Marehemu Kamanda Liberetus Barlow (kulia) enzi za uhai wake akizungumza na vyombo vya habari jijini Mwanza. |
Ilikuwa ni majira ya saa 8 usiku huu napata taarifa ambazo
hatimaye zinathibitishwa kutoka kwa waugwana kuwa Kamanda wa polisi mkoa wa
Mwanza Liberatus Barlow amefariki dunia kwa kupigwa risasi usiku huu maeneo ya
hotel Tai 5, Kitangili jijini Mwanza .
Marehemu Kamanda Liberatus Barlow
alifariki kabla ya kufikishwa katika hospitali ya Bugando ambapo inadaiwa
alivamiwa na watu takribani wanne waliokuwa wamevalia mavazi ya polisi jamii ndipo
aliposimamishwa na baada ya kusimama watu hao walimmiminia risasi kufuani na kusababisha kifo chake
Imeelezwa kwamba Marehemu Kamanda Liberatus Barlow alikuwa akitoka kwenye harusi na alikuwa na mtu mmoja kwenye gari aliyekuwa akimsindikiza mtu huyo ambaye ni mwanamke yeye hakudhurika na chochote katika tukio hilo.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.Eng. Evarist Ndikilo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama mkoani Mwanza ameshathibitisha kutokea kwa tukio hilo la kifo cha kamanda Liberatus Barlow.
Aidha taarifa zaidi kuhusu tukio hilo tutaendelea kuwajuza kwa kadri tutakavyozipata hapa
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.