VYAMA VYA NGUMI ZA KULIPWA VYAUNGANA
VYAMA vya ngumi za
kulipwa nchini vimekubali kuungana na wenzao TPBO
kushiriki mkutano wa mapromota wa ngumi na mabondia wote wa Tanzania.
Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa
vijana hall – kinondoni, siku ya jumamosi tarehe 1/2/2014
kuanzia saa nne asubuhi.
Mkutano huo ulioitishwa na TPBO chini ya udhamini wa KITWE GENERAL
TRADERS ukiwa na lengo la kuweka mikakati ya sasa na ya baadae kwa ajili ya
kuinua ngumi za hapa nchini,sanjali na kutambulikana kwa mapromota na mabondia
wenyewe kwa kutengenezewa vyeti maalum na vitambulisho, vitakavyowafanya
watambulike katika jamii ya wanamasumbwi wa hapa Tanzania na hata nje ya mipaka
ya nchi yetu,hizo ni sehemu ya mada zitakazozungumzwa.
Ibrahim
kamwe akizungumza na vyombo vya habari ,alisema ‘Mkutano huo ambao utawahusisha
mapromota wote ,pamoja na viongozi wa vyama vya ngumi za kulipwa, makocha na
mabondia wote wa ngumi za kulipwa, haijalishi wewe ni nani ili mradi ni mwalimu
wa ngumi, mratibu wa ngumi au bondia ni vema ukafika katika mkutano huo ambao
ni mara ya kwanza kufanyika katika historia ya ngumi za kulipwa
kuwakutanisha kwa pamoja waratibu, viongozi na mabondia wa nchi nzima kwa
pamoja.
Pia mkutano huo utaendana na mapromota kupewa
vyeti na kurekebisha usajili wa mabondia ambao usajili wao haujakaa
sawa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.