NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
Shirika la ICAP Tanzania limetoa mafunzo kwa wasichana rika balehe ili kuwawezesha kujilinda dhidi ya maambukizi mapya ya VVU na kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao kujikwamua kiuchumi. Mafunzo hayo ya siku 7, yametolewa na ICAP kwa kushirikiana na Shirika AVSI la nchini Uganda ambapo wasichana hao mbali na kujengewa uwezo huo, wametunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo hayo. Akizungumza kwenye hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi amewataka kutobweteka badala yake watumie elimu hiyo kuwasaidia vijana wenzao kujiepusha na tabia hatarishi zinazoweza kusababisha wapate maambukizi ya VVU. Jiji la Mwanza ndiyo lango kuu la biashara kwa nchi za maziwa makuu ambapo kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni limeshuhudia ukuaji wa sekta mbalimbali miundombinu, afya, na biashara kushamiri huku muingiliano wa watu wanaoingia na kutoka ukiongezeka hivyo kuongeza vishawishi vya masuala mbalimbali likiwemo suala la starehe. Jeh vijana wetu (wasichana) tunawaandaaje na changamoto za vishawishi vya ngono vinavyoletwa na mwingiliano mkubwa wa watu wanaoingia na kutoka wakifanya biashara jijini Mwanza? Hili ndilo swali lililo watafakarisha Shirika la ICAP Tanzania na wadau wenza na hatimaye wakaja na mpango huu.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.