Kampuni ya ESAP Mining Services Ltd inayojihusisha na uuzaji wa vilipuzi, uchorongaji na ulipuaji wa miamba kwenye Sekta ya Madini imekaribisha wadau wa madini nchini ikiwa ni pamoja na kampuni za uchimbaji wa madini na ujenzi nchini kutumia bidhaa bora, teknolojia ya kisasa na wataalam waliobobea katika masuala ya vilipuzi.
Akizungumza kwenye mahojiano maalum, Afisa Mawasiliano na Utawala wa kampuni ya ESAP, Shaban Sadick, leo Julai 09, 2023 kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kampuni hiyo iliyoanza tangu mwaka 2022 imekuwa na rekodi ya kufanya kazi na kampuni kubwa nchini kama Buckreef Gold Mine, Busolwa Gold Mine, STAMICO, Kasco Mining Ltd na Nyanza Road Construction Ltd.
Akizungumzia huduma zinavyotolewa na kampuni ya ESAP, Shaban amefafanua kuwa huduma zinapatikana nchi nzima kupitia ofisi zake zilizopo katika maeneo ya Soko la Dhahabu Geita; Kahama, Shinyanga; Mbeya na Bariadi mkoani Simiyu.
Akielezea mipango ya kampuni ya ESAP kwenye uboreshaji wa huduma, Shaban amesisitiza kuwa kampuni ina mpango wa kufungua ofisi katika mikoa yote nchini yenye uhitaji pamoja na nchi za jirani za Afrika Mashariki na Kati .
Ameendelea kusema kuwa wanapatikana kwa mawasiliano ya namba za simu 0677 800003 au 0782 800133 na email info@esap.co.tz.
“ _ESAP IS YOUR CHOICE FOR PARTNERSHIP WHICH MAY ADD THE VALUE OF YOUR OPERATING COMPANY IN TANZANIA”
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.