ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 31, 2014

ZIARA YA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI DR.TITUS KAMANI YABAINI CHANGAMOTO ZA VITENDEA KAZI KITUO CHA UTAFITI WA SAMAKI MWANZA.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Dr. Titus Kamani(kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Samaki kituo cha Mwanza  (TAFIRI) Dr. Robert Kayanda wakitazama jinsi hatua mbalimbali za utafiti zinavyofanyika ndani na nje ya ziwa.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Dr. Titus Kamani akishuka toka katika boti ya utafiti mara baada ya kuzugukia maeneo ya utafiti ziwa Victoria ambapo pia aliambatana na wadau wengine wa kitengo husika mkoa wa Mwanza..
Boti ya utafiti ikiwa na Mhe. Waziri pamoja na wadau wa utafiti.
Kituo cha Utafiti wa Samaki Tanzania kituo cha Mwanza bado kinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vitendea kwa baadhi ya boti zake hazijakarabatiwa kwa muda mrefu na moja kati ya boti za utafiti imekufa injini yake ikihitaji kufufuliwa pamoja na changamoto ya bejeti finyu ya kuendeshea mradi. Mfano kwa mwaka jana Idara ya Uvuvi mkoa wa Mwanza iliiingizia serikali kiasi cha shilingi bilioni 3 lakini bajeti iliyopata haikuzidi shilingi milioni 12. 
"Serikali haito vumilia kuona uvuvi haramu ukiendelea kushamiri badala yake itaendelea kupambana kwa hali na mali na watu wanaotengeneza zana haramu za uvuvi ili kuwepo na uvuvi endelevu wenye tija kwa nchi yetu" 
PICHA NA ZEPHANIA MANDIA.
WA G. SENGO BLOG.

MTANGAZAJI WA EATV KEN KIDAGO AFARIKI DUNIA.

NEWS:MTANGAZAJI WA TELEVISHENI YA EAST AFRICA(EATV),KEN KIDAGO AFARIKI DUNIA

Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha East Africa aliyekuwa akifanya kipindi cha 5 sports, Ken Kidago amefariki dunia.

Taarifa ambazo pia zimethibitishwa na mmoja wa wafanyakazi wa kituo hicho zinaeleza kuwa tangu jana januari 30,2014 Ken hakuonekana kazini ambapo simu zake zilikuwa zikipigwa bila majibu ikabidi uongozi wa EATV kutoa taarifa kwa jeshi la polisi nchini Tanzania,walipofika nyumbani kwake Mlalakua jijini Dar es salaam wakagonga mlango hakufungua kabidi wavunje na kuingia na kukuta amefariki.

Taarifa zinaeleza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa sababu ya kifo chake.

Ken Kidago aliwahi kuwa mtangazaji wa Radio Ukweli ya mjini Morogoro kabla ya kwenda Arusha ambapo alirejea jijini Dar es salaam hivi karibuni na kujiunga na East Africa Television

KINANA, MANGULA WAWASILI MBEYA KWA MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM.

Makamu Mwenyekiti wa CCM,Phillip Mangula akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Dk. Mary Mwanjelwa baada ya kuwasili leo asubuhi kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya , tayari akwa maadhimisho ya miaka 37 ya CCM yatakayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, jijini Mbeya Jumapili Februari 2. Kushoto ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.
 Mangula (katikati) akiwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati) akizungumza na Nape (kulia) pamoja na Zambi kwenye chumba cha watu mashuhuri (VIP) alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, Mbeya leo mchana, ttayari kwa maadhimidho hayo.
Nape (kulia) akizungumza na Kinana pamoja na Zambi kwenye Uwanja wa Ndege wa Songwe
Dk. Mary Mwanjelwa (kushoto) akijadiliana jambo na Makmu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi, Dogo Idd Mabrouk wakati wa mapokezi hayo.Picha na MichuziJr wa Michuzi Media Group.

WASHINDI WA AIRTEL ‘MIMI NI BINGWA’ WAREJEA TOKA OLD TRAFFORD

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na washindi wa tiketi wa promosheni ya Airtel ya Mimi ni Bingwa walioondoka nchini Jumapili wiki hii kwa safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda Old Trafford kuangalia mechi moja kwa moja kati ya Manchester United na Cardiff City iliyochezwa Jumanne usiku.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (katikati) katika picha ya pamoja na washindi wa tiketi wa promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya safari yao iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda Old Trafford kuangalia mechi moja kwa moja kati ya Manchester United na Cardiff City iliyochezwa Jumanne usiku.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (katikati) akifurahia jambo pamoja na washindi wa tiketi wa promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya safari yao iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda Old Trafford kuangalia mechi moja kwa moja kati ya Manchester United na Cardiff City iliyochezwa Jumanne usiku.
Baadhi ya washindi wa tiketi kupitia promosheni ya Mimi ni Bingwa inayoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakishuhudia mechi kati ya Manchester United na Cardiff City iliyochezwa hivi karibuni kwenye uwanja wa Old Trafford nchini Uingereza.Wa kwanza kulia ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando ambaye aliambatana na washindi hao.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (wa pili kutoka kulia) akipiga makofi muda mfupi baada ya wachezaji wa Manchester United kuingia uwanjani kwenye uwanja wa Old Trafford juzi nchini Uingereza. Mmbando aliambatana na washindi wa promosheni ya Mimi ni Bingwa inayoendeshwa na Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Airtel. Washindi hao walienda kushuhudia mechi kati ya Manchester United na Cardiff City.Kulia kwake ni Meneja Uhusiano wa Manchester United James Turner.
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester united Denis Irwin ( wapili kushoto) akiwa katika picha na Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (anayefatia) pamoja na mmoja kati ya washindi wa promosheni ya Mimi ni Bingwa kabla ya kuangalia mechi kati ya Manchester United na Cardiff City iliyochezwa hivi karibuni kwenye uwanja wa Old Trafford nchini Uingereza
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akiwa pamoja na mmoja kati ya washindi wa promosheni ya Mimi ni Bingwa Bw na Bibi Dickson Lyatuu muda mfupi baada ya kushuhudia mechi kati ya Manchester United na Cardiff City nchini Uingereza hivi karibuni.
 Washindi wa Airtel ‘Mimi ni Bingwa’ warejea kutoka Old Trafford
WASHINDI wa awamu ya kwanza ya promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa jana waliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere wakitokea Old Trafford ambapo walikwenda kushuhudia mechi ya moja kwa moja ‘live’ kati ya klabu ya Manchester United na Cardiff City.

Watanzania hao wamekuwa sehemu ya washabiki wa soka waliokuwa na furaha kushuhudia klabu ya Manchester United ikishinda 2-0 dhidi ya Cardiff City, wakati mchezaji Juan Mata akiichezea timu hiyo kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Old Trafford, hawakuweza kuficha furaha yao ya kuwa moja ya tukio hilo la kihistoria.   

Akizungumza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege, moja kati ya washindi wa tiketi ya Airtel Mimi ni Bingwa, Bw. Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, ambaye alisafiri na mke wake, alisema safari hiyo imekuwa ya manufaa sana katika maisha yao na kampuni hiyo ya simu imeweza kutekeleza yale yote waliyowaahidi washindi wa tiketi katika promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa.  

“Ninafuraha ya kipekee kuweza kurejea nyumbani salama baada ya safari yenye mafanikio makubwa ya kwenda Old Trafford. Suala nililojifunza nikiwa Manchester ni kwamba bado Tanzania inahitaji kufanyakazi kubwa ili kuziwezesha timu zetu kuendelea katika ulimwengu wa soka. Nawashukuru Airtel kwa kunipa mimi na mke wangu nafasi ya kuwa sehemu ya historia hii na kuweza kuyatekeleza yote waliyotuahidi,” alisema.

Meneja Uhusiano wa Aitel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando alisema wakati wa ziara ya kutembelea Old Trafford, timu ya washindi kutoka Tanzania ilionyeshwa ni jinsi gani Manchester United inawajali wachezaji wake waliostaafu, suala linalosaidia kuongeza hari katika timu na kutumia uzoefu kuiboresha timu.

“Huu ni mfano ambao wadau wetu wa michezo wanahitaji kuuiga. Tunatakiwa kuwathamini wachezaji wetu wa zamani na kutumia uzoefu wao ili kuzibadilisha timu zetu kuwa bora kimchezo kitaifa na kimataifa,” alisema.

Kwa upande wake, Andrew Muta Temwa, mshindi wa tiketi kutokea Bukoba alisema fursa ya kukutana na kocha Sir Alex Ferguson ilikuwa ni kama ndoto kwake. 

“Sikutarajia kama siku moja nitakutana na Sir Alex Ferguson moja kwa moja ‘Live’. Kupitia safari hii, Airtel imeweza kuzifanya ndoto yangu kuwa kweli. Nataka kuwahakikishia washiriki wengine wa Mimi ni Bingwa waendelee kucheza ili nao wapate fursa ya kushinda pesa taslim kupitia promosheni hii ya Airtel,” alisema.

Awamu ya kwanza ilijumuisha, Bw. Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Andrew Muta Temwa mkazi wa Bukoba, Ashraf Mohamed Adam kutoka Tanga na Salma Farid Mugheiry kutoka Dar es Salaam na wenza wao.

Airtel ilitangaza kuwa mbali na tiketi, zawadi kubwa ya shilingi milioni 50 sasa iko tayari kushindaniwa mwishoni mwa droo, ambayo kila mshiriki wa promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa ana nafasi ya kujishindia kwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neno “BINGWA” kwenda namba 15656, na kujibu maswali mengi iwezekanavyo.     

Washindi wa safari ya Old Trafford toka promosheni ilipoanza mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana ni pamoja na  Msemwa George Makuzi kutoka Dar es salaam, Edwin Edmund Kajimbo kutoka Iringa, Michael Joseph Shirima kutoka Kinondoni jijini Dar es Salaam, Bw. Shaibu Rashid Dege, Mtendaji wa kijiji cha Nang’olo wilayani Kilwa – mkoani Lindi, Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Joseph Steven Mambo kutoka Kawe jijini Dar es Salaam, Emmanuel Mahenge Jacob kutoka Njiro in Arusha, Rashid Jacob Kagombola kutoka Bukoba mkoani Kagera, Harrison Wilson Mwambogolo kutoka Kigogo jijini  Dar es Salaam na Salma Farid Mughery kutoka Dar es Salaam.

MING'ARO YA SKYLIGHT BAND HUANZIA IJUMAA.

DSC_0012
Divas wa Skylight Band wakiongozwa na Meneja wa Bendi Aneth Kushaba AK47 (katikati) kutoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar ambapo leo pia watakuwa pale pale kwenye uwanja wao wa nyumbani. Kulia ni Digna Mbepera na kushoto ni Winfrida Richard.
DSC_0028
Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa wa Bongo (kulia) akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band huku akisindikizwa na Hashim Donode.
DSC_0105
Rappa Joniko Flower akifanya yake jukwaani huku Digna Mbepera na Sony Masamba wakionyesha umahiri wao wa kusebeneka.
DSC_0081
Muziki mzuri na watu wastarabu si pengine ni Skylight Band ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar kila siku za Ijumaa kuanzia saa usiku na kuendelea.
DSC_0111
DSC_0145
Winfrida Richard akifanya yake jukwaani huku akipewa sapoti na Digna Mbepera.
DSC_0155
Mheshimiwa Bundala kama kawaida yake ndani ya Vest.
DSC_0170
Kuwafundisha tuwafundishe sie halafu mtuzidi????.... Vijana wa Skylight Band wakitikisa jukwaaa.
DSC_0189
Sam Mapenzi a.k.a Sukari ya warembo akililiwa asipande jukwaani na mashabiki wake.
DSC_0130
Kijana mtanashati kutoka kundi la Wadananda akiwa amestarehe kwenye kiti kutegeshea mrembo wa kucheza naye mdaura hapo kati..!
DSC_0139
Mdau Gerald Kilimo akiwa na mfanyakazi mwenzake walikuja kupunguza stress za kazi na burudani ya Skylight Band.
DSC_0097
Wadau wa Skylight Band na Ukodak.
DSC_0206
Wadau wa Skylight Band na Msanii Hashim Donode katika picha ya ukumbusho.
DSC_0184
Mama Kisso wakipata Ukodak na Aneth Kushaba AK 47 a.k.a Mjasiriamali mpango mzima wa kupendeza kichwani unaweza kumwona yeye...!
DSC_0197
Aneth Kushaba akibadilishana mawazo na Mtangazaji wa kipindi cha Mama land Benny Kinyaiya wa Clouds fm.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS SASA..!!


Kuwa wa kwanza kupata Breaking News za wasanii, watu maarufu na zingine kutoka Magazeti Pendwa ya IJUMAA WIKIENDA, UWAZI, RISASI, AMANI, IJUMAA na CHAMPIONI moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa shilingi 100 tu kwa SIKU!
Kujiunga tuma GLOBAL kwenda 15778
Huduma hii ni kwa watumiaji wa Vodacom pekee. Kwa maelezo zaidi LIKE Ukurasa wetu wa Facebook hapa: http://on.fb.me/L0OSPD

Thursday, January 30, 2014

MABOMU YAFURUMUSHWA KWENYE MSIBA WA ALIYEKUWA SHEIKH WA MKOANI MARA KUWAZUIA WAFUASI WA CHADEMA WASIMFANYIE FUJO MBUNGE WA ZAMANI WA MUSOMA MJINI CCM

NA. Mwandishi wetu
Musoma.

POLISI mkoani Mara wamelazimika kutumia mabomu kuwatawanya wafuasi wanaotajwa kuwa niwa Chama cha maendeleo na demokrasia nchini CHADEMA waliokuwa wakimfanyia fujo aliyekuwa mbunge wa zamani wa Musoma mjini Bw. Vedastus Manyinyi Mathayo wa CCM.

Mathayo ambaye pia alikuwa mjumbe wa NEC inatajwa kuwa amefanyiwa vurugu hizo leo wakati alipokuwa akishiriki kuhani msiba wa aliyekuwa Sheikhe wa Musoma  Othman Magee aliyefariki dunia juzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alipelekwa kwaajili ya kupatiwa matibabu mara baada ya kuhamishiwa toka hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza ambapo ilishindikana.

Taarifa zinasema kuwa mara baada ya Mkutano wa hadhara wa CHADEMA kumalizika wanachama wa chama hicho wakiwa wameambatana na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Wilbrod Slaa pamoja na mbunge wa Musoma mjini Mhe. Vicent Nyerere walielekea kwenye msiba kwaajili ya kujumuika na wafiwa na wananchi wengine.

Wanachama hao walipofika kwenye msiba huo na kumkuta mbunge wa zamani Musoma mjini Bw. Mathayo walianza kumshambulia kwa maneno na katimaye mawe huku wengine wakiburuta pikipiki zao na kulifanya eneo hilo kuwa na hali tete hata baadhi ya magari yakipondwa mawe kwenye eneo la msiba huo.

Dakika chache baadaye polisi walifika katika eneo la msiba ambalo lilikuwa si tulivu tena na kujaribu kuituliza hali kwa njia za kidiplomasia na iliposhindikana walilazimika kurusha mabomu ya machozi ili kupata kuwatawanya wafuasi hao.

Marehemu Sheikh Othman anatarajiwa kuzikwa kesho mjini Musoma.


Taarifa zaidi kuwajia:- ITAENDELEA

KERO: NANI MWENYE TENDA HII MWANZA?

Nazungumzia kampuni yenye dhamana ya kusafisha mitaro ya maeneo ya Kirumba jijini Mwanza, muhusika yapata wiki ya pili sasa tunaenda ya tatu ametoa mchanga, takataka na tope zilizokuwa kwenye mifereji na kuzirundika kandokando ya barabara bila kuzizoa.
Lundo hili la udongo toka kwenye mifareji ya maji taka halileti taswira nzuri kwa barabara hii ya pembezoni mwa uwanja wa CCM Kirumba kuelekea barabara kuu ya Makongoro Air port kupandisha kuelekea Kanisa la Roman Kirumba, Yaani ni uchafu hata barabara yenyewe iliyojengwa kwa kiwango cha lami inakosa maana. 
Ingawa ni barabara kiwango cha lami, magari yakipita ni vumbi kwa kwenda mbele .
Taswira hailipi kabisa....
Wana kusanya lakini hawazoi tatizo nini?
Taratibu wapitao wanazikanyaga taka hizo, je kwa style hii zitasalimika kurudi kwenye mitaro mvua ikinyesha? Work done zero. Au twataka tenda nyingine kuendelea kula fedha za Manispaa?
'Tenda za kupeana hazina kukoromeana' Funika kombe mwanaharamu apite maisha yaendelee.

VYAMA VYA NGUMI ZA KULIPWA KUUNGANA.

VYAMA VYA NGUMI ZA KULIPWA VYAUNGANA

VYAMA vya ngumi za kulipwa nchini  vimekubali  kuungana na wenzao TPBO kushiriki mkutano wa mapromota wa ngumi na mabondia wote wa Tanzania. 
Mkutano huo unaotarajiwa  kufanyika katika ukumbi wa vijana hall – kinondoni, siku ya jumamosi tarehe 1/2/2014 kuanzia  saa nne asubuhi. 
Mkutano huo ulioitishwa na TPBO chini ya udhamini wa KITWE GENERAL TRADERS ukiwa na lengo la kuweka mikakati ya sasa na ya baadae kwa ajili ya kuinua ngumi za hapa nchini,sanjali na kutambulikana kwa mapromota na mabondia wenyewe kwa kutengenezewa vyeti maalum na vitambulisho, vitakavyowafanya watambulike katika jamii ya wanamasumbwi wa hapa Tanzania na hata nje ya mipaka ya nchi yetu,hizo ni sehemu ya mada zitakazozungumzwa.
Ibrahim kamwe akizungumza na vyombo vya habari ,alisema ‘Mkutano huo ambao utawahusisha mapromota wote ,pamoja na viongozi wa vyama vya ngumi za kulipwa, makocha na mabondia wote wa ngumi za kulipwa, haijalishi wewe ni nani ili mradi ni mwalimu wa ngumi, mratibu wa ngumi au bondia ni vema ukafika katika mkutano huo ambao ni mara ya kwanza kufanyika  katika historia ya ngumi za kulipwa kuwakutanisha kwa pamoja waratibu, viongozi na mabondia wa nchi nzima kwa pamoja.

Pia mkutano huo utaendana na mapromota kupewa vyeti  na kurekebisha usajili wa mabondia ambao usajili wao haujakaa sawa.

LG YAZINDUA TV AINA YA OLED AMBAYO NIYA KWANZA KWA UBORA DUNIANI



Na mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
LG imezindua TV ya kwanza ulimwenguni aina ya OLED ambayo ndiyo imeingia katika soko ya nchini Tanzania, TV aina ya OLED inayojikunja ni mwanzo wa burudani ndani ya nyumba. Aina yake ya kujikunja ambayo inaitwa IMAX inatupa uzoefu wa hali ya juu pamoja na kuangalia kwa starehe kubwa.

TV hii mpya aina ya OLED kutoka LG ikiwa na teknolojia ya rangi nne, ambayo kwa mujibu wa kampuni inaongeza pikseli nyeupe kwa rangi nyekundu, kijani na blu kwa mtazamo bora. Itakuwa na screen nyembamba aina ya OLED ambayo ukubwa wake ni 4.3mm. Pamoja na stendi yake ambayo ina vipimo ifuatavyo 1227x799x192mm na uzito wa kilo 17.2.

TV aina ya OLED LG namba 55EA9800 inakuja na idadi ya chaguo ya kuunganisha ambayo ni HDMI port (x4), port ya kusikiliza muziki ( 3.5mm), RF, AV ( composite), port ya muziki, USB 2.0 (x2), USB 3.0 na LAN port.”

TV hii pia ina kitako ambacho ni wazi kama kioo ambacho TV huwa haionekani kama imeungana nacho na TV huonekana kama inaning’inia hewani. Pia TV hii imewezeshwa kuwa na muonekano wa spika tano kwenye kitako chenye LG 55EA9800 zenye uwezo waku toa sauti ya watti 40.

Bwana Rajesh Darji, wa Garnet Star Ltd Distributor wa LG Home Entertainment Products amesema“ Hii TV aina ya OLED inapatikana katika maduka makubwa ya LG na wakala wake.

Caption:

Picha 1. Bw. Valerian Banda ambaye ni msemaji wa Kampuni ya Garnet Star ambao ni wasambazaji wa vifaa vya LG akiongea kuelezea TV ya kwanza ulimwenguni aina ya OLED ambayo ndiyo imeingia katika soko ya nchini Tanzania.

 picha 2. Mkurugeni wa Kampuni ya Garnet Star ambao ni wasambazaji wa bidhaa za LG, Tanzania, Rajesh Kumar (kulia) na Meneja Masoko wa LG, Shakti Vellu (kulia) wakisaidia kuzindua TV ya kwanza ulimwenguni aina ya OLED ambayo ndiyo imeingia katika soko ya nchini Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika katika duka lao lililoko Quality Center jijini Dar es Salaam.

Picha 3. Bw. Valerian Banda ambaye ni msemaji wa Kampuni ya Garnet Star ambao ni wasambazaji wa vifaa vya LG akionyesha miwani ya 3D inayotumika kuangalia kwa TV ya kwanza ulimwenguni aina ya OLED ambayo ndiyo imeingia katika soko ya nchini Tanzania.

Wednesday, January 29, 2014

MOROGORO WALIVYO SHIRIKI OPERESHENI M4C.

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Afande Sele akiwahutubia wananchi wa Kata ya Tungi mjini Morogoro jana, katika mkutano wa hadhaa wa Operesheni M4C Pamoj Daima, ambao pia ulihutubia na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe
Sehemu ya maedlfu ya wakazi wa mji wa Ifakara, wakitawanyika baada ya mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, ambao ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mtibwa, katika mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika jana, ambao pia ulihutubia na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe,
Baadhi ya wa mji wa Ifakara wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, wakati wa mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, ambao ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana
Mwenyekiti wa Chama cha Demokreasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee wakiondoka baada ya kuhutubia mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika mjini Ifakara jana.
Mwenyekiti wa Chama ch Demokrasia na Mendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwahutubia maelfu ya wakzi wa mji wa Mtibwa katika mkutano wa Operesheni M4C pamoja Daima jana.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akimtambulisha mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Afande Sele, wakati wa mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Dama, uliofanyika katika Kata ya Tungi mjini Mororgoro jana.
Maelefu ya wakazi wa mkji wa Ifakara, wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, ambao ulihutubiwa na Mweneyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana.