Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwasalimia baadhi ya Wanawake wanaounda Baraza la Wanawake wa Chadema, waliokuwa wamefurika kwa wingi nje ya Jengo la LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam, wakati walipowasili kwa kuhutubia Baraza hilo. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Mh. Halima Mdee akizungumza na Umati wa Kinamama wa Chama hicho, uliokuwa umefurika kwa wingi nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower, Kijitonyama jijini Dar es salaam leo Agosti 27, 2015, kabla ya kufanyika kwa Mkutano wa Baraza hilo, uliohutubiwa na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.
Mke wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa akiwasalimia Wanawake wa Chama hicho waliokuwa wamefurika kwa wingi nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower, Kijitonyama jijini Dar es salaam leo Agosti 27, 2015, kabla ya kufanyika kwa Mkutano wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWICHA).
Wakinamama hao wakimshangilia Mh. Lowassa na Babu Duni wakati walipowasili Ukumbini hapo.
Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia akiwasalimia kina mama hao ambao walikosa nafasi ndani ya Ukumbi na kuamua kukaa nje.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akiwasalimia kina mama hao.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza machache wakati akiwasalimia maelfu ya Wanawake wanaounda Baraza la BAWICHA, waliokuwa wamekaa nje ya jengo la LAPF kutokana na kukosa nafasi ndani ya Ukumbi huo. Mh. Lowassa alilazimika kusimama na kuwasalimia kinamama hao kabla ya kuingia Ukumbini kulihutubia Baraza hilo.
Mh. Lowassa na Ujumbe wake wakiwasili Ukumbini.
Baadhi ya Wadau wa Sanaa ya Filamu nchini waliokuwepo kwenye Mkutano huo wa BAWICHA.
Shangwe Ukumbini.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, akiteta jambo na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea Mwenza, Dkt. Juma Haji Duni, wakati wa Mkutano wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Uliofanyika jana Agosti 27, 2015.
Mmoja wa Kinamama wanaowakilisha Watu wenye ulemavu akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mh. Kaihula na Kinamamam wenzake wakifatilia Mkutano huo.
Viongozi wa Kuu.
Keki ya Siku ya Kuzaliwa kwa Mh. Lowassa iliyotolewa na Baadhi ya Washanii wanaomuunga Mkono.
Mmoja wa Wasanii wa Filamu nchini, Jacqueline Wolper akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokea Keki ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kutoka kwa Msanii wa Filamu nchini, Aunt Ezekiel.
Jacqueline Wolper akizungumza kwa niaba ya wenzake.
Mke wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa akitoa hotuba yake mbele ya Wanawake wa Chama hicho waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower, Kijitonyama jijini Dar es salaam leo Agosti 27, 2015, wakati wa Mkutano wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWICHA).
Mh. Mbowe na Mh. Lowassa wakiteta jambo.
Taswira mbali mbali katika Mkutano huo.
Mh. Lowassa akimpongeza Mkewe kwa hotuba nzuri aliyoitoa.
Msanii na Muziki wa Injili, Florah Mbasha akitoa burudani.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, akitoa hotuba yake, kwenye Mkutano wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Uliofanyika leo Agosti 27, 2015, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower, Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Mh. Mbatia akizungumza.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni, akitoa hotuba yake, kwenye Mkutano wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Uliofanyika leo Agosti 27, 2015, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower, Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimueleza jambo, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Mh. Halima Mdee wakati akilihutubia Baraza hilo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa ,akitoa hotuba yake, kwenye Mkutano wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Uliofanyika leo Agosti 27, 2015, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower, Kijitonyama jijini Dar es salaam.