ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 28, 2015

ALLIANCE, MARSH MABINGWA AIRTEL RISING STARS MZA

Nahodha wa timu ya Alliance Academy Ally Hamisi (kushoto) akikabidhiwa kombe na Mwenyekiti wa Soka Mkoa wa Mwanza (MZFA)Bw. Jackson Songora baada ya kutwaa ubingwa wa U-17 Airtel Rising Stars mkoa wa Mwanza upande wa wavulana jana.
Nahodha wa timu ya wasichana ya Marsh Meriany Kimbuya (kushoto) akikabidhiwa na kombe na Meneja Masoko wa Airtel Kanda ya Ziwa Bw. Emmanuel Raphael baada ya kutwaa ubingwa wa U-17 Airtel Rising Stars mkoa wa Mwanza upande wa wasichana jana. 
 ALLIANCE, Marsh mabingwa Airtel Rising Stars Mza Timu ya wavulana ya Alliance Academy ya jijini Mwanza jana imetwaa uchampioni wa michuano ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Aitel Rising Stars kwa kuwafunga Misungwi Academy 3-1 kwenye uwanja wa CCM Kirumba. 

Kwa upande wa wasichana timu ya Marsh ndio iliyotawazwa mabingwa kwa kushinda timu ya TSC kwa magoli 3-2 katika mchezo mkali uliovuta hisia za watamazaji waliojitokeza kushuhuduia mtanange huo. 

Akikabidhi vikombe kwa washindi, Mwenyekiti wa soka mkoa wa Mwanza Bw. Jackson Songora amewataka wachezaji waliochaguliwa kuiwakilisha Mwanza vyema kwenye fainali za Taifa za Airtel Rising Stars zinatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 11 hadi 21. Songora alisema kwamba kikosi kilichochaguliwa kitaanza mazoezi Jumamosi. 

Naye Meneja masoka wa Airtel kanda ya Ziwa Emmanuel Raphel alizipongeza timu zote kwa kushiriki na kuwaasa wachezaji kulinda na kuviendeleza vipaji vyao ambavyo ni hazina kwa taifa. Aliseema lengo lilikuwa ni kuibua vipaji na kuwaasa vijana ambao hawakuchaguliwa kutokata tama na badala yake wajinge kufanya vizuri mwakani. 

Kukamilika kwa michuano hiyo jijini Mwanza ndio kunafunga pazia la Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa iliyoanza kutimua vumbi mwezi uliopita. 

Hivi sasa kombaini za mikoa zilizochaguliwa kuwakilisha mikoa yao zinajiandaa kwa fainali za taifa na mwenyekiti wa soka la vijana wa shirikisho la mpira nchini Bw. Ayoub Nyenzi amesema kuwa maandalizi ya michuano hiyo yamekamilika. Mashindano ya Airtel Rising Stars ambayo mwaka huu yanashirikisha mikoa ya Ilala, Kinondoni, Temeke, Morogoro, Mbeya, Mwanza na Arusha inatarajiwa kuingia kwenye hatu nyeti ya fainali za Taifa iliyopangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, kuanzia Septamba 11 hadi 21.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.