaba mjini Morogoro.

Tuo8January ni kampeni maalum iliyozinduliwa hivi karibuni ikiwa na lengo la kuwahamasisha vijana kujitokeza kushiriki mchakato wa uchaguzi  wa viongozi mbalimbali wanaowataka na wanaowaamini wana uwezo wa kuleta mabadiliko ya kinidhamu kwenye masuala ya msingi ya Taifa letu.

Kama vile haitoshi kampeni hiyo inatumika kuwahamasisha vijana wenye uwezo na sifa za kugombea nafasi za uongozi kuchukua hatua sasa za kufanya hivyo,pia kupata vijana wen,vijana wenye vigezo vya kupiga kura pia ni lazima wafanye hivyo maana ni wajibu wetu na kuwa vijana ni lazima tushiriki kikamilifu katika mchakato wa kampeni ili kuhakikisha mambo ya msingi yanajadiliwa na wagombea na yanapewa kipaumbele. 

Katika tamasha hilo Fid Q aliwahamasisha vijana mbalimbali waliojitokeza kwenye tamasha hilo,kuwa imefika wakati wa vijana kujitokeza kushiriki mambo mbalimbali ya kimsingi kwa manufaa ya nchi yao na si kukaa chini na kuanza kulalama,wakati kwenye mambo ya maamuzi wakishirikishwa hawataki kujitokeza,hivyo ni wakati wao wa kuamka na kuchagua kiongozi kijana wa kisasa na si kiongozi wa kisiasa.
 Msanii mwingine wa hip hop katika anga ya Bongofleva,ambaye amekuwa akifanya vyema kwenye muziki huo,Niki wa Pili akitumbuiza katika jukwaa la wazi la Tuo8Januari lililofanyika mjini Morogoro hapo jana.
 Baadhi ya wakazi wa mji wa Morogoro wakishangilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la Tuo8January,lililofanyika jana kwenye viwanja vya sabasaba mjini humo,tamasha hilo la wazi ambalo limewashirikisha wasanii mbalimbali,ni kampeni maalum ya kuwahamasisha vijana kushiriki katika chaguzi mbalimbali kwa njia ya matamasha.

Kampeni hiyo ilizinduliwa jijini Dar hivi karibuni na kufanyika tamasha la kwanza mkoani Njombe na sasa Mkoani Morogoro.Baadhi ya Wasanii mbalimbali wenye ushawishi mkubwa kwa vijana wameonesha kuiunga mkono kampeni hiyo,akiwemo Babu Tale, Mwana FA, Nick wa Pili, Lamar, P-Funk, Mwasiti, Barnaba, Ditto,G-nako,Fid Q,Shilole,Yamoto Band,Stamina na wengineo.
 Baadhi ya Wadau wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la Tuon8January katika viwanja vya sabasaba mjini Morogoro.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya aitwaye Linah akiimba wimbo wake wa OleThemba,mbele ya mashabiki wake (hawap pichani),waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Tuo8January,lililofanyika kwenye viwanja vya sabasaba jana jioni mjini Morogoro.
 Ilikuwa ni shangwe tu kutoka kwa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kupitia tamasha la Tuo8January
 Mmoja wa wasanii mahiri wa Hip hop,ambaye amekuwa akifanya vyema katika anga ya muziki wa kizazi kipya,aitwaye Stamina akitumbuiza mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Morogoro katika tamasha la Tuo8January,lenye lengo la kuwahamasisha vijana kujitokeza kushiriki mchakato wa uchaguzi  wa viongozi mbalimbali wanaowataka na wanaowaamini wana uwezo wa kuleta mabadiliko ya kinidhamu kwenye masuala ya msingi ya Taifa letu.
 Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza kwenye tamasha hilo la la Tuo8January,lenye lengo la kuwahamasisha vijana kujitokeza kushiriki mchakato wa uchaguzi  wa viongozi mbalimbali wanaowataka na wanaowaamini wana uwezo wa kuleta mabadiliko ya kinidhamu kwenye masuala ya msingi ya Taifa letu.
 Baadhi ya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika jukwaa la tamasha la Tuo8January,lililofanyika jana katika viwanja vya Sabasaba,mjini Morogoro.

 Pichani kulia ni Msanii Mwasiti akiimba wimbo wake wa serebuka akiungwa mkono na shabiki wake kwa kunogesha zaidi jukwaa,huku shangwe za mayowe na vifijo zikiwa zimetawala kutoka kwa mashabiki waliofika katika tamasha la Tuo8January hapo jana.
Pichani kati ni msanii Shilole akiwa sambambana madansa wake wakilishambulia jukwaa kwa pamoja mbele ya umati wa wakazi wa mji wa morogoro,waliojitokeza kwenye tamasha la Tuo8Januari,lililofanyika hapo jana katika viwanja vya sabasaba mkoani humo.
 watazajamaji wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri katika jukwaa la Tuo8January hapo jana katika uwanja wa sabasaba mjini Morogoro.
 Mkali mwingine wa kufloo freestyle,Godzilla akipanda katika jukwaa la tamasha la Tuo8January,tayari kwa kuwaburudisha wakazi wa mji wa Morogoro waliojitokeza kwa wingi katika tamasha hilo.

Tuesday, December 23, 2014

MSHINDI WA MTOKO WA MBUGANI ALAMBA MKATABA MNONO SERENGETI.

Mshindi wa kwanza wa shindano la Tutoke na Serengeti, lijulikanalo kama "MTOKO WA MBUGANI" Bw. Hassan Mfaume, akisaini mkataba wake na kampuni ya bia ya Serengeti.Katikati  ni meneja wa bia chapa ya Serengeti Bw.Rugambo Rodney na kushoto ni Meneja wa Serengeti kanda ya Dar es Salaam,Malalia Mmassy. Mkutano  ulifanyika makao makuu ya kampuni hiyo-Chan'ombe jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Serengeti kanda ya Dar es Salaam,Malalia Mmassy akisaini mkataba wa mshindi wa shindano la Tutoke na Serengeti, ambapo mshindi huyo anatarajia kusafiri hivi karibuni, Mshindi wa kwanza wa shindano la Tutoke na Serengeti, la kwenda kutalii kwenye mbuga za wanyama , Bw.Hassan Mfaume, Meneja wa bia chapa ya Serengeti,Rugambo Rodney
Meneja wa bia chapa ya Serengeti,Rugambo Rodney akimkabidhi mkataba Mshindi wa kwanza wa shindano la Tutoke na Serengeti, la kwenda mbuga za wanyama , Hassan Mfaume,katikati ni  meneja wa Serengeti kanda ya Dar es Salaam,Malalia Mmassy. Mkutano huo ulifanyika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

WAMILIKI 10 WA MADUKA BUBU WAKAMATWA WAPANDISHWA KIZIMBANI KATI 100 MSAKO KUENDELEA JIJINI MWANZA

NA PETER FABIAN.
MWANZA.


WAMILIKI wa maduka bubu ya dawa baridi wapatao 10 kati ya 100 waliokamatwa kufatria operesheni maalumu, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mukazi Wilaya ya Nyamagana kwa kosa la Jinai jijini Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari Mahakamani hapo mwishoni mwa juma lililopita, mmoja wa wanasheria kutoka Jiji la Mwanza, Alhaj Bwabo Makusudi alisema kwamba watuhumiwa hao 10 waliopandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka ya kosa la jinai mahakimu wawili tofauti wa Mahakama hiyo.

Makusudi alifafanua kukamatwa kwa watuhumiwa hao kati ya 100 kulitokana na zoezi la ukaguzi na operesheni maalumu iliyofanywa na kikosi kazi cha pamoja cha Halmashauri ya Jiji, Manispaa ya Ilemela na Idara zingine za serikali ambapo watuhumiwa 10 awali walifungiwa maduka yao lakini waliyafungua na kuendelea na utoaji huduma nyakati za usiku kabla ya kukamatwa tena.

Aliwataja watuhumiwa hao kumi waliopadishwa kizimbani na kusomewa mashitaka mbele ya Mahakimu, Ainawe Moshi na Janeti Masesa wa Mahakama hiyo, kuwa ni watuhumiwa James Warioba (30) mkazi wa Butimba, Likutuye Paschal (30) mkazi wa Mkolani, Amayo Joshua (29) mkazi wa Igoma, Issa Kubona (58) mkazi wa Igoma (wote Nyamagana) na Neema Kitinya (45) mkazi wa Kisesa (Magu).

Wengine waliopandishwa kizimbani ni Fatuma Martine (24) mkazi Kilimahewa,  Wangeta Musanya (25)  mkazi wa Butimba , Anna John (50) Uzinza (wote nyamagana na Maua Ally (23) mkazi wa Kiloleli (Ilemela) ambapo wakipatikana na hatia watapewa adhabu ya kifungo cha miaka miwili jera au kutozwa faini isiyozidi milioni 10.

Makusudi alisema watuhumiwa wengine 100 baadhi yao wametozwa faini na wengine wanaandaliwa mashitaka ili kufikishwa mahakamani kulingana na makosa waliyokamatwa nayo wakati wa utekelezwaji wa zoezi hilo linaloshirikisha Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.

Kwa upande wake, Mfamasia wa Jiji la Mwanza, Edward  Magelewanya , alisema kwamba hatua ya kuwafikisha mahakamani inatokana na watuhumiwa hao kukamatwa katika zoezi la ukaguzi na operesheni iliyofanywa tangu Desemba 8 hadi 20 mwaka katika maeneo yote ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.

Magelewanya alisema kwamba lengo kuu la ukaguzi na operesheni hiyo iliyofanywa katika maduka 171 na kikosi kazi kikihusisha Idara Afya za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela na zingine za serikali, ilikuwa na lengo la kuangalia kama sheria, kanuni, miongozo, viwango na taratibu za kutoa dawa kwa sekta binafisi zinafuatwa , zinatekelezwa na wamiliki na wanaofanyabiashara hiyo.

Alifafanua kuwa zoezi hilo pia lililenga kujilidhisha kuona kama wamiliki wana vibali kutoka Baraza la Famasi Tanzania, Leseni za biashara, Usajili wa majengo na Ubora wake, kufatilia Watalaamu wanaotoa huduma kwa walaji wa dawa kama wanakidhi vigezo na wanatambuliwa na Baraza la Phamacy’s nchini, kufatilia uwepo wa dawa za serikali katika sekta binafsi.

“Utekelezaji wa zoezi hili pia ulilenga kuchukua hatua sitahiki, kuangalia nyaraka muhimu za utendaji kazi katika maduka hayo ya watu binafsi na vitabu vya rejea na kufatilia majengo nyanayoendesha huduma hii kama yanakidhi vigezo vinavyotakiwa katika kuhifadhi dawa na kutoa huduma , ” alisisitiza na kuongeza kuwa zoezi hilo ni endelevu.

Magelewanya alisema kuwa zoezi hilo limeshirikisha Ofisi za Mganga Mkuu wa Mkoa, Waganga Wakuu wa Wilaya za Nyamagana na Ilemela, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Mkoa, Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa, Maafisa Biashara wa Mkoa na Halmashauri zote mbili, Ofisi za Mfamasia wa Jiji na Manispaa ya Ilemela na Vyombo vya Ulinzi na Usalama na watendaji wa Kata katika Halmashauri husika.

Monday, December 22, 2014

HIVI NDIVYO ALIKIBA NA JOH MAKINI WALIVYO KISANUKISHA KWENYE RED CUP PARTY @JEMBE BEACH

Mwanamuziki Alikiba huku akipata mapokezi mazito alipiga bonge la show kwa wapenzi wa burudani walioibuka kwenye bustani ya kitalii Mwanza Jembe Beach iliyoko Malimbe Mwanza.  
Joh Makini Mwamba wa Kaskazini kama ada alikisanukisha 'mbaaaaaaya' @jembenijenbe brazaz N sistaz wakimkubali bila utratra'.
Jembe ililipuka kwa shangwe.
Ni hip hop lakini ladies wanajua mstari baada ya mstari...
Kibajaji style demu anasinzia...
Pap-the PaP...!!
Khatariiii.
Yeeeeeeh.
Toka A City hadi Rock City ni Joh Makini.
Ni mwendo wa kuchukuwa kumbukumbu.
Kila mmoja alikuwa na hamu kumlaki 'Mfalme' @alikiba
See the crowd @jembenijembe.
Wow...!!
Ni red Cup Party at Jembe Beach Mwanza kuelekea sikukuu ya Christimass 
The stage ikitawaliwa na Alikiba.
WuuuP...!!
Kama mduara flani hivi...!!
Mshike mwenzio begani...
Flowers in the house.
Vijana wa Mwanza si ndiyo hawa.
Hisia kali.
Hapa ilipigwa new style iliyoko kwenye wimbo 'Mwana Dar es salaam' kisha kwa mara ya kwanza kikatambulishwa kichupa kipya cha wimbo huo.
Hii utaiona ndani ya 'Mwana Dar es salaam'
Juu kwa juu hadi angle moja ya stage.
Alikiba (L) and G. Sengo (R)
'PAMOJA SANA' Ishara ya kidole kimoja toka kwa msanii anayetikisa kanda ya ziwa right now na track yake iitwayo Changamka he goes by the name of Shaibu Sapi (L) and G. Sengo (R)
Mwanadada mbunifu na muuzaji wa mavazi Mwanza, Annet Koka (C) akiwa na Crew yake.
Whaaaaat....!!!
CEO wa Brand ya 'Jembe ni Jembe' Sebastian Ndege hapa alipata fursa ya kuwatambulisha kwa mara ya kwanza ambayo si rasmi ikisubiriwa rasmi kutambulishwa rasmi Christimass hii ambapo Kidumu na bendi yake watasindikiza uzinduzi huo.