Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
usalama ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa mwanza EVARIST NDIKILO amesema kuwa
uchunguzi dhidi ya mauaji ya KAMANDA BARLOW tayari umeanza na kwamba polisi inamshikilia
mwalimu DOROTHY MOSES ambaye alikuwa akipelekwa nyumbani na kamanda
huyo kwa mahojiano zaidi.
Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza LIBERATUS BARLOW ameuwawa kwa kupigwa risasi
na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi usiku wa kuamkia jumamosi oktoba 13 mwaka
huu katika eneo la kitangiri manispaa ya ilemela mkoani Mwanza.
|
Hili ndilo geti ambalo kifo cha Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza RPC Liberatus Barlow kilitokea usiku wa kuamkia leo wakati mwalimu Dorcas Moses alipokuwa akirudishwa nyumbani kupitia lifti ya Kamanda Barlow.
|
Taarifa ya Mkuu wa Mkoa inasema kuwa
Kamanda Barlow alikuwa akitokea kwenye kikao cha Harusi ya ndugu yake aitwaye
Sembeli Maleto kilichokuwa kikifanyika katika Hoteli ya Florida na kisha akampa
lifti mwanamke aitwaye Dorcas Moses ambaye ni mwalimu ya msingi Nyamagana
maeneo ya barabara ya kona ya Bwiru kuelekea Kitangili.
Walipofika getini kwa Dorcas walijitokeza watu wawili waliokuwa
wamevaa makoti ya Polisi Jamii, mama Dorcas akamwuliza Kamanda kama anawafahamu
watu hao, naye bila shaka akasema kuwa hao ni vijana wa ulinzi jamii wako
doria.
Sekunde
chache baadaye vijana hao wakaongezeka na kuwa sita wakaanza kuzozana huku
kamanda huyo akiwauliza kwani hamnijui mimi ni nani, wakiendelea kumtilia ngumu kutomfahamu na watu hao wakizidi kulizingira gari lake marehemu, kamanda
Barlow akajaribu kuchukuwa radio call kuwasiliana na askari wake.
Jamaa hao hawakumruhusu kamanda
afanye mawasiliano kwani papo hapo walimfyatulia risasi kichwani iliyopelekea kifo chake.
Mwili
wa marehemu LIBERATUS BARLOW umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando
kusubiri taratibu za mazishi.