ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 1, 2023

MBIO KUBWA KULIKO ZOTE KANDA YA ZIWA KUKIWASHA JUMAPILI HII 02 july 2023 MWANZA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Hayawi hayawi sasa yamekuwa hatimaye zile mbio za riadha zijulikanazo kama Transec Lake Victoria Marathon inakwenda kushika kasi yake kesho Jumapili Julai 02, 2023 jijini Mwanza. Hilda Viggo ni mratibu wa Transec Lake Victoria Marathon anasema mpaka sasa watu 1380 wamekwisha jiandikisha kwenye ushiriki wa mbio hizo, mwamko umekuwa mkubwa tofauti na miaka miwili iliyopita huu ukiwa mwaka wa 3unaoshuhudia mapinduzi makubwa hasa ya maandalizi, ubora wa tuzo na uwekaji wa kumbukumbu. Kwa mwaka huu 2023 Transec Lake Victoria Marathon imekuja ikilenga kuhamasisha utalii wa ndani, uhifadhi wa Ziwa Victoria pamoja na kusaidia matibabu ya watoto wanaotibiwa saratani katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando.

DC TANGA ATOA NENO KWA WASTAAFU KUHUSU MATAPELI

 

 


MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati akifungua Semina kwa Wanachama wanaotarajia kustaafu Jijini Tanga iliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati akifungua Semina kwa Wanachama wanaotarajia kustaafu Jijini Tanga iliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
Meneja wa Mafao wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Makao Makuu James Oigo akizungumza wakati wa semina hiyo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akifuatia na Meneja wa Pensheni wa NSSF Makao Makuu Nancy  Mwangamilo na Afisa na kushoto ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Cosmas Kadeghe na wa kwanza kulia ni  Afisa Mkuu wa Idara ya Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama 
Meneja wa Mafao wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Makao Makuu James Oigo akizungumza wakati wa semina hiyo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akifuatia na Meneja wa Pensheni wa NSSF Makao Makuu Nancy  Mwangamilo na Afisa na kushoto ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Cosmas Kadeghe na wa kwanza kulia ni  Afisa Mkuu wa Idara ya Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama
Afisa Mkuu wa Idara ya Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama akizungumza wakati wa semina hiyo kushoto ni Meneja wa Pensheni wa NSSF Makao Makuu Nancy  Mwangamilo akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa ,Meneja wa Mafao wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Makao Makuu James Oigo na  Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Cosmas Kadeghe  
Meneja wa Pensheni wa NSSF Makao Makuu Nancy  Mwangamilo akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali

Sehemu ya wanachama wanaotarajiwa kustaafu Jijini Tanga wakiwa kwenye semina hiyo  
Sehemu ya wanachama wanaotarajiwa kustaafu Jijini Tanga wakiwa kwenye semina hiyo
Meneja wa Benki ya NMB tawi la Ngamiani Elizaberth Chawinga kulia akifuatilia semina hiyo
Picha ya Pamoja 


Na Mwandishi Wetu, Tanga

MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa amefungua Semina kwa Wanachama wanaotarajia kustaafu Jijini Tanga iliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) huku akitoa wito kwa wastaafu hao kuhakikisha wanafanya uwekezaji mapema ikiwemo kuepukana na magenge ya matapeli

Mgandilwa aliyasema mwishoni mwa wiki wakati akifungua semina hiyo kwa wanachama wanaotarajiwa kustaafu Jijini Tanga iliyoandaliwa na mfuko ambapo pia aliwataka kuepukana na magenge ya matapeli ambao wanahaingaika kuwashawishi kufanya biashara ambazo mlengo wao ni kwenda kuwaibia

Alisema kwamba kuna tabia ambayo imeibuka kwamba wafanyakazi wanapokaribia kustaafu lipo genge la matapeli ambalo limekuwa likijitokeza na kuwashawishi kufanya biashara ambazo mwisho wa wiki zinapelekea kuwaibia fedha ambazo wanakuwa wamezipata kama mafao yao.

“Katika Jambo hilo niwaase wastaafu tuweni makini sana na watu wa namna hii maana tunaweza kujikuta tunapoteza fedha zetu na mwisho wa tukajuta hivyo niwaase katika kipindi cha kuelekea kustaafu ni vema tukaanza maandalizi ikiwemo uwekezaji wenye tija”Alisema Mkuu huyo wa wilaya.

“Niwapongeze NSSF kwa kazi nzuri changamoto zinazowakumba watu wanaokaribia kustaafu kuna watu ambao ni genge la matapeli wanahaingaika kuwashawishi kufanya biashara ambazo mlengo wake ni kwenda kuwaibia hivyo niwasihi hakikisheni mnakuwa makini na watu wa namna hii”Alisema

Mkuu huyo wa wilaya pia alitumia wasaa huo kuwaasa kuhakikisha wanafanya maandalizi ya kustaafu kabla ya muda wa kustaafu lakini pia ni vema kuendelea kukumbushana kuna biashara ambazo zinaibuka kwenye msimu wa watu wanapokuwa wakitaka kustaafu hivyo nitoe rai kwa wastaafu kuona umuhimu wa kuhifadhi fedha wanazozipata.

Alisema licha ya kuhifadhi fedha hizo ni vema wawekeze kwenye maeneo yenye tija kwenye fedha lakini wakumbuke kuchagua marafiki kwenye kipindi hicho kutokana na kwamba wakati huo wapo ambao wanaweza kuibuka wakiwa na nia mbaya.

Awali akizungumza wakati wa semina hiyo Meneja wa Mafao wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Makao Makuu James Oigo alisema kwamba semina hiyo ni muhimu kutokana na kwamba ni maandalizi ya kustaafu kwa wafanyakazi ambao wanatarajiwa kustaafu lengo kubwa kuwaandaa kueleza dhana nzima ya hifadhi ya Jamii nafasi ya mfuko wa (NSSF) katika maisha yao baada ya kustaafu.

Alisema pia na jinsi ambavyo wanatakiwa wajiandee kwa ajili ya kupata mafao yao na namna watakavyotumia mafao yao katika maisha yao baada ya kustaafu ikiwemo kuwaondolea hofu ambayo jamii inayofikiri hakuna maisha baada ya kustaafu.

Alisema kwamba wanataka kuwapa elimu na kuwajenga kisaikolojia kwamba maisha yapo na NSSF ina nafasi kubwa sana kwenye maisha yao kwa kila pensheni wanayoipata kila mwezi na elimu hiyo imekuwa ikitolewa kwa mikoa yote nchini .

Naye kwa upande wake Mwanachama Mstaafu wa Mfuko wa NSFF Mkoani Tanga Martha Kazala alisema kwamba wanaushukuru mfuko huo na kwamba wanapokea pensheni kila mwezi na haina matatizo yoyote.

Alisema kwenye ustaafu wake ana miaka saba na anafurahia maisha yake kwa sababu yanamsaidia katika maisha yao watu wanafikiria ukiajiriw ukitoka kazini wanadhani hakuna maisha yanayoendelea baada ya kustaafu maisha ni mazuri kubwa inatakiwa uwe mvumilivu wakati wa ajira ili uweze kufanikiwa kwenye masuala la ustaafu na malipo ya pensheni.

Hata hivyo aliwataka waajiriwa wanaotarajiwa kusfaafu wajipange ili wanapopata fedha wafanye maamuzi yaliyokuwa na busara ya mipangilio ikiwemo kuepukane na vishiwsihi sambamba na kufuata maelekezo ya mifuko ya hifadhi  za jamii ili waweze kuishi vema

TAKUKURU TANGA YAWAPANDISHA KIZIMBANI WATUHUMIWA WA MAKOSA YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI

 




Na Oscar Assenga,TANGA.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Tanga imewapandisha kizimbani watuhumiwa wane(8)kwa makosa ya rushwa na uhujumu uchumi na kuisababisha Serikali matumizi batili ya zaidi ya shilingi milioni 28.

Waliopandishwa kizimbani ni William Nguluko Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Mabokweni jijini Tanga ambaye anakabiliwa na ashitaka la ubadhirifu na ufujaji kinyume na kifungu cha 28(1)(2) sharia na kuzuia na kupambana na rushwa sura ya 329 marejeo ya mweka 2022.

Kosa jingine ni kula njama , kutenda makossa ya rushwa kinyume na kifungu na kifungu 32 sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa , kuisababishia hasara serikali kinyume na aya ya 10(1) ya jedwali la kwanza na kifungu cha 57(1) na 60(2) sharia ya uhujumu uchumi sura ya 200 marejeo ya mwaka 2002.

Mshitakiwa wa pili ni Sudi Mshamu, mwalimu wa fedha katika shule hiyo , ambaye yeye anakabilwa na na makosa 31 likiwemo kosa la kughushi kinyume na kifungu cha 333,335(111) na 338,340(2)A sharia ya kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.

Kosa jingine ni kula nyama kinyume na kifungu cha 32 sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022 ikisomwa pamoja na aya ya 21 jedwali la kwanza na kifungu cha 57 (1) na kifungu cha 60(2) sharia ya uhujumu uchumi sura ya 200 marejeo ya mwaka 2020.

Mtuhumiwa wa tatu, Mwanabakari Adhumani aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo anashitakiwa kwa tuhuma ya kula njama kifungu cha 32 ,sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022.

Kosa jingine ni kuisababishia hasara serikali kinyume na aya ya 10(1) jedwali la kwanza na kifungu cha 57(1) na 60(2) sharia ya uhujumu uchumi sura ya 200 marejeo ya mwaka 2022.

Mshitakiwa wa nne ni Yusuph Mushi mwalimu wa shule ya sekondari Saruji ambaye kati ya makossa yanayomkabili ni kula nyama kinyumea na kifungu cha 32 sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022 ikisomwa pamoja na aya ya 21 jedwali la kwanza na kifungu cha 57 (1) na 60(2) sharia ya uhujumu uchumi sura ya 200 ya mwaka 2022,mshitakiwa alikiri kutenda kosa hilo.

Mbele ya hakimu wa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kakimu Mkazi Tanga Sophia Masati mtuhumiwa wa kwanza amekataa kutenda kosa hilo,wakati wa pili mwalimu wa fedha amekiri kutenda kosa hilo na mshitakiwa wa tatu naye amekataa kutenda kosa hilo wakati mshitakiwa wa nne amekiri kutenda kosa hilo.Washitakiwa hao wamerudishwa rumande na kesi yao itawajwa tena Julay 7 mwaka huu.