ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 7, 2023

VIJANA RIKA WANOLEWA NAMNA YA KUJILINDA NA MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU

 

NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Shirika la ICAP Tanzania limetoa mafunzo kwa wasichana rika balehe ili kuwawezesha kujilinda dhidi ya maambukizi mapya ya VVU na kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao kujikwamua kiuchumi. Mafunzo hayo ya siku 7, yametolewa na ICAP kwa kushirikiana na Shirika AVSI la nchini Uganda ambapo wasichana hao mbali na kujengewa uwezo huo, wametunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo hayo. Akizungumza kwenye hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi amewataka kutobweteka badala yake watumie elimu hiyo kuwasaidia vijana wenzao kujiepusha na tabia hatarishi zinazoweza kusababisha wapate maambukizi ya VVU. Jiji la Mwanza ndiyo lango kuu la biashara kwa nchi za maziwa makuu ambapo kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni limeshuhudia ukuaji wa sekta mbalimbali miundombinu, afya, na biashara kushamiri huku muingiliano wa watu wanaoingia na kutoka ukiongezeka hivyo kuongeza vishawishi vya masuala mbalimbali likiwemo suala la starehe. Jeh vijana wetu (wasichana) tunawaandaaje na changamoto za vishawishi vya ngono vinavyoletwa na mwingiliano mkubwa wa watu wanaoingia na kutoka wakifanya biashara jijini Mwanza? Hili ndilo swali lililo watafakarisha Shirika la ICAP Tanzania na wadau wenza na hatimaye wakaja na mpango huu.

Thursday, July 6, 2023

SABA SABA HII VIJANA TUNAKESHA NA YESU KATIKA TAMASHA KUBWA LA KUSIFU NA KUABUDU JIJINI MWANZA

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

π—œπ—π—¨π— π—”π—” hii tarehe 7 mwezi wa 7 ni Sikukuu ya 7 7 vijana tunakutana katika mkesha wa kusifu na kuabudu pamoja na maombi unaofanyika katika kanisa la Philadelphia Gospel Assembly Buswelu Mwanza. Mc Suzuki anapata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wadau wahusika wa mkesha huo ambao kama ni vazi la usiku huo yaa πŸ”₯πŸ”₯π˜Ώπ™§π™šπ™¨π™¨ π™˜π™€π™™π™š - 𝙁π™ͺ𝙑𝙑 π™¬π™π™žπ™©π™š . MUDA kuanzia saa 3 usiku hadi majogoo. . ✔️π—ͺπ—”π—œπ— π—•π—”π—π—œ π—ͺπ—”π—§π—”π—žπ—”π—’π—žπ—¨π—ͺπ—˜π—£π—’. - Betha Andrew - Boaz Danken - Ester Nyanda - Goodluck Mombuli - Baraka John - Ben William - Martine Akida - Uswege Mtafya - Joel Kaema - Minister George ➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️ @boazdanken_worship_minister @im_benwilliam @mc_suzuki @jembefmtz @usegemtafya ➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️➖️

MBUNGE KIBAHA MJI APIGA JEKI ML. 3 UJENZI OFISI YA MTAA WA MAILI MOJA.

 

Na Victor Masangu,Kibaha


Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka katika kuunga kuhakikisha anasogeza huduma kwa ukaribu kwa wananchi amechangia kiasi cha shilingi milioni 3  kwa ajili ya kumalizia na kupauwa ujenzi wa mradi wa ofisi ya mtaa wa mail moja A ulipo katika halmashauri ya mji Kibaha.


Koka ameyabainisha hayo wakati wa halfa fupi ya harambee ambayo iliandaliwa kwa ajili ya kuchangia umaliziaji wa ofisi hiyo na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali,chama,wananchi pamoja na wadau wa maendeleo.
Mbunge huyo alibainisha kwamba lengo lake kubwa ni kuhakikisha anaendelea kushirikiana bega kwa bega na wananchi katika kuweka mipango madhubuti ambayo itasaidia kuleta chachu zaidi ya maendeleo katika nyanja mbali mbali ikiwemo huduma muhimu za kijamii.

"Kipindi cha nyuma eneo hili kulikuwa na kichaka lakini kutokana na mji wetu unakuwa zaidi ndio maana maendeleo tunayaona kama haya uwepo wa ujenzi wa ofisi za serikali za mitaa pamoja na kuwepo kwa kituo cha polisi kwa hivyo hii ni moja ya hatua kubwa ndugu zangu,"alisema Koka.
Aidha Mbunge huyo alisema nia yake kubwa ni kuendelea kuleta maendeleo zaidi na kuwataka wana ccm kumpa ushirikiano wa kutosha wakati yupo madarakani na kufanya siasa zenye tija na nidhamu kuliko kufanya mambo ambayo hayana manufaa katika.


Kwa Upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa maili moja A Yasin Mudhihir amemshukuru Mbunge Koka kwa juhudi zake za kuungana na wananchi katika harambee hiyo kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa ofisi hiyo.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa ofisi hiyo kutaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza kwa urahisi majukumu ya kuwasikiliza wananchi juu ya changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili.

"Kwa kweli tunamshukuru kwa dhati Mbunge wetu wa Jimbo la Kibaha mjini kwani ameweza kuendelea kushirikiana bega kwa bega wananchi wake na kwamba ameendelea kutuchangia kiasi cha milioni tatu kwa ajili ya kuweza kupauwa ofisi yetu ili iweze kuanza kutumika rasmi,"alisema Mwenyekiti huyo.

Katika hatua nyingine alisema kabla ya kuanza kwa ujenzi wa mradi huo Mbunge huyo alichangia kiasi cha shilingi laki tano kutoka mfuko wa Jimbo ambazo ziliweza kusaidia katika zoezi la kuanza ujenzi huo.

Naye Diwani wa kata ya mail moja Ramadhani Lutambi amebainisha kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo kutakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa mtaa wa mail moja kupata urahisi wa kuonana na viongozi.


Kwa kipindi cha muda mrefu mtaa wa maili moja A umekuwa ukikabiliwa na kuwa na ofisi yao ya kudumu kwa ambayo walikuwa wakiitumia katika shughuli zao walikuwa wamepewa kwa muda hivyo ofisi yao ikikamilika itakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi na viongozi husika.

RC KINDAMBA AVITAKA VYOMBO VYA SERIKALI NA TAASISI ZA UMMA KULIPA MADENI HARAKA TANGA UWASA

 

MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba wa pili kutoka kushoto akizungumza wakati  ziara yake ya kutembelea Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) kukagua vyanzo vya maji na kuona upanuzi wa eneo Mowe ambalo maji yanasafirishwa kwa ajili ya matumizi katika Mkoa na Jiji la Tanga kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo akifuatiwa na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kulia akimueleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba wakati wa ziara yake wa pili kushoto katika ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema na wa kwanza kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Henry Mwaibambe 
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Goefrey Hilly kulia akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba wa kwanza kushoto wakati wa ziara hiyo katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza mara baada ya ziara hiyo 
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza wakati wa ziara hiyo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akimueleza jambo Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly wakati wa ziara yake kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba aliyesimama katikati wakati wa ziara yake ya kutembelea Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) kukagua vyanzo vya maji na kuona upanuzi wa eneo Mowe ambalo maji yanasafirishwa kwa ajili ya matumizi katika Mkoa na Jiji la Tanga
Eneo la Mowe ambapo maji husafishwa kabla ya kwenda kwa watumiaji

Na Oscar Assenga, TANGA.

MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amevitaka vyombo vya Serikali na Taasisi za Umma wanaodaiwa madeni na Tanga Uwasa kulipa madeni hayo haraka kwa sababu itafikia mahala watakatiwa huduma hiyo.

Kindamba aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) kukagua vyanzo vya maji na kuona upanuzi wa eneo Mowe ambalo maji yanasafirishwa kwa ajili ya matumizi katika Mkoa na Jiji la Tanga

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwamba pamoja na kwamba Tanga Uwasa wamekuwa wakishirikiana na vyombo hivyo lazima wahakikishe wanalipa haraka madeni hayo kwa wale ambao ni wadaiwa sugu ambao hawaonyeshi jitihada za kuyalipa.

“Niwapongeze Tanga Uwasa kwa kufanya kazi nzuri ya kutoa huduma lakini nivitake amevitaka vyombo vya Serikali na Taasisi za Umma wanaodaiwa madeni na Tanga Uwasa kulipa madeni hayo haraka kwa sababu itafikia mahala mtasitishiwa huduma hii”Alisema RC Kindamba.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa namna anavyoendelea kugusa maisha ya wananchi wa kawaida kwa maana ukienda kwenye maji,afya na elimu utamkuta walichokwenda kushuhudia ni kitu kikubwa sana ambapo Tanga Uwasa wameweza kuongeza uwezo wa kusambaza maji kutoka lita Milioni 30,000,000 mpaka lita milioni 45,000,000.

Hata hivyo alisema mpango wa muda ujao na muda wa kati ni kupanua uwezo wa kuzalisha lita milioni 60 na hilo litawezekana kutokana na mipango waliojiwekea watakuja kutangaza kwenye masuala la hati fungani ambazo zitasaidia kupatikana mtaji wa kuweza kupanua zaidi mradi wa maji kwenye mkoa na Jiji la Tanga.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly alisema wanashirikiana vizuri na taasisi za ulinzi na usalama kutoa huduma zao kwani wao wanatoa huduma kwao.

Mhandisi Hilly alisema wakati mwengine kutokana na sababu mbalimbali kuna kukwama kwenye malipo na kwa sasa wanazidai taasisi hizo takribani Bilioni 1.8 wanashuruku wameanza kupunguza kidogo.

“Kama mlisikiliza Bunge mara ya mwisho tulikuwa tunadai Bilioni 2.4 hivyo wamejitahidi kupunguza Milioni 400 karibia 500 hivyo tunaomba wapunguze deni hilo kutokana na deni ni kubwa na linatukwamisha mambo mengi ya utoaji huduma,ununuaji madawa na ulipaji umeme”Alisema Mkurugenzi huyo.

Naye kwa upande wake Mwenyekiit wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo alisema kwamba madeni yamekuwa yakiwasumbua sana hususani vyombo vya Serikali na Taasisi za Umma.

“Kwa kweli ni wateja wetu wazuri lakini madeni yamekaa muda mrefu na tuliona tukushirikishe ili uweze kutusaidia Mkuu wa Mkoa na uwasaidia wenzetu wadai wanapodai walipwe ili waweze kutulipa”Alisema Dkt Fungo..

Wednesday, July 5, 2023

TASAC WASHIRIKI KATIKA MAONYESHO YA BIASHARA YA SABASABA

 

AFISA Masoko Mwandamizi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Martha Kelvin akitoa elimu kwa mmoja wa wananchi waliofika kwenye Banda lao katika Maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam


 Mwananchi aliyetembelea Banda la TASAC akipatiwa  zawadi katika Banda la TASAC
Watumishi \wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Martha Kelvin wa pili kutoka kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wengine wa Shirika hilo wakiwa kwenye Banda lao



Na Mwandishi Wetu,Dar es Saalam

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania, TASAC linashiriki katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa.

Maonesho hayo yenye Kauli Mbiu “Tanzania Mahali Sahihi Pa Biashara na Uwekezaji”, yameanza tarehe 28 Juni, katika viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam na yatahitimishwa tarehe 13 Julai , 2023.

Akizungumza leo Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika hilo Martha Kelvin alisema lengo la kushiriki maonesho hayo ni kujenga uelewa na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kazi na majukumu yanaotekelezwa na TASAC kwa mujibu wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura 415 na mabadiliko yake.

Hata hivyo alisema kwamba TASAC inawaalika wananchi wote kutembelea maonesho haya na kufika katika banda la TASAC lililopo katika ukumbi wa Karume banda namba 22 na 23.

Sunday, July 2, 2023

MARIOO NI MUOGA SANA, WASANII HAWANA UELEWA - MKALI WA GIBELA CHINO KIDD

 

 
Mwanamuziki Chino kiddy akizungumza na Mc Suzuki aka 'Drum Drum' mtangazaji wa Jembe fm Mwanza.